Sunday 3 October 2010

Ferguson aridhika na pointi ya Sunderland
Bosi wa Manchester United Sir Alex Ferguson amesema sare ya 0-0 waliyoipata huko Sunderland ni sawa yao kwa vile Sunderland walicheza vizuri sana.
Sare hiyo imewafanya Man United wawe wametoka droo mechi zao zote 4 za Msimu huu walizocheza ugenini na kuwafanya wawe nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu wakiwa na pointi 13 kwa mechi 7 huku Chelsea wakiwa mbele yao wakiwa na pointi 15 kwa mechi 6.
Leo, Chelsea wanaivaa Arsenal na Manchester City wanacheza na Newcastle na hizi ni mechi ambazo zitageuza msimao wa Timu 4 za juu kama inavyoonyeshwa hapa:
1 Chelsea mechi 6, pointi 15
2 Man United mechi 7 pointi 13
3 Arsenal mechi 6 pointi 11
4 Man City mechi 6 pointi 11
Ferguson amesema ameridhika kwa kutofungwa goli hata moja hasa kwa vile Msimu huu difensi yake imekuwa ikivuja lakini kwa mechi mbili sasa tangu Rio Ferdinand kupona na kurudi uwanjani kuwa patna wa Nemanja Vidic, Man United haijafungwa bao.
Juzi Jumatano waliifunga Valencia bao 1-0 kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI.
Katika mechi hiyo ya jana, Man United walimpumzisha Nyota wao Wayne Rooney ambae alikuwa akiuguza enka.
Eriksson ni Bosi mpya Leicester City
Sven-Goran Eriksson ameteuliwa kuwa Meneja mpya wa Leicester City ambayo iko Daraja la Coca Cola Championship, chini tu ya Ligi Kuu, kuchukua nafasi ya Paulo Sousa alietimuliwa juzi Ijumaa.
Eriksson, Miaka 62, na aliewahi kuwa Kocha wa England na pia Manchester City, amesaini Mkataba wa Miaka miwili na Klabu hiyo ambayo iko mkiani kwenye Ligi ya Daraja lake.
Mwenyewe Eriksson ametamka: “Nina furaha kuwa hapa. Klabu inataka kupanda Ligi Kuu na hilo pia ni lengo langu.”
Eriksson amekuwa hana kibarua tangu alipoiongoza Ivory Coast kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini Mwezi Juni na kabla ya hapo alikuwa ni Mkurugenzi wa Soka huko Notts County kazi ambayo aliichukua mara baada ya kutupwa nje kama Kocha wa Mexico ambako alidumu kuanzia Juni 2008 hadi Aprili 2009.

No comments:

Powered By Blogger