Saturday 14 August 2010

LIGI KUU ENGLAND: Yaanza kwa makeke!!!
Mabingwa Watetezi Chelsea wakiwa kwao Stamford Bridge leo wameikung’uta Klabu mpya Ligi Kuu West Bromwich Albion kwa bao 6-0 huku Drogba akipata bao 3, Malouda 2 na Lampard 1.
Katika Mechi ya kwanza kabisa, Timu zinazogombea nafasi za juu, Tottenham na Manchester City, zilitoka sare 0-0 Uwanjani White Hart Lane.
Nayo Timu mpya Ligi Kuu, Blackpool, imeanza kwa kishindo ugenini ilipoichapa Wigan bao 4-0 Uwanjani DW.
Licha ya kuondokewa na Meneja Martin O’Neill siku 5 zilizopita, Aston Villa imeanza vyema ikiwa nyumbani Villa Park kwa kuifunga West Ham 3-0.
MATOKEO KAMILI:
Chelsea 6 West Bromwich Albion 0
Tottenham 0 Man City 0
Aston Villa 3 West Ham 0
Blackburn 1 Everton 0
Bolton 0 Fulham 0
Sunderland 2 Birmingham 2
Wigan 0 Blackpool 4
Wolverhampton 2 Stoke 1
Mbrazil Ramires atua Chelsea
Mchezaji wa Kimataifa wa Brazil, Ramires, Miaka 23, anaecheza Benfica, amehamia Chelsea kwa dau la Pauni Milioni 16.3 na tayari ameshapata kibali cha kazi ambacho ndicho kilichochelewesha uhamisho wake.
Ramires ni mmoja Wachezaji wa Brazil waliong’ara huko Afrika Kusini kwenye Fainali za Kombe la Dunia.
Liverpool bado haiuziki
Ingawa kumekuwa na habari za kuuzwa kwa Liverpool huku Mfanyabiashara wa Kichina Kenny Huang na yule toka Syria Yahya Kirdi wakitajwa kuwa ndio wanunuzi wawili wakubwa walijojitokeza lakini mpaka sasa hamna dalili yeyote kuwa dili ya kuuzwa imefikiwa.
Liverpool, inayomilikiwa na Wamarekani wawili, Tom Hicks na George Gillet, imo kwenye lindi kubwa la Madeni na Wamiliki hao wamekuwa wakitafuta mnunuzi kwa muda mrefu.
Utata wa kupata Mnunuzi umethibitishwa na Bodi ya Liverpool ambayo jana ilitoa tamko rasmi kuwa hajapatikana Mnunuzi na mchakato wa kumpata bado unaendelea.

Friday 13 August 2010

Supa Mario ni Man City!!!
Manchester City imekamilisha usajili wa Mchezaji wa Inter Milan, Mario Balotelli, Miaka 20, ambae alitinga Manchester leo na kufanyiwa uchunguzi wa afya yake ambao haukuwa na dosari na hivyo kukamilisha uhamisho huo wa ada ya Pauni Milioni 24.
Usajili huu wa Supa Mario unaifanya Man City iwe tayari imetumia Pauni Milioni 100 kwa kusajili Wachezaji wapya kwa Msimu mpya wa 2010/11 unaoanza Jumamosi Agosti 14 na kitita hicho kitaongezeka ikiwa James Milner wa Aston Villa atakamilisha usajili wake.
Tayari Man City ishawanunua Jerome Boateng, David Silva, Yaya Toure na Aleksandar Kolarov.
Arsene kubaki na Arsenal yake
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger, Miaka 60, ametoboa kuwa yuko mbioni kusaini Mkataba mpya na Arsenal ambako yuko nayo tangu 1996.
Mkataba wa sasa wa Wenger unakwisha Mwaka 2011, mwishoni mwa Msimu mpya wa 2010/11.
Tangu atinge Arsenal, Wenger ameshinda Vikombe 11 katika Miaka 13 lakini ameambulia patupu tangu 2005 alipochukua Kombe la FA.
Wenger ametwaa Ubingwa wa Ligi Kuu mara 3, Mwaka 1998, 2002 na 2004, FA Cup Mwaka 1998, 2002, 2003 na 2005.
Na tangu wahamie Uwanja wao wa Emirates toka Uwanja wa zamani Highbury, Arsene na Arsenal yake wamekuwa vibonde na hawajaambua chochote.
Bellamy mguu nje Man City
Craig Bellamy huenda akatimka Manchester City baada ya jina lake kutokuwemo kwenye Listi ya Wachezaji 25 waliosajiliwa na Klabu hiyo kwa ajili ya michuano ya EUROPA LIGI.
Bellamy alitamka wazi kuwa hawezi kubaki hapo ikiwa hatakuwemo kwenye Kikosi hicho na inaelekea jina lake limekatwa dakika za mwisho ili kuliongeza jina la Robinho alielazimika kurudi Klabuni hapo baada ya Mkataba wake wa mkopo huko Santos kumalizika na Man City kugoma kumwongezea.
Robinho, alienunuliwa toka Real Madrid Septemba 2008, amekuwa Santos ya huko kwao Brazil tangu Januari Mwaka huu baada ya kushindwa kung’ara huko Manchester na pia moyo wake kutofurahishwa na Klabu hiyo hasa baada ya Roberto Mancini kutua hapo kama Meneja badala ya Mark Hughes alietimuliwa Desemba Mwaka jana.
Wachezaji wengine ambao hawamo kwenye Kikosi cha Wachezaji 25 ni Stephen Ireland, Jo na Mchezaji mpya David Silva ambae tatizo lake linahusiana na Klabu hiyo kulazimika kuitii Sheria mpya ya kuwa na Wachezaji 8 kati ya 25 ambao ni wale ‘waliolelewa’ nyumbani.
Hata hivyo, David Silva ataruhisiwa kucheza EUROPA LIGI ikiwa Man City watafuzu kutoka hatua ya Makundi na kuingia kucheza Raundi ya Mtoano ya Timu 32.
Ili kuingia hatua ya Makundi ya EUROPA LIGI, Man City lazima waitoe FC Timisoara ya Romania katika hatua ya Raundi ya Mchujo ambayo Mechi ya kwanza inachezwa Romania Agosti 19 na marudio Agosti 26.
KIKOSI KAMILI: Given, Hart, Taylor; Boateng, K. Toure, Lescott, Kolarov, Richards, Zabaleta, Bridge, Logan; A. Johnson, Barry, De Jong, Y. Toure, Kompany, M. Johnson, Vieira, Wright-Phillips; Adebayor, Robinho, Santa Cruz, Tevez.

Wednesday 11 August 2010

FIFA yasalimu amri
Rais wa FIFA, Sepp Blatter, amesema kikao cha IFAB [International Football Association Board] cha Mwezi Oktoba kitajadili utumiaji wa teknolojia ya kisasa ili kusaidia Marefa kufikia uamuzi wa haraka na sahihi kama mpira umevuka mstari wa goli au la na uamuzi huo ni kubadilika kwa msimamo wa FIFA uliokuwa ukipinga matumizi ya teknolojia hiyo.
Blatter alikuwa ndie mpinzani mkubwa wa teknolojia hiyo lakini baada ya skandali kubwa huko Afrika Kusini kwenye Fainali za Kombe la Dunia ambako Marefa walikataa magoli ya wazi, FIFA imelazimika kuliingiza suala hilo kwenye vikao kulijadili.
IFAB, inajumuisha Vyama vya Soka vya England, Wales, Scotland na Ireland, ambao ndio Waanzilishi wa Soka, na pamoja na FIFA, ndicho chombo pekee chenye mamlaka ya maamuzi ya kubadilisha Sheria za Soka Duniani.
Kuhusu malalamiko ya Mameneja wa Klabu huko Ulaya kupinga kuwepo kwa Mechi za kirafiki za Kimataifa katikati ya Wiki hii huku Misimu mingi mipya huko Ulaya ikitakiwa kuanza Wikiendi hii, Blatter amesema si sahihi kuilaumu FIFA kwani kuna tarehe mbili kwa Mwaka kwa Mechi hizo na si lazima kwa Vyama vya Soka vya Nchi kuzitumia na pia si lazima kwa Nchi kuchezesha Wachezaji wao bora katika Mechi hizo.
Blatter ametamka: “Ukitaka mechi za kirafiki chezesha Kikosi cha pili au cha tatu, hakuna atakaekudai Wachezaji bora! Usipige kelele kuilaumu FIFA, ongeeni na Vyama vyenu!”
Fergie: “Hamna tena Vigogo wanne Ligi Kuu, ni utitiri wa Timu!”
Bosi wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, anaamini kuwa Msimu huu utakuwa mgumu mno kwa Timu kumaliza nafasi nne za juu kwa vile kuna ushindani mkali na mgumu mno.
Msimu uliokwisha Manchester United walimaliza nafasi ya pili, pointi moja nyuma ya Mabingwa Chelsea, Arsenal nafasi ya 3 na Tottenham nafasi ya 4.
Kama ilivyo Msimu uliopita, Ferguson anaamini Timu kubwa zote zitapoteza pointi bila kutegemewa kwa Timu zinazodhaniwa dhaifu.
Mbali ya Chelsea, Man United, Arsenal na Tottenham, Ferguson anaamini Manchester City, Aston Villa na Everton ni miongoni mwa Klabu zitazokuwa kwenye kinyang’anyiro cha nafasi za juu Ligi Kuu.
Carvalho amfuata Mourinho Real
Beki toka Ureno, Ricardo Carvalho, yuko hatua za mwisho kusaini na Real Madrid ili ajiunge na Meneja wake wa zamani Jose Mourinho.
Carvalho, Miaka 32, atasaini Mkataba na Real kwa dau la uhamisho la Pauni Milioni 6.7.
Carvalho na Mourinho walikuwa wote FC Porto na kisha Chelsea.
Huyu ni Mchezaji wa tano kwa Real Madrid kumsaini kwa ajili ya Msimu mpya wengine wakiwa Angel di Maria, Pedro Leon, Sergio Canales na Sami Khedira.
Kwa Chelsea, yeye ni Mchezaji wa tano kuhama Stamford Bridge wengine wakiwa Joe Cole, Michael Ballack, Juliano Belletti na Deco
MECHI ZA KIMATAIFA: Matokeo
Jumanne, Agosti 10
Ivory Coast 1 Italy 0
Katika mechi iliyochezwa Upton Park, London, kichwa cha Kolo Toure cha dakika ya 55kiliwapa ushindi Ivory Coast.
USA 0 Brazil 2
Mabao ya Neymar Da Silva, dakika ya 29, na Alexandre Pato, dakika ya 45, yamewapa Brazil ushindi wa mabao 2-0.

Tuesday 10 August 2010

Man City na mgogoro wa Wachezaji
Inaelekea kuna vita ya kichinichini huko Manchester City, Klabu iliyokumbwa na utajiri mkubwa, unaowafanya ulundike Wachezaji na kufanya iibue misuguano ya kugombea namba.
Kipa Nambari Wani wa Man City, Shay Given, ametamka wazi wazi kuwa yuko tayari kuhama ikiwa katika Mechi ya kwanza ya Ligi Kuu wikiendi hii dhidi ya Tottenham atawekwa benchi na badala yake namba kupewa kijana Joe Hart.
Shay Given aliteguka bega mwishoni mwa Msimu uliopita kwenye Mechi na Arsenal na ingawa amerudi tena kucheza, katika Mechi zote za hivi karibuni za majaribio Meneja wa Man City, Roberto Mancini, amekuwa akiwapanga kwa zamu yeye na Joe Hart.
Given, Miaka 34, ametamka: “Ntaangalia Jumamosi itakuwaje. Nataka niendelee kucheza na kama sichezi ntaongea na Klabu nijue hatima yangu.”
Kipa huyo wa Kimataifa wa Ireland aliehamia Man City kutoka Newcastle amesisitiza yeye hakwenda Man City kuwa Kipa namba mbili.
Gerrard akubali kuzomewa!
Nahodha wa England, Steven Gerrard, amekiri hata yeye kama angekuwa shabiki angewazomea Wachezaji wa England Uwanjani Wembley Jumatano watakapocheza na Hungary Mechi ya kirafiki kufuatia kutofanya vizuri huko Afrika Kusini kwenye Fainali za Kombe la Dunia.
Gerrard alikubali: “Ndio, ningefanya hivyo! Najua kuna baadhi kesho watazomea kwa nyakati fulani. Lakini lazima tuwe Wanaume na tulikubali hilo. Hatukufanya vizuri lakini tutaonyesha uwezo wetu.”
Man United kuigomea France kumhoji Evra
Manchester United wanatafakari kufuata nyayo za Bayern Munich za kuigomea Ufaransa kumwita Mchezaji wao Patrice Evra, aliekuwa Nahodha wa France Kombe la Dunia huko Afrika Kusini, kwenda kuhojiwa na FFF, Chama cha Soka France, kuhusu kashfa iliyoikumba Nchi hiyo baada ya Mchezaji Nicolas Anelka kutimuliwa alipogombana na Kocha Raymond Domenech na Wachezaji kugoma kufukuzwa kwake.
FFF imewaita kwa mahojiano Evra, Franck Ribery wa Bayern Munich, Nicolas Anelka wa Chelsea, pamoja na Jeremy Toulalan na Eric Abidal, ili kuchunguza mgomo wa Wachezaji kufuatia kufukuzwa Nicolas Anelka.
Wachezaji hao wametakiwa wakutane na FFF Jumanne ijayo lakini Bayern Munich imedai Chama hicho hakina haki kuwaita Wachezaji nje ya Kalenda ya FIFA.
Evra ametamka: “Nashangaa, nilidhani kila mtu anataka ukurasa mpya baada ya Kombe la Dunia. Kwanini watake kutuadhibu zaidi baada ya kutuacha wote 23 kwa Mechi ya kirafiki na Norway?”
WIKI YA MECHI ZA KIMATAIFA: Klabu zaombea Wachezaji wasiumie!!
Klabu kubwa za Ulaya zinaomba Mungu Wachezaji wao Mastaa hawaumizwa katika Mechi za Kimataifa zitakazochezwa leo Jumanne na kesho Jumatano Duniani kote kwa mujibu wa Kalenda ya FIFA ya Mechi za Kimataifa.
Mabingwa wapya wa Dunia, Spain, wanasafiri hadi Mexico kucheza na Nchi hiyo huku wakiwa na Wachezaji wengi wa Barcelona licha ya Klabu hiyo kuomba wasichukuliwe wote.
Jumamosi ijayo Barcelona itacheza na Sevilla kugombea Super Cup na Kikosi cha Spain kitarudi kwao Ijumaa kutoka Mexico.
England wapo Jijini London, Uwanja wa Wembley, na Jumatano wanacheza na Hungary katika Mechi ambayo England wataomba matokeo mazuri ili kufuta huzuni ya kubwagwa nje ya Kombe la Dunia huko Afrika Kusini.
Argentina, bila Kocha Diego Maradona alienyimwa Mkataba mpya, watakuwa Uwanja mpya wa Aviva huko Dublin kucheza na Ireland.
Timu iliyopatwa na aibu na kashfa, France, itasafiri hadi Norway ikiwa chini ya Kocha mpya, Laurent Blanc, na Kikosi ambacho hakina hata Mchezaji mmoja kati ya 23 waliokuwa kule Afrika Kusini kwenye Fainali za Kombe la Dunia.
Kocha mpya wa Italy, Cesare Prandelli, ataiongoza Nchi yake kwenye Mechi yake ya kwanza dhidi ya Ivory Coast hapo Jumanne.
Ivory Coast nao wana Kocha mpya, Gerard Gili kutoka France, badala ya Sven-Goran Eriksson aliemaliza Mkataba.
MECHI ZA KIRAFIKI ZA KIMATAIFA:
Jumanne, Agosti 10
USA v Brazil
Italy v Ivory Coast
Jumatano, Agost 11
Israel v Gambia
South Korea v Nigeria
China PR v Bahrain
Mali v Guinea
Russia v Bulgaria
Finland v Belgium
Moldova v Georgia
Cyprus v Andorra
Malta v FYR Macedonia
Sweden v Scotland
Ukraine v Netherlands
Czech Republic v Latvia
Turkey v Romania
Albania v Uzbekistan
Austria v Switzerland
Denmark v Germany
Montenegro v Northern Ireland
Poland v Cameroon
Serbia v Greece
Slovakia v Croatia
South Africa v Ghana
Rep of Ireland v Argentina
Slovenia v Australia
Wales v Luxembourg
England v Hungary
Norway v France
Iceland v Liechtenstein
Mexico v Spain
Angola v Uruguay
Paraguay v Costa

Monday 9 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

O'Neill atimka Villa
Martin O'Neill amejiuzulu kama Meneja wa bila kutaja sababu za zilizomfanya achukue uamuzi huo.
O’Neill alianza kazi hapo Aston Villa Mwaka2006 na kuifanya Klabi hiyo iwe ikimaliza Ligi Kuu katika nafasi za juu na Msimu uliokwisha ilishika nafasi ya 6 hiyo ikiwa ni kwa mara ya tatu mfululizo.
Kevin MacDonald ameteuliwa kuwa Meneja wa muda.
NGAO YA HISANI: Man United 3 Chelsea 1
• Man United yaonyesha kuwa tishio Msimu mpya!
Manchester United hapo jana iliifumua Chelsea kwa bao 3-1 na kutwaa Ngao ya Hisani katika pambano lililochezwa Uwanja wa Wembley Jijini London.
Mbele ya Mashabiki 84,623 waliokuwa wakiwazomea Wachezaji wa England waliocheza Kombe la Dunia huko Afrika Kusini, Kiungo mkongwe wa Manchester United, Paul Scholes aling’ara na kuibuka kuwa Mchezaji Bora wa Mechi hiyo.
Man United walipata bao la kwanza kwa Soka tamu kati ya Scholes na Rooney na mpira kupelekewa Valencia aliefunga.
Mchezaji mpya wa Man United, Javier Hernandez, maarufu kama Chicharito, alionyesha cheche zake na kuamsha matumaini makubwa kwa Washabiki wa Man United na ndie aliefunga bao la pili.
Chelsea walipata bao lao kupitia Salomon Kalou baada ya Kipa Edwin van der Sar kutema shuti la Daniel Sturridge.
Vikosi:
Chelsea: Hilario, Paulo Ferreira (Bruma 79), Ivanovic, Terry, Cole (Zhirkov 79), Essien, Lampard, Mikel (Drogba 60), Kalou, Anelka (Sturridge 60), Malouda (Benayoun 72).
Akiba hawakucheza: Turnbull, Van Aanholt.
Man Utd: Van der Sar, O'Shea, Jonathan Evans, Vidic, Fabio Da Silva (Smalling 71), Valencia, Scholes (Fletcher 80), Carrick (Giggs 79), Park (Nani 46), Owen (Hernandez 46), Rooney (Berbatov 46).
Akiba hawakucheza: Kuszczak.
Refa: Andre Marriner

Sunday 8 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

NGAO YA HISANI: Leo Man United v Chelsea
Wakionyesha kujiamini mno licha ya kufanya vibaya katika mechi zao za kujipima nguvu za hivi karibuni ambazo walifungwa Mechi 3 mfululizo, Kocha wa Chelsea, Carlo Ancelotti, ameshakitangaza Kikosi chake cha Wachezaji 11 watakaoshuka Wembley leo kupambana na Manchester United kugombea Ngao ya Hisani hili likiwa pambano maalum kuufungua Msimu mpya wa Soka.
Nae Sir Alex Ferguson, Meneja wa Man United, amekiri kuwa Msimu huu mpya unaoanza ni Chelsea ndio ambao tu watakuwa tishio kwao kwa vile tu ni Mabingwa wa Ligi Kuu England na pia walinyakua Kombe la FA.
Ancelotti amesema Kipa wao atakuwa Hilario badala ya Nambari wani wao Petr Cech ambae ni majeruhi na pia Nyota wake Didier Drogba atakuwa benchi.
Man United itawakosa Michael Carrick, Anderson, Patrice Evra na Rio Ferdinand ambao ni majeruhi.
Ferguson pia alisema Mastraika Wayne Rooney na Michael Owen watacheza kwa dakika 45 tu kwa vile bado hawajawa kifiti kwa Mechi.
Vikosi vinategemewa kuwa:
Chelsea: Hilario, Ivanovic, Terry, Ferreira, Cole, Essien, Lampard, Mikel, Kalou, Anelka, Malouda.
Akiba: Turnbull, Bruma, Zhirkov, Carvalho, Benayoun, Kakuta, Drogba, Sturridge
Man United: Van der Sar, Kuszczak, O'Shea, Neville, Evans, De Laet, Vidic, Smalling, Brown, Fletcher, Scholes, Gibson, Giggs, Park, Valencia, Nani, Cleverley, Rooney, Hernandez, Berbatov, Owen, Macheda.
Wenger kuendelea Ze Gunners
Arsene Wenger, Miaka 61, ambae Mkataba wake na Arsenal umebakiza Mwaka mmoja amesisitiza kuwa hana nia ya kwenda Klabu nyingine yeyote na hivyo kuleta matumaini kuwa yupo tayari kuongeza Mkataba na Arsenal ambayo yuko nayo tangu 1996.
Wenger ametamka: “Nipo kwenye steji kuwa nikiongeza Mkataba na Arsenal ni kwamba nataka kustaafu Soka nikiwa na Klabu hiyo tu. Nikienda kwingine ni changamoto mpya na hilo halinitii hamasa. Nina Mwaka mmoja na tutakaa kuamua kuongeza.”
Kipa Robinson aigomea England na kutangaza kustaafu
Kipa wa Blackburn Paul Robinson, Miaka 30, amejitoa kwenye Kikosi cha England cha kucheza na Hungary Jumatano baada ya kuchaguliwa na Kocha wa England Fabio Capello kwenye Kikosi hicho.
Robinson, ambae aliidakia England Fainali za Kombe la Dunia Mwaka 2006 lakini hakuchukuliwa kule Afrika Kusini, ametamka: “Nilikuwa sichaguliwi na siwezi kukubali kuitwa na kuwa Kipa Nambari 2 au 3! Hilo linavunja moyo. Ni bora nistaafu!”
Robinson alianza kuichezea England Mwaka 2003 na amecheza mara 41 lakini kwenye EURO 2008 alifanya makosa hasa kwenye Mechi na Croatia wakati pasi ya Garry Neville ya kumrudishia alipoikosa na kutinga wavuni na hivyo England kukosa kuingia Fainali za EURO 2008.
Mechi yake ya mwisho ilikuwa dhidi ya Urusi ambayo pia alifanya kosa kubwa wakati shuti la mbali alishindwa kulidaka na kuutema mpira kumdondokea Roman Pavlyuchenko aliefunga bao la pili na hivyo kuibwaga England 2-1.
CHEKI: www.sokainbongo.com

England yateua Kikosi
Kocha wa England, Fabio Capello, ametangaza Kikosi chake kitakachocheza Mechi ya kirafiki na Hungary Jumatano Uwanjani Wembley na wamo Wachezaji 10 tu kati ya 23 waliokwenda Afrika Kusini kwenye Fainali za Kombe la Dunia.
Wapo Wachezaji watatu, Jack Wilshere, Kieran Gibbs na Bobby Zamora, ambao hawajawahi kuichezea England.
Wachezaji maarufu walioachwa ni pamoja na Makipa David James na Robert Green, wengine ni Joe Cole, Jermain Defoe na Peter Crouch.
Kikosi kamili:
Makipa: Ben Foster (Birmingham), Joe Hart (Manchester City), Paul Robinson (Blackburn)
Mabeki: Wes Brown (Manchester United), Gary Cahill (Bolton), Ashley Cole (Chelsea), Michael Dawson (Tottenham Hotspur), Kieran Gibbs (Arsenal), Phil Jagielka (Everton), Glen Johnson (Liverpool), John Terry (Chelsea)
Viungo: Gareth Barry (Manchester City), Steven Gerrard (Liverpool), Adam Johnson (Manchester City), Frank Lampard (Chelsea), James Milner (Aston Villa), Ashley Young (Aston Villa), Theo Walcott (Arsenal), Jack Wilshere (Arsenal)
Mafowadi: Darren Bent (Sunderland), Carlton Cole (West Ham United), Wayne Rooney (Manchester United), Bobby Zamora (Fulham)
Diouf aenda Blackburn kwa mkopo
Straika wa Manchester United Mame Biram Diouf amechukuliwa na Blackburn Rovers kwa mkopo wa Msimu mmoja.
Diouf alijiunga na Man United Mwaka jana akitokea Klabu ya Norway Molde lakini alianza kucheza Old Trafford Januari Mwaka huu.
Sir Alex Ferguson amesema amempeleka Blackburn ili apate Mechi nyingi za kucheza na kupata uzoefu kwani hapo Old Trafford kuna ushindani mkubwa wa namba za Mastraika zinazogombewa na kina Wayne Rooney, Bebatov, Michael Owen, Macheda na Chicharito.
Wachezaji wengine wanaotegemewa kwenda nje ya Man United kwa mkopo ni Danny Welbeck na Cleverly.
Powered By Blogger