Saturday 20 March 2010

LIGI KUU: Matokeo
Jumamosi, Machi 20
Aston Villa 2 v Wolves 2
Everton 2 v Bolton 0
Portsmouth 3 v Hull 2
Stoke 1 v Tottenham 2
Sunderland 3 v Birmingham 1
Wigan 1 v Burnley 0

=Arsenal v West Ham inaanza saa 2 na nusu bongo taimu.
LIGI KUU: Villa 2 Wolves 2
Katika mnechi ya kwanza ya Ligi Kuu leo Jumamosi, Aston Villa wakiwa kwao Villa Park wametoka sare na Wolverhamton Wanderers kwa bao 2-2.
Sare hii imewafanya Villa wafikishe pointi 50 sawa na Manchester City walio nafasi ya 6 na wamecheza mechi moja pungufu.
Wolves wamechupa toka nafasi ya 17 hadi ya 15.
Villa ndio walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia John Carew kwenye dakika ya 16 na Wolves wakasawazisha dakika ya 23 kwa bao la Craddock.
Katika dakika ya 38, katika hekaheka za kuokoa, James Milner akajifunga mwenyewe na kuwapa uongozi Wolves hadi dakika ya 82 ambapo John Carew alisawazisha.
LIGI KUU: Mechi za Jumamosi na Jumapili
RATIBA:
[saa za bongo]
Jumamosi, Machi 20
[saa 9 dak 45 mchana]
Aston Villa v Wolves
[saa 12 jioni]
Everton v Bolton
Portsmouth v Hull
Stoke v Tottenham
Sunderland v Birmingham
Wigan v Burnley
[saa 2 na nusu usiku]
Arsenal v West Ham
Jumapili, Machi 21
[saa 10 na nusu jioni]
Man United v Liverpool
[saa 12 jioni]
Fulham v Man City
[saa 1 usiku]
Blackburn v Chelsea
=========================================================================
MSIMAMO LIGI KUU England:
1. Man United mechi 30 pointi 66
2. Chelsea mechi 29 pointi 64
3. Arsenal mechi 30 pointi 64
4. Tottenham mechi 29 pointi 52
---------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
5. Liverpool mechi 30 pointi 51
6. Man City mechi 28 mechi 50
7. Aston Villa mechi 28 pointi 49
8. Birmingham mechi 29 pointi 44
9. Everton mechi 29 pointi 42
10. Fulham mechi 29 pointi mechi 38
11. Stoke mechi 29 pointi 36
12. Blackburn mechi 29 pointi 34
13. Bolton mechi 30 pointi 32
14. Sunderland mechi 29 pointi 31
15. Wigan mechi 30 pointi 28
16. West Ham mechi 29 pointi 27
17. Wolves mechi 29 pointi 27
--------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
18. Burnley mechi 30 pointi 24
19. Hull mechi 29 pointi 24
20. Portsmouth mechi 29 pointi 10
========================================================================
UCHAMBUZI:
BIGI MECHI: Manchester United v Liverpool [Jumapili, Old Trafford]
Bila shaka, BIGI MECHI ni Jumapili huko Old Trafford kati ya Mahasimu wakubwa Manchester United, wanaoongoza Ligi na wanaotafuta Ubingwa kwa mara ya 4 mfululizo ikiwa ni rekodi na pia kuwapiku Liverpool kwa kuchukua Ubingwa kwa mara ya 19, watakapowavaa Liverpool, Timu inayosuasua Msimu huu na huenda wakaikosa hata nafasi ya 4 na hivyo kutupwa nje ya UEFA CHAMPIONS LIGI msimu ujao.
Aston Villa v Wolves
Hii ndio mechi ya fungua dimba wikiendi hii na itachezwa saa 9 dakika 45, saa za bongo, huku Villa wakiwania nafasi ya 4 inayogombewa sana kwa vile itaifanikisha Timu itakayoitwaa kucheza UEFA CHAMPIONS LIGI hasa kwa vile nafasi 3 za juu za Ligi zimeshahodhiwa na Man United, Chelsea na Arsenal.
Villa wako pointi 3 nyuma ya Tottenham walio nafasi ya 4 lakini Villa wana mechi moja mkononi.
Wolves wanaingia mechi hii wakitoka kwenye ushindi wa nadra wa ugenini walipoifunga Burnley 2-1 mechi iliyokwisha.
Portsmouth v Hull City
Hii ni mechi ya kwanza kwa Meneja mpya wa Hull City, Ian Dowie.
Kwa Portsmouth, baada ya kukatwa pointi 9, kuporomoka Daraja ndio njia pekee kwao kwani sasa wana pointi 10 tu, wamebakisha mechi 9 na Timu iliyo juu yao iko mbele kwa pointi 14.
Kilichobaki kwao ni kucheza kulinda fahari yao.
Arsenal v West Ham United
Kwa vile Man United na Chelsea zote zinacheza Jumapili, ushindi kwa Arsenal utawafanya waongoze Ligi lakini hii ni dabi ya Timu za London na huwa haitabiriki.
Katika mechi iliyokwisha, Arsenal walipata ushindi dakika za majeruhi pale Nicklas Bendtner alipowafungia bao la pili dhidi ya Hull City.
West Ham wapo kwenye majaribuni makubwa baada ya kupoteza mechi 3 za mwisho na wako nafasi ya 16 kwenye Ligi.
Stoke City v Tottenham Hotspur
Hii ni tripu ngumu kwa Tottenham walio nafasi ya 4 watakapokuwa wageni wa Stoke Uwanjani Britannia ambako Stoke wamefungwa mechi moja tu ya Ligi Kuu katika 10 zilizochezwa uwanjani hapo.
Tottenham pia watakumbuka walipokuwa kwao White Hart Lane walifungwa na Stoke kwenye mechi ya kwanza ya Ligi.
Wigan v Burnley
Hii ni vita ya Timu zinazopigana kukimbia kuporomoka Daraja na zimetenganishwa na pointi 4 huku Burnley wakiwa moja ya Timu 3 zilizo nafasi za mwisho na hivyo eneo la kushuka Daraja.
Sunderland v Birmingham
Baada ya kucheza mechi 14 bila ushindi, Sunderland wameweza kupata pointi 5 katika mechi zao 3 za mwisho za Ligi na ushindi mwingine utawafanya Sunderland walikimbie lile eneo la hatari la kuporomoka Daraja.
Birmingham wao wako nafasi ya 8 na ni Timu iliyo na matokeo mazuri kwa jumla.
Everton v Bolton Wanderers
Ndani ya Goodison Park, Everton wanawakaribisha Bolton ambao walishinda kwa kishindo mechi yao iliyokwisha walipoitwanga Wigan 4-0 na hivyo kujiwekea tofauti ya pointi 8 na Timu zilizo hatarini kuteremka Daraja.
Everton, waloanza vibaya msimu huu, wameibuka mwaka huu 2010 na kuwa na matokeo mazuri na kuwafanya wawe nafasi ya 9.
Fulham v Manchester City
Jumapili, Uwanja wa Crave Cottage utawakutanisha wenyeji Fulham na Man City huku Fulham wakitoka kwenye furaha ya kuwanyuka 4-0 Vigogo wa Italia Juventus na kutinga Robo Fainali ya EUROPA LIGI ambako watacheza na Wolfsburg ya Ujerumani.
Fulham wakiwa nyumbani ni wagumu kwani wamepoteza mechi moja tu katika 11 lakini Man City ni goigoi wakisafiri na wameshinda mechi 2 tu katika 13.
Blackburn Rovers v Chelsea
Wakiwa nyumbani Ewood Park siku ya Jumapili, Blackburn watakutana na Chelsea waliotunguliwa na Meneja wao wa zamani Jose Mourinho na Inter Milan yake na hivyo kubwagwa nje ya UEFA CHAMPIONS LIGI.
Chelsea huwa mara nyingi wanasumbuka kushinda ugenini msimu huu na Blackburn ni wagumu mno kufungika kwao na wameshinda mechi zao 4 za mwisho.

Friday 19 March 2010

EUROPA LIGI: Fulham v Wolfsburg na Liverpool v Benfica
Timu za England, Fulham na Liverpool, zimetenganishwa na zitakuta tu kwenye Fainali endapo zitafuzu kuvuka vikwazo vya Robo Fainali kwenye Mashindano ya EUROPA LIGI.
Kwenye Robo Fainali, Fulham watacheza na Wolfsburg ya Ujerumani. Mshindi wa mechi hii atacheza na Mshindi wa mechi kati ya Hamburg v Standard Liege kwenye Nusu Fainali.
Nao Liverpool wataivaa Benfica ya Ureno kwenye Robo Fainali na Mshindi wa mechi hii atacheza na Mshindi wa Valencia v Atletico Madrid kwenye Nusu Fainali.
Robo Fainali zitachezwa Aprili 1 na marudio Aprili 8.
UEFA CHAMPIONS LIGI: Droo tayariiiiii!!!!!!!!!!!!
Ni rasmi: Arsenal v Barcelona & Man United v Bayern Munich!!!
Droo ya UEFA CHAMPIONS LIGI imefanyika na Manchester United na Arsenal zimetenganishwa na zitakutana tu kwenye Fainali ikiwa Timu hizo zitashinda mechi zao za Robo Fainali na Nusu Fainali.
Kwenye Robo Fainali, Arsenal watawakwaa Mabingwa Watetezi Barcelona na Mshindi wa mechi hiyo atakutana na Mshindi wa Inter Milan au CSKA Moscow kwenye Nusu Fainali.
Manchester United atacheza na Bayern Munich Robo Fainali na Mshindi atacheza na Mshindi wa mechi ya Lyon v Bordeaux kwenye Nusu Fainali.
Robo Fainali zitachezwa Machi 30 na 31 na kurudiwa Aprili 6 na 7.
Nusu Fainali zitakuwa Aprili 20 na 21 na marudiano ni Aprili 27 na 28.
Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI ni Mei 22 kwenye Uwanja wa Real Madrid Santiago Bernabeu huko Madrid, Spain.
Refa afungiwa maisha!!!
UEFA imempa Refa Oleh Orekhov kutoka Ukraine kifungo cha maisha katika masuala ya Soka kutokana na kuhusika na upangaji matokeo wa mechi.
UEFA imetamka kuwa Refa huyo alikiuka misingi ya uaminifu na maadili ya kandanda lakini haikutaja ni Ligi ipi au mechi zipi Refa huyo alipanga matokeo.
Taarifa hiyo ya UEFA imesema uamuzi wao unatokana na fununu walizopewa na Polisi wa Ujerumani waliokuwa wakichunguza zaidi ya mechi 200 zilizochezwa katika Nchi 11 ambazo zilikuwa zimegubikwa na utata wa upangaji matokeo.
Uamuzi huo wa UEFA umetoka kwenye Bodi yao ya Nidhamu na Udhibiti ambayo maamuzi yake yanaweza kukatiwa Rufaa ndani ya siku 3 baada ya Mtuhumiwa kupokea rasmi taarifa ya adhabu yake.
LIGI KUU England: RATIBA Wikiendi hii
[saa za bongo]
Jumamosi, Machi 20
[saa 9 dak 45 mchana]
Aston Villa v Wolves
[saa 12 jioni]
Everton v Bolton
Portsmouth v Hull
Stoke v Tottenham
Sunderland v Birmingham
Wigan v Burnley
[saa 2 na nusu usiku]
Arsenal v West Ham
Jumapili, Machi 21
[saa 10 na nusu jioni]
Man United v Liverpool
[saa 12 jioni]
Fulham v Man City
[saa 1 usiku]
Blackburn v Chelsea
Beckham kupewa wadhifa Timu ya England huko Bondeni
Huenda David Beckham, alieumia na hivyo hatoweza kuichezea England Fainali za Kombe la Dunia, akapewa wadhifa ili awe mmoja wa Maafisa wa Kikosi cha England kitakachokwenda Afrika Kusini kwa Fainali za Kombe la Dunia.
Kabla ya kuumia na kufanyiwa opersheni Nchini Finland Jumatatu iliyopita, David Beckham alitegemewa kuwa mmoja wa Wachezaji wa England na kwa vile hawezi kucheza Kocha wa England Fabio Capello anategemewa kumchukua Beckham kama mmoja wa Viongozi ili kuipa morali Timu hasa kwa vile Wachezaji wengi wanampenda na kumheshimu.
Wakati huohuo, David Beckham ametoa shukrani zake kwa Madaktari wa huko Finland pamoja na Watu wote waliomtakia heri.
EUROPA LIGI: Fulham, Liverpool zaingia Robo Fainali!
• Fulham yaibutua Juve 4-1!
Pengine jana ndio siku kubwa mno katika historia ya Fulham kwani baada ya kupigwa 3-1 katika mechi ya kwanza na Vigogo wa Italia Juventus kila mtu aliwaona wamekufa lakini hapo jana Fulham wakafufuka na kuiwasha Juventus 4-1 Uwanjani Craven Cottage na kutinga Robo Fainali ya EUROPA LIGI.
Fulham waliianza mechi hii vibaya mno pale walipofungwa bao dakika ya pili tu ya mchezo Mfungaji akiwa David Trezeguet lakini wakatulia na Bobby Zamora akasawazisha dakika ya 9.
Jahazi la Juventus likaanza kwenda mrama dakika ya 27 pale Beki wa Italia Fabio Cannavaro alipopewa Kadi Nyekundu baada ya kumchezea rafu Gera aliekuwa akienda langoni.
Gera akaipatia bao Fulham dakika ya 39 na kipindi cha pili akafunga tena kwa penalti na kufanya Fulham iwe mbele kwa bao 3-1 na hivyo kufanya Timu hizo ziwe sare kwa jumla ya bao 3-3 na endapo matokeo yangebaki hivyo basi nusu saa ya nyongeza ingebidi ichezwe.
Lakini Mchezaji alieingia kutoka benchi la akiba Clint Dempsey ndie alieleta furaha Craven Cottage kwa kupachika bao la 4 lililoipeleka Fulham Robo Fainali.
Kwa Juventus siku hiyo ilimalizika vibaya zaidi pale Zebina alipotwangwa Kadi Nyekundu na kuwaacha Juve wamalize mechi wakiwa mtu 9.
Huko Anfield, Liverpool walifuta kipigo cha mechi ya kwanza cha 1-0 mikononi mwa Lille na kuinyuka Timu hiyo bao 3-0 na kutinga Robo Fainali.
Liverpool walifunga bao la kwanza kwa penalti iliyopigwa na Kepteni Steven Gerrard na Supa Straika Fernando Torres akapachika bao 2.
Ushindi huu unawapa matumaini makubwa Liverpool kuwa huenda msimu huu angalau wakaambua Kombe moja kwani wameshatolewa Vikombe vingine vyote na kwenye LigI Kuu wanachopigania sasa ni kumaliza nafasi ya 4.
Matokeo kamili:
Sporting Lisbon 2 v Atletico Madrid 2 [jumla 2-2, Atletico wapita kwa magoli ya ugenini]
Marseille 1 v Benfica 2 [jumla 2-3]
Anderlecht 4 v Hamburg 3 [jumla 5-6]
Fulham 4 v Juventus 1 [jumla 5-4]
Liverpool 3 v Lille 0 [jumla 3-1]
Standard Liege 1 v Panathinaikos 0 [jumla 4-1]
Wolfsburg 2 v Rubin Kazan 1 [jumla 3-2]
Werder Bremen 4 v Valencia 4 [jumla 5-5, Valencia wanasonga kwa mabao ya ugenini]
Timu zilizoingia Robo Fainali:
-Atletico Madrid
-Benfica
-Hamburg
-Fulham
-Liverpool
-Standard Liege
-Wolfsburg
-Valencia
Riera atupwa nje ya Kikosi Liverpool!!
Baada ya kumbatukia Meneja wake Rafa Benitez kuwa ana chuki binafsi, Mchezaji wa Liverpool Albert Riera ameachwa kwenye Kikosi cha Liverpool kilichokuwa kikijitayarisha kucheza na Lille kwenye mechi ya EUROPA LIGI hapo jana.
Riera alitoa tuhuma hizo kwenye Radio Marca ya Spain kwa kudai anapuuzwa na Kocha wake na kutaka uhamisho aende Urusi ili kuweka hai matumaini yake kuichezea Spain Fainali za Kombe la Dunia.
Habari nyingine zimedai kuwa Riera ameambiwa asijihusishe na Timu hiyo hadi Jumatatu na hivyo hatakuwemo Kikosi cha Liverpool kitakachocheza Old Trafford Jumapili na Manchester United kwenye BIGI MECHI ya LIGI KUU.
BIGI MECHI Jumapili: Giggs ataka ushindi na Liverpool!!!
Msimu uliokwisha katika mechi ya marudio ya Ligi Kuu, Liverpool walipata ushindi wa bao 4-1 Uwanjani Old Trafford na kuwatoa nishai Mahasimu wao wakubwa Manchester United lakini hata hivyo walishindwa kunyakua Ubingwa na kuambua nafasi ya pili huku Man United wakiibuka Bingwa.
Safari hii wanakutana tena katika mechi ya marudio Old Trafford siku ya Jumapili lakini Liverpool wanachopigania safari hii ni angalau kuipata japo nafasi ya 4 tu kwa vile wamevurunda vibaya Ligi ya msimu huu.
Kwa Manchester United, waliobakisha mechi 8 kumaliza Ligi huku wakiongoza, ushindi ni muhimu mno ili kutwaa Ubingwa wa England kwa mara ya 3 mfululizo na kuweka historia.
Kiungo Veterani Ryan Giggs, ambae huenda akacheza mechi hii baada ya kuwa nje tangu mwishoni mwa Januari alipovunjika mkono kwenye mechi ya Ligi na Aston Villa, amenena: “Msimu uliokwisha hatukucheza vizuri na wao walistahili kushinda. Lakini hii ni mechi kubwa na muhimu kwetu! Wakati huu tunacheza vizuri na tunafunga magoli! Ushindi ni lazima!”
Giggs ameisaidia Man United kunyakua Ubingwa mara 11 na kuifikia rekodi ya Liverpool ya kuwa Bingwa mara 18 hivyo ushindi juu ya Liverpool ni muhimu kwake na pia kuivunja rekodi na kutwaa Ubingwa mara 19.
Hargreaves acheza mechi yake ya kwanza!!
Mchezaji wa Manchester United Owen Hargreaves ambae hajacheza tangu Septemba 2008 alipocheza mechi na Chelsea huko Stamford Bridge na kisha kusumbuliwa na matatizo ya magoti, Siku ya Alhamisi alicheza mechi yake ya kwanza kwa muda wa dakika 45 kwenye mechi ya Timu za Risevu za Manchester United na Burnley.
Hargreaves alifanyiwa operesheni za magoti yake yote mawili huko Marekani na kurudi kwake uwanjani kumekuwa kunaahirishwa mara kwa mara lakini katika mechi hiyo ya Risevu inadaiwa alicheza vizuri bila matatizo.
Hargreaves alinunuliwa kutoka Bayern Munich kwa Pauni Milioni 17 mwaka 2007 lakini ameichezea Manchester United mechi 37 tu kutokana na matatizo ya magoti.

Thursday 18 March 2010

Droo za UEFA kesho Ijumaa
Droo za Robo Fainali na Nusu Fainali za Mashindano ya UEFA ya CHAMPIONS LIGI na EUROPA LIGI zitafanyika Ijumaa Machi 19 huko Makao Makuu ya UEFA Nyon, Uswisi.
Droo hizo mbili zitahusisha Timu 8 katika kila Mashindano hayo mawili na zitakuwa wazi ikimaanisha upo uwezekano wa Timu toka Nchi moja kupambanishwa na hivyo kwenye CHAMPIONS LIGI upo uwezekano Manchester United akakutana na Arsenal.
Katika CHAMPIONS LIGI, Timu hizo 8 ni:
-Arsenal
-Bayern Munich
-Manchester United
-Lyon
-Barcelona
-Bordeaux
-Inter Milan
-CSKA Moscow
Timu 8 za EUROPA LIGI zitakazoingia kwenye Droo zitajulikana baadae leo usiku baada ya mechi za Ligi hiyo za marudiano kukamilika leo.
Robo Fainali za UEFA CHAMPIONS LIGI zitachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini hapo Machi 30 na 31 na marudiano yake ni Aprili 6 na 7.
Vile vile itafanyika Droo ya Nusu Fainali na hivyo mbali ya kujua Wapinzani wao wa Robo Fainali Timu zitajua nani watakutana nao Nusu Fainali wakipita Robo Fainali.
Nusu Fainali pia zitachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini na mechi za kwanza zitakuwa Aprili 20 na 21 na marudiano ni Aprili 27 na 28.
Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI ni Mei 22 kwenye Uwanja wa Real Madrid Santiago Bernabeu huko Madrid, Spain.
Kwa EUROPA LIGI, Droo yake itakuwa sawa kama CHAMPIONS LIGI na Robo Fainali zitachezwa Aprili 1 na 8 na Nusu Fainali ni Aprili 22 na 29.
Fainali ya EUROPA LIGI ni Mei 12 Uwanja wa Hamburg Arena Mjini Hamburg, Ujerumani.
Mchezaji Liverpool ambatukia Meneja wake!!
Mchezaji wa Liverpool Albert Riera ametoboa kuwa uhusiano wake na Meneja wake Rafa Benitez ambae ni Mhispania mwenzake umezorota kiasi ambacho anahisi Meneja huyo ana chuki binafsi na yeye.
Riera amedai Rafa ni ‘kiziwi’ kwa Wachezaji na ameielezea Timu ya Liverpool kama Meli ‘inayozama’.
Riera ameichezea Liverpool mara mbili toka mwishoni mwa Januari huku akianza mechi moja na nyingine akitokea benchi la akiba.
Riera amesema anafikiria sana kuhama ili ajijengee mazingira mazuri ya kuchukuliwa Kikosi cha Spain cha Kombe la Dunia.
Riera amesema yuko tayari kwenda Urusi kwa vile Soko la Wachezaji huko liko wazi kwa vile msimu wao mpya ndio kwanza umeanza.
Riera amenukuliwa na Radio Marca ya huko Spain akisema: “Kama Kocha hakuambii chochote na wewe uko fiti na unafanya tizi vizuri tu bila shaka utafikiria kuna chuki! Timu inacheza vibaya, mabadiliko yanatakiwa! Kama ninafanya vibaya ni wajibu wa Kocha kuniambia kosa langu ili nijirekebishe! Kinachouma hakwambia kitu na hilo si kwa mimi pekee! Wako Wachezaji wengine pia!”
UEFA CHAMPIONS LIGI: Barca na Bordeaux hao Robo Fainali!!
Jana, Barcelona wakiwa nyumbani Nou Camp, waliichapa VfB Stuttgart bao 4-0 na kutinga Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI kwa jumla ya bao 5-1.
Katika mechi nyingine, Bordeaux walishinda 2-1 dhidi ya Olympiakos na hivyo
kuingia Robo Fainali kwa jumla ya bao 3-1.
Mechi za jana zimekamilisha Timu 8 zitakazocheza Robo Fainali ambazo zitachezwa Machi 30 na 31 kwa mechi za kwanza na marudio ni Aprili 6 na 7.
Droo ya kupanga mechi za Robo Fainali itafanyika kesho.
Timu zilizo Robo Fainali:
-Arsenal
-Bayern Munich
-Manchester United
-Lyon
-Inter Milan
-CSKA Moscow
-Barcelona
-Bordeaux
LEO EUROPA LIGI: Nani kutinga Robo Fainali?
Leo usiku ni mechi za marudio za EUROPA LIGI zitakazoamua Timu 8 zitakazofuzu kuingia Robo Fainali huku wawakilishi wa England, Liverpool na Fulham, wakiwa na kibarua kigumu baada ya kufungwa ugenini mechi zao za kwanza.
Liverpool wako Anfield kurudiana na Lille ya Ufaransa baada ya kupigwa 1-0.
Fulham wako kwao Craven Cottage kucheza na Vigogo wa Italia Juventus ambao walishinda 3-1.
EUROPA LIGI: Matokeo mechi za kwanza
Atletico Madrid 0 v Sporting Lisbon 0
Benfica 1 v Marseille 1
Hamburg 3 v Anderlecht 1
Juventus 3 v Fulham 1
Lille 1 v Liverpool 0
Panathinaikos 1 v Standard Liege 3
Rubin Kazan 1 v Wolfsburg 1
Valencia 1 v Werder Bremen 1
RATIBA:
Sporting Lisbon v Atletico Madrid
Marseille v Benfica
Anderlecht v Hamburg
Fulham v Juventus
Liverpool v Lille
Standard Liege v Panathinaikos
Wolfsburg v Rubin Kazan
Werder Bremen v Valencia

Wednesday 17 March 2010

Pompey wakatwa pointi 9!!!
Kushuka Daraja ni uhakika!!!
Klabu iliyo kwenye matatizo makubwa kifedha na ambayo pia ipo mkiani mwa Ligi Kuu, Portsmouth, leo imekatwa pointi 9 na Ligi Kuu kwa kukiuka taratibu za Ligi Kuu baada ya kukabidhiwa kwa Msimamizi maalum ili kuinusuru isifilisiwe.
Hatua hiyo ya Ligi Kuu inafuatia Mahakama Kuu kuamua hapo jana kuwa Msimamizi huyo ni halali na hivyo Klabu hiyo isifilisiwe na Mamlaka ya Kodi waliotaka amri ya kufilisiwa itolewa kwa Klabu hiyo baada ya kushindwa kulipa kodi.
Wasimamizi wa Ligi Kuu wamethibitisha hatua ya Portsmouth kukatwa pointi 9 na hivyo kubakishwa na pointi 10 tu na sasa wako nyuma ya Timu za 18 na 19 kwenye msimamo Hull City na Burnley kwa pointi 14.
Hatua hiyo ya Ligi Kuu, bila shaka, itaiporomosha Daraja Portsmouth kwani wamebakiza mechi 9 tu.
Hull City yamteua Dowie Meneja mpya!!
Meneja wa zamani wa Crystal Palace, Ian Dowie, ametajwa kuwa ndie Meneja mpya wa Hull City kuchukua nafasi ya Phil Brown aliefukuzwa majuzi.
Dowie ameletwa hapo mahsusi ili kuinusuru Hull City isiporomoke Daraja kutoka Ligi Kuu.
Hull ipo nafasi moja toka mkiani ikiwa na pointi 24 na imebakisha mechi 9.
Msimu uliokwisha Hull ilinusurika kushushwa kwenye mechi ya mwisho ya Ligi.
Terry amgonga na gari Mlinzi wao Stamford Bridge!!
Kuna ripoti kuwa Nahodha wa Chelsea John Terry amemvunja mguu Mlinzi wa Chelsea wa Uwanjani Stamford Bridge kwa gari lake mara baada ya mechi ya jana usiku ambayo Chelsea walifungwa 1-0 na Inter Milan na kutupwa nje ya UEFA CHAMPIONS LIGI.
Inasemekana wakati Terry akiondoka Uwanjani hapo gari lake likiwa kwenye msongamano wa magari na mwendo wa polepole huku likizongwa na Washabiki na Waandishi wa Habari Mlinzi huyo alianguka na ndipo akavunjwa mguu na gari la Terry.
Inadaiwa Terry ametoa pole kwa Mlinzi huyo na Polisi wanachunguza tukio hilo.
UEFA CHAMPIONS LIGI:
Leo Barca v Stuttgart na Bordeaux v Olympiakos!
• Droo ya Robo Fainali Ijumaa!!
• Chelsea nje, Drogba Nyekundu, Mourinho kidedea!!!
Leo usiku kuna mechi mbili zitakazotoa Timu 2 za mwisho kuungana na Arsenal, Manchester United, Lyon, Bayern Munich, Inter Milan na CSKA Moscow kwenye Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Barcelona ambao walitoka sare 1-1 na VfB Stuttgart katika mechi ya kwanza leo wako nyumbani Nou Camp na wanahitaji sare ya 0-0 au ushindi wowote ili watinge Robo Fainali.
Kwa Stuttgart, sare ya zaidi ya goli mbili ni ushindi kwao kwa sheria ya magoli ya ugenini.
Nao, Bordeaux, baada ya kushinda ugenini bao 1-0, leo wako nyumbani na wanahitaji sare tu ili Olympiakos na kusonga mbele.
Droo ya kupanga mechi za Robo Fainali itafanyika Ijumaa Machi 19.
Katika mechi za jana, Sevilla ilitunguliwa 2-1 wakiwa kwao na CSKA Moscow na hivyo CSKA kusonga mbele.
Mechi ya kwanza kwa Timu hizo ilikuwa ni sare ya 1-1.
Nako huko Stamford Bridge, Jose Mourinho alipokewa vizuri na Mashabiki wa Timu yake ya zamani Chelsea lakini bila shaka mwishoni walimlaani kwani Inter Milan waliifunga tena Chelsea na kuwabwaga nje ya UEFA CHAMPIONS LIGI.
Inter Milan ilishinda bao 1-0 kwa bao la Samuel Eto’o la dakika ya 79.
Na Nyota wa Chelsea Didier Drogba aliwashwa Kadi Nyekundu kwa mchezo mbaya na huenda UEFA ikamchukulia hatua kali zaidi kwani Drogba bado yuko kwenye uangalizi baada ya kutolewa kwenye mechi ya UEFA CHAMPIONS LIGI msimu uliokwisha kwa Kadi Nyekundu baada ya kumvaa Refa kwenye mechi ya Nusu Fainali na Barcelona na kufungiwa mechi 4 lakini akatumia kifungo cha mechi 2 na mbili kuwekwa kiporo kuchunga tabia yake.
Man United yakerwa na kutoadhibiwa Gerrard
Kwa mara ya pili ndani ya wiki moja Nahodha wa Liverpool Steven Gerrard ameyakwepa marungu ya FA baada ya Marefa kumwokoa kwa kudai waliviona vitendo vyake kwenye mechi na hivyo hastahili kuadhibiwa tena.
Wiki iliyopita, kwenye mechi Liverpool aliyopigwa 1-0 na Wigan, Refa Andre Marriner alionekana kutukanwa na Gerrard na pia kuonyeshwa alama ya vidole ya V lakini Refa huyo alisema aliona vituko hivyo na kuvipuuza.
Juzi, kwenye ushindi wa Liverpool wa 4-1 dhidi ya Portsmouth, kamera zilimnasa Gerrard akimpiga kipepsi Mchezaji wa Portsmouth Michael Brown lakini Refa wa mechi hiyo Stuart Attwell amedai vitendo vya Gerrard havikustahili Kadi na hivyo FA haiwezi kuchukua hatua yeyote.
Jumapili Manchester United wanaikaribisha Liverpool Old Trafford kwenye mechi ya Ligi Kuu na endapo Gerrard angeshitakiwa na FA basi angeikosa mechi hiyo na Mahasimu wao wakubwa.
Manchester United haijazungumza kitu lakini taarifa zinadai wamekasirishwa na hatua ya FA ya kumtazama tu Gerrard mara mbili mfululizo wakati Mchezaji wao Rio Ferdinand alifungiwa mechi 3 na kuongezwa mechi moja zaidi alipokata rufaa kwa makosa kama ya Gerrard.
Hilo limewadhihirishia Manchester United kuwa wao hawatendewi haki na Marefa pamoja na FA.
Hii ni mara ya pili kwa Wachezaji wa Liverpool kutoadhibiwa kwa makosa ya wazi wakati Javier Mascherano alipoachiwa tu baada ya kuonekana wazi akimpiga Straika wa Leeds Jermaine Beckford mwezi Septemba mwaka jana kwenye mechi ya FA.

Tuesday 16 March 2010

Beckham afanyiwa upasuaji, pengine nje Miezi 6!!
Profesa Sakari Orava, Daktari aliemfanyia operesheni Nyota David Beckham huko Finland kuiunga musuli toka kisiginoni hadi nyuma ya ugoko mguuni, amesema upasuaji huo ulikwenda vizuri na pengine hatacheza mpira kwa muda wa miezi 6.
Beckham aliumia Jumapili akiichezea AC Milan iliyoifunga Chievo.
Hili ni pigo binafsi kwa Beckham kwani nia yake ilikuwa awe Mchezaji wa kwanza toka England aliecheza Fainali za Kombe la Dunia mara 4.
Mpaka sasa Beckham, ambae anashikilia rekodi ya Mchezaji wa mbele aliechezea England mara nyingi akiwa amewakilisha mara 115, amefungana na Mastaa wa zamani Bobby Moore na Kipa Peter Shilton kwa kucheza Fainali 3 za Kombe la Dunia.
Liverpool yaibomoa Kibonde Portsmouth!!!
• Pengine Gerrard kutwangwa rungu na FA!!!
Jana, katika mechi pekee ya Ligi Kuu iliyochezwa Uwanja wa Anfield, Liverpool iliwafumua Portsmouth bao 4-1 na kuendelea kuwadidimiza mkiani.
Mabao matatu ya Kipindi cha kwanza yaliyofungwa na Torres, Babel na Aquilani na la 4 la Torres tena ndio yaliwapa ushindi Liverpool.
Bao la Portsmouth lilifungwa na Nadir Belhadj.
Hata hivyo huenda Liverpool wakakumbwa na balaa la kupewa adhabu Nahodha wao Steven Gerrard baada ya kamera kumnasa akimpiga kipepsi Mchezaji Michael Brown wa Portsmouth kwenye dakika ya 73.
Refa Stuart Attwell alitoa faulo kwa kosa hilo lakini huenda akaombwa na FA kuliangalia tena tukio hilo kwenye video na atoe maoni yake.
Wiki iliyopita, Gerrard alinusurika rungu la FA baada ya pia kunaswa kwenye kamera akimtukana Refa Andre Marriner na kuonyesha alama ya V kwa vidole lakini Refa huyo alisema aliliona na kuamua ni kosa dogo na ndio maana hakumchukulia hatua yeyote.
LEO LIGI KUU: Wigan v Aston Villa
Katika mechi pekee ya Ligi Kuu leo usiku saa 4 dakika 45 saa za bongo, Wigan wataikaribisha Aston Villa uwanja wa DW.
Aston Villa wako nafasi ya 7 na wana pointi 46.
Wigan wao wako nafasi ya 15 wakiwa na pointi 28.
Fergie atabiri mwisho mgumu Ligi Kuu
Bosi wa Manchester United Sir Alex Ferguson ametabiri kuwa msimu huu Ligi Kuu England ndio ngumu kuitabiri katika historia ya Ligi hiyo.
Ingawa amekiri Bingwa atatoka kati ya Timu yake, Chelsea au Arsenal, Ferguson amesema: “Ni ngumu kujua nani Bingwa! Tuna mechi 8 zimebaki. Chelsea ana 9. Wote tuna mashindano Ulaya na Chelsea pia yupo kwenye Kombe la FA.”
Ni mara tatu tu Ubingwa wa Ligi Kuu umeamuliwa kwa tofauti ya pointi moja tu na mara ya kwanza ilikuwa pale msimu wa 1994/94 Blackburn Rovers ilipoipiku Man United, ya pili ilikuwa mwaka 1997/98 Arsenal alipoitoa Man United na mwaka 1998/9 Man United wakalipa kisasi kwa Arsenal.
=======================================================================
MSIMAMO LIGI KUU England:
1. Man United mechi 30 pointi 66
2. Chelsea mechi 29 pointi 64
3. Arsenal mechi 30 pointi 64
4. Tottenham mechi 29 pointi 52
------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
5. Liverpool mechi 30 pointi 51
6. Man City mechi 28 mechi 50
7. Aston Villa mechi 27 pointi 46
8. Birmingham mechi 29 pointi 44
9. Everton mechi 29 pointi 42
10. Fulham mechi 29 pointi mechi 38
11. Stoke mechi 29 pointi 36
12. Blackburn mechi 29 pointi 34
13. Bolton mechi 30 pointi 32
14. Sunderland mechi 29 pointi 31
15. Wigan mechi 29 pointi 28
16. West Ham mechi 29 pointi 27
17. Wolves mechi 29 pointi 27
-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
18. Burnley mechi 30 pointi 24
19. Hull mechi 29 pointi 24
20. Portsmouth mechi 29 pointi 19
======================================================================
Manchester United, wanaoongoza kwa pointi 2 juu ya Chelsea ambao wana mechi moja mkononi, wana mechi mbili ngumu zinazofuata ingawa zote ni za nyumbani Old Trafford watakapozivaa Liverpool na kisha Chelsea lakini Ferguson amesema: “Ni lazima ufikirie tofauti ya magoli. Sisi tupo mbele kwa goli 4 kwa Chelsea ingawa ningependa ingekuwa 14! Kitu rahisi kufikiria ni kuwa sisi na Chelsea tucheze na kushinda mechi zetu zote lakini maisha si rahisi kiasi hicho!”

Monday 15 March 2010

UEFA CHAMPIONS LIGI: Jumanne na Jumatano kimbembe cha kuingia Robo Fainali!!
RATIBA [Mechi za marudiano]
Jumanne, 16 Machi 2010
Chelsea v Inter Milan
Sevilla v CSKA Moscow
Jumatano, 17 Machi 2010
Barcelona v VfB Stuttgart
Bordeaux v Olympiakos
MATOKEO MECHI ZA KWANZA:
Olympiakos 0 v Bordeaux 1
VfB Stuttgart 1 v Barcelona 1
CSKA Moscow 1 v Sevilla 1
Inter Milan 2 v Chelsea 1
Timu tayari ziko Robo Fainali:
-Arsenal
-Bayern Munich
-Manchester United
-Lyon
TATHMINI:
Siku ya Jumanne Machi 16, Chelsea inahitaji kumfunga Inter Milan japo bao 1-0 ili itinge Robo Fainali kwa vile Chelsea alipigwa 2-1 na Inter Milan katika mechi ya kwanza.
Katika mechi nyingine ya siku ya Jumanne ni marudiano ya Sevilla na CSKA Moscow na suluhu ya 0-0 ni tosha kwa Sevilla kufuzu Robo Fainali.
Lakini, kwa vile vile Timu hizo zilitoka 1-1 kwenye mechi ya kwanza, sare ya zaidi ya mabao 1-1 ni nzuri kwa CSKA kwani watapita kwa wingi wa mabao ya ugenini.
Jumatano ni marudio kati ya Barcelona v VfB Stuttgart na Bordeaux v Olympiakos.
Katika mechi ya Barcelona v VfB Stuttgart, hali ni kama ya mechi ya Sevilla na CSKA Moscow kwani Barcelona anahitaji sare ya 0-0 apite lakini sare ya magoli zaidi ya 1-1 ni nzuri kwa VfB Stuttgart.
Bordeaux wao wanahitaji sare ya aina yoyote ili waibwage Olympiakos kwa vile walishinda 1-0 ugenini.
Ili Olympiakos apite ni lazima aifunge Bordeaux bao 2 au apate ushindi wowote wa bao zaidi ya 2.
Hull City yamtimua Phil Brown
Timu iliyo ya pili toka mkiani Hull City leo imemwondoa kazini aliekuwa Meneja wao Phil Brown na kutangaza kuwa Wasaidizi wake Brian Horton na Steve Parkin ndio watakaoiongoza Timu hiyo.
Brown alianza kazi Hull City mwaka 2007 na ndani ya msimu mmoja tu akaipandisha Daraja na kuingia Ligi Kuu mwaka 2008 na kuiwezesha kubaki hapo msimu uliopita japo ilibidi isubiri hadi mechi ya mwisho ya Ligi kujihakikishia wanabaki Ligi Kuu.
Msimu huu mambo yameenda vibaya na wakiwa wamebakisha mechi 9 kumalizi Ligi Menejimenti ya Hull imeamua kubadilisha mwelekeo ili kujinusuru.
LEO LIGI KUU: Liverpool v Portsmouth
Ndani ya Anfield, Liverpool leo wanaivaa Timu ya mkiani Portsmouth kwenye mechi ya pekee ya Ligi Kuu.
Kimsimamo, Liverpool wapo nafasi ya 6 wakiwa wamecheza mechi 29 na wana pointi 48 na juu yao wapo Manchester City walio na pointi 50 kwa mechi 28.
Nafasi ya 4 inashikiliwa na Tottenham wenye pointi 52 kwa mechi 29.
BECKHAM: Bai Bai Kombe la Dunia!! Kuwa nje Miezi 4!!
Daktari ambae atamfanyia upasuaji David Beckham amethibitisha kuwa Nyota huyo atakuwa nje ya uwanja hadi miezi minne baada ya kuumia musuli ya mguu inayounganisha kisigino cha mguu na nyuma ya ugoko katika mechi ya Klabu yake ya mkopo AC Milan na Chievo siku ya Jumapili.
Beckham alitegemewa kuwemo kwenye Kikosi cha Timu ya England kitakachocheza Fainali za Kombe la Dunia linaloanza Juni 11 lakini Dokta Sakari Orava ambae ndie atafanya upasuaji ili kumuunga musuli hiyo iliyokatika alisema itachukua miezi mitatu ili aweze kupona na kuanza tena mazoezi na muda wa mwezi mmoja zaidi unatakiwa ili kumweka fiti tena.
Hali hiyo inamaanisha Beckham hawezi kupona kwa wakati ili kucheza Fainali za Kombe la Dunia.
Mourinho: “Mourinho hafungwi Stamford Bridge!!!”
Ballack: “Mourinho ni historia! Tuna njaa ya Ubingwa Ulaya!”
Jose Mourinho ana matumaini makubwa ya kurudi tena Uwanja wa Stamford Bridge kwa furaha na amedai Mourinho hafungiki Stamford Bridge.
Mourinho alikuwa Kocha wa Chelsea kuanzia 2004 hadi 2007 na alitwaa Vikombe kadhaa na pia kuifanya Stamford Bridge iwe ngome isiyofungika ya Chelsea.
Mourinho atakuwa na Timu yake ya sasa Inter Milan itakayokwaana na Chelsea kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI hapo Jumanne hii ikiwa ni mechi ya marudio.
Inter Milan iliibwaga Chelsea 2-1 katika mechi ya kwanza.
Jose Mourinho alijigamba: “Kila mtu anajua Mourinho hafungiki Stamford Bridge! Rekodi yangu hapo nlipokuwa na Chelsea kila mtu anaijua!”
Hata hivyo Kiungo wa Chelsea, Mjerumani Michael Ballack, amempinga kwa kudai Mouronhi sasa ni historia tu na wao wana njaa kubwa ya kutwaa Ubingwa wa Ulaya.
LIGI KUU England: MATOKEO
Jumamosi, Machi 13
Tottenham 3 v Blackburn 1
Birmingham 2 v Everton 2
Bolton 4 v Wigan 0
Burnley 1 v Wolves 2
Chelsea 4 v West Ham 1
Stoke 0 v Aston Villa 0
Hull 1 v Arsenal 2
Jumapili, Machi 14
Man United 3 v Fulham 0
Sunderland 1 v Man City 1
Powered By Blogger