Saturday 20 February 2010

Fergie: “Tumepigwa vibaya!!”
Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson mara baada ya Timu yake kupokea kipigo cha mabao 3-1 huko Goodison Park toka kwa Everton amekubali Timu yake imetandikwa vibaya na inawasikitisha.
Ferguson alisema: “Tumepigwa vibaya, huo ndio ukweli! Imenisikitisha na Wachezaji wanasikitika! Wao ni binadamu na wanachezea Manchester United na hawapendi kufungwa! Lakini tumefungwa hapa!”
Nae Meneja wa Everton David Moyes amedai kuwa sasa Everton haiogopi mtu na inaweza kuifunga Timu yeyote.
Katika mechi mbili mfululizo, Everton imezifunga Timu za juu za Ligi Kuu baada ya kuitandika Chelsea 2-1 na kisha Man United 3-1.
Everton wako nafasi ya 8 kwenye msimamo wa Ligi na wana pointi 38.
Chelsea ndie anaeongoza akiwa na pointi 61, Man United wa pili pointi 57 na Arsenal ni wa 3 akiwa na pointi 55.
Arsenal 2 Sunderland 0
Uwanjani Emirates Arsenal imeifunga Sunderland bao 2-0 na kujichimbia nafasi ya 3 kwenye Ligi Kuu wakiwa pointi mbili nyuma ya Manchester United.
Bao la kwanza la Arsenal lilifungwa kipindi cha kwanza na Nicklas Bendtner na la pili alifunga Nahodha Fabregas kwa penalti kwenye dakika za majeruhi.
Vikosi vilivyoanza:
Arsenal: Almunia, Eboue, Silvestre, Vermaelen, Clichy, Song, Walcott, Fabregas, Ramsey, Nasri, Bendtner.
Akiba: Fabianski, Sagna, Rosicky, Vela, Denilson, Traore, Campbell.
Sunderland: Gordon, Hutton, Mensah, Turner, McCartney, Campbell, Cana, Ferdinand, Richardson, Bent, Jones.
Akiba: Carson, Bardsley, Zenden, Malbranque, Da Silva, Kilgallon, Mwaruwari.
Refa: Steve Bennett
Wolves 0 Chelsea 2
Mabao mawili ya Didier Drogba, moja kila kipindi, yameipa Chelsea ushindi wa bao 2-0 ugenini na kuzidi kupaa kileleni mwa Ligi Kuu sasa wakiwa pointi 4 mbele ya Timu ya pili Manchester United waliofungwa 3-1 na Everton katika mechi yao ya leo iliyoisha mapema.
Vikosi vilivyoanza:
Wolves: Hahnemann, Zubar, Craddock, Berra, Ward, Foley, Guedioura, Henry, David Jones, Jarvis, Doyle.
Akiba: Hennessey, Elokobi, Ebanks-Blake, Halford, Vokes, Milijas, Mujangi Bia.
Chelsea: Cech, Paulo Ferreira, Ivanovic, Terry, Zhirkov, Joe Cole, Mikel, Ballack, Anelka, Drogba, Malouda.
Akiba: Hilario, Kalou, Sturridge, Matic, Bruma, Kakuta, Borini.
Refa: Kevin Friend
West Ham 3 Hull City 0
Wakiwa nyumbani Uptown Park, West Ham wameweza kujikakamua na kuifunga Timu inayosuasua Hull City bao 3-0 na hivyo kupanda kwenye msimamo wa Ligi sasa wakiwa nafasi ya 13 na wana pointi 27.
Hull City wako nafasi ya 17 na wana pointi 24.
Mabao ya West Ham yalifungwa na Behrami, Carlton Cole na Julien Faubert.
RATIBA Ligi Kuu: Jumapili, Februar 21 [saa za bongo]
[saa 11 jioni]
Aston Villa v Burnley
[saa 12 jioni]
Fulham v Birmingham]
Man City v Liverpool
[saa 1 na robo usiku]
Wigan v Tottenham
Droo Kombe la Mataifa Afrika 2012 tayari!!
Katika Droo iliyofanyika leo, Bongo imepangwa Kundi la 4 pamoja na Algeria, Morocco na Jamhuri ya Afrika ya Kati katika mechi za mtoano kupata Timu zitakazocheza Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2012 zitakayofanyika katika Nchi za Gabon na Equatorial Guinea ambao watakuwa Wenyeji wa pamoja.
Makundi yapo 11 na Mshindi wa kila Kundi pamoja na Timu za pili 3 za Makundi zilizo na matokeo bora ndizo zitajumuika na Wenyeji hao wawili katika Fainali hizo na kufanya jumla ya Nchi 16.
Togo haikuwekwa kwenye Droo hiyo kwani inatumikia kifungo cha kutokucheza Mashindano mawili ya Kombe hilo walichopewa na CAF kwa kujitoa Fainali zilizochezwa mwezi Januari huko Angola.
Togo, waliojitoa baada ya Basi lao kupigwa risasi na kuuliwa watu watatu, wamekata rufaa Mahakama ya Usuluhishi Michezoni ambayo imeshaiambia CAF kuwa endapo Togo watashinda rufaa yao itabidi waingizwe kwenye michuano ya Afrika.
Mechi hizi za Makundi zitaanza Septemba mwaka huu.
MAKUNDI:
KUNDI 1: Mali, Cape Verde Islands, Zimbabwe, Liberia
KUNDI 2: Nigeria, Guinea, Ethiopia, Madagascar
KUNDI 3: Zambia, Mozambique, Libya, Comoros Islands
KUNDI 4: Algeria, Morocco, Tanzania, Central African Republic
KUNDI 5: Cameroon, Senegal, DR Congo, Mauritius
KUNDI 6: Burkina Faso, Gambia, Namibia, Mauritania
KUNDI 7: Egypt, South Africa, Sierra Leone, Niger
KUNDI 8: Ivory Coast, Benin, Rwanda, Burundi
KUNDI 9: Ghana, Congo, Sudan, Swaziland
KUNDI 10: Angola, Uganda, Kenya, Guinea Bissau
KUNDI 11: Tunisia, Malawi, Chad, Botswana
Man United yakung’utwa 3-1!
Baada ya kuipiga Chelsea 2-1 mechi iliyopita, leo Eveton imeitandika Manchester United 3-1 katika mechi ya Ligi Kuu.
Man United ndio walikuwa wa kwanza kufunga bao dakika ya 16 mfungaji akiwa Berbatov lakini Everton walisawazisha dakika 3 baadae kwa kigongo cha Bilyaletdinov.
Hadi mapumziko bao zilikuwa 1-1.
Everton walipata bao la pili kupitia Gosling alieingizwa kipindi cha pili na la tatu lilifungwa na Rodwell ambae pia aliingia kipindi cha pili.
Manchester United wanabaki nafasi ya pili nyuma ya Chelsea.
Vikosi vilivyoanza:
Everton: Howard, Baines, Heitinga, Distin, Neville, Bilyaletdinov, Donovan, Arteta, Pienaar, Osman, Saha.
Akiba: Nash, Yobo, Coleman, Gosling, Rodwell, Vaughan, Yakubu.
Man United: Van der Sar, Neville, Evra, Brown, Evans, Park, Carrick, Fletcher, Valencia, Berbatov, Rooney.
Akiba: Foster, Vidic, Rafael, Scholes, Gibson, Owen, Obertan
Refa: Howard Webb
LIGI KUU yaikata maini Pompey!!!
Ligi Kuu England imelikataa ombi la Portsmouth la kutaka kuruhusiwa kuuza Wachezaji licha ya Dirisha la Uhamisho kufungwa.
Portsmouth, wenye matatizo makubwa kifedha na Machi 1 wako Mahakamani wakitaka kufilisiwa na Mamlaka ya Kodi kwa kutokulipa Kodi, walitoa ombi hilo maalum ili haraka wapate fedha kukabiliana na kesi hiyo.
Inasadikiwa Portsmouth wana deni la Pauni Milioni 60.
Ingawa inaaminika FA na FIFA zilikuwa tayari kulikubali ombi la Portsmouth ili kukwepa madhara ya kufilisiwa kwa Portsmouth, Ligi Kuu ambayo ndiyo inaiendesha Ligi hiyo England imelikataa ombi hilo na imesema imetafakari kila kitu na imeona huu si muda muafaka kuwaruhusu Portsmouth kuuza Wachezaji.
Kwa mwaka kuna Madirisha mawili ya Uhamisho yanayotambulika na FIFA nayo ni lile la Januari 1 hadi 31 na la pili lile la Juni 1 hadi Agosti 31.
Washabiki Man United wapinga kina Glazer!!!
• Wavaa Kijani na Dhahabu ishara ya upinzani!!
Hivi karibuni katika kila mechi ya Manchester United, rangi za kijani na dhahabu zimekuwa zikionekana miongoni mwa Washabiki wa Klabu hiyo na hizi ni rangi za Klabu ya Newton Heath iliyoanzishwa mwaka 1878 na hapo tarehe 26 Aprili 1902 kubadilishwa jina kuitwa Manchester United na rangi kuwa nyekundu, nyeusi na nyeupe.
Newton Heath ilianzishwa na Wafanyakazi wa Depo iliyokuwepo Newton Heath la Reli ya Lancashire na Yorkshire..
Mwaka 2005 Familia ya Matajiri kutoka Florida Marekani iitwayo Glazer iliinunua Manchester United na kuiingiza kwenye deni kubwa ambalo, ingawa Menejimenti ya Klabu inadai hilo deni ni kitu cha kawaida na uwezo wa kulilipa upo, Washabiki hawapendeziwi nalo na wameanzisha upinzani mkubwa kwa Familia ya Glazer.
Ndio maana Mashabiki, kwenye mechi za Manchester United, wanavaa skafu, fulana na kofia rangi za kijani na dhahabu ikiwa ni alama ya chimbuko la Manchester United, Klabu ya Newton Heath iliyoanzishwa na Wafanyakazi makabwela wa Depo ya Reli.
Nje ya Uwanja wa Old Trafford fulana za rangi hiyo ya kijani na dhahabu huuzwa huku nyuma zina maandishi [Shairi la Kiingereza] na tafsiri ya haraka ni:
“Roho ya United haiuzwi, Ndio maana kwa fahari tunavaa Kijani na Dhahabu,
Hatutavaa ile Jezi Nyekundu inayosifika, Mpaka Glazer waondoke au wafe,
Hivyo inua viwango vya zamani juu, Kwa Kijani na Dhahabu tutaishi na kufa,
Na hakika siku itafika tena, Tutakapovaa Nyekundu yetu kwa mara nyingine tena!”
Upinzani huu wa Washabiki umepamba moto na sasa kuna habari kwamba kuna Kikundi cha Matajiri ambao ni Mashabiki wa Manchester United wameanzisha umoja ili kuing’oa Klabu hiyo mikononi mwa Familia ya Glazer.
Matajiri hao wanafanya mikakati na kukusanya uwezo ili kuinunua Klabu hiyo.
Nae Sir Alex Ferguson, Meneja wa Manchester United, akizungumzia sakata hilo la Mashabiki amesema anaelewa uchungu wa Mashabiki ingawa amekiri wale walio madarakani wanafanya kila lililo sahihi kwa maendeleo ya Klabu hiyo.
Inasemekana Mashabiki wanajikusanya ili kufanya maandamano huku kila mtu akivaa kijani na dhahabu kabla ya mechi ya Machi 10 ya marudiano ya UEFA CHAMPIONS LIGI na AC Milan Uwanjani Old Trafford.
Ferguson amesema: “Hilo halinihusu. Hatujali wanavaa rangi gani kwani wote bado wanaisapoti Timu moja tu! Hili linaonyesha Mashabiki wana uchungu na Timu yao!”
Ferguson ameongeza: “Kila Shabiki ana haki ya kulalamika kwa kile wanachoona ni haki lakini inabidi na sie tuiendeshe Klabu kwa njia sahihi. Misingi ya Klabu hii bado ni mizuri! Tuna Timu ya Vijana nzuri na Timu ya kwanza inafanya vizuri sana! Sisi tunaendelea na upande wa soka na wao waendelee tu mradi hawaathiri Timu.”
Wenger kulikwaa rungu la UEFA?
Huenda Meneja wa Arsenal Arsene Wenger akazivaa hasira za UEFA baada ya kumshambulia Refa Martin Hansson aliechezesha mechi yao ya UEFA CHAMPIONS LIGI waliyofungwa na FC Porto bao 2-1 Jumatano huko Ureno kwa kuikubali frikiki tata ya FC Porto iliyozaa bao la ushindi.
Refa Martin Hansson si mgeni kwa migogoro kwani ndie Refa ‘alieibeba’ Ufaransa kuingia Fainali za Kombe la Dunia pale alipogeuka ‘kipofu’ wakati Thierry Henry akiukontroli mpira kwa mkono na kumpasia William Gallas aliesawazisha bao na kuwang’oa Ireland.
Arsene Wenger amemwita Refa huyo hana uwezo wa kuchezesha na hilo linaweza kumtia matatani na UEFA na huenda akashitakiwa na kufungiwa.
Wenger amesema: “Naaminini Refa pengine hana uwezo au si mwaminifu. Lakini ningependa kuamini hana uwezo. Utachukuaje mpira na kumpa Mchezaji na kisha kumwambia funga goli?”
Wenger amedai Refa huyo katika maamuzi yake kuhusu frikiki hiyo iliyozaa goli alifanya makosa matano ya kiufundi ambayo hayakubaliki kwenye mashindano makubwa kama UEFA.
Wenger ameyataja makosa hayo ya Refa kuwa:
-Hakutoa frikiki pale ilipotendeka.
-Hakusimama pale Refa anatakiwa kusimama.
-Hakupanga ukuta katika umbali unaotakiwa.
-Hakupaswa kutoa idhini ya kupigwa frikiki ya haraka wakati yeye mwenyewe yuko katikati ya tukio hilo la kupigwa frikiki.
-Hakunyosha mkono kwa wakati kuashiria sio frikiki ya moja kwa moja [kuwa ni indirect freekick].
Baadhi ya Wadau wamekumbusha ile hadithi ya mkuki kwa nguruwe kwani Arsenal washawahi kunufaika kwa frikiki za aina hiyo hiyo pale Thierry Henry alipofunga magoli mawili dhidi ya Chelsea kwa frikiki za haraka haraka kabla watu hawajajipanga.
Fergie amtaka Scholes aongeze mkataba
Bosi wa Manchester United Sir Alex Ferguson anataka Paul Scholes aachane na fikra za kustaafu na aongeze mkataba wake kwa mwaka mmoja zaidi.
Mkataba wa Scholes unakwisha Juni mwaka huu na mwaka jana Scholes alitamka kuwa msimu huu, pengine, ndio wa mwisho.
Scholes, mwenye miaka 35, bado anaendelea kung’ara na juzi huko Milan, Italia alifunga bao moja katika ushindi wa bao 3-2 dhidi ya AC Milan kwenye mechi ya UEFA.
Ferguson amesema Scholes bado ana uwezo mkubwa wa kucheza na wataongea nae ili kurefusha mkataba wake.
Msimu huu Scholes amecheza mechi 25 kati ya 40 za Man United na amefunga bao 5.
Scholes alianza kuichezea Manchester United tangu akiwa mtoto na ameshacheza zaidi ya mechi 600 na kushinda Ubingwa wa Ligi Kuu mara 9 na Ubingwa wa Ulaya mara mbili, mwaka 1999 na 2008.
Ameichezea England mara 65 na kuamua kustaafu mwaka 2004 ili atilie mkazo kuichezea Man United tu.
Wachezaji Chelsea waambiwa: “Shikeni adabu zenu!”
Menejimenti ya Chelsea, hasa Mmiliki, Roman Abramovich, imewataka Wachezaji wa Chelsea kuchunga tabia na mienendo yao ili kujiepusha kuingizwa katika skandali ambazo licha ya kuwachafulia majina yao pia inaharibu jina la Klabu ya Chelsea.
Wito huo umefuatia kashfa ya Nahodha wao John Terry aliehusishwa na kutembea na gelfrendi wa Mchezaji mwenzake Wayne Bridge na skandali hiyo ilimsababisha kuvuliwa Unahodha wa England.
Pia kumekuwa na taarifa zinazomtaja Ashley Cole kukumbwa na kashfa inayotingisha ndoa yake.
Ron Gourlay, Mkurugenzi Mtendaji wa Chelsea, alifanya mkutano na Wachezaji wote wa Klabu hiyo na kuwataka wajichunge au Klabu italazimika kutoa adhabu kali.

Friday 19 February 2010

LIGI KUU: Tathmini mechi za Jumamosi
Jumamosi, Februari 20
[saa 9 dak 45 mchana]
Everton v Manchester United
[saa 12 jioni]
Arsenal v Sunderland
West Ham v Hull City
Woves v Chelsea
[saa 2 na nusu usiku]
Portsmouth v Stoke City
Everton v Manchester United
Wayne Rooney anarudi Goodison Park uwanja alioibukia katika uchezaji wake kupambana na Klabu yake ya zamani Everton.
Rooney kwa sasa ni moto wa kuotea mbali na ameshafunga magoli 25 katika mechi zote alizocheza msimu huu na ndie aneongoza kwa ufungaji katika Ligi Kuu kwa kuwa na goli 21.
Lakini Everton pia wako kwenye fomu na katika mechi yao ya mwisho ya Ligi Kuu waliipiga Chelsea 2-1.
Lakini katika mechi hii Everton itawakosa Wachezaji wao mahiri Marouane Fellaini, Tim Cahill, Tony Hibbert na Phil Jagielka ambao ni majeruhi.
Nao Manchester United, endapo wakishinda mechi hii watachukua uongozi kwa vile Chelsea wanacheza baada ya mechi hii, itawakosa Nani na Rio Ferdinand ambao wako kwenye adhabu za kufungiwa na Ryan Giggs alievunjika mkono.
Katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu huko Old Trafford, Man United ilishinda bao 3-0.
Vikosi vinategemewa:
Everton (4-4-1-1): Howard; Neville, Distin, Yobo, Baines; Pienaar, Osman, Arteta, Donovan; Bilyaletdinov; Saha.
Man United (4-4-2): Van der Sar; Rafael, Evans, Brown, Evra; Scholes, Carrick, Fletcher, Park; Berbatov, Rooney.
Refa: Howard Webb.
Arsenal v Sunderland
Arsenal, wakitoka freshi kwenye kipigo cha Ureno mikononi mwa FC Porto, wanaikaribisha Uwanjani Emirates Sunderland ambayo imekuwa na matokeo mabaya na haijashinda katika mechi 12 lakini mechi yao ya mwisho kushinda ilikuwa ni ile waliyoifunga Arsenal.
Sunderland itawakosa Lee Cattermole na David Meyler, waliofungiwa, huku Kieron Richardson, Andy Reid, John Mensah, Fraizer Campbell, Anton Ferdinand, Jordan Henderson na Steed Malbranque ni majeruhi..
Arsenal huko Ureno walipofungwa na FC Porto iliwakosa Manuel Almunia, William Gallas, Alex Song, Eduardo na Andrei Arshavin lakini wote huenda wakacheza Jumamosi.
Vikosi vinategemewa:
Arsenal (4-3-3): Almunia; Sagna, Gallas, Vermaelen, Clichy; Fabregas, Song, Denilson; Nasri, Arshavin, Rosicky.
Sunderland (4-3-3): Gordon; Hutton, Turner, Kilgallon, McCartney; Malbranque, Cana, Zenden; Benjani, Bent, Jones.
Refa: Steve Bennett.
West Ham v Hull City
Hii ni mechi kati ya Timu zilizo chini kwenye msimamo wa Ligi zenye pointi sawa 24 ila West Ham iko juu ya Hull City kwa ubora wa magoli.
West Ham walikuwa hawajashinda katika mechi zao sita za nyuma lakini walishinda mechi yao ya mwisho.
Hull City wao msimu wote huu hawajashinda hata mechi moja ugenini.
Woves v Chelsea
Katika mechi yao ya mwisho kati ya Timu hizi Chelsea iliifunga vibaya Wolves kwa bao 4-0.
Baada ya kupigwa 2-1 na Everton katika mechi yao ya mwisho bila shaka Chelsea watakuwa mbogo katika mechi hii.
Vikosi vinategemewa:
Wolves (4-5-1): Hahnemann; Zubar, Craddock, Berra, Ward; Foley, Mancienne, Jones, Henry, Jarvis; Doyle.
Chelsea (4-4-2): Cech; Ivanovic, Terry, Carvalho, Zhirkov; Mikel, Ballack, Lampard, Malouda; Drogba, Anelka.
Refa: Kevin Friend.
Portsmouth v Stoke City
Timu taabani iliyo mkiani na yenye matatizo makubwa kifedha inaikaribisha Stoke City ambayo ina ahueni kubwa katika msimamo wa Ligi.
Kuanzia sasa, ili Portsmouth wapone kushuka Daraja, kila mechi kwao ni lazima iwe kama fainali au itakuwa baibai kwao.
MSIMAMO LIGI KUU England:
[Timu zimecheza mechi 26 isipokuwa inapotajwa]
1 Chelsea pointi 58
2 Man Utd pointi 57
3 Arsenal pointi 52
4 Man City pointi 45 [mechi 25]
5 Liverpool pointi 44
6 Tottenham pointi 43
7 Aston Villa pointi 42 [mechi 25]
8 Birmingham pointi 37 [mechi 25]
9 Everton pointi 35 [mechi 25]
10 Fulham pointi 34
11 Stoke pointi 31 [mechi 25]
12 Blackburn pointi 31
13 Sunderland pointi 26 [mechi 25]
14 Wigan pointi 25 [mechi 25]
15 West Ham pointi 24 [mechi 25]
16 Wolves pointi 24 [mechi 25]
17 Hull pointi 24
18 Bolton pointi 23 [mechi 25]
19 Burnley pointi 23 [mechi 25]
20 Portsmouth pointi 16 [mechi 25]
LEO MIAKA 100 YA OLD TRAFFORD
Miaka 100 iliyokwisha, tarehe 19 Februari 1910, Uwanja wa Old Trafford ulifunguliwa rasmi kwa mechi kati ya Manchester United na Liverpool ambayo Liverpool walishinda 4-3 mbele ya Watazamaji 45,000.
Uwanja huu kwa sasa unaweza kuchukua Watazamaji 75,957 na ni wa pili kwa ukubwa baada ya Wembley Stadium huko England.
Old Trafford ulibatizwa jina la “Theatre of Dreams”, yaani “Jukwaa la Ndoto” na Sir Bobby Charlton aliekuwa Mchezaji wa zamani mahiri wa Manchester United na England.
Mwaka 1909, Mwenyekiti wa Manchester United, John Henry Davies, alitoa Pauni Elfu 60 toka mfukoni mwake mwenyewe na kuujenga Uwanja huo.
Siku hiyo Februari 19, 1910, Kikosi cha kwanza kabisa kuchezea Manchester United kilikuwa: Harry Moger; George Stacey, Vince Hayes; Dick Duckworth, Charlie Roberts, Sam Blott; Billy Meredith, Harold Halse, Tom Homer, Sandy Turnbull, George Wall.
KWINGINEKO ULAYA: MECHI ZA WIKIENDI
BUNDESLIGA
Ijumaa, Februari 19
1899 Hoffenheim v Borussia Moenchengladbach
Jumamosi, Februari 20
Nurnberg v Bayern Munich
Borussia Dortmund v Hannover
Hamburg v Eintracht Frankfurt
Mainz 05 v Bochum
Cologne v Stuttgart
Jumapili, Februari 21
Freiburg v Hertha Berlin
Wolfsburg v Schalke
Werder Bremen v Bayer Leverkusen
LA LIGA
Jumamosi, Februari 20
Deportivo La Coruna v Xerez
Real Mallorca v Sevilla
Barcelona v Racing Santander
Jumapili, Februari 21
Real Madrid v Villarea
Osasuna v Valladolid
Malaga v Espanyol
SERIE A
Jumamosi, Februari 20
Inter Milan v Sampdoria
Genoa v Udinese
Jumapili, Februari 21
Atalanta v Chievo
Bologna v Juventus
Palermo v Lazio
Fiorentina v Livorno
Togo kuendelea kusota kifungoni
CAS, Mahakama ya Usuluhishi Michezoni [CAS: Court of Arbitration of Sports], imetupilia mbali matakwa ya Togo ya kutofungiwa kucheza Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika yajayo mawili na imesema kifungo hicho kinabaki palepale hadi uamuzi kamili wa kifungo cha Togo utakapotolewa na Mahakama hiyo iliyo Mjini Lausanne, Uswisi.
Uamuzi wa CAS unamaanisha Togo haitakuwemo kwenye Droo ya Jumamosi ya kupanga mechi za awali za mtoano za Kombe la Afrika zitazoanza kuchezwa Septemba mwaka huu.
Hata hivyo CAS imetamka kuwa endapo Togo watashinda kesi yao na kufunguliwa na CAS basi CAF itabidi waipange Togo kwenye mechi hizo za Kombe la Afrika.
CAF iliifungia Togo kutoshiriki kucheza Mashindano mawili yajayo ya Kombe la Mataifa ya Afrika baada kujitoa Fainali za Kombe hilo zilizofanyika Nchini Angola mwezi Januari.
Togo walijitoa kufuatia maafa waliyoyapata ya kushambuliwa wakati wakisafiri kutoka Congo na kuingia Angola Jimbo la Cabinda na ndipo Basi lao likapigwa risasi na Waasi wa Cabinda na kumuua Dereva wa Basi hilo pamoja na Maafisa wawili wa msafara wa Togo.
Serikali ya Togo ikaamrisha Kikosi chake kirudi nyumbani na CAF imeuchukulia uamuzi huo kama Serikali kuingilia masuala ya Soka na hivyo kuwafungia.
Wadau wengi wanahisi adhabu hii kwa Togo haikustahili ukichukulia misingi ya ubinadamu.
EUROPA LIGI: Liverpool, Fulham zashinda nyumbani
Bao la dakika ya 80 la David Ngog limeipa ushindi Liverpool wa bao 1-0 walipocheza kwao Anfield na Timu ya Rumania FC Unirea Urziceni.
Huko Craven Cottage, Fulham walitumia uwanja wa nyumbani vyema waliposhinda mabao 2-1 dhidi ya Timu ya Ukraine FC Shakhtar Donetsk ambao ndio wanaoshikilia Kombe la UEFA ambalo msimu huu limebadilishwa na kuwa EUROPA LIGI.
Bao la ushindi la Fulham lilifungwa na Bobby Zamora.
Mechi za marudiano zitakuwa ugenini wiki ijayo huko Rumania na Ukraine.
MATOKEO:
FC Rubin Kazan 3 v Hapoel Tel aviv 0
Ajax 1 v Juventus 2
Club Brugge 1 v Valencia 0
Villareal 2 v Wolfsburg 2
Standard Liege 3 v Red Bull Salzburg 2
FC Twente 1 v Werder Bremen 0
Lille 2 v Fenerbahce 1
Athletic de Bilbao 1 v Anderlecht 1
FC Kobenhavn 1 v Olympique de Marseille 2
Panathinaikos 3 v AS Roma 2
Atletico de Madrid 1 v Galatasaray 1
Fulham 2 v FC Shakhtar Donetsk 1
Liverpool 1 v FC Unirea Urziceni 0
Hamburger SV 1 v PSV Eindhoven 0
Hertha Berlin 1 v Benfica 1
Wolves yatwangwa Faini kwa kuchezesha Kikosi dhaifu!!
Klabu ya Ligi Kuu, Wolverhampton Wanderers, imetwangwa faini ya Pauni Elfu 25 kwa kuchezesha Kikosi dhaifu kwenye mechi ya Ligi waliyocheza Desemba 15 huko Old Trafford dhidi ya Manchester United na kufungwa 3-0.
Hata hivyo faini hiyo haitakiwi kulipwa kwa sasa.
Wolves ilibadili Wachezaji wote 10 wa mbele walipocheza na Man United siku 4 tu baada ya kuifunga Tottenham kwenye Ligi bao 1-0 na siku chache baada ya mechi ya Man United ilipanga tena Kikosi kamili na kuifunga Burnley 2-0.
Msemaji wa Ligi Kuu amesema hatua hiyo ya kuiadhibu Wolves imechukuliwa kwani ilikuwa ni kinyume kwa sheria za Ligi Kuu zinazotaka kila Timu kuchezesha Kikosi chao kamili.
Meneja wa Wolves Mick McCarthy amesema ameukubali uamuzi wa Ligi Kuu na yeye hakuwa na nia ya kuvunja sheria ila alichagua Kikosi ambacho alikiona ni sahihi kwa mechi na Man United.
Viera akubali kosa, kukosa mechi 3!!
Kiungo wa Manchester CityPatrick Vieira atazikosa mechi zijazo tatu za Manchester City baada ya kukubali kosa aliloshitakiwa na FA la kumpiga teke Glenn Whelan wa Stoke City kwenye mechi ya juzi ya Ligi na tukio hilo halikuadhibiwa na Refa.
FA ilichunguza video ya tukio na kuamua kumshitaki Viera.
Adhabu ya Viera inamaanisha atazikosa mechi za Manchester City dhidi ya Liverpool ya Jumapili, mechi ya FA Cup na Stoke City na ile ya Ligi na Chelsea.
Pompey waomba kibali kuuza Wachezaji
Portsmouth ambayo ina matatizo makubwa ya fedha imeomba kibali cha Ligi Kuu ili kuuza Wachezaji nje ya dirisha la uhamisho ili wakabiliane na matatizo yao ya kifedha yakiwa pamoja na kutaka kufilisiwa na Mamlaka ya Kodi kwa kutolipa kodi.
Hata hivyo ombi hilo la Portsmouth linahitaji kibali cha FIFA kwani madirisha ya uhamisho ni mawili tu nayo ni Januari 1 hadi 31 na jingine ni Juni 1 hadi Agosti 31.
Portsmouth wanasadikiwa kuwa na madeni ya kiasi cha Pauni Milioni 60 na hawajasema Mchezaji yupi anauzwa ingawa inaaminika Wachezaji Nadir Belhadj wa Algeria, Kevin Prince-Boateng na Marc Wilson ndio walengwa.
Msimu huu Portsmouth imeshamilikiwa na Matajiri wanne tofauti na wote wameshindwa kuinusuru balaa la kifedha linalosababisha hata Wachezaji kuchelewa kupata Mishahara na sasa ipo mkiani mwa Ligi Kuu hivyo kuandamwa na balaa la kushuka Daraja.

Thursday 18 February 2010

Leo ni usiku wa EUROPA LIGI!!!
• Mechi bwelele!!!
Leo kona mbalimbali za Ulaya zitawaka moto kwa mechi mbalimbali za EUROPA LIGI za Raundi ya Mtoano ya Timu 32.
Kuna mechi kadhaa tamu kama vile Ajax v Juventus, Villareal v Wolfsburg, Lille v Fenerbahce na kadhalika.
Timu za England, mbali ya Everton iliyocheza juzu na Sporting Lisbon na kushinda 2-1, zilizomo kwenye EUROPA LIGI ni Liverpool na Fulham.
Leo Liverpool itaikwaa FC Unirea Urziceni ya Romania wakiwa nyumbani Anfield.
Fulham pia wako nyumbani Craven Cottage na leo watacheza na FC Shakhtar Donetsk ya Ukraine.
RATIBA KAMILI:
FC Rubin Kazan v Hapoel Tel aviv
Ajax v Juventus
Club Brugge v Valencia
Villareal v Wolfsburg
Standard Liege v Red Bull Salzburg
FC Twente v Werder Bremen
Lille v Fenerbahce
Athletic de Bilbao v Anderlecht
FC Kobenhavn v Olympique de Marseille
Panathinaikos v AS Roma
Atletico de Madrid v Galatasaray
Fulham v FC Shakhtar Donetsk
Liverpool v FC Unirea Urziceni
Hamburger SV v PSV Eindhoven
Hertha Berlin v Benfica
Wenger alia na Refa kwa bao la Porto!!
Kufuatia kipigo cha bao 2-1 walichokipata jana huko Ureno, Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amedai FC Porto hawakustahili kupewa frikiki iliyozaa bao la pili na la ushindi kwa Porto kwa vile mpira alioudaka Kipa Lukasz Fabianski haukuwa pasi kwa Kipa ya kukusudia.
Wenger amedai: “Campbell alirudisha mpira kwa Kipa kwa bahati mbaya! Mpira ulimgonga Campbell na kwenda kwa Kipa.”
Lakini Wadau wanashangaa hata kama Campbell hakukusudia kwa nini Kipa Fabianski aliudaka wakati alikuwa na uwezo wa kuupiga.
Baada ya Refa kuamua ni frikiki, Porto, kabla Arsenal hawajajipanga, wakapasiana na kufunga kwa kushtukiza.
Hata goli la kwanza walilofungwa Arsenal Wadau wamemlaumu Kipa huyo kwa makosa.
Nahodha Cesc Fabregas wa Arsenal yeye hakuficha, alitoboa: “Magoli yote tuliyofungwa ni makosa ya kitoto! Silalamikii goli la pili, hata mie kama Mchezaji ningefanya vilevile na kupiga frikiki haraka!”
Alipohojiwa kuhusu makosa ya Kipa Fabianski, Arsene Wenger alikataa kumlaumu na alidai makosa yote yanapaswa kulaumiwa Timu nzima na si mtu mmoja.
Vidic ni utata!!
Kuna hali ya utata mkubwa kuhusu kuendelea kwa Nemanja Vidic kuchezea Manchester United huku kukiwa na habari nzito kuwa anadengua ili alazimishe kuihama Manchester United na kwenda Real Madrid au AC Milan.
Habari hizo zilipamba moto baada ya Vidic, alietegemewa kuwemo kwenye Kikosi cha Manchester United kilichosafiri kwenda Milan, Italia kucheza na AC Milan hapo Jumanne, kujitoa Kikosini dakika za mwisho na inadaiwa alifanya hivyo kwa madai bado hajawa fiti kucheza.
Ingawa Sir Alex Ferguson amekataa kuzungumza kwa undani kuhusu Vidic mbali ya kusema wanataka abaki Man United, hatima yake imekuwa gizani hasa baada ya Daktari wa Timu ya Taifa ya Serbia, Miodrag Mladenovic, kudai Manchester United haitaki kuwapa taarifa kuhusu maumivu ya Mchezaji huyo licha ya kuwaomba wajulishwe kwa vile Vidic ni muhimu kwa Timu ya Serbia.
Hata hivyo mwenyewe Vidic amedaiwa kusema yeye ni Mchezaji wa Manchester United hadi mkataba wake utakapoisha mwaka 2010 na hajazungumza na mtu yeyote kuhusu kuhama.
Kuhusu kutokucheza, Vidic amedai bado hayuko fiti na hawezi kujifosi tu kwani anaweza kujiletea madhara makubwa.
Kocha wa Serbia, Raddy Antic, amesema habari za kutokuwa fiti kwa Vidic ni kweli ingawa ataonekana uwanjani hivi karibuni.
UEFA CHAMPIONS LIGI: Porto, Bayern Munich zashinda nyumbani!!!
FC Porto imeifunga Arsenal mabao 2-1 huko Ureno na Bayern Munich, ikiwa nyumbani, imeipiga Fiorentina pia mabao 2-1.
Huko Ureno, FC Porto ndio ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia Varella lakini Sol Campbell wa Arsenal akasawazisha kwa kichwa.
Hadi mapumziko, Porto 1 Arsenal 1.
Porto ilipata bao la pili katika mazingira ya kushangaza kwani Beki Sol Campbell alitoa pasi ya nyuma kwa Kipa wake Fabianski na badala ya Kipa huyo kuupiga mpira huo mbele yeye akaudaka na Refa akaamua ipigwe frikiki isio ya moja kwa moja langoni kwa Arsenal.
Ndipo, kabla Arsenal hawajakaa vizuri, Ruben Micael haraka haraka akampasia Falcao aliefunga wakati Arsenal wameduwaa.
Huko Ujerumani, Bayern Munich iliitoa Fiorentina kwa bao 2-1 na bao la pili la Bayern lilifungwa na Miroslav Klose ambae alionekana waziwazi kuwa ofsaidi.
Katika mechi hii, Mchezaji wa Fiorentina Massimo Gobbi alipewa Kadi Nyekundu kwa kumchezea faulo Arjen Robben wa Bayern Munich.
Mechi za marudiano za Arsenal v FC Porto na Fiorentina v Bayern Munich zitafanyika Machi 9.
LIGI KUU: Wigan 0 Bolton 0
Katika mechi pekee ya Ligi Kuu siku ya Jumatano, huko KC Stadium, Timu zinazosuasua chini kwenye msimamo wa Ligi, wenyeji Wigan na Bolton zilitoka suluhu ya 0-0.
MECHI ZA LIGI KUU WIKIENDI HII:
Jumamosi, Februari 20
[saa 9 dak 45 mchana]
Everton v Manchester United
[saa 12 jioni]
Arsenal v Sunderland
West Ham v Hull City
Woves v Chelsea
[saa 2 na nusu usiku]
Portsmouth v Stoke City
Jumapili, Februari 21
[saa 11 jioni]
Aston Villa v Burnley
[saa 12 jioni]
Fulham v Birmingham
Man City v Liverpool
[saa 1 na robo usiku]
Wigan v Tottenham
Jumatatu, Februari 22
[saa 5 usiku]
Blackburn v Bolton
Viera ana kesi FA!!
Kiungo wa Manchester City Patrick Viera amefunguliwa mashtaka ya kutumia mabavu kufuatia kumpiga teke Mchezaji wa Stoke City Glenn Whelan katika mechi ya Ligi Kuu siku ya Jumanne katika tukio ambalo Refa Alan Wiley hakulichukulia hatua na alibaki kuongea na Viera tu.
Mechi hiyo ya Ligi Kuu kati ya Stoke na Man City uwanjani Britannia ilimalizika 1-1.
Baada ya mechi hiyo, Meneja wa Stoke, Tony Pulis, aliitaka FA ichunguze video za tukio hilo.
Akipatikana na hatia, Viera atafungiwa mechi 3 na atazikosa mechi za Timu yake Manchester City dhidi ya Liverpool, siku ya Jumapili, Stoke City ya FA Cup na ya Chelsea kwenye Ligi.
Viera, ambae aliichezea Arsenal kabla ya kwenda Italia, alishawahi kupewa Kadi Nyekundu mara 10 katika miaka 9 aliyokuwa Arsenal.
Viera amepewa muda mpaka Alhamisi jioni ili aweze kukata rufaa na Kamisheni ya Sheria itakaa Ijumaa kuamua shauri lake.
Mabosi wa Klabu wapinga michuano maalum kupata Timu ya 4 kucheza Ulaya!!!
Mara baada ya kuibuka habari kuwa FA inatafakari kuweka michuano maalum kwa Timu zitakazomaliza Ligi nafasi ya 4 hadi ya 7 kushindana ili kupata Timu moja itakayojumuika na Timu 3 za juu kucheza mashindano ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE, Mabosi kadhaa wa Ligi Kuu nao wameibuka kupinga mpango huo.
Kwa taratibu za sasa Timu 4 za juu ndizo zinaingia moja kwa moja kucheza UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
Majuzi, Meneja wa Everton, David Moyes, ameupinga mpango huo kwa kuusema hauna maana na unaleta msongamano bure wa mechi.
Nae Bosi wa Liverpool, Rafa Benitez, ameupuuza mpango huo na kusema utaupa mzigo zaidi Timu za Ligi Kuu ambazo zinakabiliwa na mechi nyingi kwa sasa.
Benitez amesema: “Hivi kuna faida gani kwa Timu inayomaliza nafasi ya 4 kucheza na Timu ya nafasi ya 7 ambayo pengine iko nyuma yake pointi 20?”
Benitez ameongeza kwa kusema kwa taratibu za sasa tayari Timu zina mechi nyingi na wanapata majeruhi wengi.

Wednesday 17 February 2010

Stoke City wanataka Viera asulubiwe!!
Tony Pulis, Meneja wa Stoke City, anataka Mchezaji wa Manchester City Patrick Viera aadhibiwe na FA kwa kosa la kumpiga teke Kiungo wao Glenn Whelan wakati Wachezaji hao walipoanguka chini baada ya kugombea mpira.
Tukio hilo lilitokea kwenye mechi ya jana ya Ligi Kuu iliyotoka sare 1-1 na Refa Alan Wiley hakuchukua hatua yeyote kwa Viera mbali ya kuongea nae.
Pulis anataka FA walitazame tukio hilo kwenye video baada ya Timu yake Stoke kuadhibiwa mwezi Oktoba mwaka jana pale Difenda wao Robert Huth alipofungiwa mechi 3 kwa kumpiga Beki wa West Ham Mathew Upson tukio ambalo Refa hakuliona na adhabu hiyo ilitolewa baada ya kuchunguzwa kwenye video.
Fellaini wa Everton nje msimu wote!!
Kiungo wa Everton Marouane Fellaini atakosa kipindi chote kilichobaki cha msimu huu baada ya kuthibitika ameumia vibaya enka kuliko ilivyokisiwa na maumivu hayo yamefananishwa na kama yale ya Straika wa Arsenal Robin van Persie.
Fellaini, miaka 22, aliumizwa na Beki wa Liverpool Sotirios Kyrgiakos hapo Februari 6 kwenye mechi ya Ligi ambayo Liverpool walishinda 1-0 licha ya kucheza pungufu baada ya Beki huyo kupewa Kadi Nyekundu kwa kumuumiza Fellaini.
Kyrgiakos sasa anatumikia adhabu ya kufungiwa mechi 3 kwa Kadi hiyo.
UEFA CHAMPIONS LIGI: FC Porto v Arsenal
FC Porto ni wenyeji wa Arsenal Uwanjani Estadio do Dragao huko Porto, Ureno katika mechi ya kwanza ya mtoano ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Fc Porto inaongozwa na Meneja Jesualdo Ferreira ambae alikuwa Mwalimu wa Jose Mourinho kwenye Chuo cha Elimu ya Viungo huko Lisbon, Ureno lakini baadae akapigwa stopu na Mourinho kuwa Meneja Msaidizi FC Porto wakati Mourinho ni Meneja hapo Klabuni.
FC Porto ina Wachezaji kadhaa mahiri akiwamo Nahodha wao Bruno Alves anaechezea Ureno, Kiungo Raul Meireles ambae pia yupo Timu ya Taifa ya Ureno.
Huko mbele wana Straika mkali ambae ashawahi kuchezea Brazil aitwae Hulk.
Arsenal wana tatizo kubwa la majeruhi ingawa wako Wachezaji wanaoweza kuziba vizuri mapengo hayo.
Majeruhi hao ni pamoja na wa muda mrefu Robin van Persie na kina Gallas, Eduardo, Song, Kipa Almunia na Arshavin.
Pia historia haiwapendi Arsenal huko Ureno kwani katika mechi 4 walizocheza huko wametoka suluhu 3 na kufungwa moja na kipigo hicho kikiwa msimu uliokwisha walipofungwa 2-0 kwenye mechi ya Makundi na FC Porto.
Magazeti Italia: “Milan wanatengeneza, Rooney anabomoa!”
Gazeti moja kubwa huko Mjini Milan, Italia limebeba bango kubwa likisema “Milan inatengeneza, Rooney anabomoa!” kufuatia kipigo cha jana cha 3-2 cha AC Milan mikononi mwa Manchester United huku Rooney akipachika bao mbili na kuwa mkuki moyoni mwa AC Milan katika mechi ya kwanza ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE iliyochezwa uwanja wa San Siro huko Milan, Italia.
Gazeti hilo limesema AC Milan walitawala pambano hilo lakini wamefungwa kwa sababu ya Wayne Rooney na sasa wanakabiliwa na kazi ngumu ya kushinda 2-0 huko Old Trafford kitu ambacho Gazeti hilo kubwa limedai hakiwezekani.
Gazeti jiingine limedai Manchester United, ikicheza kama Timu mahiri ya Italia, imeiteka San Siro kwa kutawala kipindi cha pili hasa kwa kazi ya Rooney.
Timu hizo Manchester United na AC Milan zitarudiana Old Trafford Machi 10.
Carrick astushwa na Kadi Nyekundu
Michael Carrick wa Manchester United amesema amestushwa sana na Kadi Nyekundu aliyopewa jana katika mechi waliyowafunga AC Milan 3-2 huko San Siro.
Kiungo huyo alionyeshwa Kadi ya pili ya Njano na hivyo kupewa Nyekundu na Refa kutoka Ureno Olegario Benquerenca katika dakika za majeruhi kwa kuupiga mpira baada ya Refa huyo kuashiria kuwa Evra alimchezea faulo Pato wa AC Milan.
Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson amesema Carrick alifanya uzembe na Refa huyo alichofanya ni sahihi lakini mwenyewe Carrick, ambae hii ni mara ya kwanza kutolewa nje, amesema Refa amechukua uamuzi mkali kwa vile yeye aliubetua tu mpira na hakuna kitu kilichocheleweshwa.
Kwa Kadi hiyo Nyekundu, Carrick ataikosa mechi ya marudiano ya Timu hizo hapo Machi 10.
UEFA CHAMPIONS LIGI: AC Milan 2 Man United 3
Ingawa mechi hii iltawaliwa kidogo na AC Milan lakini Manchester United ndio wameibuka kidedea kwa kushinda kwa mabao 3-2 huu ukiwa ushindi wao wa kwanza hapo San Siro katika mechi 4 walizocheza na AC Milan Uwanjani hapo.
AC Milan ndio walioanza mechi hii kwa kishindo kwa mkwaju wa Ronaldinho kumbabatiza Michael Carrick na kumbabaisha Kipa Van der Sar na kutinga wavuni ikiwa ni dakika ya 3 tu ya mchezo.
Scholes alisawazishia Man United dakika ya 36 na hadi mapumziko bao zilikuwa 1-1.
Mabao mawili ya vichwa ya Wayne Rooney kwenye dakika ya 66 na 74 yalifanya ngoma iwe 3-1 lakini kazi nzuri ya Ronaldinho ilimaliziwa na Clarence Serdorf aliefunga bao la pili kwa Milan dakika ya 85.
Katika dakika za majeruhi Kiungo wa Man United Michael Carrick alipata Kadi ya Pili ya Njano na hivyo kupewa Nyekundu na kutolewa na sasa ataikosa mechi ya marudiano hapo Machi 10.
Vikosi vilivyoanza:
AC Milan: Dida, Bonera, Nesta, Thiago Silva, Antonini, Beckham, Pirlo, Ambrosini, Ronaldinho, Alexandre Pato, Huntelaar.
Akiba: Abbiati, Gattuso, Inzaghi, Seedorf, Flamini, Favalli, Abate.
Man Utd: Van der Sar, Rafael Da Silva, Ferdinand, Jonathan Evans, Evra, Nani, Carrick, Scholes, Fletcher, Park, Rooney.
Akiba: Kuszczak, Neville, Brown, Owen, Berbatov, Valencia, Gibson.
Refa: Olegario Benquerenca (Portugal)
UEFA CHAMPIONS LIGI: Lyon 1 Real Madrid 0
Bao la Jean Makoun limeiwezesha Lyon kuifunga bao 1-0 Timu kigogo Real Madrid katika mechi iliyochezwa Ufaransa.
Timu hizi zitarudiana huko Uwanja wa Bernabeau, Madrid, Spain Machi 10.
LIGI KUU: Stoke City 1 Man City 1
Katika mechi pekee ya Ligi Kuu iliyochezwa Jumanne huko Britannia Stadium mtu 10 Stoke City walipata sare ya 1-1 na Manchester City.
Timu hizi zilikutana juzi kwenye Kombe la FA na kutoka sare na watarudiana tena Februari 24 kupata mshindi atakaeingia Robo Fainali ya Kombe hilo.
Stoke City, wakicheza pungufu baada ya Difenda Abdoulaye Faye kupewa Kadi Nyekundu kwa kumwangusha Adebayor wakati akiwa mtu wa mwisho.
Lakini, huku wakiwa watu 10, Stoke ndio walipata bao la kuongoza kupitia Glenn Whelan.
Man City walisawazisha kwa bao la Gareth Barry aliepokea mpira wa kichwa kutoka kwa Adebayor.
Kwa sare hii, Man City wameipiku Liverpool na kuchukua nafasi ya 4 wakiwa pointi moja mbele ya Liverpool na huku wana mechi moja mkononi.
EUROPA LIGI: Everton 2 Sporting Lisbon 1
Everton wameichapa Sporting Lisbon ya Ureno mabao 2-1 katika mechi ya kwanza ya EUROPA LIGI iliyochezwa Goodison Park huko Liverpool.
Mabao ya Everton yalifungwa na Steven Pienaar na Distin.
Sporting Lisbon walipata bao lao kwa penalti iliyosababisha pia Difenda wa Everton Distin apewe Kadi Nyekundu na penalti hiyo kufungwa na Miguel Veloso.

Tuesday 16 February 2010

UEFA yabadili ratiba ili Wadau wafurahie!!
UEFA imesema ratiba ya mwaka huu ya mechi za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 imebadilishwa ili kutoa nafasi kwa Mashabiki wengi kuona mechi hizo laivu.
Mechi za kwanza za Raundi hii ya Mtoano zitaanza leo Februari 16 na kumalizika Februari 24 na marudiano yake ni kuanzia Machi 9 hadi Machi 17.
Wiki hii kuna mechi 4 yaani Jumanne mechi mbili na Jumatano mechi mbili na wiki ijayo ni hivyo hivyo yaani Jumanne mechi 2 na Jumatano mechi mbili.
Pia safari hii Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI itafanyika Jumamosi badala ya ile Jumatano tuliyoizoea na Fainali hiyo itafanyika Uwanja wa Real Madrid uitwao Bernabeau.
RATIBA NI:
Jumanne, 16 Februar1 2010
AC Milan v Man U
Lyon v Real Madrid
Jumatano, 17 Februari 2010
Bayern Munich v Fiorentina
FC Porto v Arsenal
Jumanne, 23 Februari 2010
Olympiakos v Bordeaux
VfB Stuttgart v Barcelona
Jumatano, 24 Februari 2010
CSKA Moscow v Sevilla
Inter Milan v Chelsea
MECHI ZA MARUDIANO:
Jumanne, 9 Machi 2010
Arsenal v FC Porto
Fiorentina v Bayern Munich
Jumatano, 10 Machi 2010
Man U v AC Milan
Real Madrid v Lyon
Jumanne, 16 Machi 2010
Chelsea v Inter Milan
Sevilla v CSKA Moscow
Jumatano, 17 Machi 2010
Barcelona v VfB Stuttgart
Bordeaux v Olympiakos
Bunduki 5 hazipo kwa Gunners!!!
• Ni Gallas, Almunia, Arshavin, Song & Eduardo nje!!!
Imethibitika kuwa Arsenal itawakosa Wachezaji wake watano kwenye mechi ya UEFA CHAMPIONS LIGI ya kesho wanayocheza Ureno na FC Porto kwa ajili ya kuumia.
Wachezaji hao ni Eduardo, Arshavin, Alex Song, Gallas na Manuel Almunia.
Tatizo kubwa la Arsenal litakuwa kwa Mafowadi kwani Robin van Persie ni majeruhi wa muda mrefu na hivyo itabidi wamtegemee Bendtner ambae ndio kwanza anarudi kutoka kuuguza majeraha yake ya muda mrefu.
Nafasi ya Gallas inaweza ikazibwa na Mkongwe Sol Campbell atakaeshirikiana na Thomas Vermaelen.
Nafasi ya Kipa Almunia itachukuliwa na Lukasz Fabianski.
FA yamtaka Warnock ajieleze kwa kutaka Refa Msaidizi afungiwe
Chama cha Soka England, FA, kimemtaka Meneja wa Crystal Palace Neil Warnock atoe maelezo kuhusu kauli yake aliyoitoa Jumapili mara baada ya sare ya 2-2 na Aston Villa ya mechi ya FA Cup Raundi ya 5 kwamba Refa Msaidizi alikosea kuwapa Aston Villa kona iliyozaa bao la pili la Villa la kusawazisha la dakika ya 87 na hivyo afungiwe kwa kosa hilo.
FA imempa Warnock wiki moja atoe maelezo yake ambayo ndiyo yataamua kama afunguliwe mashtaka au la
Fergie azungumzia Mastaa wake wa zamani
Akihojiwa na Waandishi wa Habari kabla ya pambano lao la UEFA CHAMPIONS LIGI la leo usiku na AC Milan, Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, alijikuta muda mwingi akijibu na kuelezea kuhusu Wachezaji wake Mastaa walioihama Timu yake.
David Baeckham, kwa vile yupo AC Milan kwa mkopo, alitajwa sana na mwenyewe Beckham alishasema hata akifunga goli hatasherehekea.
Ferguson alitania kuhusu kauli hiyo ya Beckham: “Naomba asisherehekee!”
Akimaanisha Beckham asifunge goli.
Lakini akaongeza kwa kusema Beckham kwa vile amechezea zaidi ya mechi 100 na England na kuchezea Klabu za AC Milan, Real Madrid, Man United yupo sawa kama Wachezaji wazoefu wengine wa AC Milan kama vile Seerdof, Pirlo, Ambrossini, Nesta na Inzaghi na hilo ni manufaa kwa AC Milan katika mechi kubwa.
Ferguson alikiri Beckham bado ni shujaa kwa Mashabiki wengi wa Manchester United hasa kwa vile alikulia na kuendelezwa Klabuni hapo.
Kuhusu Ronaldo, Ferguson alisema huyo ni Mchezaji bora duniani na kumpoteza ni pengo kubwa lakini inabidi umsahau, usonge mbele na kuijenga upya Timu.
AC Milan iliifunga Manchester United miaka mitatu iliyopita na Ferguson amesema anajua walifungwaje na moja ya sababu ni uchovu wao lakini wao wikiendi hii hawakucheza mechi na hilo litawasaidia kwani watakuwa freshi.
EUROPA LIGI:
Everton v Sporting Lisbon
[saa 2 dak 45 usiku, saa za bongo]
Leo usiku Everton watashuka Uwanjani kwao Goodison Park kucheza na Sporting Lisbon ya Ureno katika mechi ya kwanza ya EUROPA LIGI na itawakosa Wachezaji wao bora kwa siku za hivi karibuni, John Heitinga na Marouane Fellaini.
Fellaini ni majeruhi na Heitinga haruhusiwi kucheza EUROPA LIGI kwa vile aliichezea Klabu yake ya zamani Atletico Madrid hapo awali.
Everton watalichukulia pambano la leo kwa tahadhari kubwa kwa sababu walishaonja joto ya jiwe walipocheza na Timu nyingine ya Ureno katika mechi za Makundi ya EUROPA LIGI mwanzoni, Benfica, iliyowafunga mechi zote mbili 5-0 na 2-0 na hivyo watakuwa makini na mechi hii na Sporting Lisbon ambao ni wapinzani wakuu wa Benfica.
Kikosi cha Everton kitatokana na: Howard, Neville, Distin, Baines, Senderos, Yobo, Cahill, Rodwell, Arteta, Osman, Pienaar, Bilyaletdinov, Coleman, Saha, Donovan, Yakubu, Vaughan, Duffy, Baxter, Nash.
Mourinho aibeza Chelsea
Jose Mourinho, aliewahi kuwa Kocha wa Chelsea lakini sasa yuko Inter Milan, ameibeza Chelsea na kutia utambi kabla ya Timu hizi kupambana wiki ijayo katika mechi ya UEFA CHAMPIONS LIGI kwa kudai yeye ndie aliefanikisha kuleta Vikombe vingi Klabuni hapo.
Mourinho aliachana na Chelsea Septemba 2007 na tangu wakati huo Klabu hiyo imechukua Kikombe kimoja tu cha FA mwaka jana wakati yeye katika miaka mitatu aliyokaa Stamford Bridge alitwaa Ubingwa wa England mara 2, Carling Cup mara 2 na FA Cup mara moja.
Mourinho amejigamba: “Chelsea wameathirika tangu niondoke mimi! Tulikuwa na uhusiano mzuri mimi, Wachezaji na Mashabiki na ukiuvunja uhusiano namna hiyo basi utaumia tu!”
Mourinho akaongeza: “Baada yangu wamekuwa na Makocha wengi na wengine hawakustahili kuwa hapo na pengine walitaka kuleta makubwa yasiyowezekana!”
Mourinho pia alidai kuwa Mmiliki wao Roman Abramovich ni mtu anaependa ushindi tu na usipofanikiwa upo nje.
Chelsea kwa sasa inafundishwa na Carlo Ancelotti ambae ametokea AC Milan ambao ni wapinzani wakubwa wa Inter Milan na Mourinho na Ancelotti washawahi kukwaruzana hapo nyuma.
Kuhusu hilo, Mourinho amesema: “Ancelotti si rafiki yangu na hili halibadiliki! Nchini England unaheshimiwa ukiwa kama Kocha mwenye ujuzi lakini Italia ukiwa mgeni hamna! Utaheshimiwa ukiwa Mtaliana tu na ndio maana nina furaha kufanya kazi England!”
Mourinho akabainisha kuwa yeye ni sehemu ya historia ya Chelsea na ana hamu kuona kama Ancelotti atamalizia muda wake hapo Chelsea akiwa na rekodi kama yake.
UEFA CHAMPIONS LEAGUE: Leo ni Leo!!
[Saa 4 dak 45 usiku saa za bongo]
Jumanne, 16 Februar1 2010
AC Milan v Man U
Lyon v Real Madrid
Lyon v Real Madrid
Katika miaka mitano, mara ya mwisho ikiwa 2004, Real Madrid ambao wamewahi kuwa Mabingwa wa Ulaya mara 9, hawajawahi kutinga Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI na safari hii ili kuingia Robo Fainali ni lazima waitoe Timu ngumu ya Ufaransa Lyon wakiwa kwao Stade Gerland katika mechi ya kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16.
Marudiano ni Machi 10 huko Uhispania, Uwanja wa Bernabeau.
Tangu wakati huo Real imetolewa katika hatua hii na Klabu za Juventus, Arsenal, Bayern Munich, Roma na mwaka jana na Liverpool.
Kwa Real Madrid kufika Fainali ni kitu muhimu mno kwa vile tu Fainali ya mwaka huu inafanyika nyumbani kwao Uwanja wao wa Bernabeau.
Kabla ya mechi ya leo, Real Madrid walishinda mechi yao ya La Liga majuzi walipoipiga Xerez bao 3-0 huku Cristiano Ronaldo, akitoka kifungo cha mechi mbili, akifunga bao 2.
Ushindi huo wa Real Madrid na kufungwa kwa Wapinzani wao FC Barcelona na Athletic Madrid kwenye Ligi Jumapili na kuwafanya wawe pointi 2 tu nyuma ya Barca kumewapa furaha kubwa Real na watataka furaha yao idumu kwa matokeo mazuri katika mechi na Lyon.
Real pia wana habari nzuri kwani Straika wao Karim Benzema waliemnunua kutoka Lyon aliekuwa kaumia sasa yuko fiti na tayari kuikabili Klabu yake ya zamani.
AC Milan v Manchester United
Leo katika Stadio Giuseppe Meazza, hilo ndio jina halisi la Uwanja ambao wengi tumeuzoea kama San Siro, AC Milan na Manchester United zitakumbana katika mechi ya kwanza ya UEFA CHAMPIONS LIGI huku marudio yakiwa Old Trafford Machi 10.
Kwa Wadau mvuto mkubwa wa mechi hii ni David Beckham, alie AC Milan kwa mkopo kutoka Klabu yake ya Marekani LA Galaxy, kucheza na Klabu yake ya zamani Manchester United ambayo aliihama mwaka 2003 kwenda Real Madrid kwa mara ya kwanza tangu ahame.
Mwenyewe Beckham amesema mechi hii na Man United si kisasi kwake kwani yeye bado ana mapenzi makubwa na Man United na pia mpaka leo anamtambua na kumuheshimu Sir Alex Ferguson kama Baba yake.
AC Milan, chini ya Kocha Mbrazil Leonardo, wanatoka kwenye ushindi wa jasho wa Serie A wa 3-2 dhidi ya Udinese walioupata Ijumaa na ushindi huo ulifuta uteja wa mechi 3 mfululizo kwenye Ligi.
Kwa Manchester United, ambao sasa wako kwenye wimbi la ushindi wakiwa washatinga Fainali ya Carling Cup baada ya kuwabwaga Mahasimu wao Manchester City na wapo pointi moja tu kwenye Ligi nyuma ya Chelsea huku Straika wao Rooney akifunga magoli kama mashine, wanaingia Uwanja wa San Siro kupambana na AC Milan kwa mara ya 4 wakiwa wamecheza nao mwaka 1958, 1969, 2005 na 2007 bila ya kumudu kufunga hata goli moja mara zote hizo!
UEFA CHAMPIONS LEAGUE: Kesho!!
[Saa 4 dak 45 usiku saa za bongo]
Jumatano, 17 Februari 2010
Bayern Munich v Fiorentina
FC Porto v Arsenal

Monday 15 February 2010

Man United safarini Milan!!!
Nemanja Vidic na Anderson hawakuwamo kwenye Kikosi cha Wachezaji 22 wa Manchester United waliosafiri leo kutoka Manchester kwenda Milan, Italia kwa pambano la kesho huko San Siro na AC Milan la UEFA CHAMPIONS LIGI.
Wachezaji hao wanasemekana bado ni majeruhi.
Mchezaji mwingine aliebaki Jijini Manchester ni Mkongwe Ryan Giggs ambae amevunjika mkono.
Nani na Rio Ferdinand ambao wanatumikia vifungo vya mechi 3 na 4 kila mmoja huko England wamo Kikosini na vifungo vyao havihusu mechi za Ulaya na hivyo wanaweza kucheza kesho.
Kikosi kamili kilichosafiri: Van der Sar, Foster, Kuszczak; Neville, Brown, J Evans, Ferdinand, Fabio, Rafael, Evra; Valencia, Park, Nani, Obertan, Scholes, Fletcher, Carrick, Gibson; Rooney, Berbatov, Owen, Diouf.
LIGI KUU kuanzisha michuano maalum kuipata Timu ya 4 kucheza UEFA!!
Vigogo wapinga!!
Ligi Kuu England ipo mbioni kutaka kuanzisha michuano maalum ili kuipata Timu ya nne itakayocheza UEFA CHAMPIONS LIGI badala ya ule mtindo wa sasa wa Timu 4 za juu zinazomaliza Ligi kwenda moja kwa moja UEFA CHAMPIONS LIGI.
Mpango huo mpya utafanya Timu 3 tu za juu ndizo ziingie moja kwa moja UEFA na Timu zitakazomaliza nafasi ya 4 hadi ya 7 zicheze michuano maalum ili kuipata Timu moja itakayojumuika na hizo Timu 3 za juu.
Nia ya kuanzisha michuano hiyo maalum ni kuleta ushindani mkubwa kwenye Ligi Kuu baada ya kuwa inatawaliwa na Timu 4, nazo ni Chelsea, Manchester United, Arsenal na Liverpool, miaka nenda rudi.
Mpango huo wa michuano maalum umeungwa mkono na Timu zote isipokuwa vigogo hao wanne.
LIGI KUU: Huko mkiani, kuzama au kuzuka!!!
Nani Bingwa ni swali la Wadau wengi kwani Chelsea, Manchester United na Arsenal ndio wanaoelekea kuwa ndio wagombea pekee wa taji hilo kwa Timu zilizo juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu lakini huko mkiani nako kuna vita na mvutano mkubwa na wa kusisimua.
Portsmouth ndio iko mkiani kabisa na wengi wameshaiteua kuwa ndio moja ya Timu 3 zitakazoshuka Daraja msimu huu kwani licha ya nafasi yao hiyo ya mwisho, Klabu hiyo pia iko mashakani nje ya uwanja kwa kukabiliwa na matatizo makubwa ya kifedha na hata pia kuwa na kesi Mahakamani wanayotishiwa kufilisiwa.
Lakini, ukweli ni kwamba, juu ya Portsmouth kuna Timu 7 zilizotenganishwa na pointi 4 tu.
---------------------------------------------------------------------------------
MSIMAMO LIGI KUU England: [Timu zimecheza mechi 26 isipokuwa inapotajwa]
1 Chelsea pointi 58
2 Man Utd pointi 57
3 Arsenal pointi 52
4 Liverpool pointi 44
5 Man City pointi 44 [mechi 24]
6 Tottenham pointi 43]
7 Aston Villa pointi 42 [mechi 25]
8 Birmingham pointi 37 [mechi 25]
9 Everton pointi 35 [mechi 25]
10 Fulham pointi 34
11 Blackburn pointi 31
12 Stoke pointi 30 [mechi 24]
13 Sunderland pointi 26 [mechi 25]
14 West Ham pointi 24 [mechi 25]
15 Wolves pointi 25 [mechi 24]
16 Wigan pointi 24 [mechi 24]
17 Hull pointi 24
18 Burnley pointi 23 [mechi 25]
19 Bolton pointi 22 [mechi 24]
20 Portsmouth pointi 16 [mechi 25]
----------------------------------------------------------------------------------
Ukweli mwingine ni kwamba Ligi ya msimu huu imekuwa haitabiriki na hata zile Timu vigogo kama vile Manchester United, Chelsea, Arsenal na Liverpool zimepoteza mechi nyingi mno kupita ilivyo kawaida katika misimu mingine.
Kuna nadharia nyingi kuhusu matokeo ya kushangaza ya msimu huu.
Kuna wengine wanasema Ligi ya msimu huu si kali kama misimu mingine na wengine wanasema Timu za chini zimekuwa ngumu kufungika lakini kama hilo ni kweli mbona bado Timu za juu ni zilezile, yaani Chelsea, Man United na Arsenal?
Portsmouth ndio huyo ana nafasi kubwa ya kuporomoka ikizingatiwa yuko mkiani, hali yao kifedha ni duni na mechi zao zilizobaki ili waweze kujinusuru ndio zinazidi kuyoyoma.
Je nani wengine wanaweza kuungana nae?
Burnley ina hali tata licha ya kuwa inashinda sana nyumbani lakini tatizo lao kubwa ni kuwa nyanya ugenini.
Wolves nao wako mkumbo huo na pia wana tatizo kubwa la ufungaji magoli.
Hull City pia wako kwenye kundi hili la Burnley na Wolves na hawa wanajumuika pamoja na Wigan.
Bolton nao wako hatarini na mechi zao 6 zinazofuata- dhidi ya Wigan, Blackburn, Wolves, West Ham, Sunderland na Wigan [kwa mara ya pili] ndizo zitakazoamua hatima yao.
West Ham na Sunderland nazo zipo hatarini lakini hizi kidogo zinaonekana ni Timu nzuri na zikitulia zinaweza kujinasua.
Hali hii ya kutokuwa na fununu nani Bingwa na nani ndie mporomokaji kumeifanya Ligi ya msimu huu iwe tamu sana na wiki zijazo, bila shaka, zitatupa uhondo mtamu zaidi.
RATIBA WIKI HII:
UEFA CHAMPIONS LEAGUE, RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 16:
[Mechi zote kuanza Saa 4 dak 45 usiku saa za bongo]
Jumanne, 16 Februar1 2010
AC Milan v Man U
Lyon v Real Madrid
Jumatano, 17 Februari 2010
Bayern Munich v Fiorentina
FC Porto v Arsenal
LIGI KUU:
Jumanne, Februari 16
Stoke City v Man City
Jumatano, Februri 17
Wigan v Bolton
Bosi wa Palace ataka Mshika kibendera afungiwe!
Meneja wa Crystal Palace Neil Warnock ametaka afungiwe Refa Msaidizi Trevor Massey ambae alishika kibendera katika mechi ya jana ya FA Cup kati ya Crystal Palace na Aston Villa iliyoisha 2-2 baada ya Villa kusawazisha bao dakika ya 87 kufuatia kona ambayo Mchezaji alietoa mpira nje alikuwa ni wa Villa na hivyo ilipaswa kuwa golikiki badala ya kona.
Warnock amelalamika: “Goli lao la pili ni aibu! Tumetoka jasho na kupigana kufa na kupona na mwisho tunauawa kwa uzembe wa mtu! Nimeambiwa ikiwa Massey alikosea atasimamishwa lakini hilo linatusaidia nini?”
Sasa Aston Villa na Crystal Palace itabidi zirudiane huko Villa Park tarehe 24 Februari.
Warnock aliendelea kulalama: “Nilimwambia akatizame video na ataona kosa lake! Siwezi kusema zaidi kwani wanasikiliza na sitaki kupoteza pesa zangu kwa kulipa faini! Lakini huu ni wizi!”
Kwa Crystal Palace, ingawa wataona wameonewa kwa mechi kurudiwa, lakini ni bora kwao kifedha kwani Klabu hiyo ipo mikononi kwa Mfilisi kwa vile ina matatizo ya kifedha.
Mshindi kati ya Aston Villa na Crystal Palace atacheza na mshindi kati ya Reading au West Bromwich katika Robo Fainali ya Kombe hili la FA.

Sunday 14 February 2010

DROO YA ROBO FAINALI FA CUP:
Mara baada ya mechi ya mwisho ya Raundi ya 5 ya Kombe la FA hivi leo imefanyika Droo ya mechi za Robo Fainali ambazo zinatakiwa zichezwe Machi 6 na 7.
RATIBA NI [Timu inayotajwa kwanza ipo nyumbani]:
Chelsea v Man City au Stoke City
Fulham v Bolton au Tottenham
Reading au West Brom v Crystal Palace au Aston Villa
Portsmouth v Birmingham
FA Cup: Palace 2 Villa 2
Goli la dakika ya 87 la Petrov limeiokoa Aston Villa kutupwa nje ya Kombe la FA na hivyo kupata suluhu 2-2 huko Selhurts Park nyumbani kwa Timu Mufilisi Crystal Palace ambayo ni taabani kifedha.
Timu hizi sasa zitarudiana Villa Park Febrruari 24 kupata mshindi atakaeingia Robo fainali.
FA Cup: Fulham 4 Notts County 0
Fulham, wakiwa nyumbani Craven Cottage, wametinga Robo Failali ya Kombe la FA baada ya kuifumua Notts County manao 4-0.
Hadi mapumziko Fulham walikuwa mbele kwa bao 2-0 Wafungaji wakiwa Simon Davies na Bobby Zamora.
Kipindi cha pili, Damien Duff na Stefano Okaka wakaongeza bao 2 kwa Fulham.
Fujo baada ya mechi ya FA Cup jana!!
Mashabiki na Polisi walipambana mjini Southampton hapo jana mara baada ya Klabu ya Southampton kubamizwa 4-1 na jirani zao Portsmouth kwenye mechi ya Kombe la FA.
Fujo hizo za Mashabiki zilishamira nje ya Uwanja wa Mtakatifu Maria, Uwanja wa Southampton, huku matofali, chupa na viti vikirushwa kila upande na Polisi kulazimika kuwakamata Mashabiki kadhaa.
Mara nyingi Klabu hizi zilizo jirani zikikutana huwa kunatokea vurugu kati ya Mashabiki wao.
Jana Polisi walilazimika kufunga baa zote karibu ya Uwanja kwa masaa mawili ili kuzuia mlipuko wa fujo.
FA Cup: Bolton 1 Tottenham 1
Bolton na Tottenham itabidi zirudiane huko White Hart Lane baada ya kutoka suluhu 1-1 nyumbani kwa Bolton Reebok Stadium lakini Tottenham itabidi wajilaumu kwa kuukosa ushindi kwani walipewa penalti kipindi cha pili huku gemu ikiwa 1-1 iliyopigwa na Huddlestone lakini Kipa Jussi Jaaskelainen wa Bolton akaokoa.
Nahodha wa Bolton Kevin Davies ndie alifunga bao lao lililodumu hadi mapumziko lakini Jermaine Defoe akasawazisha kwa bomba kali kipindi cha pili.
Timu hizi zinategemewa kurudiana Februari 24.
Terry akiri makosa!!
Nahodha wa Chelsea John Terry amekubali kwamba yeye ndie alifanya makosa yaliyoruhusu bao zote mbili alizofunga Luis Saha Everton walipoibwaga Chelsea 2-1 hapo juzi huko Goodison Park.
Terry, alievuliwa Unahodha wa England kufuatia kashfa ya kutembea na gelfrendi wa Wayne Bridge aliekuwa Mchezaji mwenzake Chelsea, amepewa likizo fupi na Klabu yake ili apoze akili kufuatia skandali hilo na jana hakuwepo wakati Chelsea ilipoibamiza Cardiff 4-1 kwenye FA Cup.
Terry amewaomba radhi Mashabiki wa Chelsea kwa makosa yake na pia kwa kutokwenda upande wa jukwaa walilokaa Washabiki wa Chelsea huko Goodison Park kuwashkuru baada ya kipigo chao toka kwa Everton.
Terry ameahidi kuwa kuanzia sasa watahakikisha Wachezaji wote wanaenda kutoa shukrani kwa Washabiki baada ya mechi hata kama matokeo yakiwa mabaya.
Ferguson: Bora kucheza na Milan bila Kaka!
• Man United wako imara kwenda San Siro kuliko 2007
Sir Alex Ferguson amesema Manchester United haiwezi kutawaliwa na AC Milan Uwanjani San Siro kama ilivyotokea mwaka 2007 kwenye Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE waliyofungwa 3-0 na Kaka akiwa ndani ya Milan.
Manchester United watacheza na AC Milan hapo Jumanne huko San Siro kwenye mechi ya kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 na marudiano ni Machi 10 huko Old Trafford lakini safari hii Kaka hayuko tena na Timu hiyo kwani ameshahamia Real Madrid.
“Ni wakati muafaka kwenda San Siro.” Ferguson amesema. “Wikiendi hii wamecheza na kuifunga Udinese 3-2, wamempoteza Kaka na wana majeruhi! Sisi tumepumzika!”
Ferguson akaendelea kuongea kwa kuichambua AC Milan na kutamka kuwa imebadilika baada ya Kaka kuondoka na sasa wanatumia mfumo wa 4-3-3 huku Washambuliaji wakiwa Marco Borriello akiwa kati na pembeni mwake ni Ronaldinho kushoto na Pato kulia.
Pato hajacheza mechi hivi karibuni kwa sababu ya maumivu na Ferguson amesema ikiwa Pato hatocheza David Beckham atakuwa Winga ya kulia na itabidi wachunge krosi zake.
Ferguson amekiri kuumia kwa Giggs, alievunjika mkono, ni pigo lakini lakini amesema Timu yake nzima ni nzuri.
Fa Cup: Mechi za leo
Jumapili, Februari 14
[saa za bongo]
[saa 10 na nusu jioni]
Bolton v Tottenham
[saa 12 jioni]
Fulham v Notts County
[saa 12 dakika 45]
Crystal Palace v Aston Villa
FA Cup: Man City ulimi nje kwa Stoke!!
Straika wa Stoke City Ricardo Fuller ambae majuzi tu alikuwa mikononi mwa Polisi baada ya kupata tafarani kwenye Naiti Klabu ameiwezesha Stoke kupata suluhu ya 1-1na Man City na hivyo kulazimisha mechi yao ya Raundi ya 5 ya Kombe la FA kurudiwa uwanjani kwao.
Man City ndio walikuwa wa kwanza kufunga bao kupitia Shaun Wright-Phillips ambalo hasa unaweza kusema ni kama mchezo wa Ze Komedi kwa jinsi lilivyochekesha jinsi lilivyofungwa.
CAF CHAMPIONS LEAGUE: MATOKEO Jumamosi Februari 13
Yanga 2 v Saint Eloi Lupopo [Congo DR] 3
Sofapa [Kenya] 0 v El Ismaily [Misri] 0
Gaborone United [Botswana] 0 v Orlando Pirates [Afrika Kusini] 0
URA [Uganda] 1 v Zanaco [Zambia] 0
Armed Forces [Gambia] 1 v JS Kabyle [Algeria] 2
OS Balantas [Guinea-Bissau] 0 v Difaa El Jadida [Morocco] 0
KWINGINEKO ULAYA: Matokeo jana
BUNDESLIGA
Jumamosi, Februari 13
Stuttgart 1 v Hamburg 3
Bayer Leverkusen 2 v Wolfsburg 1
Hertha Berlin 1 v Mainz 05 1
Hannover 1 v Werder Bremen 5
Bochum 2 v 1899 Hoffenheim 1
Bayern Munich 3 v Borussia Dortmund 1
SERIE A
Jumamosi, Februari 13
Sampdoria 2 v Fiorentina 0
Roma 4 v Palermo 1
LA LIGA
Jumamosi, Februari 13
Xerez 0 v Real Madrid 3
Villareal 2 v Athletic Bilbao 1
Sporting Gijon 1 v Valencia 1
Powered By Blogger