Sunday 3 October 2010

Liverpool wapigwa kwao Anfield!
• Liverpool 1 Blackpool 2
Liverpool leo wamedidimizwa mkiani na kupelekwa nafasi ya 3 toka chini baada ya kutandikwa bao 2-1 na Blackpool uwanjani kwao Anfield.
Licha ya kufungwa, Liverpool pia wameingizwa kwenye wasiwasi baada ya Straika wao Nyota Fernando Torres kucheza dakika 9 tu na kisha kutolewa akiwa majeruhi.
Ni mabao ya kipindi cha kwanza ya Blackpool yaliyofungwa na Charlie Adam kwa penati baada ya Beki wa Liverpool Glen Johnson kumchezea rafu Luke Varney na la pili kufungwa na Luke Varney ndio yaliyowaibua Blackpool kidedea katika mechi yao ya kwanza hapo Anfield tangu Mwaka 1971.
Kipindi cha pili Liverpool waliibuka na kujipa matumaini pale Beki Kyrgiakos alipofunga kwa kichwa baada ya friki ya Steven Gerrard lakini Blackpool walisimama imara na kumaliza gemu washindi.
Vikosi vilivyoanza:
Liverpool: Reina, Johnson, Kyrgiakos, Skrtel, Carragher, Poulsen, Meireles, Kuyt, Gerrard, Cole, Torres.
Akiba: Jones, Jovanovic, Maxi, Lucas, Ngog, Spearing, Kelly.
Blackpool: Gilks, Eardley, Evatt, Cathcart, Crainey, Vaughan, Adam, Campbell, Grandin, Varney, Taylor-Fletcher.
Akiba: Halstead, Southern, Harewood, Ormerod, Sylvestre, Phillips, Keinan.
Refa: Michael Jones

No comments:

Powered By Blogger