Saturday 6 March 2010

FA CUP: Taabani Pompey watinga Nusu Fainali!!
Portsmouth, Klabu inayochungulia kushuka Daraja kutoka Ligi Kuu huku ikiwa na matatizo kibao ya fedha na ipo hatarini kufilisiwa, leo imetinga Nusu Fainali ya Kombe la FA pale ilipoichapa Birmingham bao 2-0 Uwanjani Fratton Park.
Piquionne ndie shujaa wa Portsmouth alipofunga bao mbili dakika ya 67 na 77 na kupieleka Portsmouth Wembley kucheza Nusu Fainali ya FA Cup.
Mechi nyingine ya Robo Fainali ya Kombe la FA ni baadae leo kati ya Fulham na Tottenham.
Maandalizi ya England Kombe la Dunia
England wamepanga kucheza mechi 2 za majaribio kabla ya kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia.
Mechi hizo za majaribio ni dhidi ya Mexico na Japan na zitachezwa mwezi Mei kabla Capello hajateua Kikosi chake cha Wachezaji 23 cha Kombe la Dunia hapo Juni 1.
Capello anategemewa kukitaja Kikosi cha awali hapo Mei 17 kitakachokuwa na Wachezaji 30 na siku hiyo ni siku moja tu baada ya Fainali ya Kombe la FA.
Kambi ya awali ya England inategemewa kuwa Nchini Austria na itafanya mazoezi yake kwa siri.
England inacheza mechi yake ya kwanza kwenye Kundi lake la Fainali za Kombe la Dunia hapo Juni 12 watakapocheza na USA kisha Juni 18 wanacheza na Algeria.
Mechi yao ya mwisho kwenye Makundi ni ile ya Juni 23 na Slovenia.
MAN UNITED HAINUNULIKI!!!
Mkurugenzi Mkuu wa Manchester United, David Gill, amesema uongozi wa Klabu hiyo unaheshimu msimamo wa ‘Wakombozi Wekundu’ [Red Knights] wanaotaka kuinunua Man United kutoka kwa Wamiliki wake wa sasa Familia ya Glazer lakini Gill amesema Klabu hiyo haiuzwi.
Mbali ya ‘Wakombozi Wekundu’ ambao ni Kikundi cha Watu Matajiri Mashabiki wa Manchester United, kuna Kikundi kingine cha Masapota kinachoitwa MUST [Manchester United Supporters Trust] ambacho pia kinataka Familia ya Glazer ing’oke Manchester United.
Vikundi hivyo viwili, Red Knights na MUST, vimesema vitakusanya nguvu zao kwa pamoja ili kushinda vita yao.
Inasadikiwa kuwa MUST sasa imefikisha idadi ya Watu 100,000 kwenye safu yao.
Lakini, kuna Wataalam wa ishu za ununuzi wa Makampuni ambao wametoa sababu 5 zitakazofanya Red Knights na MUST kushindwa kuwatoa kina Glazer.
Nazo ni:
BEI: Manchester United ina deni la zaidi ya Pauni Milioni 700.
Familia ya Glazer waliinunua Man United kwa dau la Pauni Milioni 272 na lazima watataka kupata faida ya pesa zao. Hivyo inakisiwa dau la ununuzi litakuwa Pauni Bilioni 1 na nusu na bei hiyo huenda ikawafanya kina Glazer kukubali kukaa mezani na kuzungumzia biashara hiyo.
MFUMO: Red Knights wanataka kuwakusanya Wawekezaji 40 kila mmoja akitoa Mamilioni ili kuinunua Manchester United.
Kwa sababu ni kundi kubwa huenda kukatokea misuguano na kufanya azma yao isifanikiwe.
MENEJIMENTI: Hata kama Red Knights watafanikiwa kuinunua Manchester United kuiendesha Klabu hii kubwa kutakuwa tatizo kubwa hasa ukizingatia Wawekezaji wake ni wengi. Kina Glazer wana Menejimenti nzuri mno huku masuala yote ya mechi na Wachezaji yakiwa chini ya Sir Alex Ferguson na mafanikio yake ni makubwa mno.
Kwa upande wa masuala ya biashara, Klabu hiyo inaendeshwa wakiwa na Ofisi mbili moja Mjini London na moja ikiwa Manchester na Ofisi hizo zimekuwa zikizalisha pesa kwa faida.
GLAZER: Familia ya Glazer imesema Manchester United haiuzwi na hawana presha yoyote ya kuuza.
Pia walipouza Hati za Dhamana hivi karibuni zimesaidia sana kukusanya mtaji wa kulipia deni na kumewafanya kina Glazer waidhibiti vizuri Klabu hiyo.
UTANGULIZI: Haijawahi kutokea kwa Masapota wa Klabu kuichukua Klabu ya Ligi Kuu ingawa kwenye Ligi za chini imeshatokea pale Kabu za Exeter City, Notts County na York City ziliponunuliwa na Mashabiki.
Mashabiki wa Liverpool mwaka jana waliunda Kikundi kinachoitwa Share Liverpool ili kuiteka Klabu hiyo kutoka kwa Wamiliki wake Wamarekani wawili lakini walishindwa kuitwaa.
Piga hesabu, piga ramli, amua Bingwa Nani!!!!!
Kwa wengi, Ubingwa ni wa ama Chelsea, Manchester United au Arsenal na Timu hizi 3 zimeshacheza mechi 28 na kubakiza mechi 10 kila mmoja.
Msimamo kwa Timu za juu ni kama ifuatavyo:
1. Chelsea mechi 28 pointi 61
2. Man United mechi 28 pointi 60
3. Arsenal mechi 28 pointi 58
4. Tottenham mechi 28 pointi 49
5. Man City mechi 27 pointi 49
6. Liverpool mechi 28 pointi 48
7. Aston Villa mechi 26 pointi 45
Zifuatazo ni mechi zilizobaki kwa Timu hizo 3 vigogo:
ARSENAL
Machi 6=Arsenal v Burnley
Machi 13=Hull City v Arsenal
Machi 20=Arsenal v West Ham
Machi 27=Birmingham v Arsenal
Aprili 3=Arsenal v Wolves
Aprili 10=Tottenham v Arsenal
Aprili 18=Wigan v Arsenal
Aprili 24=Arsenal v Man City
Mei 1=Blackburn v Arsenal
Mei 9=Arsenal v Fulham
CHELSEA
Machi 13=Chelsea v West Ham
Machi 21=Blackburn v Chelsea
Machi 24=Portsmouth v Chelsea
Machi 27=Chelsea v Aston Villa
Aprili 3=Man United v Chelsea
Aprili 12=Chelsea v Bolton
Aprili 17=Tottenham v Chelsea
Aprili 25=Chelsea v Stoke
Mei 1=Liverpool v Chelsea
Mei 9=Chelsea v Wigan
MAN UNITED
Machi 6=Wolves v Man United
Machi 14=Man United v Fulham
Machi 21=Man United v Liverpool
Machi 27=Bolton v Man United
Aprili 3=Man United v Chelsea
Aprili 11=Blackburn v Man United
Aprili 17=Man City v Man United
Aprili 25=Man United v Tottenham
Mei 1=Sunderland v Man United
Mei 9=Man United v Stoke
MECHI ZIJAZO:
Jumamosi, Machi 6
LIGI KUU
[saa 12 jioni]
Arsenal v Burnley
West Ham v Bolton
[saa 2 na nusu usiku]
Wolves v Man United
FA CUP
[saa 9 na nusu mchana]
Portsmouth v Birmingham
[saa 2 dak 20 usiku]
Fulham v Tottenham
Jumapili, Machi 7
LIGI KUU
[saa 1 usiku]
Everton v Hull City
FA CUP
[saa 10 dak 45 jioni]
Reading v Aston Villa
[saa 1 usiku]
Chelsea v Stoke
Jumatatu, Machi 8
[saa 5 usiku]
Wigan v Liverpool
Jumanne, Machi 9
UEFA CHAMPIONS LIGI
[saa 4 dak 45 usiku]
Arsenal v FC Porto
Fiorentina v Bayern Munich
[saa 4 dak 45 usiku]
Portsmouth v Birmingham
Sunderland v Bolton
Jumatano, Machi 10
UEFA CHAMPIONS LIGI
Manchester United v AC Milan
Real Madrid v Lyon
LIGI KUU
Burnley v Stoke
Alhamisi, Machi 11
EUROPA LIGI: RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 16
Juventus v Fulham
Atletico Madrid v Sporting Lisbon
Valencia v Werder Bremen
Hamburg v Anderlecht
Benfica v Marseille
Lille v Liverpool
Panathinaikos v Standard Liege
Rubin Kazan v Wolfsburg
Jumamosi, Machi 13
LIGI KUU
[saa 9 dak 45 mchana]
Tottenham v Blackburn
[saa 12 jioni]
Birmingham v Everton
Bolton v wigan
Burnley v Wolves
Chelsea v West Ham
Stoke v Aston Villa
[saa 2 na nusu usiku]
Hull v Arsenal
Jumapili, Machi 14
LIGI KUU
[saa 10 na nusu jioni]
Man United v Fulham
[saa 1 usiku]
Sunderland v Man City
Jumatatu, Machi 15
LIGI KUU
[saa 5 usiku]
Liverpool v Portsmouth
Jumanne, Machi 16
LIGI KUU
[saa 4 dak 45 usiku]
Wigan v Aston Villa
Wenger ajibiwa: “Wachezaji wako hawawindwi kuumizwa!”
Bosi wa Bolton Wanderers Owen Coyle amezijibu tuhuma za Meneja wa Arsenal Arsene Wenger kuwa Wachezaji wake wanawindwa makusudi waumizwe kwa kuzipuuza tuhuma hizo na kuzikataa kabisa.
Wikiendi iliyokwisha, Chipukizi wa Arsenal Aaron Ramsey alivunjwa mguu na Mchezaji wa Stoke City Ryan Shawacross katika mechi ya Ligi Kuu na Wenger alikasirishwa sana hasa akizingatia Wachezaji wake wengine Abou Diaby na Eduardo waliumizwa vibaya kwa rafu mbaya sana.
Lakini Owen Coyle amesema hakuna Timu au Mchezaji anaedhamiria kumuumiza mwenzake.
Coyle amesema: “Wachezaji na washindani na hawapendi kushindwa. Hivyo hucheza kwa nguvu zote. Hatuwaambii Wachezaji wetu nenda kamvunje mtu mguu! Shawcross aliupoteza mpira na akajikita kuuchukua tena na nadhani hata hakujua kama Ramsey yupo karibu! Lilikuwa tukio baya lakini si sawa kuanza kudai watu wanafanya kusudi!”
Tevez adai hakukwaruzana na Terry kwa ajili ya Bridge!!
Katika pambano la Ligi Kuu wikiendi iliyokwisha ambalo Manchester City iliichakaza Chelsea kwao Stamford Bridge kwa bao 4-2, kipindi cha pili kulitokea tukio la Carlos Tevez wa Man City na John Terry, Nahodha wa Chelsea, kukwaruzana vikali.
Tevez amejitokeza na kuweka mambo sawa kuwa ugomvi wake na Terry haukuhusu bifu la Terry na mwenzake wa Man City Wayne Bridge linalohusu kashfa iliyomwandamwa Terry kuwa ametembea na gelfrendi wa Bridge.
Kabla ya mechi hiyo kuanza watu wengi walikuwa na shauku kuona kama Terry na Bridge watapeana mikono lakini Bridge hakutoa mkono kwa Terry.
Tevez amesema: “Sikugombana na Terry kwa sababu ya Bridge! Tulikwaruzana kwa sababu alinivuta jezi na sikupenda hilo! Ni ngumu kuzungumzia kitendo cha Terry kwa Bridge! Huwezi kufanya yale na ingekuwa hilo limetokea ninakotoka mimi basi huna miguu au utauawa! “
Tevez pia akatoboa pia kuwa siku zote wakicheza na Michael Ballack huwa anapata matatizo nae na akasema anadhani Ballack hampendi yeye.
Tevez amesema: “Kiwanjani, sielewi nini anasema kwangu na nina hakika hanielewi pia!”

Thursday 4 March 2010

England 3 Misri 1
Mabingwa wa Afrika, Misri, waliianza mechi hii ya kirafiki Uwanjani Wembley, kwa kuwashtukiza England na kupachika bao dakika ya 23 mfungaji akiwa Zidan, bao ambalo lilidumu hadi mapumziko.
Kipindi cha pili England walizinduka na kufunga bao 3, wafungaji wakiwa Peter Crouch, mabao mawili dakika ya 56 na 80, na Shaun Wright-Phillips, dakika ya 75.
Katika mechi hii kikundi kidogo cha Mashabiki kilikuwa kikimzomea Nahodha wa zamani wa England, John Tery, alievuliwa cheo hicho kwa kashfa, lakini baadae walikuwa wakimshangilia.
Kwa England, kufuatia kuumia kwa Ashley Cole na kugoma kucheza kwa Wayne Bridge, Beki ya kushoto ilizibwa na Leighton Baines wa Everton ambae alicheza vizuri na huenda akaikwaa namba hiyo kwa kudumu.
Kwa ujumla, Mabingwa wa Afrika, Misri, walicheza vizuri na hawakustahili kufungwa bao la 3 la Crouch kwani mfungaji alikuwa ofsaidi.
VIKOSI:
England: Green, Brown, Terry, Upson, Baines, Walcott (Wright-Phillips 57), Lampard (Carrick 46), Barry, Gerrard (Milner 73), Rooney (Cole 86), Defoe (Crouch 46).
Akiba hawakucheza: James, Warnock, Lescott, Shawcross, Beckham, Heskey, Downing, Hart.
Egypt: El Hadari, Al-Muhammadi, Said (Salem 86), Fathi, Gomaa, Ghaly, Moawad (Abdelshafy 76), Hassan (Nagy 64), Abd Rabou, Zidan (Aboutreika 76), Ebdelmaby (Zaki 64).
Akiba hawakucheza: El Sayed, Fathallah, Tawfik, El Saka, Raouf, Eid, Hamdy.
MATOKEO: Mechi za Kirafiki za Kimataifa
Jumanne, Machi 2
Ireland 0 v Brazil 2
Jumatano, Machi 3
Albania 1 v Northern Ireland 0
Algeria 0 v Serbia 3
Angola 1 v Latvia 1
Austria 2 v Denmark 1
Belgium 0 v Croatia 1
England 3 v Egypt 1
France 0 v Spain 2
Germany 0 v Argentina 1
Greece 0 v Senegal 2
Hungary 1 v Russia 1
Italy 0 v Cameroun 0
Ivory Coast 0 v South Korea 2
Nerthelands 2 v USA 1
Portugal 2 v China 0
Poland 2 v Bulgaria 0
Scotland 1 v Czech Republic 0
Slovakia 0 v Norway 1
Slovenia 4 v Qatar 1
South Africa 1 v Namibia 1
Switzerland 1 v Uruguay 3
Turkey 2 v Honduras 0
Wales 0 v Sweden 1

Wednesday 3 March 2010

Leo England v Misri, Wembley Stadium
England leo saa 5 usiku saa za bongo itakwaana na Mabingwa wa Afrika kwa mara 3 mfululizo, Misri, Uwanjani Wembley, Jijini London.
Ingawa pambano hili ni mechi ya kirafiki lakini kwa England limekuwa likitangazwa kwa sababu zisizohusu mechi hii kutokana na skandali la aliekuwa Nahodha wa England, John Terry, ambae amekumbwa na kashafa ya kutembea na gelfrendi wa Mchezaji mwenzake Wayne Bridge.
Kashfa hiyo ikasababisha John Terry kutemwa Unahodha wa England na Wayne Bridge kugoma kuichezea England ili asikutane na Terry kwenye Kikosi hicho.
Misri imechaguliwa kuipa mazoezi England hasa kwa vile kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini, England iko Kundi moja na Algeria, Timu ambayo iliibwaga Misri nje ya Fainali za Kombe la Dunia.
Kocha wa Misri, Hassan Shehata, amesema ingawa England ina Wachezaji wazuri sana wao hawaihofii na England isiwadharau wao.
Vikosi vinategemewa kuwa:
England: Hart, Brown, Terry, Upson, Baines, Lampard, Barry, Walcott, Gerrard, Rooney, Heskey.
Egypt: El Hadary, Fathi, Gomaa, Said, Nagy, Abd Rabo, Hassan, Ghaly, Moawad, Zidan, Moteab.
Rio aliona yeye ni Kepteni England kwenye TV!!
Rio Ferdinand amekiri kuwa hakuambiwa yeye ndie Kepteni mpya wa England na badala yake aliona tu taarifa kwenye TV.
Mwezi uliokwisha, aliekuwa Nahodha wa England, John Terry, alipokonywa Ukepteni baada ya kuibuka skandali kuwa ametembea na gelfrendi wa Mchezaji mwenzake Wayne Bridge.
Rio Ferdinand ndie alikuwa Makamu Kepteni wa England na Kocha wa England, Fabio Capello, alimthibitisha Rio ndie Kepteni mpya baada ya Terry kuvuliwa madaraka hayo.
Hata hivyo, Rio amesema hajaongea lolote na Capello na Kocha huyo hajaieleza chochote Timu ya England.
Pia Rio Ferdinand amemsifia Capello na kumfananisha na sir Alex Ferguson, Meneja wa Klabu yake, Manchester United, kwa umahiri, umakini wa kazi yake na kuwa mkweli.
Bongo 2 Uganda 3
Katika mechi ya kirafiki kati ya Taifa Stars, Timu ya Taifa ya Tanzania, na Uganda iliyochezwa leo jioni, Tanzania imebwagwa kwa bao 3-2.
Ireland 0 Brazil 2
Bao la kujifunga wenyewe Ireland kwenye dakika ya 44 baada ya krosi ya Robinho kumgonga Kevin Doyle na kuingia na lile la Robinho la dakika ya 76, liliwapa ushindi Brazil wa 2-0 juu ya Ireland ndani ya Uwanja wa Emirates Jijini London hapo jana Jumanne usiku katika mechi ya kirafiki.
Brazil walitawala na kucheza vizuri sana Kipindi cha Pili na bao lao la pili la Robinho lilifungwa baada ya pasi zao 22 na Getafe kumpasia kwa kisigino Robinho alieupindisha mpira wavuni.
Bila shaka, uchezaji wa Timu ya Brazil utamfurahisha sana Kocha wao Dunga kwani walicheza kwa kiwango cha kuridhisha na hayo ni mazoezi tosha kwa Fainali za Kombe la Dunia.
Brazil wataanza kucheza Fainali Kombe la Dunia huko Afrika Kusini hapo Juni 15 kwa mechi dhidi ya Korea Kaskazini huko johannesburg.
Vikosi vilivyoanza:
Ireland: Shay Givens, Kelly, St. Ledger, McShane, Kilbane, Lawrence, Whelan, Keith Andrews, Duff, Kevin Doyle, Robbie Keane.
Brazil: Julio Cesar, Maicon, Lucio, Juan, Michel Bastos, Ramires, Silva, Felipe Melo, Kaka, Adriano, Robinho

Tuesday 2 March 2010

Klabu Tajiri 20 Duniani
Listi ya Klabu Tajiri Duniani imetolewa na Kampuni ya Wataalam wa Fedha, Deloitte, na imeonyesha kuwa Real Madrid bado inaongoza kwa kuwa na Mapato makubwa kupita Klabu nyingine huku Manchester United ikiporomoka kutoka nafasi ya 2 kwenda ya 3.
LISTI KAMILI:
1 Real Madrid, Spain
2 Barcelona, Spain
3 Manchester United, England
4 Bayern Munich, Germany
5 Arsenal, England
6 Chelsea, England
7 Liverpool, England
8 Juventus, Italy
9t Inter Milan, Italy
9t AC Milan, Italy
11 Hamburg, Germany
12 AS Roma, Italy
13 Lyon, France
14 Marseille, France
15 Tottenham, England
16 Schalke, Germany
17 Werder Bremen, Germany
18 Borussia Dortmund, Germany
19 Manchester City, England
20 Newcastle, England
Umiliki Man United: Vizito ‘Wakombozi Wekundu” wakutana kuiteka toka kwa kina Glazer!!!
Matajiri wakubwa ambao ni Masapota wakubwa wa Manchester United waliovumishwa kutaka kuinunua Klabu ya Manchester United kutoka kwa Familia ya Kimarekani ya kina Glazer wamekutana kwa mara ya kwanza kujadili mbinu na mikakati ya kuing’oa Klabu hiyo kutoka mikononi mwa Wamarekani hao walioingiza Man United kwenye deni la zaidi ya Pauni Milioni 700.
Kundi hilo, lilobatizwa jina la “Wakombozi Wekundu” limeunga mkono harakati za Masapota wa Klabu wanaojiita ‘MUST’ ‘[Manchester United Supporters Trust] wanaoendesha upinzani kwa ishara ya rangi za Kijani na Dhahabu, ambazo zilikuwa ni jezi za Klabu anzilishi ya Man United, Newton Heath, na pia limesema wao wanawapinga kina Glazer tu na wanaridhishwa na kazi na utawala wa Mkurugenzi Mtendaji David Gill pamoja na Meneja Sir Alex Ferguson.
‘Wakombozi Wekundu” hao ni kundi linalowaunganisha Matajiri Wakubwa ambao ni Wapenzi wa damu wa Manchester United kina Jim O’Neill, ambae ni Mchumi, Mwanasheria Mark Rawlinson na Mtaalam wa Fedha Keith Harris.
Habari toka ndani ya Kundi hilo lilithibitisha kuwepo Mkutano wao na pia kusema sasa wanafanyia kazi mbinu za kuiteka Man United na wamewataka Mashabiki wote wa Manchester United duniani kote kuwasaidia.
Hata hivyo, Msemaji wa Familia ya Glazer amesema Klabu haiuzwi.
FIFA: Bondeni wako tayari kwa Kombe la Dunia!
Mkuu wa FIFA Sepp Blatter amesema Afrika Kusini iko tayari kabisa kwa Fainali za Kombe la Dunia zitakazochezwa Nchini humo kuanzia Juni 11.
Kumekuwa na minong’ono ya muda mrefu kuwa hali si nzuri katika matayarisho ya Fainali hizo lakini Blatter ameondoa shaka hiyo huku ikianza hesabu ya siku 100 kabla ya Fainali hizo.
FIFA imetamka mpaka sasa zimeshauzwa Tiketi Milioni 2.2 kati ya jumla ya Tiketi Milioni 2.9 ingawa uuzwaji unaendelea polepole mno.
Inategemwa Wageni zaidi ya 450,000 watatua Afrika Kusini katika Fainali hizo.
Blatter alitoa kauli yake mara baada ya kutembelea Viwanja 10 vitakavyochezwa mechi za Fainali na kushuhudia vyote vikiwa vimekamilika.

Monday 1 March 2010

Zidane kamwe kumtaka radhi Materazzi!!
Supastaa wa Ufaransa Zinedine Zidane amesema ni heri kufa kuliko kumwomba radhi Marco Materazzi kwa kichwa alichomtwisha kwenye Fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2006.
Zidane, kwenye Fainali hiyo ikiwa ni mechi yake ya mwisho kabla kustaafu, alimpiga kichwa Materazzi kwenye muda wa nyongeza wa Fainali ambayo baadae Italia walinyakua Ubingwa wa Dunia kwa kushinda mikwaju ya penalti.
Zidane amekiri kujutia kitendo chake lakini hawezi kuomba radhi kwa vile Materazzi alimtukania Mama yake.
Zidane amesema: “Najuta! Lakini nikiomba radhi ni sawa na kukubali walichofanya ni sawa. Wakati huo Mama yangu alikuwa mgonjwa. Alikuwa hospitali. Ulikuwa wakati mbaya kwangu. Ingekuwa kitendo kile kafanya Kaka, ambae ni muungwana, ningeomba radhi! Lakini huyu, ntakuwa najikosea heshima mwenyewe!”
Wenger aomba kuumia Ramsey kusilete dosari
Arsenae Wenger anaomba sana kuumia vibaya kwa Kijana Aaron Ramsey katika mechi ya Ligi Kuu na Stoke City siku ya Jumamosi kusije kukaleta madhara kwa Wachezaji wake na kuwaathiri kisaikolojia.
Ramsey alivunjwa vibaya mguu na Mchezaji wa Stoke Ryan Shawcross ambae alipewa Kadi Nyekundu.
Kuumia huko kwa Ramsey kumemkasirisha Wenger ambae amedai Timu yake yenye Wachezaji wengi Chipukizi hukamiwa na kuchezewa undava na kuumizwa.
Ramsey alipelekwa hospitali na kufanyiwa operesheni na Madaktari wamesema wanategemea atapona vizuri.
Arsenal wameshawahi kuumiziwa Wachezaji wao vibaya kwa rafu mbaya ambazo ziliwaumiza Abou Diaby na hasa Eduardo ambae alikaa muda mrefu nje ya Uwanja baada ya kuumizwa na kuvunjwa enka.
Wenger anasema: “Katika Kiungo tuna Wachezaji kama Fabregas, Nasri na Eboue ambao wastani wa umri wao ni miaka 21 tu! Mbele yupo Bendtner, ana miaka 20 tu! Wachezaji wazuri sana lakini unawateketeza kwa kuwajeruhi! Hawatakuwa Wachezaji tena! Hii ni kashfa!”
Wiki ya Mechi za Kirafiki za Kimataifa
Hii ni wiki ambayo ipo kwenye Kalenda ya FIFA kwa Timu za Taifa za Nchi mbalimbali kukutana katika mechi za kirafiki.
Ifuatayo ni Ratiba ya baadhi ya mechi hizo za kirafiki:
Jumanne, Machi 2
Ireland v Brazil [Uwanja wa Emirates]
Jumatano, Machi 3
Albania v Northern Ireland
Algeria v Serbia
Angola v Latvia
Austria v Denmark
Belgium v Croatia
England v Egypt
France v Spain
Germany v Argentina
Greece v Senegal
Hungary v Russia
Italy v Cameroun
Ivory Coast v South Korea
Nerthelands v USA
Portugal v China
Poland v Bulgaria
Scotland v Czech Republic
Slovakia v Norway
Slovenia v Qatar
South Africa v Namibia
Switzerland v Uruguay
Turkey v Honduras
Wales v Sweden
Fergie abeba Kikombe cha 34!!!
Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson jana alinyakua Kikombe chake cha 34 tangu atue Manchester United baada ya Timu yake kuipiga Aston Villa 2-1 na kutwaa Kombe la Carling Uwanjani Wembley.
Bao la ushindi la Manchester United lilifungwa na Wayne Rooney dakika ya 74 katika mechi ambayo Aston Villa ndio walioanza kufunga dakika ya 3 tu ya mchezo walipopewa penalti baada ya Nemanja Vidic kumvuta jezi Gabriel Agbonlahor kitendo ambacho Meneja wa Aston Villa Martin O’Neill amedai kilistahili Kadi Nyekundu.
Hata hivyo, Michael Owen aliisawazishia Man United bao dakika ya 12 ya mchezo.
Kuhusu faulo ya Vidic kwa Agbonlahor, Ferguson alisema walibahatika sana kwa Vidic kutopewa Kadi yeyote na Refa Phil Dowd.
Ingawa Martin O’Neill alitaka Vidic atolewe, Nahodha wake Richard Dunne amesema haoni kama ingewasaidia endapo Man United wangecheza mtu 10 kwani katika mechi ya Ligi Kuu hivi karibuni Man United walicheza mtu 10 na Villa baada ya Winga Nani kutolewa kwa Kadi Nyekundu kwa zaidi ya saa nzima na wakacheza vizuri sana na kupata sare ya 1-1 nyumbani kwa Villa.
KWINGINEKO ULAYA: Matokeo
BUNDESLIGA
Jumapili, Februari 28
Hannover 0 Wolfsburg 1
Bayern Munich 1 Hamburg 0
LA LIGA
Jumapili, Februari 28
Xerez 1 Espanyol 1
Villareal 1 Deportivo la Coruna 0
Sporting Gijon 3 Osasuna 2
SERIE A
Jumapili, Februari 28
Napoli 2 AS Roma 2
Genoa 3 Bologna 4
Juventus 0 Palermo 2
Parma 1 Sampdoria 0
AC Milan 3 Atalanta 1
Udinese 2 inter milan 3
Livorno 1 Siena 2
Chievo 2 Cagliari 1

Sunday 28 February 2010

Man United Mabingwa!!!!
Aston Villa 1 Man United 2
Wayne Rooney, alieanza benchi na kuingizwa kumbadilisha Michael Owen alieumia dakika ya 42, ndie aliewapa kikombe Manchester United kwa kufunga bao la pili na kuwang’oa Aston Villa kwa bao 2-1 na kutwaa Kombe la Carling leo Uwanjani Wembley Jijini London.
Hiii ni mara ya pili mfululizo kwa Manchester United kutwaa Kombe hilo baada ya kushinda msimu uliokwisha kwa kuwabwaga Tottenham Fainali.
Aston Villa ndio waliokuwa wa kwanza kufunga pale walipopewa penalti dakika ya 5 tu ya mchezo baada ya Beki wa Man United Nemanja Vidic kumchezea rafu Gabriel Agbonlahor na Refa Phil Dowd kutoa penalti iliyofungwa na James Milner.
Michael Owen aliisawazishia Man United dakika ya 12 baada ya upiganaji mzuri wa Dimitar Berbatov.
Owen akaumia dakika ya 42 na kutoka na nafasi yake kushikwa na Wayne Rooney.
Hadi mapumziko bao zilikuwa 1-1.
Kipindi cha pili, dakika ya 74, gonga safi kati ya Berbatov na Valencia, Mchezaji aliepewa Tuzo ya Mchezaji Bora wa mechi, ilimaliziwa na krosi murua ya Valencia na Rooney akajitwisha na kufunga kwa kichwa safi.
Rooney alikosa kufunga bao la 3 pale kichwa chake kufuatia krosi ya Valencia kupiga posti huku Kipa wa Villa Brad Friedel akigalagala.
Vikosi vilivyoanza:
Aston Villa: Friedel, Cuellar, Collins, Dunne, Warnock, Ashley Young, Milner, Petrov, Downing, Heskey, Agbonlahor.
Akiba: Guzan, Luke Young, Sidwell, Carew, Delfouneso, Delph, Beye.
Man Utd: Kuszczak, Rafael Da Silva, Vidic, J Evans, Evra, Valencia, Fletcher, Carrick, Park, Owen, Berbatov.
Akiba: Foster, Neville, Brown, Rooney, Scholes, Gibson, Diouf.
Refa: Phil Dowd
LIGI KUU:
Liverpool 2 Blackburn Rovers 1
Uwanjani Anfield, Liverpool walipata ushindi wa 2-1 mbele ya Blackburn kwenye mechi ya Ligi Kuu na sasa wapo nafasi ya 6 kwenye Ligi wakiwa na pointi 48 kwa mechi 28 wakiwa pointi moja tu nyuma ya Tottenham na Man City zilizofungana kwa pointi ingawa Tottenham yuko juu kwa magoli lakini Man City wana mechi moja pungufu.
Liverpool walipata bao la kwanza dakika ya 20 kupitia Steven Gerrard na Blackburn wasawazisha dakika ya 40 kwa penalti iliyopigwa na Keith Andrews baada ya Jamie Carragher kushika mpira.
Fernando Torres akawapa ushindi Liverpool kwa kufunga bao la pili dakika ya 44.
Sunderland 0 Fulham 0
Ndani ya Stadium of Light, Sunderland wameshindwa kupata ushindi na kwenda sare ya 0-0 na Fulham katika mechi ya Ligi Kuu hii ikiwa ni mechi ya 14 kwa Sunderland bila ushindi.
Mechi ya mwisho Sunderland kuonja ushindi ni Novemba mwaka jana walipoifunga Arsenal.
LIGI KUU: Tottenham 2 Everton 1
Mabao mawili ya kipindi cha kwanza yaliyofungwa na Roman Pavlyuchenko na Luka Modric yamewapa ushindi Tottenham wa bao 2-1 wakiwa nyumbani White Hart Lane dhidi ya Everton.
Bao la Everton lilifungwa na Yakubu.
Ushindi wa leo umeifanya Tottenham ishike nafasi ya 4 ikiwa na pointi 49 kwa mechi 28 na Manchester City iko nyuma yao ikiwa na pointi sawa lakini wana tofauti ya magoli ndogo na wamecheza mechi moja pungufu.
WABABE SCOTLAND: Rangers 1 Celtic 0
Leo, Watoto wa Jiji la Glasgow na Wababe wa Scotland, Rangers na Celtic, walivaana kwenye Ligi ya Scotland na ni Rangers ndio waliibuka kidedea kwa ushindi wa bao 1-0, ushindi ambao umeipa Rangers uongozi wa pointi 10 mbele ya Celtic.
Celtic walipata pigo pale Nahodha wao Scott Brown alipopewa Kadi Nyekundu kwa kumpiga kichwa Lafferty wa Rangers.
Bao la ushindi la Rangers lilipatikana dakika ya 92 kilipotokea kizaazaa langoni mwa Celtic kufuatia kona na piga nikupige hiyo ikatua miguuni mwa Maurice Edu, alieanzia mechi hii benchi la akiba, ambae aliachia shuti hadi wavuni.
KWINGINEKO ULAYA: Matokeo
BUNDESLIGA
Ijumaa, Februari 26
Schalke 2 v Borussia Dortmund 1
Jumamosi, Februari 27
Mainz 05 1 v Werder Bremen 2
Hertha Berlin 0 v 1899 Hoffenheim 2
Bochum 0 v Nurnberg 0
Stuttgart 2 v Eintrancht Frankfurt 1
Borussia Moechengladbach 1 v Freiburg 1
Bayer Leverkusen 0 v Cologne 2
LA LIGA
Jumamosi, Februari 27
Barcelona 2 v Malaga 1
Getafe 0 v Real Zaragoza 2
Tenerife 1 v Real Madrid 5
SERIE A
Jumamosi, Februari 27
Catania 4 v Bari 0
Kikosi cha England hadharani!!
• Aliemvunja Ramsey yumo Kikosini!
Fabio Capello amekitaja Kikosi cha England kitakachocheza mechi ya kirafiki na Misri hapo Jumatano Uwanjani Wembley na Kikosini yumo Mchezaji wa Stoke City Ryan Shawcross aliemvunja mguu Aaron Ramsey wa Arsenal hapo jana Timu hizo zilipocheza kwenye Ligi Kuu.
Kikosi kamili: James (Portsmouth), Green (West Ham), Hart (Birmingham), Brown (Man Utd), Terry (Chelsea), Upson (West Ham), Lescott (Man City), Shawcross (Stoke), Baines (Everton), Warnock (Aston Villa), Milner (Aston Villa), Beckham (AC Milan), Walcott (Arsenal), Lampard (Chelsea), Barry (Man City), Gerrard (Liverpool), Carrick (Man Utd), Wright-Phillips (Man City), Downing (Aston Villa), Heskey (Aston Villa), Defoe (Tottenham), Rooney (Man Utd), Crouch (Tottenham), Carlton Cole (West Ham).
Stoke 1 Arsenal 3
• Ushindi waingia doa kwa kuumia vibaya Ramsey!
Jana kwenye Uwanja wa Britannia Arsenal ilipata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Stoke City kwenye Ligi Kuu na kufikisha pointi 58 wakiwa nafasi ya 3 huku juu yao wapo Manchester United wenye pointi 60 na vinara Chelsea wenye pointi 61.
Ushindi huo wa Arsenal umeingia dosari kubwa kwa kuumia vibaya kwa Mchezaji wao Chipukizi Aaron Ramsey alievunjwa mguu na Mchezaji wa Stoke Ryan Shawcross aliepewa moja kwa moja Kadi Nyekundu.
Kuumia kwa Ramsey kunafanana na kuumia kwa Mchezaji mwingine wa Arsenal Eduardo alieuvunjwa na Martin Taylor wa Birmingham miaka miwili iliyopita.
Ramsey alifanyiwa upasuaji na atakuwa nje msimu wote.
Powered By Blogger