Wednesday 25 November 2009

UEFA CHAMPIONS LEAGUE Leo:
FC Porto v Chelsea
Ingawa Klabu zote hizi mbili zimeshatinga Raundi nyingine ya mashindano haya, pambano hili la leo linalochezwa Estadio do Dragao huko Ureno lina umuhimu wa kuamua nani atamaliza yuko juu KUNDI D.
Chelsea wana pointi 10 toka mechi 4 na Porto wana 9.
Kocha wa Chelsea Catrlo Ancelotti amesema atawapumzisha Michael Essien na Didier Dogba ili wauguze maumivu yao na wawe fiti kwa mechi ya wikiendi ijayo ambapo Jumapili Chelsea watacheza na Arsenal kwenye Ligi Kuu.
Hata hivyo, Ancelotti amethibitisha kuwa Wachezaji wake wawili ambao ni Raia wa Ureno, Carvalho na Deco, watacheza mechi hiyo.
Man U v Besiktas
Manchester United tayari wameshaingia hatua inayofuata ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE na Sir Alex Ferguson ameshadokeza kuwa mechi hii ni sahihi kuwapa uzoefu Chipukizi wake kina Danny Welbeck, Obertan, Federico Macheda na Darren Gibson.
Pia, golini anaweza kuwepo Tomasz Kuszczak au Ben Foster ili kumpumzisha mkongwe Edwin van der Sar.
Kocha wa Besiktas, Mustafa Denizli, amekiri kuwa ni afadhali akutane na Timu kamili ya Man U kuliko Chipukizi wake kwa sababu wanawafahamu vizuri hao wakongwe na ni ngumu kuwakabili hao Chipukizi kwani hawawajui.
Kieran Gibbs wa Arsenal avunjika mguu!!!
Arsenal jana walipata pigo jingine la kuumia Mchezaji wao Kieran Gibbs katika mechi ya jana ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE ambayo Arsenal waliifunga Standard Liege 2-0 na kujikita Raundi inayofuata.
Gibbs alivunjika mfupa wa kidole cha mguuni na hivyo atakuwa nje miezi mitatu.
Hili ni pengo kubwa kwani Gibbs hucheza Beki tatu na yeye amepata namba baada ya Beki wa kawaida nafasi hiyo Gael Clichy kuwa majeruhi wa muda mrefu.
Sasa huenda nafasi hiyo ya Beki tatu ikazibwa na Mkongwe Mikael Silvestre katika mechi ijayo ambayo Arsenal watakwaana na Chelsea kwenye Ligi Kuu.
BENITEZ- Liverpool wasema yuko salama!!!
Rafa Benitez amegoma kukubali kuwa kutolewa kwa Timu yake Liverpool nje ya mashindano ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE ni maafa makubwa kwao na pia kuiweka kazi yake katika hatihati.
Benitez ameng’ang’ania Liverpool watamaliza Ligi Kuu wakiwa kwenye 4 bora.
Ili kumpa moyo, Menejimenti ya Liverpool imetamka kuwa Benitez hayupo hatarini kutimuliwa licha ya matokeo mabovu msimu huu.
Benitez amesema: “Tumecheza Ulaya miaka mitano mfululizo na kutwaa Kombe hilo, kutolewa ni kawaida kwenye soka! Sasa tujitayarisha na mechi ngumu wikiendi ijayo!”
Jumapili ijayo, Liverpool wanapambana na watani wao wa jadi Everton katika debi ya Mji wa Liverpool.
UEFA CHAMPIONS LEAGUE: Nini kilijiri jana Kundi hadi Kundi
KUNDI E
Fiorentina baada ya kuifunga Lyon 1-0 hapo jana imekwaa kilele cha Kundi hili huku Lyon wameporomoka hadi nafasi ya pili lakini Timu zote hizi zinasonga mbele kuingia Raundi inayofuata na kuwaacha Liverpool nje ya Kombe hili na sasa wanasubiri kuingizwa EUROPA LIGI.
Debrecen ya Hungary inaungana na Liverpool nje ya mashindano.
KUNDI F
Barcelona waliwapiga Inter Milan 2-0 hapo jana bila ya Nyota wao Lionel Messi na Zlatan Ibrahimovic ambao ni majeruhi.
Barcelona sasa wanaongoza Kundi hili wakiwa pointi 2 mbele ya Inter Milan huku Rubin Kazan wakifuatia na Dynamo Kiev wakishika mkia.
KUNDI H
Sevilla wameshatinga Raundi inayofuata lakini jana walifungwa na Unirea Urziceni bao 1-0 ambao wamejiongezea matumaini ya kusonga mbele na sasa wako pointi 2 mbele ya Timu ya 3 Stuttgart waliowachapa Rangers bao 2-0.
KUNDI H
Arsenal jana walitinga Raundi inayofuata itakayozihusisha Timu 16 zitakazocheza mtoano kwa kuishinda Standard Liege bao 2-0 Uwanja wa Emirates.
Olympiakos kwa kutoka dro 0-0 na AZ Alkmaar jana walikosa kujihakikishia kusonga mbele na sasa wanahitaji angalau pointi moja katika mechi yao ya mwisho watakayocheza na Standard Liege ili wasonge mbele.
UEFA CHAMPIONS LEAGUE: Liverpool NJEEEEEE!!!! Arsenal yasongaaaa!!!!!
Fiorentina imewafunga Lyon bao 1-0 huko Florence, Italia na hivyo kuhakikisha Liverpool wanatupwa nje ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE licha ya Liverpool kushinda ugenini huko Hungary walipoitungua Debrecen 1-0.
Kwenye Kundi hili ni Lyon na Fiorentina ndio wanasonga mbele kuingia Raundi ijayo ya Mtoano.
Liverpool sasa wanategemewa kuingizwa kwenye Raundi ifuatayo ya EUROPA LIGI.
Vikosi:
Debrecen: Poleksic, Bodnar, Meszaros, Mijadinoski, Fodor, Szelesi, Kiss, Szakaly, Czvitkovics, Laczko, Rudolf.
Akiba: Pantic, Ramos, Dombi, Komlosi, Bernath, Varga, Coulibaly.
Liverpool: Reina, Johnson, Carragher, Agger, Insua, Kuyt, Lucas, Mascherano, Aurelio, Gerrard, Ngog.
Akiba: Cavalieri, Aquilani, Benayoun, Kyrgiakos, Spearing, Skrtel, Dossena.
Refa: Bjorn Kuipers (Holland)
Nao Arsenal wakicheza nyumbani Uwanja wa Emirates huku wakihitaji pointi moja tu ili kusonga mbele Raundi ijayo waliwafunga Standard Liege bao 2-0.
Vikosi:
Arsenal: Almunia, Eboue, Gallas, Vermaelen, Gibbs, Fabregas, Song Billong, Denilson, Nasri, Arshavin, Vela.
Akiba: Mannone, Sagna, Rosicky, Eduardo, Walcott, Silvestre, Traore.
Standard Liege: Bolat, Camozzato, Sarr, Felipe, Mulemo, Goreux, Witsel, Mangala, Carcela-Gonzalez, Dalmat, Mbokani.
Akiba: Van Hout, Victor Ramos, Rocha, Traore, Gershon, Nicaise, Gohi-Bi.
Refa: Konrad Plautz (Austria)
MATOKEO: Jumanne, Novemba 24
Arsenal 2 v Standard Liege 0
AZ Alkmaar 0 v Olympiakos 0
Barcelona 2 v Inter Milan 0,
Debrecen 0 v Liverpool 1
Fiorentina 1 v Lyon 0
Rangers 0 v VfB Stuttgart 2
Rubin Kazan 0 v Dynamo Kiev 0
Unirea Urziceni 1 v Sevilla 0
RATIBA MECHI ZA Jumatano, Novemba 25
AC Milan v Marseille
Apoel Nicosia v Atletico Madrid
Bayern Munich v Maccabi Haifa
Bordeaux v Juventus
CSKA Moscow v Wolfsburg
Porto v Chelsea
Man U v Besiktas
Real Madrid v FC Zurich

Tuesday 24 November 2009

Portsmouth wamtimua Meneja!!!
Klabu ya Portsmouth ambayo ndiyo inashika mkia kwenye msimamo wa Ligi Kuu England leo imemfukuza kazi Meneja wao Paul Hart.
Msimu huu, Portsmouth imecheza mechi 13 za Ligi Kuu na kushinda 2, kutoka sare 1 na kufungwa mechi 10.
Portsmouth imesema haikutaka kumfukuza Hart na ilitaka kumbadili kazi na kumpa posti ya Mkurugenzi wa Ufundi ili asimamie na kukuza vipaji vya Timu yao ya Vijana wa kati ya umri wa miaka 18 hadi 21 lakini Hart akagomea mabadiliko hayo.
Klabu hiyo imesema sasa Timu itakuwa chini ya Makocha wa Timu ya Kwanza Paul Groves na Ian Woan hadi hapo atakapopatikana mtu wa kudumu.
Portsmouth imekuwa ikikumbwa na matatizo ya kifedha na iliuzwa hivi karibuni lakini mnunuzi huyo nae akaiuza na mpaka sasa ina utata kwenye umilikwaji wake.
UEFA CHAMPIONS LEAGUE: Leo Liverpool wanaombea maajabu!!! Arsenal wanahitaji pointi moja tu kusonga mbele!!
Liverpool wako ugenini huko Hungary kupambana na Debrecen na ili wabaki na matumaini ya kusonga mbele kwenye michuano ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE ni lazima washinde na pia waombe Mungu Fiorentina wasiifunge Lyon katika mechi zinazochezwa leo za KUNDI E.
Katika KUNDI H, Arsenal leo wako nyumbani Emirates Stadium kucheza na Timu ya Ubelgiji Standard Lege na Arsenal, wakiwa wamebakisha mechi 2 katika Kundi lao, wanahitaji pointi moja tu katika hizo mechi 2 ili kusonga Raundi ya Pili ya Mtoano.
Mechi nyingine kwenye Kundi la Arsenal ni kati ya Olympiakos na AZ Alkmaar.
Refa Alan Wiley hamshitaki Fergie!
Refa Alan Wiley amesema kuwa hana nia ya kumshitaki Sir Alex Ferguson Mahakamani ili kudai fidia kwa kauli ya kashfa aliyoitoa Meneja huyo wa Manchester United alipodai Refa huyo hayuko fiti kuchezesha mechi.
Ferguson alitoa kauli hiyo Oktoba 3 mara baada ya Man U kutoka sare 2-2 na Sunderland katika mechi ya Ligi Kuu iliyochezwa Old Trafford.
Wiley amethibitisha hataki kuendeleza ugomvi na Ferguson licha ya Allan Leighton, Katibu wa Chama che Kutetea Maslahi Marefa, kutoa shinikizo Ferguson adaiwe fidia Mahakamani.
Ferguson alimwomba msamaha Refa Wiley na pia kukiri makosa yake kwa FA waliomshitaki na kisha kumwadhibu kufungiwa mechi 2 huku mechi 2 nyingine zikiwekwa kiporo ili kuchunga mwenendo wake hadi msimu wa 2010/11 utakapoisha na pia alipigwa faini ya Pauni 20,000.
Wachezaji Wigan kurudisha viingilio vya Mashabiki wao walioshuhudia kipigo chao cha mabao 9!!!!!
Mashabiki 400 wa Wigan waliosafiri hadi Jijini London Uwanjani White Hart Lane na kushuhudia Timu yao ikifumuliwa mabao 9-1 na Tottenham kwenye mechi ya Ligi Kuu iliyochezwa Jumamosi watarudishiwa pesa walizolipa kiingilio na watakaolipa pesa hizo ni Wachezaji wenyewe wa Wigan.
Kipigo hicho cha Wigan cha 9-1 ni kikubwa cha pili kwenye historia ya Ligi Kuu cha kwanza kikiwa kile cha mwaka 1995 wakati Manchester United walipowashushia Ipswich Town kipigo cha mabao 9-0.
Nahodha wa Wigan, Mario Melchiott, amesema wao wamehuzunika na ili kuomba msamaha kwa Mashabiki wao, wameamua wao wenyewe kutoa pesa zao wenyewe kuwarudishia Mashabiki wao walioshuhudia kipigo hicho.
FIFA yaitisha kikao cha dharura Desemba!!!
FIFA imeitisha kikao cha dharura mwezi ujao ili kujadili matukio yaliyotokea kwenye mechi za Mtoano kutafuta Timu za mwisho zilizoingia Fainali Kombe la Dunia.
Tukio kubwa lililoitikisa Dunia ya Soka ni pale Ufaransa walipotinga Fainali za Kombe la Dunia kwa msaada wa ‘upofu’ wa Refa Martin Hansson wa Sweden ambae hakumwona Thierry Henry akishika mpira na kumpasia William Gallas katika dakika ya 104 ya dakika za nyongeza na Gallas kuisawazishia Ufaransa na kufanya matokeo kuwa 1-1 dhidi ya Ireland na hivyo kuingia Fainali.
Licha ya Henry kukiri maovu yake na Ireland kudai mechi irudiwe, FIFA iling’ang’ana ‘uamuzi wa Refa ni wa mwisho’.
Matukio mengine ni yale yaliohusu mechi za Misri na Algeria ambazo zilibidi zirudiane uwanja nyutro huko Khartoum, Sudan baada ya kulingana kila kitu na ambako, hatimaye, Algeria alishinda 1-0 na kuingia Fainali Kombe la Dunia.
Kabla ya mechi ya awali iliyochezwa huko Cairo, Misri basi la Wachezaji wa Algeria lilipigwa mawe na Wachezaji kadhaa wakajeruhiwa. Kitendo hicho kiliibua hasira huko Nchini Algeria ambako Raia kadhaa wa Misri waishio huko waliumizwa, mali zao kuharibiwa na wengine walilazimika kuikimbia Nchi hiyo.
Vilevile, mechi kadhaa za Kombe la Dunia zilikuwa zimegubikwa na maamuzi ya utata wa Marefa.
Pia, FIFA imekisimamisha Chama cha Soka cha Iraq baada ya Chama hicho kuingiliwa na Serikali ya Iraq katika uendeshwaji wake.
Kikao hicho kinategemewa kufanyika wiki ijayo huko Cape Town, Afrika Kusini ambako pia kutapangwa Makundi na Ratiba ya Fainali za Kombe la Dunia.

Monday 23 November 2009

Licha ya kusuasua, Benitez aota kumaliza Ligi wakiwa juu!!!
Bosi wa Liverpool Rafael Benitez amesisitiza Timu yake itamaliza Ligi Kuu England ikiwa kwenye 4 bora na hivyo kucheza Ulaya licha ya juzi kutoka sare 2-2 na Manchester City kwenye mechi ya Ligi Kuu, hiyo ikimaanisha katika mechi 13 za Ligi Kuu walizocheza msimu huu wameshinda 6, suluhu 2 na kufungwa mechi 5 na wako pointi 13 nyuma ya vinara Chelsea huku wakiwa nafasi ya 7.
Ndoto ya Benitez imekuja huku akijipa matumaini kuwa Kikosi chake kina majeruhi kadhaa na wakipona basi wataonyesha makali yao.
Benitez ametamka: “Wachezaji wetu wote wakirudi tutaanza kushinda!”
Huenda FIFA ikamwadhibu Henry!!!
Kuna taarifa kuwa Kamisheni ya Nidhamu ya FIFA inachunguza tukio la Thierry Henry kuushika mpira na kumpasia mwenzake William Gallas aliefunga bao na kufanya mechi ya Ufaransa na Republic of Ireland iwe 1-1 na hivyo kuipa Ufaransa ushindi wa kuingia Fainali Kombe la Dunia.
Kitendo hicho hakikuonekana na Refa Martin Hansson.
Licha ya Thierry Henry mwenyewe kuungama makosa yake na madai ya Ireland na Wadau wengine kutaka mechi hiyo irudiwe, FIFA imeng’ang’ania msimamo wake wa kihistoria kuwa ‘uamuzi wa Refa ni wa mwisho’ na hivyo hamna uwezekano mechi hiyo kurudiwa.
Taarifa hizo zimesema ndani ya wiki mbili zijazo Kamisheni hiyo itakutana na kutoa uamuzi kama Henry anastahili adhabu kwa ‘kitendo kisicho cha uanamichezo’.
Taarifa hizo zimetoa mifano ya FIFA kuwachukulia hatua Wachezaji hapo nyuma kwa makosa ambayo Refa hakuyaona na ametajwa Mchezaji Marco Materazzi wa Italia aliefungiwa mechi 2 na kupigwa faini Pauni 4,500 kwa kumchokoza Mfaransa Zinedine Zidane katika Fainali ya Kombe la Dunia na kumsababisha Zidane akasirike na kumtwanga kichwa Materazzi na hivyo Zidane kupewa Kadi Nyekundu na Refa huku Materazzi hakupewa Kadi yeyote.
Wakati huohuo Refa aliehusika na mzozo wa Thierry Henry kuushika mpira, Martin Hansson kutoka Sweden ambae hakuona kitendo hicho, huenda asipate msukosuko wowote toka FIFA kwani yumo kwenye listi ya awali ya Marefa watakaochezesha Fainali Kombe la Dunia.
Timu ya Beckham LA Galaxy yaukosa Ubingwa Marekani!!
Los Angeles Galaxy leo alfajiri imefungwa kwa penalti kwenye Fainali ya Ubingwa wa Marekani, MLS, na Real Salt Lake ambao wameutwaa Ubingwa wa Marekani.
Timu hizo zilitoka sare 1-1 na ndipo kwenye penalti LA Galaxy wakatolewa 5-4.
Mechi hiyo ilichezwa Mjini Seattle huko Marekani.
Ferguson: “England hawawezi kuchukua Kombe la Dunia!”
Licha ya uwezekano wa Wachezaji wake 9 kuwemo kwenye Kikosi cha England kitakachocheza Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwakani, Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson ametamka haamini kama England watashinda na anaiona Brazil kama ndio watakaobeba Kombe hilo.
Ferguson amenena: “Sioni mtu atakaepita kwa Brazil! Wao ni kama mtambo wa Wachezaji bora! Msimu uliokwisha kwenye UEFA CHAMPIONS LEAGUE, Brazil walitoa Wachezaji 103 na ni 13 tu walitoka England!”
Wachezaji wa Manchester United ambao wamo kwenye uwezekano wa kuwa kwenye Kikosi hicho cha Kombe la Dunia ni Wayne Rooney, Rio Ferdinand, Michael Carrick, Wes Brown, Ben Foster, Owen Hargreaves, Michael Owen, Gary Neville na Danny Welbeck.
GOLI 9 ZAMFEDHEHESHA KOCHA WIGAN!!!
Martinez: "Haikubaliki na hatukutegemea!"
Kocha wa Wigan, Roberto Martinez, amesema kipigo walichokipata jana Uwanjani White Hart Lane nyumbani kwa Tottenham ni fedheha na aibu kubwa.
Martinez amesema: "Ni fedheha! Tulilinda lango letu kijinga! Sijawahi kuhusika na gemu kama hii!"
Martinez ameendelea kusema walicheza vizuri hadi mapumziko huku Tottenham wakiongoza kwa bao la Peter Crouch lakini bao 5 za Jermaine Defoe kipindi cha pili ziliwaumiza.
Martinez ameongeza: "Tutachunguza kila kitu na kuangalia kila kitu! Inabidi tujue nini kilitokea na hilo litatufanya tuwe na nguvu baadae!"
Nae Meneja wa Tottenham, Harry Redknapp, amesema: "Ni siku mbaya kwa Martinez na ninamuheshimu sana!! Ni Meneja kijana mdogo mwenye kipaji na nina uhakika ataimarika zaidi na watalipiza kisasi kwa mtu!"

Sunday 22 November 2009

Tottenham 9 Wigan 1
Defoe afunga 5!!!
Mechi hii ya Ligi Kuu iliyochezwa leo huko White Hart Lane ilikuwa 1-0 mpaka haftaimu huku Tottenham wakiwa mbele kwa bao la Peter Crouch.
Lakini kipindi cha pili mambo yaligeuka na Mshambuliaji wa Tottenham Jermaine Defoe akacharuka na kufunga bao 5 na kumfanya aweke rekodi ya kuwa mmoja wa Wachezaji watatu waliowahi kufunga bao 5 katika mechi moja ya Ligi Kuu wengine wakiwa ni Alan Shearer wa Newcastle na Andy Cole wa Manchester United.
Na hii ni mara ya pili kwa Timu kuifunga Timu nyingine kwenye Ligi Kuu mabao 9 mara ya kwanza ikiwa ni mwaka 1995 pale Manchester United walipoibamiza Ipswich Town mabao 9-0.
Wafungaji wengine wa Tottenham mbali ya bao la kwanza la Crouch na 5 za Defoe ni Aaron Lennon, Niko Krancjar na Kipa wa Wigan Chris Kirkland kujifunga mwenyewe baada ya mpira kugonga posti na kumpiga mgongoni.
Bao la Wigan lilifungwa na Paul Scharner.
RATIBA YA MECHI ZA WIKI IJAJO:
[saa za bongo]
UEFA CHAMPIONS LEAGUE
[saa 4 dak 45 usiku]
Jumanne, Novemba 24
Arsenal v Standard Liege
AZ Alkmaar v Olympiakos
Barcelona v Inter Milan,
Debrecen vLiverpool
Fiorentina v Lyon
Rangers v VfB Stuttgart
Rubin Kazan v Dynamo Kiev
Unirea Urziceni v Sevilla
Jumatano, Novemba 25
AC Milan v Marseille
Apoel Nicosia v Atletico Madrid
Bayern Munich v Maccabi Haifa
Bordeaux v Juventus
CSKA Moscow v Wolfsburg [Itaanza mapema]
FC Porto v Chelsea
Man U v Besiktas
Real Madrid v FC Zurich
LIGI KUU ENGLAND
Jumatano, Novemba 25
[saa 4 dak 45 usiku]
Hull v Everton
[saa 5 usiku]
Fulham v Blackburn
Jumamosi, Novemba 28
[saa 12 jioni]
Blackburn v Stoke
Fulham v Bolton
Man City v Hull
Portsmouth v Man U
West Ham v Burnley
Wigan v Sunderland
[saa 2 na nusu usiku]
Aston Villa v Tottenham
Jumapili, Novemba 29
[saa 9 mchana]
Wolves v Birmingham
[saa 10 na nusu jioni]
Everton v Liverpool
[saa 1 usiku]
Arsenal v Chelsea
Bolton 0 Blackburn 2
Bolton leo wamepata kipigo cha 2-0 wakiwa nyumbani kwao toka kwa Blackburn ambao hawajahi kushinda mechi ya Ligi Kuu wakiwa ugenini katika mechi 10 za mwisho za ugenini walizocheza mpaka hii leo.
Blackburn leo wamecheza mechi hii bila ya Meneja wao Sam Allardyce ambae ni mgonjwa anaetegemewa kufanyiwa operesheni ya moyo wiki hii.
Nafasi yake ilichukuliwa na Meneja Msaidizi Neil McDonald.
Bao la kwanza lilifungwa na David Dunn kwa shuti kali akiwa nje ya boksi kwenye dakika ya 30 kipindi cha kwanza.
Dakika ya 74, Blackburn wakapata bao la pili ambalo Bolton walijifunga wenyewe na jinsi lilivyofungwa ilikuwa kama Ze Komedi!
Brett Emerton wa Blackburn akiwa winga ya kulia alipiga krosi ambayo kwa wengi ilikuwa ni ya kubahatisha lakini Kipa wa Bolton Jussi Jaaskelainen akatoka golini kuifuata bila Sentahafu wake Sam Ricketts kujua na Ricketts akairukia krosi hiyo na kupiga kichwa kuelekea golini kumrudishia Kipa akidhani Kipa Jaaskelainen yupo kumbe ni goli tupu na kujifunga mwenyewe!
Wenger: “Tunazungumza na Gallas, Rosicky na Vela kuwaongezea mkataba”
Arsene Wenger ametangaza kuwa wako kwenye mazungumzo na Wachezaji wake William Gallas, Tomas Rosicky na Carlos Vela ili waongezewe na kupewa mikataba mipya.
Gallas na Rosicky wako kwenye mwaka wa mwisho wa mikataba yao inayoisha mwishoni mwa msimu huu na kisheria ifikapo Januari watakuwa huru kuongea na Klabu nyingine yeyote ili kuhamia Klabu hizo.
Lakini Meneja wa Arsenal Wenger anaamini Wachezaji hao watabaki Arsenal.
Kuhusu Vela, Wenger amesema: “Hatujapata ofa yeyote kuhusu Vela na sisi tunataka kuuboresha mkataba wake. Ni Mchezaji mdogo lakini mbele yake kuna Vijana wazuri kama yeye. Alipoondoka Adebayor sikuhangaika kupata mbadala wake kwani najua Vela yupo na ni mzuri!”
Fergie: “Ni ngumu kununua Mchezaji Januari!”
Bosi wa Manchester United Sir Alex Ferguson amesema hadhani kama atanunua Mchezaji wakati dirisha la uhamisho litakapofunguliwa mwezi Januari ingawa amehusishwa na Wachezaji kadhaa akiwepo Kijana mzuri sana wa Everton Jack Rodwell.
Lakini Ferguson amekataa na kusisitiza hawezi kulipa dau la bei mbaya kwa Mchezaji yeyote na vile vile hana tatizo na Kikosi chake cha sasa.
Ferguson amesema: “Kuna Wachezaji wengi kwenye soko lakini Klabu zao zinawathamini kwa dau la Pauni Milioni 50! Kwa bei hiyo sioni kama Wachezaji hao wana thamani hiyo!”
Powered By Blogger