Saturday 27 February 2010

LIGI KUU: Pompey, Birmingham ushindi kwa tuta!!!
Pompey washinda ugenini!!!
Portsmouth wameyaondoa matatizo yao ya nje ya uwanja kwa kupata ushindi mtamu ugenini kwa kuipiga Burnley bao 2-1.
Portsmouth walipata bao la kwanza kupitia Frederic Piquionne lakini Burnsley wakasawazisha kwa bao la Martin Paterson.
Jamie O’Hara akaikosesha Pompey bao la pili pale alipokosa penalti kwa Kipa wa Burnley Brian Jensen kuokoa.
Lakini Pompey wakapata penalti ya pili baadae na safari hii ikapigwa na Mchezaji toka Algeria Hassan Yebda na akafunga bao la pili na la ushindi.
Portsmouth walimaliza mechi hii wakiwa Watu 10 baada ya Mchezaji wao Ricardo Rocha kupata Kadi Nyekundu kwenye dakika za majeruhi baada ya kulambwa Kadi za Njano mbili.
Birmingham 1 Wigan 0
Bao la penalti iliyopigwa na James McFadden dakika chache kabla haftaimu limeipa ushindi Birmingham wakiwa nyumbani dhidi ya Wigan.
Penalti hiyo ilitolewa baada ya Beki wa Wigan Mario Melchiott kumkata ngwala Keith Fahey ndani ya boksi.
Mwishoni mechi hii iliongezwa dakika 7 kufidia muda iliposimama baada ya Msaidizi wa Refa, mshika kibendera, Trevor Massey, kuumizwa na kupasuliwa kichwani na kibendera cha kona kilichompiga baada ya Beki wa Birmingham Ridgewell kumkata McCarthy na kukivaa kibendera hicho kilichoruka.
Bolton 1 Wolves 0
Mlinzi Zat Knight aliuondoa ukame wa magoli wa Bolton uliodumu zaidi ya masaa 9 pale alipofunga goli dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza baada ya pande tamu la mwenzake Chung-Yong Lee.
Kipindi cha pili, Wolves walikosa bao za wazi kadhaa zikiwemo mbili zilizogonga posti.
Chelsea 2 Man City 4
• Bifu la Terry v Bridge: Bridge hakutoa mkono kwa Terry!!
Dunia nzima ilikaza macho kutaka kuona kama mwanzoni mwa mechi Wayne Bridge na John Terry watapeana mikono kufuatia skandali la Terry kutembea na gelfrendi wa Bridge lililozua Terry kufukuzwa Unahodha England na Bridge kugoma kuichezea England na dunia nzima ikaona Bridge hakutoa mkono huku mkono wa Terry ukielea hewani.
Pia dunia nzima ikashuhudia Manchester City wakiipa Chelsea, wakiwa nyumbani kwao Stamford Bridge, kipondo cha bao 4-2 kwenye mechi ya Ligi Kuu na kuwafanya wamalize mechi hii wakiwa mtu 9 tu baada ya Juliano Belleti na Michael Ballack kupewa Kadi Nyekundu katika nyakati tofauti na Refa Mike Dean.
Sasa uongozi wa Chelsea kwenye Ligi ni pointi moja tu mbele ya Manchester United.
Kwa ushindi wa leo Manchester City wamechukua nafasi ya 4 wakiwa pointi 3 mbele ya Tottenham.
Chelsea ndio waliopata bao mwanzo mfungaji akiwa Frank Lampard dakika ya 42 lakini dakika chache baadae Carlo Tevez alisawazisha kwa goli lilojaa vituko.
Goli hilo la Tevez lilianzia kwa Mikel Obi kupiga kichwa nyuma na Terry kuukosa mpira huo na kumfikia Tevez aliewahadaa Terry na Carvalho lakini akaparaza shuti lake huku Kipa Hilario nae akauparaza mpira kwa mkono na pole pole ukatiririka wavuni.
Kipindi cha pili Craig Bellamy akafunga bao la pili dakika ya 51 na Tevez akapachika bao la 3 dakika ya 76 kwa penalti iliyompa Kadi Nyekundu Belleti kwa kumchezea rafu Gareth Barry ndani ya boksi.
Bao la 4 la Man City lilifungwa na Bellamy kufuatia kaunta ataki kwenye dakika ya 86.
Chelsea walipata bao lao la pili dakika ya 90 kwa penalti aliyopiga Lampard baada ya Gareth Barry kumchezea rafu Anelka.
Vikosi:
Chelsea: Hilario, Ivanovic, Carvalho, Terry, Malouda, Ballack, Mikel, Lampard, Anelka, Drogba, Joe Cole.
Akiba: Turnbull, Paulo Ferreira, Kalou, Sturridge, Matic, Alex, Belletti.
Man City: Given, Richards, Kompany, Lescott, Bridge, Zabaleta, De Jong, Barry, Bellamy, Tevez, Adam Johnson.
Akiba: Taylor, Onuoha, Wright-Phillips, Santa Cruz, Sylvinho, Toure, Ibrahim.
Refa: Mike Dean
KIJANI & DHAHABU: Mashabiki Man United wajizatiti kuwang’oa kina Glazer!
Kikundi cha Mashabiki wa Manchester United, wanaojiita ‘MUST’ [Manchester United Supporters Trust], kimetangaza kuwa kimeiteua Kampuni ya ushauri ya kwenye mtandao ambayo ilishiriki uchaguzi wa Marekani na kufanikisha ushindi wa Obama mtandaoni, ili kuongeza nguvu kampeni yao na kupata Masapota watakaofikia idadi ya Watu 100,000 ili kuing’oa Familia ya Glazer katika umiliki wa Manchester United.
Mashabiki hao wa Man United, wanaovaa rangi za kijani na dhahabu hizi zikiwa ndizo rangi za kwanza za Newton Heath Timu anzilishi ya Man United na hiyo ikiwa ishara yao ya upinzani, kwa sasa wanakadiriwa kufikia Watu 52,000.
Kwenye Fainali ya Carling Cup Jumapili huko Wembley, Manchester United watakapocheza na Aston Villa, wimbi la kijani na dhahabu linategemewa kutanda miongoni mwa Mashabiki wa Man United ikionyesha kupamba moto kwa upinzani huo.
Nigeria yamteua Msweden Lagerback Kocha
Nigeria imemteua aliekuwa Kocha wa Sweden Lars Lagerback kuwa Kocha wa Timu ya Taifa yao ambayo ipo Fainali Kombe la Dunia.
Mara baada ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika huko Angola mwezi Januari walikofika Nusu Fainali, Nigeria walimtimua kazi Kocha wao Shuaibu Amodu licha ya kuwaingiza Fainali Kombe la Dunia.
Lagerback alikuwa Kocha wa Sweden lakini alijuzulu baada ya Sweden kushindwa kufuzu kuingia Fainali Kombe la Dunia.
Lagerback amepewa mkataba wa miezi mitano ambao utamuwezesha kuwepo kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini ambapo Nigeria wapo Kundi moja na Argentina, Ugiriki na Korea ya Kusini.
Majina ya vigogo waliohusishwa na kazi ya Ukocha Nigeria ni pamoja na Glenn Hoddle, Sven Goran Eriksson na Bruno Metsu.
SAKATA LA POMPEY: Msimamizi spesheli atua, asema Grant anabaki!!!
Msimamizi Maalum wa kuinusuru Portsmouth isifilisiwe, Andrew Andronikou, ameshatua Klabuni hapo na licha ya kuahidi kuisafisha Klabu hiyo pia amethibitisha Meneja Avram Grant atabaki Klabuni hapo hadi mwishoni mwa msimu na pia hakutakuwa na uuzwaji wa Wachezaji wa chapuchapu ili kupata fedha.
Portsmouth inakisiwa kuwa na deni la Pauni Milioni 60 na Jumatatu ipo Mahakama Kuu kwenye kesi ambayo Mamlaka ya Kodi iliitaka Mahakama hiyo iitangaze Klabu hiyo imefilisika kwa sababu ilishindwa kulipa kodi lakini kwa vile Klabu hiyo ipo chini ya Msimamizi Maalum uamuzi wa kuifilisi utaondolewa na Mahakama hiyo.
Hata hivyo, Portsmouth inakabiliwa na adhabu ya kukatwa pointi 9 na Ligi Kuu kwa vile imekiuka taratibu kwa kuwa mikononi mwa Msimamizi na adhabu hii, ukichukua hali ya Pompey kuwa mkiani ikiwa na pointi 17 tu, ni lazima itaishusha Daraja.
Andrew Andronikou ametamka: “Hamna kuuza Wachezaji chapuchapu! Lakini, ninahitaji mtaji wa kufanyia kazi hivyo tutaongea na Ligi Kuu tupate kibali cha kuuza Mchezaji mmoja au wawili!”
Andronikou atasaidiwa kwenye kazi yake hiyo na Peter Kubik na amesema kazi yake ya kwanza ni kutathmini nini kimeharibika na baada ya wiki 8 atakutana na Wadai wote.
Msimamizi huyo amewaomba Mashabiki wote wa Pompey kuisaidia Klabu hiyo na kuendelea kuisapoti katika mechi zilizobaki za msimu huu.
FAINALI : Safari ya Wembley
Fainali ya Kombe la Carling ni Jumapili Februari 28 Uwanja wa Wembley kati ya Mabingwa Watetezi wa Kombe hilo Manchester United na Aston Villa na mechi hii itaanza saa 12 jioni saa za bongo chini ya usimamizi wa Refa Phil Dowd.
Safari ya Timu hizi kufika Wembley ilianza Raundi ya 3 na mechi zao zilikuwa:
RAUNDI YA 3
Man United 1 Wolves 0
Aston Villa 1 Cardiff 0
RAUNDI YA 4
Barnsley 0 Man United 2
Sunderland 0 Aston Vill 0 [Villa walishinda 3-1 kwa penalti]
ROBO FAINALI
Portsmouth 2 Aston Villa 4
Man United 2 Tottenham 0
NUSU FAINALI
-Mechi za kwanza
Manchester City 2 Man United 1
Blackburn 0 Aston Villa 1
-Mechi za marudiano
Man United 3 Man City 1
Aston Villa 6 Blackburn 4
NI FAINALI!!!!
Wakati Martin O'Neill bado anasaka Kombe tangu aanze kazi ya Umeneja Aston Villa ingawa aliwahi kuvitwaa Vikombe viwili alipokuwa Leicester City, Manchester United ndio Mabingwa Watetezi wa Kombe hili la Carling baada ya kulitwaa msimu uliopita walipowabwaga Tottenham kwa penalti.
Aston Villa kama Klabu mara ya mwisho kuchukua Kikombe ni mwaka 1996 walipotwaa Kombe la Ligi ambalo sasa ndio Carling walipowatoa Leeds United Fainali.
Msimu huu, Aston Villa na Manchester United zimecheza mara mbili na Villa walishinda Old Trafford 1-0 na hivi majuzi walitoka sare 1-1 Villa Park huku Man United ikicheza mtu 10 kwa karibu saa nzima baada ya Winga wao Nani kupewa Kadi Nyekundu.
Sir Alex Ferguson, Meneja wa Manchester United, amekuwa akichezesha Chipukizi kwenye mechi za Raundi za mwanzo za michuano hii lakini walipofika Nusu Fainali na kukutana na Mahasimu wao wakubwa Manchester City aliweka Wachezaji wazoefu.
Akizungumzia Fainali, Ferguson alisema: “Kucheza Wembley ni tukio kubwa. Lakini utaiskia raha tu ya kucheza Wembley ukishinda! Tuna nafasi ya kushinda!”
Nae Martin O’Neill, Meneja wa Aston Villa, anasema: “Hapa Klabuni, tuna picha nyingi za Timu zetu za zamani zilizobeba Vikombe! Sisi je? Mafanikio ya Timu hizo ni changamoto kwetu na tunataka kushinda!”
Ingawa msimu huu Aston Villa wamegangamara kwa Manchester United lakini katika mapambano 37 kati yao Villa wameshinda mara mbili tu.
Wakati Villa haina majeruhi, Manchester United itawakosa majeruhi Rio Ferdinand, Ryan Giggs na Anderson, na Nani hawezi kucheza kwani yuko kifungoni mechi 3 kwa kupewa Kadi Nyekundu mechi ya Ligi na Aston Villa.
Vikosi vinategemewa:
Aston Villa (4-4-2): Friedel; Cuellar, Dunne, Collns, Warnock; A Young, Milner, Petrov, Downing; Agbonlahor, Heskey.
United: (4-4-2) Foster; Neville, Vidic, Brown, Evra; Scholes, Fletcher, Carrick, Park; Rooney, Berbatov.
Refa: Phil Dowd.
LIGI KUU England: Mechi za wikiendi
Jumamosi
Chelsea v Man City
Birmingham v Wigan
Bolton v Wolves
Burnley v Portsmouth
Stoke v Arsenal
Jumapili
Tottenham v Everton
Liverpool v Blackburn
Sunderland v Fulham
Mabingwa Watetezi Manchester United hawachezi Ligi Kuu wikiendi hii na badala yake watakuwepo Uwanjani Wembley Jumapili kucheza Fainali ya Kombe la Carling na Aston Villa.
Mechi za Ligi Kuu Jumamosi zitaanza kwa mechi ya mapema huko Stamford Bridge kati ya wenyeji na vinara wa Ligi Chelsea na Manchester City.
Mechi hii ya Chelsea v Man City licha ya kuzikutanisha Timu iliyo kileleni na inayotaka kubakia huko Chelsea na Man City inayogombea nafasi ya 4, mvuto mkubwa ni yule alietimuliwa Unahodha wa England ambae ni Nahodha wa Chelsea, John Terry, kukutana uso kwa uso na ‘mbaya wake’ Wayne Bridge wa Man City, mtu ambae gelfrendi wake ndie anaesemekana alitembea na Terry na skandali hilo likamfukuzisha Terry Unahodha wa England.
Kashfa hiyo ya Terry pia imemfanya Bridge ajiuzulu kuichezea England ili asikutane na Terry.
Na sasa watakutana Stamford Bridge wakiwa Timu pinzani na swali lililo kinywani mwa kila mtu ni: je watapeana mikono kabla ya mechi?
Wapinzani wengine kwenye mechi hii ni Mameneja wa Timu hizo, Chelsea na Man City, ambao wote ni Wataliana, Carlo Ancelotti wa Chelsea na Roberto Mancini wa Man City.
Wataliana hao walikuwa Timu pinzani huko Italia, Ancelotti akiwa AC Milan na Mancini akiwa Inter Milan.
Chelsea watamkosa Kipa wao nambari wani Petr Cech alieumia kwenye kipigo cha huko San Siro toka kwa Inter Milan cha 2-1.
Man City watamkosa Adebayor aliefungiwa mechi 4 kwa kumpiga Mchezaji wa Stoke kwenye mechi ya marudiano ya FA Cup hapo juzi lakini Carlos Tevez amesharudi toka kwao Argentina alikoenda kwa matatizo ya kifamilia.
Arsenal wataenda Britannia Stadium ambako mara nyingi huumbuka ili kukutana na Stoke City na msimu uliokwisha Arsenal alipigwa 2-1.
Msimu huu, Stoke na Arsenal zilikutana kwenye FA Cup na Arsenal akachapwa 3-1.
Msimi huu, Stoke haijafungwa.
Burnley v Portsmouth ni mechi ya Timu za mkiani huku Portsmouth wakiwa pengine washajilaani kushushwa daraja baada ya kukabidhiwa mikononi mwa Msimamizi maalum ili kuwanusuru wasifilisiwe na hilo huadhibiwa kwa kukatwa pointi 9 kitu ambacho wasimamizi wa Ligi Kuu wanangojewa kukithibitisha.
Huko Reebok, Bolton wanaikaribisha Wolves na mpaka sasa ni mechi 5 tangu Bolton wafunge goli. Bolton na Wolves ziko mwishoni mwa msimamo wa Ligi na Wolves wako pointi moja tu mbele ya Bolton.
Birmingham wako nafasi ya 10 na wako pointi 12 mbele ya Wigan watakaocheza nao Uwanja wa Mtakatifu Andrew.
Siku ya Jumapili, Uwanjani White Hart Lane, wenyeji Tottenham Hotspur watacheza na Everton wanaotoka kwenye kipigo cha 3-0 mikononi mwa Sporting Lisbon kilichowatupa nje ya EUROPA LIGI.
Kwenye Ligi Kuu, Everton imeshinda mechi zao mbili za mwisho kwa kuwafunga vigogo Chelsea na Manchester United.
Tottenham wako nafasi ya 4 na watataka kujichimbia hapo.
Uwanjani Anfield, Liverpool wataikwaa Blackburn Rovers ambao siku za hivi karibuni wamegangamara na kujikwamua kutoka chini na sasa wako nafasi ya 12 kwenye Ligi.
Liverpool wako nafasi ya 6 na watataka ushindi baada ya kufungwa na Arsenal kisha kutoka sare na Manchester City katika mechi zao za mwisho.
Mara ya mwisho Sunderland kushinda ilikuwa ni mechi 13 nyuma na Sunderland watacheza na Timu ngumu Fulham wikiendi hii wakiwa nyumbani Stadium of Light.
Ushindi huo wa mwisho wa Sunderland ulikuwa Novemba 21, 2009 walipoipiga Arsenal.
Fulham nao ni magoigoi wakicheza ugenini na hawajashinda katika mechi 12 za ugenini.
Van der Sar asaini mkataba mpya
Kipa nambari wani wa Manchester United Edwin van der Sar amesaini mkataba mpya wa mwaka mmoja utakaomweka Old Trafford hadi 2011 na atakuwa amefikisha umri wa miaka 40 wakati huo.
Van der Sar ametamka kwa furaha: “Hii ni Klabu kubwa na walinionyeshea utu na uungwana mwezi Desemba na Januari Mke wangu alipougua! Nina furaha hapa!”
Nae Bosi wa Manchester United Sir Alex Ferguson amesema: “Edwin ni mtu anaeheshimu kazi na amejitunza vizuri. Ana uzoefu mkubwa na tuna furaha kuwa nae.”
Skrtel avunjika!!
Difenda wa Liverpool kutoka Slovakia Martin Skrtel amethibitika amevunjika mfupa wa kidole cha mguu wa kulia kwenye mechi ya Alhamisi ya EUROPA LIGI huko Romania Liverpool walipoifunga Unirea Urziceni bao 3-1.
Skrtel anategemewa kuwa nje kwa wiki kadhaa kama ilivyothibitishwa na Meneja Rafa Benitez ambae pia alisema Beki wao wa kulia Glen Johnson aliekuwa majeruhi ameaanza mazoezi mepesi.
Johnson alikuwa ameumia goti na alikuwa nje ya uwanja tangu Desemba.

Friday 26 February 2010

Jahazi latota Pompey lakini Wachezaji waungwana!!!
Meneja wa Portsmouth Avram Grant amesema Wachezaji wake wawili wamekubali punguzo la mishahara yao ili kuokoa ajira za Wafanyakazi wa kawaida wa Klabu hiyo yenye matatizo makubwa ya fedha na sasa iko chini ya Msimamizi maalum ili kuinusuru isitangazwe mufilisi.
Kwa kuwekwa chini ya Msimaizi maalum tayari Portsmouth imekiuka sheria za Ligi Kuu England na itakatwa pointi 9 na hilo, ni wazi, litaishusha Daraja kwani mpaka sasa wako mkiani na wana pointi 16 tu.
Grant amesema atakutana na Wachezaji wote ili kuongea jinsi ya kunusuru ajira za Wafanyakazi wa kawaida wengine.
Grant amenena: “Inasikitisha! Lakini tutakutana kuangalia nini tufanye tusaidie wengine!
Diouf: “Mimi ni dume!”
Mchezaji wa Blackburn Rovers anaetoka Senegal El-Hadji Diouf amechokoza hasira za Liverpool, Klabu aliyoihamia kutoka Lens ya Ufaransa mwaka 2002 na kukaa miaka mitatu, kwa kudai Blackburn itawafunga kirahisi Liverpool watakapocheza mechi ya Ligi Kuu Jumapili.
Diouf amedai: “Si ngumu kwenda Anfield na kuwafunga! Hapa England, kila Timu inaweza kuifunga nyingine! Utaona Timu kama Watford ishashuka Daraja lakini inaifunga Manchester United! Siogopi kuzomewa na kama sizomewi siwezi kucheza! Mie ni dume na ninahitaji kuonyesha watu mie ni dume!!”
Portsmouth kuporomoka!!!
• Kukatwa Pointi 9!!!
Imethibitika Portsmouth ndio itakuwa Klabu ya kwanza ya Ligi Kuu England kuangukia kwenye mikono mibaya ya kuwa chini ya Msimamizi maalum ili kuepuka kutangazwa Mufilisi.
Portsmouth, ambayo msimu huu mmoja imebadili Wamiliki wanne, imeshindwa kupata Mnunuzi na Jumatatu iko Mahakamani kwenye kesi iliyofunguliwa na Mamlaka ya Kodi inayotaka Klabu hiyo ifilisiwe kwa kushindwa kulipa kodi.
Msimamizi huyo maalum atakuwa na kazi ya kurekebisha muundo wa uendeshwaji wa Klabu hiyo ili kuifanya iwe inavutia kwa Wanunuzi.
Lakini hatua hii ya kuiweka chini ya Msimamizi maalum kuinusuru isifilisiwe, ingawa ni hatua nzuri kwa uhai wa Klabu, ni kinyume cha sheria za Ligi Kuu na Klabu hiyo itakatwa pointi 9.
Portsmouth wapo mkiani mwa Ligi Kuu na wana pointi 16 tu na kukatwa pointi 9 ni wazi kunawahukumu washushwe Daraja mwishoni mwa msimu.
KANDANDA WIKIENDI:
Jumamosi, February 27
LIGI KUU
[saa 9 dak 45 mchana]
Chelsea v Man City
[saa 12 jioni]
Birmingham v Wigan
Bolton v Wolves
Burnley v Portsmouth
[saa 2 na nusu usiku]
Stoke v Arsenal
Jumapili, Februari 28
LIGI KUU
[saa 10 jioni]
Tottenham v Everton
[saa 12 jioni]
Liverpool v Blackburn
Sunderland v Fulham
FAINALI CARLING CUP
[saa 12 jioni]
Manchester United v Aston Villa
KWINGINEKO ULAYA:
BUNDESLIGA
Ijumaa, Februari 26
Schalke v Borussia Dortmund
Jumamosi, Februari 27
Mainz 05 v Werder Bremen
Hertha Berlin v 1899 Hoffenheim
Bochum v Nurnberg
Stuttgart v Eintrancht Frankfurt
Borussia Moechengladbach v Freiburg
Bayer Leverkusen v Cologne
Jumapili, Februari 28
Hannover v Wolfsburg
Bayern Munich v Hamburg
LA LIGA
Jumamosi, Februari 27
Barcelona v Malaga
Getafe v Real Zaragoza
Tenerife v Real Madrid
Jumapili, Februari 28
Xerez v Espanyol
Villareal v Deportivo la Coruna
Sporting Gijon v Osasuna
SERIE A
Jumamosi, Februari 27
Catania v Bari
Lazio v Fiorentina
Jumapili, Februari 28
Napoli v AS Roma
Genoa v Bologna
Adebayor kifungoni mechi 4
Straika wa Manchester City Emmanuel Adebayor atazikosa mechi zote za timu yake za mwezi Machi baada ya kufungiwa mechi 3 kwa kutolewa kwa Kadi Nyekundu kwa kumpiga Mchezaji wa Stoke kwenye mechi ya FA siku ya Jumatano walipofungwa 3-1 na adhabu hiyo moja kwa moja imeongezwa mechi moja kwa vile alishafungiwa mwezi Septemba kwa kero zake katika mechi ya Arsenal.
Adebayor atazikosa mechi za Manchester City na Chelsea, Sunderland, Fulham na Wigan.
SKANDALI LA TERRY: Sasa Bifu la Terry v Bridge!!!!!
Juzi Wayne Bridge alitangaza kujiuzulu kuichezea Timu ya Taifa ya England ili asigongane na John Terry anaetuhumiwa kutembea na gelfrendi wake ambae ni Mama wa Mtoto wake na sasa vita ya chini kwa chini ya Terry na Bridge imeibuka huku Wachezaji hao wakitazamiwa kupambana Uwanjani Stamford Bridge kwenye mechi ya Ligi Kuu kati ya Timu ya Bridge Manchester City na Timu ya Terry Chelsea siku ya Jumamosi.
Inadaiwa marafiki wa Terry wameanza kuzoza kuwa Bridge ni mwoga na ndio maana amejitoa Timu ya Taifa ya England.
Kocha wa England Fabio Capello akizungumzia kujitoa kwa Bridge alisema bado ana matumaini Mchezaji huyo anaweza akabadili mawazo na taimu bado ipo kumwita Kikosini ili acheze Fainali za Kombe la Dunia linaloanza Juni huko Afrika Kusini.
Wayne Bridge ndie mrithi wa dhahiri wa nafasi ya Beki wa kushoto Ashley Cole alieumia vibaya enka yake na itabidi Capello awafikirie Wachezaji Stephen Warnock wa Aston Villa na Leighton Baines wa Everton kuchukua nafasi hiyo.
Mchezaji mwingine ambae pengine agekuwa nambari wani kuchukua nafasi hiyo ni Kieran Gibbs wa Arsenal lakini nae kavunjika mfupa wa kidoleni mguuni.
Bridge, aliechezea England mara 36, alitoa tamko la kujiuzulu England kupitia Mawakili wake na alisema kujitoa kwake ni kwa sababu huu si wakati muafaka na kuwepo kwake kunaweza kuleta mgawanyiko Kikosini England.
Lakini, chinichini, inadaiwa Bridge na Terry waliongea kwa simu ili kutuliza sakata hilo linalowahusu lakini mazungumzo hayo yakaisha kwa simu kukatwa baada ya kutoafikiana.
Mechi ya Jumamosi huko Stamford Bridge kati ya Chelsea na Manchester City itafuatiliwa na wengi na kamera, bila shaka, zitalenga kuona kama Terry na Bridge watapeana mikono kabla kuanza mechi kama ilivyo kawaida.
EUROPA LIGI: Everton nje, Fulham, Liverpool zapeta!!
Timu za Fulham na Liverpool, zikicheza ugenini, zilipata matokeo mazuri na hivyo kusonga mbele kuingia Raundi ya Mtoano ya Timu 16 lakini wenzao Everton walichapwa mabao 3-0 huko Ureno mikononi mwa Sporting Lisbon na hivyo kubwagwa nje ya EUROPA LIGI.
Huko Ukraine, Fulham walitangulia kupata bao dakika ya 33 lakini Shakhtar Donetsk walisawazisha dakika ya 69 na mechi ikaisha 1-1.
Shakhtar Donetsk ndio walikuwa wameshinda Kombe la UEFA msimu uliopita na Kombe hilo sasa linaitwa EUROPA LIGI.
Fulham walishinda mechi ya kwanza 2-1 na hivyo kufuzu kwa jumla ya mabao 3-2.
Katika mechi hiyo Danny Murphy wa Fulham alipewa Kadi Nyekundu dakika ya 90 kwa kumpiga teke Mchezaji wa Donetsk.
Huko Romania, Liverpool waliichapa Unirea Urziceni mabao 3-1 na kusonga mbele kwa jumla ya mabao 4-1.
Unirea ndio waliopata bao la kwanza kupitia Joao Bruno Fernandes lakini Javier Mascherano wa Liverpool akasawazisha.
Ryan Babel na Steven Gerrard wakaongeza bao mbili na kuwafanya Liverpool wakutane na Lille ya Ufaransa Raundi ijayo ya Mtoano.
Huko Ureno mabao ya Sporting Lisbon yaliyofungwa na Miguel Veloso, Pedro Mendes na Fernandez yamewabwaga nje Everton kwa jumla ya mabao 3-2.
Everton walishinda mechi ya kwanza 2-1.
MATOKEO Mechi za Marudiano
Alhamisi, Februari 25
Anderlecht 4 v Athletci Bilbao 0 [jumla mabao 5-1]
Fenerbahce 1 v Lille 1 [2-3]
Galatasaray 1 v Atletico Madrid 2 [2-3]
Hapoel Tel Aviv 0 v Rubin Kazan 0 [0-3]
Juventus 0 v Ajax 0 [2-1]
Marseille 3 v FC Copenhagen 1 [6-2]
PSV 3 v Hamburg 2 [3-3, Hamburg wamefuzu kwa magoli ya ugenini]
Roma 2 v Panathinaikos 3 [4-6]
SV Red Bull Salzburg 0 v Standard Liege 0 [4-6]
Shakhtar Donetsk 1 v Fulham 1 [2-3]
Sporting Lisbon 3 v Everton 0 [4-2]
Unirea Urziceni 1 v Liverpool 3 [1-4]
Valencia 3 v Club Brugge 0 [3-1]
Werder Bremen 4 v FC Twente 1 [4-2]
Wolfsburg 4 v Villareal 1[6-3]
RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 16
Alhamisi, Machi 11
Juventus v Fulham
Atletico Madrid v Sporting Lisbon
Valencia v Werder Bremen
Hamburg v Anderlecht
Benfica v Marseille
Lille v Liverpool
Panathinaikos v Standard Liege
Rubin Kazan v Wolfsburg
[MECHI ZA MARUDIANO MACHI 18]

Thursday 25 February 2010

EUROPA LIGI: Timu za England zipo ugenini leo!
Leo Ulaya yote ni mechi za marudiano za EUROPA LIGI na Timu 3 za England zilizomo kinyang’anyiro hicho zote zipo ugenini na zote zipo huko huku zikiwa na ushindi mwembamba wa mechi za kwanza.
Liverpool leo ipo Romania kucheza na Unirea Urziceni na inabidi waulinde ushindi wao wa bao 1-0 walioupata nyumbani kwao Uwanjani Anfield wiki iliyopita.
Nao Everton wako Ureno kucheza na Sporting Lisbon na wao pia inabidi waulinde ushindi wa bao 2-1 walioupata kwao Goodison Park wiki iliyopita.
Kwa Fulham, ambao wanacheza huko Ukraine watakaporudiana na Shakhtar Donetsk, hali ni hiyo hiyo ya kulinda ushindi wao wa bao 2-1 walioupata kwao Craven Cottage.
Mbali ya mechi ya Timu hizi 3 za England leo pia kuna mechi 12 nyingine za EUROPA LIGI.
Timu pekee ambayo tayari ishatinga Raundi inayofuata ya Mtoano ya Timu 16 ni Benfica ambayo juzi iliirarua Hertha Berlin bao 4-0 baada ya kutoka sare 1-1 mechi ya kwanza.
Mourinho atamba kuingia Robo Fainali UEFA!
Kocha wa Inter Milan Jose Mourinho baada ya kuifunga Chelsea 2-1 hapo jana Uwanjani San Siro amejigamba kuwa wao wataingia Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI na hana wasiwasi na mechi ya marudiano Machi 16 huko Stamford Bridge.
Mourinho ametamba: “Mourinho hafungwi Stamford Bridge!”
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kurudi Stamford Bridge kwa Mourinho tangu aihame Klabu hiyo Septemba 2007 na amesema mechi ya marudiano mabao si muhimu bali ni matokeo tu yatakayomfanya asonge mbele.
Pia Mourinho allikiri kuwa katika mechi ya jana Chelsea walistahili kupata penalti kipindi cha kwanza.
Wayne Bridge ajitoa kuchaguliwa England
Wayne Bridge ametangaza kuwa hawezi kuwepo katika uteuzi wa Wachezaji watakaounda Kikosi cha England kitakachocheza mechi ya kirafiki Machi 3 na Misri.
Kocha wa England Fabio Capello anatarajiwa kufanya uteuzi huo Jumapili lakini Bridge amejitoa kwa kusema si muafaka na pengine uteuzi wake utaigawa England hasa ukizingatia skandali la John Terry ambae alivuliwa Unahodha wa England kwa kuhusishwa na kutembea na gelfrendi wa Wayne Bridge.
Uteuzi wa Bridge kwenye Timu ya England ulikuwa ni wazi hasa baada ya kuumia kwa Beki wa kushoto wa kudumu wa Timu hiyo Ashley Cole.
Hata hivyo Wayne Bridge na John Terry watakuwa Uwanja mmoja siku ya Jumamosi pale Klabu ya Terry Chelsea itakapovaana na Manchester City Klabu ya Bridge huko Stamford Bridge kwenye mechi ya Ligi Kuu.
Anderson nje msimu wote!
Kiungo kutoka Brazil wa Manchester United Anderson amepata pigo kubwa kwa kuumia goti litakalomuweka nje ya uwanja msimu wote na hivyo kulikosa Kombe la Dunia ambalo alikuwa na matumaini makubwa kuchukuliwa na Brazil.
Anderson aliumia dakika ya 19 ya mchezo kati ya Manchester United na West Ham ambapo Man United walishinda 3-0 hapo juzi Jumanne Uwanjani Old Trafford.
Vile vile, Rio Ferdinand yupo nje kwa kuuumia tena mgongo ambao umekuwa ukimsumbua muda mrefu.
Ni majuzi tu Rio alirudi kucheza tena baada ya kukaa nje miezi mitatu kwa kuumwa mgongo lakini alicheza mechi moja tu na akapata mkosi wa kufungiwa mechi 4 kwa kupatikana na hatia ya kumpiga Craig Fagan wa Hull City Man United ilipocheza na Timu hiyo.
Rio ataikosa Fainali ya Carling Cup hapo Jumapili Manchester United watakapokumbana na Aston Villa na pia mechi ya kirafiki ya England na Misri Jumatano ijayo ambayo ndio ingekuwa mechi yake ya kwanza kama Kepteni wa England baada ya kutimuliwa John Terry.
Lakini Meneja wake Sir Alex Ferguson ana mategemeo makubwa Rio safari hii atarudi uwanjani mapema.
UEFA CHAMPIONS LIGI: CSKA, Sevilla droo, Chelsea yafa!
Huko Urusi, CSKA Moscow ilitoka sare 1-1 na Sevilla na lile pambano la hamu kati ya Inter Milan na Chelsea lilimalizika kwa ushindi wa 2-1 kwa Inter Milan nyumbani San Siro.
Inter Milan ndio walipata bao la kwanza dakika ya 3 tu kupitia Milito.
Chelesea walisawazisha kwenye dakika ya 51 kwa bao la Kalou lakini Inter Milan walifunga bao la pili na la ushindi dakika ya 55 lililofungwa na Cambiasso.
Timu hizi zitarudiana Machi 9 huko Stamford Bridge.
MATOKEO MARUDIO FA CUP:
Tottenham 4 Bolton 0
Stoke City 4 Man City 3 [baada ya muda wa nyongeza]
Aston Villa 3 Crystal Palace 1
EUROPA LIGI: Ratiba Mechi za Marudiano
Alhamisi, Februari 25
Anderlecht v Athletci Bilbao [mechi ya kwanza 1-1]
Fenerbahce v Lille [mechi ya kwanza 1-2]
Galatasaray v Atletico Madrid [1-1]
Hapoel Tel Aviv v Rubin Kazan [0-3]
Juventus v Ajax [2-1]
Marseille v FC Copenhagen [3-1]
PSV v Hamburg [0-1]
Roma v Panathinaikos [2-3]
SV Red Bull Salzburg v Standard Liege [2-3]
Shakhtar Donetsk v Fulham [1-2]
Sporting Lisbon v Everton [1-2]
Unirea Urziceni v Liverpool [0-1]
Valencia v Club Brugge [0-1]
Werder Bremen v FC Twente [0-1]
Wolfsburg v Villareal [2-2]

Wednesday 24 February 2010

Leo marudio FA Cup
Mechi za Raundi ya 5 ya FA Cup ambazo Timu zilitoka sare zinarudiwa leo na mechi hizo ni:
-Stoke City v Man City
-Aston Villa v Crystal Palace
-Tottenham v Bolton
Washindi wa mechi za leo wanasonga Robo Fainali ya Kombe hili.
Vidic afurahi kurudi tena dimbani, Rio mashakani!
Hajacheza mechi yeyote tangu 2010 ianze kwa kuandamwa na maumivu lakini jana Beki wa Manchester United Nemnja Vidic alikuwepo uwanjani Old Trafford na kuisaidia Timu yake kifunga West Ham bao 3-0 katika mechi ya LigI Kuu.
Mwenyewe Vidic amefurahia kupona kwake na amebashiri kuwa ingawa Man United iko nyuma ya Chelsea kwenye msimamo wa Ligi lakini wao wana imani Ubingwa ni wao tena.
Ingawa Man United wanafurahia kurudi kwa Vidic lakini huenda wakamkosa tena Difenda wao mkubwa Rio Ferdinand ambae alishindwa kucheza mechi ya jana na West Ham baada ya tatizo lake la mgongo kumrudia tena na huenda akaikosa Fainali ya Kombe la Carling na Aston Villa hapo Jumapili.
Mourinho atabiri ngoma ngumu leo!!
Jose Mourinho, aliewahi kuwa Kocha wa Chelsea na sasa yuko Inter Milan, ametabiri kuwa pambano la leo ni gumu mno na halitabiriki.
Inter Milan na Chelsea leo zinakutana huko San Siro katika mechi ya kwanza ya UEFA CHAMPIONS LIGI na marudio yake ni Machi 9 huko Stamford Bridge.
Mourinho amesema licha ya yeye kuijua nje ndani Chelsea hilo haliisaidii Inter Milan kushinda mechi hiyo na akatoa mfano alipokuwa na Chelsea walicheza na FC Porto Timu yake ya zamani lakini hilo halikumsaidia kuishinda FC Porto na badala yake walishinda moja na kufungwa moja.
Vile vile Mourinho alisema Carlo Ancelotti, Kocha wa Chelsea, hanufaiki na chochote kwa kuijua Inter Milan nje ndani kwa vile tu alikaa na Wapinzani wao wakubwa AC Milan na maisha yote kuishi Italia.
Nae Ancelotti amekanusha yale madai kuwa alitoa matamshi kwamba Italia yote haitaki Mourinho na Inter Milan kushinda na akasema mechi ya Jumatano ni ngumu na haitabiriki.
LIGI KUU: Man United 3 West Ham 0
Manchester United wameinyuka West Ham mabao 3-0 katika mechi pekee ya Ligi Kuu iliyochezwa Old Trafford Jumanne usiku na kuikaribia Chelsea inayoongoza Ligi wakiwa pointi moja nyuma yao.
Bao la kwanza lilianzishwa na Park, alieingia dakika ya 19 baada ya Anderson kuumia, kumpa Berbatov aliempasia haraka Valencia pembeni nae bila kusita alitia krosi kwa Rooney aliefunga kwa kichwa dakika ya 38.
Bao la pili pia lilitokana na krosi ya Valencia kumaliziwa kwa kichwa na Rooney kwenye dakika ya 55.
Michael Owen, alieingizwa dakika ya 78, alipachika bao la 3 dakika ya 80.
Mechi inayofuata kwa Manchester United ni Fainali ya Kombe la Carling Uwanjani Wembley hapo Jumapili watakapovaana na Aston Villa.
Vikosi:
Man Utd: Foster, Neville, Brown, Vidic, Evra, Valencia, Gibson, Scholes, Anderson [Park, 19], Berbatov [Owen, 78], Rooney [Diouf, 78].
Akiba: Kuszczak, Owen, Park, Rafael, Evans, Fletcher, Diouf.
West Ham: Green, Faubert, Tomkins, Upson, Spector, Behrami [Cllison, 63], Noble, Kovac, Diamanti, Franco [Mido, 46], Cole.
Akiba: Stech, Dyer, Ilan, Mido, Da Costa, Collison, Daprela.
Refa: Alan Wiley
UEFA CHAMPIONS LIGI:
Olympiakos 0 Bordeaux 1
Stuttgart 1 Barcelona 1
Ciani aliifungia Bordeaux bao moja na la ushindi wakiwa ugenini huko Ugiriki na kuichapa Olympiakos 1-0 katika mechi ya kwanza ya UEFA CHAMPIONS LIGI.
Timu hizi zitarudiana Machi 9 huko Ufaransa.
Nao Mabingwa Watetezi Barcelona wametoka sare ya 1-1 na Stuttgart ugenini huko Ujerumani na ni Ibrahimovic aliewapa droo hiyo baada ya kusawazisha bao dakika ya 52.
Stuttgart ndio walipata bao la kwanza dakika ya 25 Mfungaji akiwa Cacau.
Timu hizi zitarudiana Uwanja wa Nou Camp nyumbani kwa Barcelona Machi 9.
EUROPA LIGI: Benfica 4 Hertha Berlin 0
Benfica wameitandika Hertha Berlin ya Ujerumani 4-0 na kusonga mbele Raundi ya Mtoano ya Timu 16 kwa jumla ya mabao 5-1.
Mabao ya Benfica yalifungwa na Oscar Cardozo, bao 2, Pablo Aimar na Javi Garcia.
Timu hizi zilitoka sare 1-1 katika mechi ya kwanza wiki iliyopita.
Benfica watacheza na mshindi kati ya FC Copenhagen au Marseille raundi ijayo.
Mechi nyingine za EUROPA LIGI zitachezwa Alhamisi ili kukamilisha jumla ya Timu 16 kwenye raundi inayofuata ya mtoano.

Tuesday 23 February 2010

Nyota wa Everton toka Bondeni abambwa akiwa njwiiii!!!
Kiungo wa Everton anaetoka Afrika Kusini Steven Pienaar amekamatwa akiendesha gari huku akiwa amelewa chakari asubuhi ya Jumapili.
Pienaar, miaka 27, aliichezea Everton Jumamosi walipoifunga Manchester United 3-1 kwenue Ligi Kuu.
Pienaar sasa atapanda kizimbani Machi 9 kujibu mashitaka dhidi yake.
Anderson njia panda Man United?
Huenda siku za Anderson kubakia Manchester United zimeanza kuhesabiki baada ya kuwa na matatizo na Meneja wake Sir Alex Ferguson kitu ambacho kimefanya Kijana huyo toka Brazil akose namba kwa Mabingwa hao.
Mechi ya mwisho kwa Anderson kuichezea Man United ni Januari 19 alipokuwemo kwenye Kikosi kilichofungwa 2-1 na Manchester City kwenye Nusu Fainali ya kwanza ya Kombe la Carling.
Inadaiwa Ferguson alimfokea Anderson kwa kucheza chini ya kiwango katika mechi hiyo na akamtema katika mechi iliyofuata Man United waliyocheza na Hull City na hilo likamkasirisha Anderson alietimkia kwao Brazil bila ruhusa ya Klabu.
Si Anderson wala Ferguson waliozungumza chochote kuhusu madai hayo ya mfarakano kati yao ila mwenyewe Anderson amesisitiza yeye matumaini yake bado yapo Man United na anachotaka ni namba ya kudumu ili Kocha Dunga wa Brazil amchukue kwenye Kombe la Dunia.
SKANDALI LA TERRY: Bridge & Terry si tatizo kuwa England!!!
Mmoja wa Wasaidizi wa Kocha wa England Fabio Capello, Stuart Pearce anaamini kuwa hakutakuwa na tatizo lolote kwa John Terry na Wayne Bridge kuichezea England pamoja baada ya Terry kukumbwa na kashfa ya kutangazwa kutembea na gelfrendi wa Bridge sakata ambalo limemfanya Capello amtimue Unahodha wa England.
Capello anategemewa kutangaza Kikosi cha England kitakachocheza mechi ya kirafiki na Misri Jumatano ijayo wikiendi hii na Wachezaji hao wawili huenda wakawemo.
Uteuzi wa Wayne Bridge kwa England ni kitu kisichoepukika hasa kwa vile Beki wa kushoto wa kutumainiwa Ashley Cole ni majeruhi.
Hata hivyo Wachezaji hao wanaweza wakakutana Uwanjani kabla ya kuwa Kikosi cha England kwa vile Klabu ya Terry Chelsea itacheza na Klabu ya Bridge Manchester City Jumamosi huko Stamford Bridge kwenye Ligi Kuu.
Stuart Pearce amesisitiza kuwepo pamoja Wachezaji hao si tatizo kwani kuichezea England ni kitu muhimu sana kuliko ubinafsi na wote, Terry na Bridge, ni Wachezaji thabiti wa kulipwa wanaoheshimu maadili ya kazi yao.
LIGI KUU LEO: Man United v West Ham
Leo saa 5 usiku, saa za bongo, Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu, Manchester United watajimwaga uwanjani nyumbani Old Trafford kuivaa West Ham katika mechi pekee ya Ligi Kuu.
Katika mechi yao ya mwisho ya Ligi, Man United walifungwa na Everton huko Goodison Park mabao 3-1.
West Ham walishinda mechi yao ya mwisho walipoipiga Wigan bao 3-0.
Leo Man United huenda wakawa na Madifenda wao wa kati, Rio Ferdinand na Nemanja Vidic, ambao hawajacheza pamoja kwa vile wote walikuwa majeruhi lakini Ferdinand alipopona na kucheza mechi yake ya kwanza akaadhibiwa na kufungiwa mechi.
Katika mechi yao ya kwanza ya Ligi huko Upton Park, Man United ilishinda bao 4-0.
Vikosi leo vitatokana na:
Man United: Van der Sar, Neville, Brown, Rafael, Ferdinand, Vidic, Evans, Fabio, Park, Anderson, Valencia, Carrick, Scholes, Fletcher, Obertan, Gibson, Rooney, Owen, Berbatov, Diouf
West Ham: Green, Stech, Spector, Faubert, Upson, Tomkins, Da Costa, Daprela, Parker, Behrami, Kovac, Collison, Noble, Diamanti, Stamislas, Cole, Mido, Ilan, Franco, McCarthy
Refa: Alan Wiley
Ancelotti achochea mechi ya Inter Milan v Chelsea
Meneja wa Chelsea Carlo Ancelotti amechochea moto mbele ya pambano lao na Inter Milan huko San Siro, Milan, Italia la hapo kesho la UEFA CHAMPIONS LIGI kwa kudai kuwa Italia yote inataka Jose Mourinho ashindwe.
Mvutano wa Mourinho na Anceotti ni wa tangu Ancelotti alipokuwa Bosi AC Milan ambao ni Mahasimu wakubwa wa Inter Milan.
Mourinho ana uhusiano mbovu na Makocha wengine wa Klabu za Serie A pamoja na Viongozi wa Chama cha Soka cha Italia kufuatia kubatuka ovyo kwake na hilo limempa kichwa Carlo Ancelotti adai Italia nzima inataka Mourinho na Timu yake Inter Milan washindwe.
Ancelotti ameliambia Gazeti moja la Italia kuwa ‘Italia yote, ukiondoa Mashabiki wa Inter Milan, watakuwa wakiisapoti Chelsea hapo kesho!’
Ancelotti pia amemponda Mourinho kwa kujigamba kuwa alipoondoka yeye Chelsea hamna mtu alieleta Kikombe huko Stamford Bridge.
Ronaldo wa Brazil kung’atuka 2011
Ronaldo ametangaza kuwa mwakani atastaafu kucheza soka.
Ronaldo, ambae ameshanyakua Kombe la Dunia mara mbili akiwa na Brazil, amesema: “Nishaamua- miaka hii miwili ni ya mwisho!”
Ronaldo, miaka 33, kwa sasa anachezea Soka lake huko kwao Brazil akiwa na Klabu ya Corinthians na pia ameshachezea Klabu za Ulaya kama vile PSV Eindhoven, Barcelona, Inter Milan, Real Madrid na AC Milan.
Ameichezea Timu ya Brazil mara 97 na kufunga bao 62 na kunyakua nayo Kombe la Dunia mwaka 1994 na 2002.
Katika Fainali za Kombe la Dunia yeye ndie mwenye rekodi ya kufunga bao nyingi na ana jumla ya mabao 15.
Ronaldo ameshashinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa FIFA mwaka 1996, 1997 na 2002. Ameshinda Ballon D’or, Tuzo inayoashiria Mchezaji Bora Ulaya, mwaka 1997 na 2002.
Ronaldo katika miaka ya hivi karibuni amekuwa na matatizo makubwa ya kuumia hasa goti na pengine hilo ndilo limemfanya aamue kujiuzulu.
ISHARA YA PINGU YAMPA KIFUNGO MOURINHO
Jose Mourinho, Meneja wa Inter Milan, amefungiwa mechi 3 na kutwangwa faini ya Euro 40,000 kufuatia kitendo chake cha kutoa ishara ya pingu kwa mikono yake katika mechi ya Ligi Serie A ya Jumamosi waliyotoka sare 0-0 na Smpdoria na ambayo Wachezaji wa Inter Milan wawili walitolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Mabeki wa Inter Walter Samuel na Ivan Cordoba walipotolewa ndipo Mourinho akatoa ishara ya pingu akionyesha Timu yake inaonewa na Marefa.
Kitendo hicho cha pingu kinafuata kauli yake aliyoitoa siku moja kabla ya mechi hiyo ya Jumamosi aliposema: “Hapa Italia kuna Timu moja yenye eneo la penalti refu kupita nyingine!”
Mreno huyo alikuwa akiimaanisha Juventus wakati Fowadi wao Alessandro Del Piero alipochezewa rafu nje ya boksi na ikatolewa penalti. Mourinho amekuwa akisakamwa sana huko Italia kwa kauli na vitendo vyake.
Kifungo cha Mourinho kitamfanya azikose mechi za Serie A dhidi ya Udinese, Genoa na Catania na Wachezaji wake Sulley Muntari na Cambiasso wamefungiwa mechi 2 kila mmoja kwa rabsha kwenye mechi hiyo hiyo na Sampdoria iliyomfunga Mourinho.
Wachezaji, Samuel na Cordoba, kwa Kadi Nyekundu katika mechi hiyo watakosa mechi moja.
Inter Milan bado wapo kileleni mwa Ligi kwa pointi 5 mbele ya AS Roma.
TATHMINI: UEFA CHAMPIONS LEAGUE
[mechi zote saa 4 dak 45 usiku isipokuwa inapotajwa]
Jumanne, Februari 23
Stuttgart v Barcelona
Olympiakos v Bordeaux
Jumatano, Februari 24
CSKA Moscow v Sevilla [saa 2 na nusu usiku]
Inter Milan v Chelsea
Hii ni wiki ya pili ya mechi za UEFA CHAMPIONS LIGI baada ya mechi 4 za wiki iliyopita za Raundi ya Mtoano ya Timu 16.
Bila shaka, Bigi Mechi ya wiki hii ni ile ya San Siro kati ya Inter Milan na Chelsea ambayo wengi wameibatiza Mourinho v Chelsea kwa vile tu Meneja wa Inter Milan Jose Mourinho alikuwa Bosi wa Chelsea kabla ya kuhamia Inter Milan.
Timu hizo, Inter Milan na Chelsea, hazijawahi kukutana kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI lakini Mameneja wao wanazijua Timu pinzani vilivyo huku Mourinho akiijua Chelsea nje ndani na Carlo Ancelotti lazima ataijua Inter Milan kwa vile tu alikaa misimu minane kwa Wapinzani wa Inter, AC Milan.
Chelsea na Inter ndizo zinazoongoza Ligi zao kwa sasa.
Inter Milan msimu uliokwisha waling’olewa kwenye hatua hii ya UEFA na Manchester United walipopigwa jumla ya bao 2-0.
Mabingwa Watetezi wa UEFA CHAMPIONS LIGI, Barcelona watakuwa Ujerumani kucheza na Stuttgart bila ya Wachezaji Mabeki Eric Abidal na Dani Alves na Viungo Xavi Hernandez na Syedou Keita walio majeruhi.
Wakati Barcelona ndio wanaongoza Ligi yao La Liga, Stuttgart wanaelea katikati kwenye msimamo wa Bundesliga ingawa mechi yao ya juzi waliishindilia Cologne bao 5-1.
Kwenye mechi na Barcelona, Stuttagrt wakiongozwa na Kocha Christian Goss watawakosa Wachezaji wao Ciprian Marica, Arthur Boka na Sami Khedira.
Bordeaux, ambao wako ugenini huko Ugiriki kucheza na Olympiakos, wanaingia kwenye mechi hii ya Jumanne wakiwa na rekodi nzuri kwenye mechi zao za Makundi za Mashindano haya pale waliposhinda mechi 5, sare moja na kufungwa goli 2 tu.
Olympiakos sasa wako chini ya Kocha Bozidar Bandovic aliechukua hatamu toka kwa Zico wa Brazil na wao walimaliza mechi zao za Makundi wakiwa nyuma ya Arsenal na walishinda mechi zao zote za nyumbani bila kufungwa hata goli moja.
CSKA Moscow hawajacheza hata mechi moja tangu Novemba msimu wa Ligi ya Urusi ulipomalizika na wanawakaribisha Sevilla Jumatano.
Hata hivyo, pengine silaha kubwa ya CSKA kwenye mechi hii na Sevilla ni baridi kali itakayowakumba Sevilla.
Katika msimu wa Ligi ya Urusi uliokwisha Novemba, CSKA wamemaliza Ligi hiyo wakiwa nafasi ya 5.
Kwenye Makundi ya Mashindano haya, CSKA walimaliza nyuma ya Manchester United na kuzipiku Wolfsburg na Besiktas.

Monday 22 February 2010

Mourinho, Chelsea hawana siri!!
Jose Mourinho anajiamini anajua jinsi Chelsea itakavyocheza siku watakapokutana na Timu yake ya sasa Inter Milan kwenye mpambano wa UEFA CHAMPIONS LIGI hapo Jumatano ijayo Februari 24 Uwanjani San Siro.
Hivi karibuni, Mourinho alikwenda Stamford Bridge kuishuhudia Chelsea ilipocheza mechi ya Ligi Kuu na Fulham na kushinda 2-1.
Mourinho, aliekuwa Meneja wa Chelsea kwa miaka mitatu na kushinda Vikombe vitano kabla kuondoka Septemba 2007, amedai hakuna kitu kilichobadilika tangu aondoke.
Mourinho amedai: “Nilipokwenda Stamford Bridge nilitazama kila kitu! Kabla ya mechi bado wanapasha miili joto kama walivyokuwa wakifanya walipokuwa chini yangu! Niliona wakijihami kutoka frikiki kama vile tulivyokuwa tukifanya! Mara nyingine hucheza fomesheni ya 4-4-2 yenye umbo la almasi wakishambulia, mara nyingine 4-3-3 na hiyo ni sawa kabisa na mifumo tuliyokuwa tukitumia!”
Mourinho ameendelea kudai kuwa kwa vile Ancelotti amebakisha vitu vingi alivyokuwa akifanya yeye bila kuleta mabadiliko makubwa ndio maana Timu imetulia na ina mafanikio kwa sasa.
Mourinho ameongeza kwa kusema Chelsea haina siri kwake na Timu ina watu wapya Anelka na Ivanovic tu na waliobaki kina Cech, Carvalho, Terry, Cole, Essien, Mikel, Drogba, Malouda, Joe Cole na Kalou ni Vijana wake.
Mourinho ametamka: “Chelsea hawana siri kwangu! Mimi kama Kocha sina siri kwao!”
Je Mourinho na Chelsea ya Ancelotti nani mbabe?
Mancini ataka Tevez arudi haraka kuokoa jahazi!!
Carlos Tevez ambae yuko kwao Argentina kwa matatizo ya kifamilia kwa siku 9 sasa na kuzikosa mechi 3 za Timu yake Manchester City ametakiwa arudi haraka na Bosi wake Roberto Mancini ili kuokoa jahazi.
Man City jana walitoka suluhu 0-0 na Liverpool kwenye Ligi Kuu na kukosekana kwa Carlos Tevez kulionekana wazi wazi kwenye mechi hiyo.
Jumatano, Man City wanarudiana na Stoke City kwenye mechi ya Raundi ya 5 ya FA Cup na Jumamosi wana kindumbwendumbwe na Chelsea huko Stamford Bridge kwenye Ligi Kuu.
Man City kwa sasa wako nafasi ya 5 kwenye Ligi Kuu na wanapigania nafasi ya 4 ili wafuzu kucheza UEFA msimu ujao lakini zipo Timu 4 zilizotenganishwa na pointi moja tu zinazogombea nafasi hiyo.
Timi hizo ni:
-Tottenham [walio nafasi ya 4] wana pointi 46 [kwa mechi 27]
-Man City pointi 46 [mechi 26]
-Liverpool pointi 45 [mechi 27]
-Aston Villa pointi 45 [mechi 26]
Mancini amekiri kumkosa Tevez ni matatizo makubwa kwao na wanapigana kumrudisha haraka Manchester ili angalau awahi mechi ya Jumamosi na Chelsea.
Owen akata tamaa kuitwa Kombe la Dunia!!
Straika wa Manchester United Michael Owen ameanza kukata tamaa kuhusu kuwemo kwenye Kikosi cha England cha Fainali za Kombe la Dunia.
Owen, miaka 30, amesema: “Ni muda mrefu tangu nichezee England. Huwezi kukata tamaa kuchezea tena lakini inaelekea nafasi yangu ni finyu!”
Wakati Kocha wa England Fabio Capello amekuwa akitilia mkazo kwamba Wachezaji wa England ni wale fiti tu na wanaocheza kila mara Kikosi cha kwanza cha Klabu zao, Owen ameweza kuanza mechi 5 tu za Klabu yake Man United za Ligi Kuu na kufunga goli 2 na amefunga bao 5 katika mechi nyingine.
Mechi pekee Owen aliyocheza na kutia fora ni ile ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE alipofunga bao zote 3 katika ushindi wa Man United wa 3-1 dhidi ya Wolfsburg.
England watacheza mechi ya kirafiki Machi 3 na Misri huko Wembley na Capello atateua Kikosi chake wikiendi hii inayokuja.
Pia Capello anatakiwa ateue Kikosi cha awali cha Kombe la Dunia cha Wachezaji 35 kabla ya Mei 12 na ikifika Juni 1 Kikosi cha watu 23 lazima kifikishwe FIFA tayari kwa Fainali za Kombe la Dunia zinazoanza Juni 10 huko Afrika Kusini.
Capello pia anakabiliwa na utata mkubwa kuhusu uteuzi wa Mchezaji Wayne Bridge ambae ndie mrithi wa wazi wa Beki wa kushoto Ashley Cole alie majeruhi lakini kuna skandali kubwa la John Terry alievuliwa Unahodha wa England kwa kashfa ya kutembea na gelfrendi wa Wayne Bridge.
Je wawili hao, Terry na Bridge, wanaweza kucheza pamoja Difensi ya England?
KANDANDA LA WIKI:
Jumanne, Februari 23
LIGI KUU
[saa 5 usiku]
Man United v West Ham
UEFA CHAMPIONS LIGI
Olympiakos v Bordeaux
VfB Stuttgart v Barcelona
EUROPA LIGI
Benfica v Hertha Berlin
Jumatano, 24 Februari 2010
UEFA CHAMPIONS LIGI
CSKA Moscow v Sevilla
Inter Milan v Chelsea
Alhamisi, Februari 25
EUROPA LIGI:
Sporting Lisbon v Everton
Hapoel Tel aviv vFC Rubin Kazan
Juventus vAjax
Valencia v Club Brugge
Wolfsburg v Villareal
Red Bull Salzburg v Standard Liege
Werder Bremen v FC Twente
Fenerbahce v Lille
Anderlecht v Athletic de Bilbao
Olympique de Marseille v FC Kobenhavn
AS Roma v AS Roma
Galatasaray vAtletico de Madrid
Shakhtar Donetsk v Fulham
FC Unirea Urziceni v Liverpool
PSV Eindhoven v Hamburger SV
Jumamosi, February 27
LIGI KUU
[saa 9 dak 45 mchana]
Chelsea v Man City
[saa 12 jioni]
Birmingham v Wigan
Bolton v Wolves
Burnley v Portsmouth
[saa 2 na nusu usiku]
Stoke v Arsenal
Jumapili, Februari 28
LIGI KUU
[saa 10 jioni]
Tottenham v Everton
[saa 12 jioni]
Liverpool v Blackburn
Sunderland v Fulham
FAINALI CARLING CUP
[saa 12 jioni]
Manchester United v Aston Villa
KWINGINEKO ULAYA: Matokeo Jumapili
LA LIGA
Jumapili, Februari 21
Real Madrid 6 Villareal 2
Osasuna 1 Valladolid 1
Malaga 2 Espanyol 1
Athletic Bilbao 4 Tenerife 1
Real Zaragoza 1 Sporting Gijon 3
SERIE A
Jumapili, Februari 21
Atalanta 0 Chievo 1
Bologna 1 Juventus 2
Palermo 3 Lazio 1
Fiorentina 2 Livorno 1
Bari 0 AC Milan 2
Siena 0 Napoli 0
Palermo 3 Parma 0
BUNDESLIGA
Jumapili, Februari 21
Freiburg 0 Hertha Berlin 3
Wolfsburg 2 Schalke 1
Werder Bremen 2 Bayer Leverkusen 2
Spurs wachukua nafasi ya 4
Tottenham Hotspurs, wakicheza ugenini Uwanja wa DW uliokuwa kama zizi la ng'ombe kwa jinsi ulivyojaa tope katikati kwa mvua kubwa, waliwafunga wenyeji wao Wigan bao 3-0 na kuchukua nafasi ya 4 kwenye Ligi Kuu sasa wakiwa na pointi 46 sawa na Manchester City lakini Spurs wana goli bora.
Nafasi za 5 hadi za 7 ni za Man City [pointi 46], Liverpool [pointi 45] na Aston Villa [pointi 45].
Jermaine Defoe ndie aliefungua kitabu cha Spurs kwa kuandika bao dakika ya 27 ingawa alionekana kuwa 'maili' moja ofsaidi.
Kipindi cha pili, Defoe alitolewa na kuingizwa Mrusi Roman Pavlyuchenko, ambae anadaiwa kutaka kuihama Spurs, na huyu ndie aliewaua kabisa Wigan pale alipopachika bao 2.
MECHI INAYOKUJA LIGI KUU:
Jumanne, Februari 23 [saa 5 usiku saa za bongo]
Man United v West Ham

Sunday 21 February 2010

Man City, Liverpool ngoma ngumu!!
Manchester City na Liverpool leo zimeshindwa kupata mbabe katika mechi ya Ligi Kuu iliyochezwa Uwanja wa City of Manchester walipotoka suluhu 0-0.
Mechi hii muda mwingi ilichezwa katikati na Makipa wote hawakupata hekaheka kubwa katika dakika zote 90.
Washabiki wa Liverpool watapata furaha kidogo baada ya kumuona Straika wao wa kutegemewa Fernando Torres akiingizwa mwishoni baada ya kutoonekana kitambo kutokana na kuwa majeruhi.
Vile vile Mchezaji mwingine wa Liverpool wa kutumainiwa, Yossi Benayoun, aliekuwa nje kwa muda sasa kwa tatizo la kuvunjika mbavu leo aliingizwa kipindi cha pili na hilo nalo litaleta faraja huko Anfield.
Nao Mashabiki wa Man City watakuwa wakiomba Straika wao Carlos Tevez arudi haraka kutoka kwao Argentina alikokwenda kwa matatizo ya kifamilia kwani Fowadi yao ilikosa kabisa uhai wa kuleta mikikimikiki ya kutafuta goli kama afanyavyo Tevez.
Fulham 2 Birmingham 1
Katika dakika ya 3 tu ya mchezo, Fulham wakiwa nyumbani Craven Cottage, walijikuta wako nyuma kwa bao walilojifunga wenyewe kupitia Mchezaji wao Baird.
Hadi mapumziko Fulham 0 Birmongham 1.
Kipindi Damien Duff alifumua shuti kwa guu lake la kushoto na kutingisha nyavu ikiwa ni dakika ya 59 na hivyo kufanya Fulham wawe sare.
Katika dakika ya 90, frikiki ya Bobby Zamora ilitinga na kuipa ushindi Fulham wa bao 2-1.
Timu hizi Fulham na Birmingham zimefungana zote zikiwa na pointi 37 lakini Fulham wako nafasi ya 9 na Birmingham wako ya 10 kwa ubora wao wa magoli.
Villa yaitandika Burnley 5-2
Ndani ya Villa Park, Aston Villa wameichabanga Burnley 5-2 katika mechi ya pili ya Ligi Kuu leo Jumapili.
Burnley ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao baada ya gonga zao tamu kuichana difensi ya Villa na Fletcher kufunga kirahisi.
Villa walisawazisha kwa bao la Ashley Young ambalo shuti lake lilipenya katikati ya miguu ya Madifenda wa Burnley na kuparaza miguu yao na kutikisa wavu.
Hadi mapumziko bao zilikuwa 1-1.
Ndipo kipindi cha pili mvua ya magoli ikaanguka kwa bao 2 za haraka za Stewart Downing na kuifanya Villa iwe mbele 3-1.
Emile Heskey akafunga la 4 na Agbonlahor akapachika bao la 5 huku Paterson akiifungia Burnley bao lao la pili.
Van der Sar kurefusha mkataba
Kipa wa Manchester United Edwin van der Sar atasaini mkataba mpya utakaomuweka Old Trafford hadi 2011 baada ya mkataba wake wa sasa kumalizika mwishoni mwa msimu huu.
Van der Sar, miaka 39, amesema: “Nataka kuendelea kucheza hivyo ntasaini mkataba mpya. Klabu inataka nibaki na nina furaha hapa. Bado niko fiti!”
Kipa huyo ambae aliwahi kuzichezea Ajax na Juventus amekuwa na msimu mgumu safari hii na kuzikosa baadhi ya mechi kwanza alipoumia kidole halafu goti na wakati huo huo Mkewe akaugua ghafla na ikabidi arudi kwao Uholanzi kumuuguza.
Blackburn 3 Bolton 0
Katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu leo Jumapili, Blackburn wameipiga Bolton mabao 3-0 huku barafu ikidondoka mtindo mmoja kipindi cha pili.
Blackburn walipata bao la kwanza kabla ya haftaimu mfungaji akiwa Nicola Kalinic baada ya kupokea pasi toka kwa Junior Hoilett.
Kipindi cha pili Jason Roberts na Gael Givet waliongeza mabao ya Blackburn na kuifikisha nafasi ya 12 wakiwa na pointi 34.
Bolton wako nafasi ya pili toka mkiani wakiwa na pointi 23.
Maskini Pompey!!
Waliongoza 1-0 kwa bao la Piquionne dakika ya 35 lakini Portsmouth, Timu iliyo matatizoni nje na ndani ya uwanja wakikabiliwa na ukata na wako mkiani kwenye Ligi Kuu, ilijikuta ikitandikwa 2-1 nyumbani kwao Fratton Park hapo jana Jumamosi kwenye mechi ya Ligi.
Robert Huth aliisawazishia Stoke City dakika ya 50 na Stoke wakapata pigo pale Mchezaji wao Andy Wilkinson alipopewa Kadi mbili za Njano na hivyo kutolewa kwa Kadi Nyekundu lakini ni wao walioshinda baada ya Mchezaji wao wa akiba Salif Diao kupachika bao la pili dakika ya 91.
Kwa ushindi huo, Stoke wako nafasi ya 11 wakiwa na pointi 34 na Portsmouth bado wako nafasi ya 20 ikiwa ya mwisho na wana pointi 16 tu.
KWINGINEKO ULAYA: Matokeo
BUNDESLIGA
Ijumaa, Februari 19
1899 Hoffenheim 2 v Borussia Moenchengladbach 2
Jumamosi, Februari 20
Nurnberg 1 v Bayern Munich 1
Borussia Dortmund 4 v Hannover 1
Hamburg 0 v Eintracht Frankfurt 0
Mainz 05 0 v Bochum 0
Cologne 1 v Stuttgart 5
SERIE A
Jumamosi, Februari 20
Inter Milan 0 v Sampdoria 0
Genoa 3 v Udinese 0
LA LIGA
Jumamosi, Februari 20
Deportivo La Coruna 2 v Xerez 1
Real Mallorca 1 v Sevilla 3
Barcelona 4 v Racing Santander 0
Powered By Blogger