Friday 8 October 2010

CHEKI KITU MPYA: www.sokainbongo.com


Morocco kuwakamia Mastaa wa Taifa Stars
Morocco, maarufu kama Simba wa Atlas, wamesema wanawatambua Wachezaji wazuri na hatari wa Taifa Stars na washabuni mbinu za kuwadhibiti kwenye mechi ya Kundi lao kuwania kufuzu kuingia Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Mwaka 2012 itakayochezwa hapo kesho Jumamosi Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Morocco imesema Wachezaji hao ni Kiungo Nizar Khalfan na Nahodha Shadrack Nsajigwa.
Timu kwenye Kundi D ni Algeria, Tanzania, Morocco na Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Katika mechi za kwanza, Algeria na Tanzania zilitoka sare 1-1 huko Algiers na Morocco, ikiwa nyumbani ilitoka 0-0 na Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Msemaji wa Msafara wa Morocco uliokuwa na Watu 40 amesema wameridhishwa na mapokezi yao tangu wawasili Dar es Salaam Jumatano usiku.
Msemaji huyo alitamka: “Tumefurahi. Tulipokuwa tukiingia Uwanja wa Taifa kwa mazoezi Mashabiki watushangilia na kutupungia mikono huku wakitaja majina ya Wachezaji wetu!”
Wengi wa Mashabiki hao walikuwa wakimtaja Straika wa Arsenal, Marouane Chamakh, ambae yupo kwenye Kikosi hicho.
Nae Kocha wa Morocco, Dominic Cuperly, amekisifia kiwanja cha kuchezea cha Uwanja wa Taifa na kusema ni moja ya viwanja bora Barani Afrika.
Wakati huo huo, Timu ya watu 26 ya Kituo cha TV maarufu cha Michezo Barani Afrika, Supersport, kimetua Dar es Salaam tayari kwa kulirusha moja kwa moja pambano hilo la Tanzania na Morocco kwenye Chaneli maarufu ya Soka Supersport 3, SS3.
Macheda amtaka radhi Rooney
Baada ya kukaririwa na Gazeti moja huko Italia akimsema Mchezaji mwenzake wa Manchester United, Wayne Rooney, kuwa ni mtu mzuri alietoka familia ya kimasikini na hana elimu lakini sasa anatamba kwa utajiri, Chipukizi Kiko Macheda imebidi aombe radhi kwa maneno hayo.
Inasemekana Macheda alimbembeleza Rio Ferdinand amwombee msamaha kwa Rooney .
Hata hivyo, marafiki wa Macheda, mwenye umri wa Miaka 19, wamedai Macheda mwenyewe ni kama Rooney tu kwa vile nae ametoka familia ya kimaskini na hana elimu.
Mmoja wa hao marafiki wa Macheda alisema: “Baba yake Macheda ni deiwaka! Mama yake ni mfagiaji! Macheda ni kama Rooney tu!”

No comments:

Powered By Blogger