Saturday 31 October 2009

Man U 2 Blackburn 0
Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu England, Manchester United, wamewafunga Blackburn mabao mawili kwa bila katika mechi ambayo waliitawala kabisa na ambayo tofauti na mechi nyingi za leo Kadi Nyekundu haikutoka.
Magoli ya Berbatov na Rooney ndio yaliyowapa ushindi Man U.
Man Utd: Van der Sar, O'Shea, Brown, Jonathan Evans, Evra, Valencia, Carrick, Anderson, Nani, Berbatov, Rooney.
Akiba: Kuszczak, Owen, Scholes, Fabio Da Silva, Fletcher, Obertan, De Laet.
Blackburn: Robinson, Chimbonda, Samba, Nelsen, Givet, Nzonzi, Emerton, Dunn, Andrews, Diouf, Di Santo.
Akiba: Brown, McCarthy, Grella, Pedersen, Kalinic, Hoilett, Salgado.
Refa: Phil Dowd
Laana ya kuifunga Man U yawakumba Liverpool!!!
Chelsea wajikita kileleni!!!
Kadi Nyekundu bwelele, 8 zatembezwa!!!
Baada ya furaha ya kuwafunga Manchester United wiki iliyokwisha leo Liverpool wamelizwa vibaya na, bahati mbaya kwao, Refa hakuwa upande wao baada ya kuwanyuka Kadi nyekundu mbili.
Wakiwa ugenini Craven Cottage, Liverpool walishindiliwa mabao 3-1 na Fulham na kumaliza mechi wakiwa mtu 9 baada ya Degen na Carragher kupewa Kadi Nyekundu.
Chelsea, wakicheza ugenini, waliishindilia Bolton mabao 4-0 na kujikita vizuri kileleni mwa Ligi Kuu.
Mbali ya stori ya leo ya kufungwa Liverpool, vichwa vya habari ni Kadi Nyekundu 8 zilizotolewa leo.
Wachezaji waliolambwa NYEKUNDU mechi za leo ni:
-Samuel [FULHAM]
-Kenwyne Jones [SUNDERLAND]
-Kovac [West Ham]
-Carragher LIVERPOOL]
-Degen [LIVERPOOL]
-Giovanni [HULL]
-Bilyaletdinox [EVERTON]
-Cuellar [ASTON VILLA]
MATOKEO KAMILI:
Jumamosi, Oktoba 31
Arsenal 3 v Tottenham 0
Bolton 0 v Chelsea 4
Burnley 2 v Hull 0
Everton 1 v Aston Villa 1
Fulham 3 v Liverpool 1
Portsmouth 4 v Wigan 0
Stoke City 2 v Wolverhampton Wanderers 2
Sunderland 2 v West Ham 2
Arsenal wawatoa nishai jirani zao Tottenham!!
Arsenal 3 Tottenham 0
Katika dabi ya Timu za Kaskazini ya London, Arsenal wakiwa kwao Emirates Stadium waliwapiga Tottenham mabao 3-0 kwenye mechi ya Ligi Kuu iliyoanza mapema kuliko mechi nyingine za leo Jumamosi Oktoba 31.
Mpaka mapumziko Arsenal walikuwa mbele kwa bao 2-0 kwa mabao yaliyofungwa ndani ya dakika moja katika dakika ya 43 Mfungaji akiwa Van Persie na la pili sekunde chache baadae kwa bao zuri sana la Nahodha Fabregas.
Bao la 3 alifunga Van Persie.
Vikosi:
Arsenal: Almunia, Sagna, Gallas, Vermaelen, Clichy, Fabregas, Song Billong, Diaby, Bendtner, van Persie, Arshavin.
AKIBA: Mannone, Senderos, Nasri, Eduardo, Ramsey, Eboue, Gibbs.
Tottenham: Gomes, Corluka, King, Bassong, Assou-Ekotto, Bentley, Huddlestone, Palacios, Jenas, Keane, Crouch.
AKIBA: Button, Hutton, Bale, Pavlyuchenko, Dawson, Kranjcar, Woodgate.
Refa: Mark Clattenburg
KOMBE LA CARLING: DROO YA ROBO FAINALI YATANGAZWA!!
Blackburn v Chelsea
Manchester City v Arsenal
Manchester United v Tottenham
Portsmouth v Aston Villa
Mabingwa Watetezi Manchester United watakuwa wenyeji wa Tottenham kwenye Robo Fainali ya Kombe la Carling, timu ambayo ndiyo waliifunga kwenye Fainali na kutwaa Kombe hilo.
Manchester City watawakaribisha Arsenal City of Manchester Stadium na hii mechi inategemewa kuleta msisimko kwani kwenye mechi ya Ligi Kuu uwanjani hapo mwanzoni mwa msimu ambayo Man City waliikung’uta Arsenal 4-2 vituko vya Mshambuliaji wa Man City, Emmanuel Adebayor, vilizua kasheshe kubwa na kusababisha Mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal afungiwe kwa kumtimba Van Persie na kupigwa faini kwa kwenda kuwabeza Washabiki wa Arsenal mara baada ya kufunga goli.
Mechi hizo za Robo Fainali zitachezwa wiki ya kuanzia Novemba 30.
Mchezaji Marlon King alie lupango azua mjadala!!
Wenger asema akitoka jela aendelee kucheza!!
Mchezaji wa Wigan, Marlon King, aliefungwa miezi 18 kwa kumshambulia na kumvunja pua mwanamke ndani ya baa jijini London amezua mjadala mkali unaohusu ajira yake mara baada kutoka jela.
Mara baada ya hukumu hiyo, Klabu yake ya Wigan imesema itampa notisi ya siku 14 na kumfukuza.
Mwenyekiti wa Wigan Dave Whelan amezitaka Klabu za England zisimpe nafasi ya kucheza tena soka England.
Lakini Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, amemtetea na kusema: “Naamini kuna sheria na haki hapa Uingereza na hiyo jela ndiyo haki aliyopata. Akimaliza kifungo yuko huru basi Klabu inayomtaka imchukue tu!”
Wachezaji wanne wa England wamo Listi ya FIFA ya Wagombea MCHEZAJI BORA DUNIANI!!!
Ni Terry, Lampard, Gerrard na Rooney!!
Mastaa wa England John Terry, Frank Lampard, Steven Gerrard na Wayne Rooney ni miongoni mwa Listi ya Wachezaji 23 watakaoshindania Tuzo ya MCHEZAJI BORA DUNIANI WA MWAKA.
Miongoni mwao yumo Lionel Messi anaetegemewa kuinyakua Tuzo hiyo na pia yumo Mshindi wa mwaka jana Cristiano Ronaldo.
Kwa upande wa Wanawake kuna majina 10 likiwemo la Marta wa Brazil Mshindi wa mwaka jana.
Manahodha na Makocha wa Timu za Taifa ndio watawapigia kura wagombea na Washindi wa 5 wa juu watakaoingia fainali watatangazwa mwanzoni mwa Desemba.
Mshindi wa Tuzo atatangazwa Desemba 21.
Listi kamili:
WANAUME: Michael Ballack, Gianluigi Buffon, Iker Casillas, Cristiano Ronaldo, Diego, Didier Drogba, Michael Essien, Samuel Eto’o, Steven Gerrard, Thierry Henry, Zlatan Ibrahimovic, Andres Iniesta, Kaka, Frank Lampard, Luis Fabiano, Lionel Messi, Carles Puyol, Franck Ribery, Wayne Rooney, John Terry, Fernando Torres, David Villa, Xavi.
WANAWAKE: Nadine Angerer, Sonia Bompastor, Cristiane, Inka Grings, Mana Iwabuchi, Simone Laudehr, Marta, Brigit Prinz, Kelly Smith, Abby Wambach.
LIGI KUU ENGLAND Wikiendi hii:
Leo ni dabi ya London Kaskazini: Arsenal v Tottenham!!!
*************************************************************
RATIBA LIGI KUU ENGLAND:
[Saa za Bongo]
Jumamosi, Oktoba 31
Arsenal v Tottenham [saa 9 dak 45 mchana]
[saa 12 jioni]
Bolton v Chelsea
Burnley v Hull
Everton v Aston Villa
Fulham v Liverpool
Portsmouth v Wigan
Stoke City v Wolverhampton Wanderers
Sunderland v West Ham
Manchester United v Blackburn Rovers [saa 2 na nusu usiku]
Jumapili, Novemba 1
[saa 1 usiku]
Birmingham v Manchester City
*******************************************************************************
Arsenal v Tottenham
Ligi Kuu England leo itaanza kuchezwa kwa pambano la Mahasimu wa Jiji moja, eneo moja, London Kaskazini, kati ya Arsenal na Tottenham Uwanjani Emirates.
Msimu uliokwisha, mechi kama hii, ikiwa ni mechi ya kwanza kwa Harry Redknapp tangu ateuliwe Meneja wa Tottenham, mechi iliisha kwa suluhu ya 4-4.
Ushindani na ushabiki kwa pambano hilo tayari ushapamba moto huku Redknapp akisema Arsenal hawawezi kuchukua Ubingwa na akawapa Chelsea na Manchester United nafasi kubwa.
Juu ya yote, Tottenham haijawahi kuifunga Arsenal katika mechi yeyote ya Ligi kwa miaka 10 sasa.
Bolton v Chelsea
Vinara wa Ligi Kuu Chelsea leo wanasafiri hadi Kaskazini Magharibi mwa England kucheza na Bolton Wanderers na hii itakuwa mechi ya pili kati ya Timu hizi ndani ya wiki moja kwani majuzi kwenye Kombe la Carling Chelsea waliitandika Bolton 4-0 uwanjani Stamford Bridge.
Hata hivyo, Chelsea kati mechi 2 zilizopita za Ligi walizocheza ugenini zote wamefungwa na hilo pengine litawapa matumaini Bolton.
Fulham v Liverpool
Baada ya kuwafunga Mabingwa Manchester United bao 2-0 mechi iliyopita, leo Liverpool wapo Craven Cottage kucheza na Fulham bila Nahodha wao Steven Gerrard ambae bado ni majeruhi.
Kiungo mpya wa Liverpool, Alberto Aquilani, ambae alicheza robo saa katika kipigo cha Kombe la Carling Jumatano walichokipata kwa Arsenal, huenda leo akacheza mechi yake ya kwanza ya Ligi.
Manchester United v Blackburn Rovers
Bila shaka leo Man U watashuka uwanjani huku wakitaka ushindi kwa kila hali baada ya kufungwa na Mahasimu wao Liverpool wiki iliyopita.
Man U leo huenda ikawa na pengo kwenye ulinzi kufuatia kuumia kwa Masentahafu Rio Ferdinand na Nemanja Vidic.
Blackburn nao wmekumbwa na gonjwa la Mafua ya Nguruwe hivyo inawezekana wakawakosa Wachezaji wao kama Chris Samba, Dunn na Jason Roberts.
Pengine kivutio kikuu kwenye mechi hii atakuwa Refa Phil Dowd ambae mechi yake ya mwisho kuichezesha Man U walipocheza na Fulham msimu uliopita aliwapa Kadi Nyekundu Scholes na Rooney na hivyo Wadau watafuatilia uchezeshaji wake hasa kufuatia ugomvi wa Sir Alex Ferguson na Marefa pale alipomsema Refa Alan Wiley hayuko fiti na baada ya hapo mechi zote za Man U zimekumbwa na maumuzi tata kwa Man U zikiwemo Kadi Nyekundu na kubeba wapinzani wao.
FIFA U-17 WORLD CUP NIGERIA 2009
Nigeria, Argentina, Uswisi na Mexico zaingia Raundi ya Pili!
Germany na Brazil zasubiri kama zitasonga kwa ushindi wa 3!!!
MATOKEO MECHI ZA Ijumaa, Oktoba 30:
KUNDI A
Germany 3 v Honduras 1
Argentina 1 v Nigeria 2
KUNDI B
Japan 0 v Mexico 2
Switzerland 1 v Brazil 0
Wenyeji Nigeria, baada ya kuanza kwa suluhu mechi yao ya kwanza, hatimaye jana waliifunga Timu ngumu Argentina 2-1 na kuingia Raundi ya Pili kama Washindi wa kwanza wa Kundi lao.
Licha ya kufungwa, Argentina nao wamesonga mbele kama Washindi wa Pili KUNDI A huku Germany anasubiri matokeo ya Makundi mengine ili kujua kama atafaulu kusonga mbele kama mmoja wa Washindi wa Tatu bora wanne.
Katika Kundi B Uswisi na Mexico zimemaliza nafasi za kwanza na za pili na hivyo kusonga mbele na kuwaacha Brazil wakisubiri hatima yao kama Mshindi wa 3.
MECHI ZA LEO Jumamosi, Oktoba 31:
KUNDI C
31/10/09 Gambia v Colombia
31/10/09 Netherlands v Iran
KUNDI D
31/10/09 Burkina Faso v Costa Rica
31/10/09 New Zealand v Turkey

Friday 30 October 2009

KESI YA MARADONA FIFA: AFA wawasilisha utetezi FIFA
AFA, Chama cha Soka cha Argentina, kimepeleka ripoti yao FIFA ili uwe utetezi wa Maradona baada ya FIFA kumfungulia uchunguzi kufuatia matusi aliyoyatoa kwenye TV laivu mara baada ya Argentina kuifunga Uruguay 1-0 huko Montevideo, Uruguay Oktoba 14 na kufuzu kuingia Fainali Kombe la Dunia mwakani.
Mwanasheria wa AFA, Hugo Passos, amesema Maradona alikuwa amekasirishwa na Waandishi wa Habari waliomwekea presha kuwa Argentina haitafika Fainali Kombe la Dunia na ndio maana akakasirishwa na kuwatukana mara baada ya kufanikiwa kuiingiza Argentina Fainali.
Endapo FIFA itamtia hatiani Maradona basi anaweza kupigwa Faini na kufungiwa mechi 5 na hilo linaweza kumwondoa asiisimamie Argentina Fainali Kombe la Dunia.
Mwenyewe Maradona amekataa kuomba radhi kuhusu tukio hilo la Montevideo.
Tangu Maradona achukue Ukocha Argentina Novemba 2008 baada ya kujiuzulu Alfio Basile amekuwa na migongano na Wachezaji, Makocha, Waandishi na Wakurugenzi.
Mchezaji Juan Roman Riquelme ambae ni Kiungo Nyota wa Argentina alijitoa kuichezea Argentina kwa sababu ya Maradona na amemsema Kocha huyo ‘haishi kwa kufuata anachokisema’.
Maradona pia aligombana na Carlos Bilardo ambae alikuwa Kocha wa Argentina iliyotwaa Kombe la Dunia mwaka 1986 ambae aliteuliwa na AFA awe Mkurugenzi wa Ufundi wa Argentina ili kumsaidia Maradona na Maradona akatamka Bilardo ni Mzee anaestahili kuvaa suti na tai na kukaa tu kwenye jukwaa la Waheshimiwa na si kumsaidia yeye.
Fergie alaumu England kucheza mechi za kirafiki katikati ya msimu!!
Bosi wa Manchester United Sir Alex Ferguson amesema uamuzi wa FA wa kupanga mechi za kirafiki kwa Timu ya Taifa ya England ambayo tayari imeshajikita Fainali za Kombe la Dunia mwakani huko Afrika Kusini unaziathiri Klabu za Ligi Kuu England ambazo sasa zinakabiliwa na mechi ngumu za Ligi, UEFA CHAMPIONS LEAGUE, Makombe ya FA na Carling.
Ingawa Ferguson hakuitaja mechi ipi inamkera lakini Wadau wanahisi ni ile mechi ya kirafiki katikati ya Novemba na Brazil ambayo itachezwa Doha, Qatar na hivyo kuwalazimu Wachezaji kusafiri safari ndefu kwenda kuicheza.
Ferguson ametamka: "Kila Klabu inapenda Wachezaji wake wachezee Timu ya Taifa. Hilo ni muhimu kwao na mimi nataka hivyo. Lakini sisi Makocha tunataka ziwe mechi za Kombe la Dunia au Mashindano ya Ulaya na si mechi ya kirafiki katika Nchi ya mbali!”
Blatter aunga mkono dawa ya kuwekea alama Frikiki!
Rais wa FIFA, Sepp Blatter, ameunga mkono matumizi ya dawa ya kupuliza ambayo hutumiwa na Marefa kuweka alama wapi Frikiki ipigwe na wapi Walinzi waweke ukuta wao wa kujihami ambayo sasa iko majaribioni huko Marekani ya Kusini katika Mashindano ya COPA SUDAMERICANA, Kombe lambalo ipo sawa na Mashindano ya EUROPA LIGI huko Ulaya.
CSF, Shirikisho la Soka la Nchi za Marekani Kusini, limebariki utumiaji wa dawa hiyo ya kusprei ambayo huweza kutumika kwenye nyasi orijino au bandia na hata kwenye viwanja vya udongo na ambayo pia haina madhara.
Baada ya kupulizwa na Refa wapi frikiki ipigwe na wapi Walinzi waweke ukuta wao, dawa hiyo hufutika baada ya sekundi 45 hadi dakika 2.
Marefa hukiweka kikopo cha dawa hiyo kwenye mkanda wao wa kiunoni.
Mvumbuzi wa dawa hiyo Pablo Silva amesema CSF ikiridhika dawa hiyo ina mafanikio basi itajaribiwa pia kwenye Mashindano ya COPA LIBERTADORES ambalo ni Kombe sawa na UEFA CHAMPIONS LEAGUE huko Ulaya.
Kwa sasa dawa ya aina hiyo hutumika kwenye Ligi za Brazil, Mexico na Argentina na imeondoa udanganyifu wa kusogeza mpira wakati wa frikiki na pia kuhadaa ukuta uwekwe wapi.
Wa Bondeni kupiga kambi Majuu!!
Wenyeji wa Kombe la Dunia, Afrika Kusini, watapiga kambi za mazoezi Brazil na Ujerumani ili kujitayarisha na Fainali za mashindano hayo yatakayochezwa Afrika Kusini kuanzia Juni 11 hadi Julai 11, 2010.
SAFA, Chama cha Soka Afrika Kusini, kimesema watakuwa na kambi 4 kwa ajili ya Bafana Bafana.
Kambi ya kwanza ni Januari huko huko kwao wakati Ligi yao itakaposimama ili kuruhusu Wachezaji wao wanaocheza huko nyumbani ambao ni nusu ya Kikosi cha Bafana Bafana wapige kambi ya kujizoeza kucheza kwenye maeneo yenye mwinuko wa juu sana toka usawa wa bahari ambako oksijeni huwa pungufu na hivyo kusababisha Wachezaji kuishiwa pumzi ili kuwazoeza kupata stamina zaidi.
Mwezi Machi 2010 watapiga kambi Brazil na baadae Aprili huko Ujerumani.
Kambi ya nne na ya mwisho itaanza Mei 6, 2010 huko Afrika Kusini ikijumuisha Wachezaji wote na hii ndio itaendelea hadi Fainali kuanza.
Meneja Mkuu wa Bafana Bafana, Sipho Nkumane, amesema mipango yote ilifanywa kabla ya uteuzi wa hivi majuzi wa Kocha toka Brazil Carlos Alberto Prreira lakini mchango wake utakuwa ni muhimu sana.
Bafana Bafana imepangiwa kucheza mechi 4 za Kimataifa katika miezi 6 ijayo ikiwa ni na Japan Novemba 14, Jamaica Novemba 17, Chile Machi 3, 2010 na Jamaica tena Machi 10, 2010.
Nkumane amesema mazungumzo yanaendelea ili Nchi zote mbili za Korea, Kusini na Kaskazini, ambazo zipo Fainali Kombe la Dunia, zicheze na Bafana Bafana Januari, 2010, na mwezi Machi wacheze na Argentina, Costa Rica na Paraguay.
Baada ya uteuzi wa hivi majuzi wa Carlos Alberto Parreira, SAFA ilibidi wawaombe Wadau wa Soka Afrika Kusini wamuunge mkono Kocha huyo baada ya kuonekana kuna upinzani huku wengi wakitaka Mzawa ndie aiongoze Bafana Bafana.
Baada ya Afrika Kusini kuchaguliwa kuwa Mwenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2010 Parreira aliteuliwa kuwa Kocha wa Bafana Bafana lakini ilibidi arudi Brazil mwaka jana baada ya mkewe kuugua na kumpisha mwenzake Joel Santana ambae alitimuliwa hivi karibuni baada ya matokeo mabaya yakihusu kufungwa kwa Timu hiyo mechi 8 kati ya 9 za mwisho walizocheza.

Thursday 29 October 2009

RATIBA LIGI KUU ENGLAND:
[Saa za Bongo]
Jumamosi, Oktoba 31
Arsenal v Tottenham [saa 9 dak 45 mchana]
[saa 12 jioni]
Bolton v Chelsea
Burnley v Hull
Everton v Aston Villa
Fulham v Liverpool
Portsmouth v Wigan
Stoke City v Wolverhampton Wanderers
Sunderland v West Ham
Manchester United v Blackburn Rovers [saa 2 na nusu usiku]
Jumapili, Novemba 1
[saa 1 usiku]
Birmingham v Manchester City
FIFA U-17 WORLD CUP NIGERIA 2009
MATOKEO MECHI ZA Alhamisi Oktoba 29:
Italy 2 v Korea Republic 1
Uruguay 2 v Algeria 0
USA 1 v Malawi 0
UAE 1 v Spain 3
Turkey 4 v Costa Rica 1
RATIBA MECHI ZA Ijumaa, Oktoba 30:
KUNDI A
Germany v Honduras
Argentina v Nigeria
KUNDI B
Japan v Mexico
Switzerland v Brazil
Larsson astaafu Soka huku akimwaga machozi!!!
Henrik Larsson amestaafu kucheza soka ya kulipwa mara baada ya kuichezea Klabu ya Helsingborg ya Sweden ambayo ipo mji aliozaliwa ilipokuwa ikicheza na Djurgarden na kufungwa 2-0.
Larsson, umri miaka 38, alianza soka akichezea Klabu ya Hogaborg kisha Helsingborg, Feyernoord, Celtic, Barcelona na Manchester United na kufunga jumla ya mabao 415.
Larsson pia ameichezea Timu ya Taifa ya Sweden mara 100 na kufunga mabao 37.
Mshambuliaji Nyota huyu ameshashinda Ubingwa wa Scotland mara 4 akiwa na Celtic, Ubingwa wa Spain mara 2 na Barcelona na pia UEFA CHAMPIONS LEAGUE na Barca mwaka 2006.
Alipokuwa na Manchester United aliisaidia klabu hiyo kutwaa Ubingwa wa England.
Mara baada ya mechi yake hiyo ya mwisho skrini kubwa hapo uwanjani ziliwaonyesha Sir Alex Ferguson, Meneja wa zamani wa Sweden Lars Lagerback na Mchezaji Zlatan Ibrahimovich wakitoa pongezi zao kwa Larsson kwa mafanikio yake kati historia yake ya Uchezaji na hilo lilimfanya Henrik Larsson alengwe na machozi.
Klabu yake ya Helsingborg imeamua kuistaafisha jezi namba 17 aliyokuwa akiivaa Larsson.
Mchezaji wa Ligi Kuu Lupango Miezi 18!!!!
Klabu yake Wigan yamfukuza!!!!
Marlon King, umri miaka 29 na Raia wa Jamaica anaechezea Wigan, amehukumiwa kifungo cha miezi 18 jela kwa kosa la kumshambulia na kumvunja pua Mwanamke wa miaka 20 kwenye baa.
Tukio hilo lilitokea Desemba mwaka jana na leo ndio ilikuwa hukumu ya kesi yake.
Mara baada ya hukumu, Mwenyekiti wa Wigan Dave Whelan ametangaza kuwa Mchezaji huyo atafukuzwa moja kwa moja mara baada ya notisi kwake ya siku 14 kumalizika.
Whelan ametamka: “Hana nafasi hapa! Hatukubali uhuni huo!”
FIFA U-17 WORLD CUP NIGERIA 2009
Mashindano ya kugombea Kombe la Dunia kwa Vijana Chini ya Miaka 17 yananguruma katika Miji mbalimbali huko Nigeria na yalianza rasmi Oktoba 24 kwa Wenyeji Nigeria, ambao ndio Mabingwa Watetezi wa Kombe hili walipolinyakua huko Korea mwaka 2007, kutoka suluhu 3-3 na Ujerumani.
Mataifa 24 yamo kwenye Fainali hizo na yamegawanywa katika Makundi 6 ya Nchi nne nne na Timu 2 za juu toka kila Kundi zitaingia Raundi ya Pili moja kwa moja na zitajumuika na Timu 4 zitakazomaliza nafasi za 3 Bora katika Makundi hayo 6 kufanya jumla ya Timu 16 zinazoingia Raundi ya Pili.
Fainali itachezwa Novemba 15.
MATOKEO NA RATIBA:
KUNDI A
24/10/09 Nigeria 3 Germany 3
24/10/09 Honduras 0 Argentina 1
27/10/09 Nigeria 1 Honduras 0
27/10/09 Argentina 2 Germany 1
30/10/09 Germany v Honduras
30/10/09 Argentina v Nigeria
KUNDI B
24/10/09 Brazil 3 Japan 2
24/10/09 Mexico 0 Switzerland 2
27/10/09 Switzerland 4 Japan 3
27/10/09 Brazil 0 v Mexico 1
30/10/09 Japan v Mexico
30/10/09 Switzerland v Brazil
KUNDI C
25/10/09 Iran 2 Gambia 0
25/10/09 Colombia 2 Netherlands 1
28/10/09 Netherlands 2 Gambia 1
28/10/09 Iran 0 Colombia 0
31/10/09 Gambia v Colombia
31/10/09 Netherlands v Iran
KUNDI D
25/10/09 Turkey 1 Burkina Faso 0
25/10/09 Costa Rica 1 New Zealand 1
28/10/09 New Zealand 1 Burkina Faso 1
29/10/09 Turkey v Costa Rica
31/10/09 Burkina Faso v Costa Rica
31/10/09 New Zealand v Turkey
KUNDI E
26/10/09 UAE 2 Malawi 0
26/10/09 Spain 2 USA 1
29/10/09 USA V Malawi
29/10/09 UAE v Spain
1/11/09 Malawi v Spain
1/11/09 UAE v USA
KUNDI F
26/10/09 Uruguay 1 Korea Republic 3
26/10/09 Algeria 0 Italy 1
29/10/09 Italy v Korea Republic
29/10/09 Uruguay v Algeria
1/11/09 Korea Republic v Algeria
1/11/09 Italy v Uruguay
MAPACHA WA MAN U FABIO & RAFAEL WAMCHANGANYA REFA!!!!
Manchester United wamekata rufaa kwa FA kupinga Kadi ya Njano aliyopewa Fabio da Silva kwenye mechi ya Kombe la Carling hapo juzi walipowafunga Barnsley mabao 2-0 kwa madai kuwa Refa Chris Foy alijichanganya na kumpa Kadi wakati si yeye aliemchezea Rafu Winga wa Barnsley Jamal Campbell-Ryce.
Aliestahili kupata Kadi hiyo alikuwa ni Ndugu yake na Pacha mwenzake, Rafael, ambae wamefanana kupindukia.
Mapacha hao kutoka Brazil wamezaliwa Julai 9, 1990.
FA imethibitisha kupokea rufaa hiyo na itasikilizwa siku ya Jumanne na Kamisheni yao ya Sheria.
Katika mechi hiyo Manchester United walimaliza mechi wakiwa mtu 10 baada ya Nahodha wao Gary Neville kupewa moja kwa moja Kadi Nyekundu kwa kumvaa Adam Hammill ingawa ilionekana dhahiri Neville aliucheza mpira kwanza na ndipo akamgusa Mchezaji huyo wa Barnsley.
Kutolewa kwa Neville kulimfanya Sir Alex Ferguson atamke kuwa haishangazi kwa Nahodha wake kupewa Kadi Nyekundu kwa vile hali ya hewa ya sawa imeruhusu hayo.
Ferguson alikuwa akimaanisha jinsi wanavyominywa na Marefa katika mechi za hivi karibuni baada ya yeye kumponda Refa Alan Wiley na kumsema hayuko fiti.
Martinez ampigia simu Ferguson kujieleza!
Meneja wa Wigan Roberto Martinez amempigia simu Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson ili kukanusha taarifa zilizozagaa hapo jana kuwa alitamka Ferguson anaogopewa na FA na pia anasaidiwa na Mameneja wengine wa Klabu za Ligi Kuu, hasa Steve Bruce na Sam Allardyce, ili kumsakama Mhispania mwenzake Rafa Benitez ambae ni Meneja wa Liverpool.
Martinez vilevile amewapigia simu Steve Bruce na Sam Allardyce kukanusha taarifa hizo na kujieleza zaidi binafsi kwao.
Inasemekana taarifa za hayo madai ya Martinez chanzo chake ni Vyombo vya Habari vya Spain.
Martinez, mwenye umri wa miaka 36, amesema: “Ni bahati mbaya lakini watu lazima wanielewe! Mimi siwezi kuwasema hao Mameneja wenzangu! Kwanza mie ni mdogo, sijashinda Ligi! Sir Alex ni Meneja Bora Duniani! Steve Bruce nina uhusiano mzuri nae na alikuwa hapa Wigan kabla yangu! Na naheshimu mafanikio ya Allardyce kwenye Ligi Kuu!”
Martinez vilevile amekijulisha Chama cha Mameneja wa Ligi [LMA=League Managers Association] nini kilichotokea ili kuepusha kuonekana mbaya.
KOMBE LA CARLING: Droo ya Robo Fainali kufanyika Jumamosi
Droo ya kupanga Timu gani zitakutana Robo Fainali ya Kombe la Carling itafanyika Jumamosi tarehe 31 Oktoba 2009.
Mechi za Robo Fainali zinatakiwa zichezwe wiki ya kuanzia Jumatatu ya tarehe 30 Novemba 2009.
Timu ambazo zimetinga Robo Fainali ni pamoja na Mabingwa Watetezi wa Kombe hilo, Manchester United, Chelsea, Arsenal, Manchester City, Portsmouth, Aston Villa, Blackburn Rovers na Tottenham.
KOMBE LA CARLING: Liverpool nje!!! Chelsea, Arsenal na Man City zaingia Robo Fainali!!!
Arsenal 2 Liverpool 1
Arsenal, ikichezesha kikosi mchanganyiko wa Chipukizi na Maveterani wachache, kiliitupa Liverpool nje ya Kombe la Carling baada ya kuifunga bao 2-1 Uwanjani Emirates.
Mabao ya Arsenal yalifungwa na Fran Merida na Nicklas Bendtner. Liverpool walifunga kupitia Emiliano Insua.
Vikosi vilikuwa:
Arsenal: Fabianski, Gilbert, Silvestre, Senderos, Gibbs, Eastmond, Merida, Bendtner, Ramsey, Nasri, Eduardo.
Liverpool: Cavalieri, Degen, Skrtel, Kyrgiakos, Insua, Plessis, Spearing, Babel, Voronin, Kuyt, Ngog.
Refa: Alan Wiley
Chelsea 4 Bolton 0
Mabao ya Saloman Kalou, Florent Malouda, Deco na Drogba yaliwapa ushindi Chelsea wa bao 4-0 dhidi ya Bolton Wanderers na kutinga Robo Fainali ya Kombe la Carling.
Man City 5 Scunthorpe 1
Huku wakichezesha Wachezaji wengi wao nyota, Manchester City wakiwa nyumbani City of Manchester Stadium, waliipa mkong’oto Timu ya Daraja la Chini, Scunthorpe, wa mabao 5-1 na kuingia Robo Fainali ya Kombe la Carling.
Mabao ya Man City yalifungwa na Stephen Ireland, Roque Santa Cruz, Joleon Lescott, Carlos Tevez na Michael Johnson.
Bao la Scunthorpe lilifungwa na Jonathan Forte.

Wednesday 28 October 2009

Blackburn yakumbwa na Homa ya Mafua ya Kitimoto!!!
Bosi wa Blackburn Sam Allardyce anawakimbia Wachezaji wake kwa sababu hajasikii vizuri huku Wachezaji watatu wa Timu hiyo tayari washakumbwa na Homa ya Mafua ya nguruwe.
Jana Sam Allardyce hakukaa kwenye benchi la ufundi la Timu hiyo katika mechi waliyoshinda 5-2 dhidi ya Peterborough ya kugombea Kombe la Carling.
Inasadikiwa kuna Watu watano wameathirika na ugonjwa huo hapo Blackburn na Jumamosi kwenye kipigo cha 5-0 mikononi mwa Chelsea kwenye mechi ya Ligi Kuu Wachezaji wa kutumainiwa Beki Chris Samba na Kiungo David Dunn hawakucheza kwa kuwa wagonjwa na inasadikiwa wameathirika kwa Homa hiyo.
Jumamosi ijayo Blackburn ni wageni wa Mabingwa Manchester United kwenye Ligi Kuu uwanjani Old Trafford.
FA kuchunguza Mashabiki mechi ya Man U!!!
FA, Chama cha Soka England, kitafanya uchunguzi baada ya kutokea fujo za mashabiki kwenye mechi ya Kombe la Carling kati ya Barnsley na Mabingwa Watetezi wa Kombe hilo Manchester United ambayo Barnsley walifungwa 2-0.
Kufuatia matukio kadhaa ya fujo, FA inasubiri kupokea ripoti kutoka kwa Refa wa mechi hiyo Chris Foy na Mshauri wa Udhibiti wa Watazamaji wa FA aliyekuwepo kwenye mechi hiyo.
Mashabiki 9 waliswekwa ndani na Polsi katika fujo hizo ambazo chanzo chake ni kunyimwa kuuziwa pombe wakati wa haftaimu.
Mashabiki watatu wa Barnsley walivamia uwanja wakati mechi inaendelea lakini walikamatwa.
Refa aliewatwanga Scholes na Rooney Kadi Nyekundu kuchezesha mechi ya Man U v Blackburn Jumamosi!!!!
Inaelekea balaa la Marefa kuwasakama Manchester United tangu Meneja wao Sir Alex Ferguson kutamka Refa Alan Wiley hayuko fiti linazidi kuwaandama kwani Jumamosi wamepangiwa Refa Phil Dowd kuchezesha mechi yao ya Ligi Kuu na Blackburn Rovers uwanjani Old Trafford na Refa huyo anakumbukwa na Man U kwa kuwatoa Wachezaji wawili wao, Paul Scholes na Wayne Rooney, wote katika mechi moja dhidi ya Fulham walipofungwa 2-0 msimu uliopita.
Mabingwa Manchester United wanahisi wanasakamwa na Marefa kufuatia maamuzi yao ya utata hasa mechi na Liverpool na ya jana na Barnsley na hili wanahisi limekuja baada ya kauli ya Ferguson kumponda Refa Alan Wiley.
Kupangwa kwa Refa Phil Dowd kuchezesha mechi hiyo kutawatia wasiwasi Manchester United na kuendelea kuamini Marefa wana kampeni dhidi yao.
Meneja wa Wigan adai Ferguson anaogopewa England!!!
Katika hali ya kushangaza na bila shaka ya kumuunga mkono Mhispania mwenzake Rafa Benitez, Meneja wa Wigan, Roberto Martinez, ameibuka na kudai Sir Alex Ferguson ana nguvu sana katika Soka la England na anaogopewa na FA, Chama cha Soka cha England.
Martinez pia amedai Ferguson anaungwa mkono na Mameneja wengi kuliko Benitez na ndio maana wanamuonea Benitez.
Bila shaka Martinez hajui kuwa kwa sasa Ferguson ameshitakiwa na FA kwa kauli yake kuwa Refa Alan Wiley hayuko fiti kauli aliyoitoa mara baada ya mechi ya Ligi Kuu hapo Oktoba 3 kati ya Manchester United na Sunderland iliyomalizika 2-2 na kuibua mzozo mkubwa huku Chama cha Marefa wakitaka Ferguson apewe adhabu kali.
Wadau na Wachunguzi wa mambo wanahisi kauli ya Ferguson kumponda Refa Alan Wiley sasa imeanza kuisakama Manchester United kwani kwenye mechi Liverpool aliyoifunga Man U Jumapili bao 2-0 Refa Andre Marriner alionyesha waziwazi kuibeba Liverpool.
Martinez ametoa madai yake kwa kusema: “Ferguson yuko hapa ‘milele’ na ni mtu mzito! Ferguson ana kundi lake kama kina Steve Bruce aliekuwa Mchezaji wake na Sam Allardyce anaedhani atakuwa Meneja Man U Ferguson akiondoka!!”
Mechi ya pili mfululizo, Man U wapewa Kadi Nyekundu!!!
Katika mechi ya jana ya Kombe la Carling, Mabingwa Watetezi, Manchester United, waliifunga Barnsley bao 2-0 lakini walimaliza mechi wakiwa mtu 10 baada ya Nahodha wao Garry Neville kupewa Kadi Nyekundu licha ya kuonekana dhahiri akiucheza mpira kwanza na ndipo kumgusa Mchezaji wa Barnsley, Adam Hammill kwenye dakika ya 63.
Kitendo hicho kilimfanya Ferguson atamke: “Katika hali ya hewa ya sasa, Kadi hiyo Nyekundu inaeleweka!”
Mabao ya Man U yalifungwa na Danny Welbeck na Michael Owen.
Katika mechi zingine za Kombe la Carling hapo jana matokeo ni:
Blackburn 5 Peterborough 2
Portsmouth 4 Stoke 0
Sunderland 0 Aston Villa 0 [Aston Villa walishinda mechi hii kwa mikwaju ya penalti 3-1]
Tottenham 2 Everton 0
MECHI ZA LEO za KOMBE LA CARLING:
[saa 4 dak 45 usiku bongo taimu]
Arsenal v Liverpool
Chelsea v Bolton
Manchester City v Scunthorpe
Real Madrid yatandikwa na TIMU YA KIJIJINI!!!
Kwenye mechi ya Kombe la Mfalme wa Spain, Real Madrid imekung’utwa na Timu ya Kijijini inayocheza Daraja la 3, Alcorcon, kwa mabao 4-0 licha ya Real kuchezesha Kikosi chenye nguvu.
Kipigo hicho kimefanya zizagae habari kuwa endapo Real watafungwa mechi ya Ligi wikiendi ijayo watakapocheza na Getafe au kupigwa na AC Milan Jumanne ijayo kwenye UEFA CHAMPIONS LEAGUE, basi hiyo itakuwa baibai kwa Kocha Manuel Pellegrini.
Wachezaji wa Stoke City wapata dharura kwenye Ndege angani!!!
Ndege iliyokuwa imewabeba Wachezaji wa Stoke City wakiwa wanatoka kwenye mechi ya Kombe la Carling waliyofungwa na Portsmouth 4-0 ilipata hitilafu angani ikitokea Uwanja wa Ndege wa Southampton baada ya Wachezaji kumjulisha Rubani kuwa wanasikia harufu ya kuungua kitu na ikalazimu Ndege hiyo itue kwa dharura Uwanja wa Ndege wa Gatwick huku ikisindikizwa na Magari ya Faya.
Ingawa Ndege hiyo ilikaguliwa na kukutwa haikuwa na hitilafu, Timu ya Stoke City ilirudi nyumbani kwao kwa basi.
Portsmouth wapigwa marufuku kusajili Wachezaji!!
Klabu ya Portsmouth imezuiwa kusajili Wachezaji na Wasimamizi wa Ligi Kuu England hadi hapo watakapomaliza kulipa madeni ya Usajili na Ununuzi wa Wachezaji wanayodaiwa na Klabu nyingine.
Klabu hiyo ipo kwenye ukata licha ya kunuliwa na Tajiri kutoka UAE Sulaiman Al Fahim ambae baada ya kuimiliki wiki chache tu akamuuzia Mfanya Biashara wa Saudi Arabia Ali Al Faraj ambae amekiri hajui lolote kuhusu michezo na nia yake ilikuwa kuiuza kwa faida.
Wiki chache zilizopita Wachezaji wa Portsmouth walikosa mishahara na ikabidi Sulaiman Al Fahim atoe hela za dharura kuwalipa.
Powered By Blogger