Saturday 10 October 2009

Rio asema akiachwa Fainali Kombe la Dunia akiwa sio fiti halalamiki!!
Rio Ferdinand amesema akiikosa Fainali ya Kombe la Dunia mwakani kwa sababu hayuko fiti au ni majeruhi hawezi kulalamika kwa sababu Meneja wa sasa hajali majina bali huchagua Wachezaji fiti tu na walio kwenye fomu tu.
Rio amezungumzia hilo hasa kwa vile yeye kwa sasa anasakamwa na majeruhi mfululizo yaliyomfanya katika mwaka huu acheze mechi 26 kati ya 40 angezoweza kuchezea Klabu yake Manchester United na England.
Rio, atakaetimiza miaka 30 mwezi ujao, amesema: “Capello ni mkweli! Ameweka bayana anachagua mtu akiwa fiti na kwenye fomu tu na sio jina! Maishani sijaandamwa na majeruhi kama sasa! Na si tatizo moja tu linalonisumbua! Msimu uliokwisha niliumia mgongo, msimu huu nimeumia musuli nyuma ya ugoko na kisha musuli pajani! Ni vitu tofauti na sasa nafanyiwa mazoezi ili kujifua nisipate matatizo ya aina hii!”
Rio Ferdinand anategemewa kucheza mechi ya leo ya Kombe la Dunia ugenini na Ukraine.
Rooney na Ronaldo wataniana!!
Fowadi wa England, Wayne Rooney, ambae Timu yake ishafuzu kuingia Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwakani huku wakiwa wamebakisha mechi mbili amesema atafurahi sana ikiwa Cristiano Ronaldo na Ureno yake watashindwa kwenda Fainali hizo.
Ureno iko hatarini kuzikosa Fainali hizo na wako nafasi ya 3 Kundini mwao pointi 2 nyuma ya Sweden walio nafasi ya pili huku Denmark akiongoza Kundi hilo.
Rooney alisema: “Katika Kombe la Dunia mwaka 2006 Ureno walitung’oa Robo Fainali na mie nilipewa Kadi Nyekundu! Na tulipotolewa EURO 2008 Ronaldo alitucheka sana tulipokuwa nae Manchester United! Sasa bora wao wasiende Afrika Kusini!”
Ronaldo alipoulizwa kuhusu kauli ya Rooney alijibu kuwa anadhani rafiki yake huyo anawatania tu.
Fergie amwomba msamaha Refa Wiley
Bosi wa Manchester United Sir Alex Ferguson ameomba msamaha kwa Refa Alan Wiley kwa kauli yake kwamba Refa huyo hayuko ‘fiti’ kuchezesha mechi kauli aliyoitoa mara baada ya mechi ya Ligi Kuu ya Manchester United na Sunderland iliyoisha 2-2 huko Old Trafford wikiendi iliyokwisha.
Mara baada ya kauli hiyo ya Sir Alex Ferguson, FA, Chama cha Soka England, kilimwandikia barua Ferguson kumtaka ajieleze.
Taarifa iliyotoka kwenye tovuti ya Manchester United imemkariri Ferguson akisema: “Naomba msamaha kwa Bw. Wiley kwa kumfedhehesha na kwa FA kwa kutoa mawazo yangu hadharani. Haikuwa nia yangu kumfanya Bw. Wiley amulikwe na Waandishi wa Habari. Nia yangu ni kukutana nae na kumwomba msamaha uso kwa uso mara nitakaporudi safari yangu nje ya Nchi.”
Ferguson aliongeza kwamba anamheshimu Refa Wiley na kauli yake haikumaanisha:
-Wiley ni Refa mbaya.
-Wiley anapendelea.
-Uamuzi wake kwenye mechi ile ulikuwa dhaifu.
-Kwamba alipitwa na matukio muhimu kwenye mechi ile.
Mara baada ya Ferguson kusema maneno kwamba Wiley ‘hayuko fiti’ mjadala na mzozo mkubwa uliibuka kwenye Vyombo vya Habari huko England.
Nahodha wa Italia Cannavaro mashakani!
Kuumwa na Dondola kwamletea kasheshe!!!
Nahodha wa Timu ya Taifa ya Italia, Fabio Cannavaro, yupo kwenye uchunguzi wa Maafisa wa Madawa yaliyopigwa marufuku baada ya kupimwa na kugundulika alitumia dawa ambayo hairuhusiwi.
Inasemekana Cannavaro aliumwa na Dondola mwezi Agosti na Klabu yake Juventus ikampa dawa ya kuzuia madhara ya Dondola huyo kwa vile hudhurika akiumwa na Wadudu.
Lakini dawa waliyompa ina chembechembe za ‘cortisone’ ambayo ni marufuku kwa Wanamichezo.
Klabu yake Juventus ilimwombea kibali cha kutumia dawa hiyo na wakati ombi hilo bado halijashughulikiwa Wapima Wachezaji wanaocheki utumiaji Madawa Marufuku wakampima Cannavaro na kugundua ukiukwaji huo.
Kamati ya Olimpiki ya Italia inayoshughulikia Madawa kwa Wachezaji imemwita Cannavaro ili ajieleze.
Cannavaro ndie Mchezaji aliechezea Timu ya Taifa ya Italia mechi nyingi na ndie aliekuwa mhimili wa Italia kunyakua Kombe la Dunia mwaka 2006.
Italia leo wako mjini Dublin, Ireland kucheza na Ireland na wanahitaji sare tu ili waingie Fainali huko Afrika Kusini mwakani.
Capello: ‘Tunataka ushindi leo!’
Ingawa England imeshafaulu kuingia Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwakani baada ya kushinda mechi zao zote 8 katika Kundi lao na bado wakiwa na mechi 2 mkononi mojawapo ikichezwa ugenini leo na Ukraine, Kocha wa England, Fabio Capello ametaka Timu yake isibweteke na icheze kwa moyo wa ushindi.
Capello alisema: “Timu lazima icheze kwa moyo uleule! Ntachagua Kikosi bora! Mechi hii ni muhimu kuijenga Timu iwe bora!”
Timu ya Capello itatokana na :
MAKIPA: Paul Robinson (Blackburn), Robert Green (West Ham), David James (Portsmouth)
WALINZI: Ashley Cole (Chelsea), John Terry (Chelsea), Glen Johnson (Liverpool), Wayne Bridge (Manchester City), Joleon Lescott (Manchester City), Wes Brown (Manchester United), Rio Ferdinand (Manchester United), Matthew Upson (West Ham).
VIUNGO: James Milner (Aston Villa), Frank Lampard (Chelsea), David Beckham (Los Angeles Galaxy), Steven Gerrard (Liverpool), Gareth Barry (Manchester City), Shaun Wright-Phillips (Manchester City), Michael Carrick (Manchester United), Aaron Lennon (Tottenham)
WASHAMBULIAJI: Gabriel Agbonlahor (Aston Villa), Emile Heskey (Aston Villa), Peter Crouch (Tottenham), Carlton Cole (West Ham), Wayne Rooney (Manchester United)
Uruguay waibiwa huko Ecuador!!!
Timu ya Taifa ya Uruguay imelalamika kuwa imeibiwa Mipira, Viatu na Jezi hotelini mwao Nchini Ecuador ambako leo wanapambana na Ecuador kwenye mechi muhimu ya Kombe la Dunia huku Timu zote zikiwania kunyakua nafasi mbili zilizosalia kati ya 4 za Nchi za Marekani ya Kusini kuingia Fainali.
Wakati tayari Brazil na Paraguay zipo Fainali huku nafasi 2 zikibaki pambano lao la leo ni muhimu sana kwani Uruguay wapo nafasi ya 6 wakiwa na pointi 21 na Ecuador wako nafasi ya 4 wakiwa na pointi 23.
Timu hizi zilitoka 0-0 mechi ya kwanza Nchini Uruguay. Eduardo Di Maggio, Mkuu wa Vifaa vya Uruguay, aliwajulisha Polisi wa Mji wa Guayaqil, Ecuador walipofikia Uruguay, kuhusu tukio hilo la wizi.
Urguay walifikia Guayaqil mapema ili kujizoeza hali ya hewa kabla ya kusafiri kwenda Quito Mji ulio Futi zaidi ya Elfu 7 toka usawa wa bahari hali inayofanya kupumua kuwe ni kwa shida kwa ajili ya hewa kuwa nyepesi na upungufu wa Oksejeni.
FIFA U-20 WORLD CUP EGYPT 2009
Wawikilishi pekee wa Ghana kwenye Kombe la Dunia kwa Vijana Chini ya Miaka 20 jana waliifunga South Korea mabao 3-2 na kuingia Nusu Fainali.
Nusu Fainali Ghana watakutana na Hungary walioitoa Italy 3-2 baada ya dakika 120 kufuatia mechi kuwa 1-1 kwenye dakika 90 za kawaida.
ROBO FAINALI:
09/10/09: South Korea 2 v Ghana 3
09/10/09: Italy 2 v Hungary 3
MECHI ZA LEO Jumamosi, Oktoba 10:
10/10/09: Brazil v Germany
10/10/09: UAE v Costa Rica
NUSU FAINALI:
Oktoba 13:
Ghana v Hungary
Brazil/Germany v UAE/Costa Rica
FAINALI:
Oktoba 16:

Friday 9 October 2009

FIFA U-20 WORLD CUP EGYPT 2009
Huku Wenyeji Misri wakiwa wamebwagwa nje na Afrika imebaki Nchi moja tu, Ghana, Kombe la Dunia kwa Vijana Chini ya Miaka 20 leo linaingia hatua ya Robo Fainali kwa mechi mbili leo na mechi mbili kesho.
ROBO FAINALI:
09/10/09: South Korea v Ghana
09/10/09: Italy v Hungary
10/10/09: Brazil v Germany
10/10/09: UAE v Costa Rica
NUSU FAINALI:
Oktoba 13:
South Korea/Ghana v Italy/Hungary
Brazil/Germany v UAE/Costa Rica
FAINALI:
Oktoba 16
KOMBE LA DUNIA Afrika Kusini 2010
Wakati kona mbalimbali za Dunia zitawaka moto wikiendi hii na Jumatano ijayo ili kukamilisha Nchi 32 zitakazoingia Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwakani zitakazochezwa Juni 11 hadi Julai 11, mpaka sasa ni Timu 11 zifuatazo ndizo tayari zishaingia Fainali hiyo:
South Africa (Wenyeji), Ghana, Australia, Japan, South Korea, North Korea, Brazil, Paraguay, Spain, England na Uholanzi
Ifuatayo ni tathmini ya hali ilivywo katika Makundi mbalimbali kona zote za Dunia.
AFRICA
WALIOFUZU: South Africa [Wenyeji] na Ghana
Kama Wenyeji, Afrika Kusini tayari wako Fainali pamoja na Ghana ambao wamefuzu huku wakiwa na mechi mbili mkononi..
Timu katika kila Kundi zimebakiwa na mechi 2 na Timu ya juu ndio inatinga Fainali.
Cameron wako juu kwenye Kundi lao Kundi A wakiwa na pointi 7 wakifuatiwa na Gabon pointi 6, Togo pointi 5 na Morocco pointi 3.
Kundi B Tunisia yuko juu na pointi 8, Nigeria pointi 6, Mozambique pointi 4 na Kenya pointi 3.
Kundi C, Algeria wanaongoza wakiwa na pointi 10, Egypt pointi 7, Zambia pointi 4 na Rwanda 1.
Kundi D, Ghana mwenye pointi 12 tayari ashafuzu kuingia Fainali huku wakibaki Mali pointi 5, Benin 4 na Sudan 1.
Kundi E ni Ivory Coast mwenye nafasi nzuri akiwa na pointi 12 na anahitaji pointi moja tu katika mechi zake mbili ili aingie Fainali.
Burkina Faso anafuata na pointi 6 huku Guinea na Malawi wakiwa na pointi 3 kila mmoja.
ASIA
WALIOFUZU: Australia, Japan, South Korea na North Korea.
Tayari Australia, Japan, Korea ya Kusini na Korea ya Kaskazini wako Fainali na itapatikana Timu moja nyingine itakayoungana nao baada ya mtoano kati ya Bahrain na New Zealand utakaochezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.
MAREKANI YA KASKAZINI, KATI NA CARIBBEAN
WALIOFUZU: Bado Kupatikana
Endapo USA na Mexico watashinda mechi moja tu kati ya mbili walizobakiwa nazo watatinga Fainali wakiwaacha Honduras na Costa Rica kugombea nafasi ya 3 itakayowawezesha kutinga Fainali moja kwa moja ingawa El Salvador nao wapo kwenye mahesabu.
Hata hivyo, kwa jinsi hali ilivyo, El Salvador huenda akaambulia nafasi ya 4 na hivyo kwenda kucheza mtoano na Timu itakayomaliza nafasi ya 5 toka Nchi za Marekani ya Kusini.
MAREKANI YA KUSINI
WALIOFUZU: Brazil na Paraguay
Brazil na Paraguay tayari zimetinga Fainali huku wakiwa na mechi 2 mkononi huku Chile, alie nafasi ya 3, akihitaji kushinda mechi moja tu kati ya mbili alizokuwa nazo kuungana nao.
Balaa lipo kwenye nani atachukua nafasi ya 4 ili kuingia Fainali moja kwa moja na ile ya 5 ili kwenda kucheza kwenye mtoano na Timu inayomaliza nafasi ya 4 toka Kundi la Nchi za Marekani ya Kaskazini, Kati na Carribean.
Kukiwa kumebaki mechi 2, Ecuador yuko nafasi ya 4 akiwa na pointi 23, Argentina wa 5 pointi 22, Uruguay na Venezuela wana pointi sawa 21 kila mmoja ila Uruguay yuko mbele ya Venezuela kwa magoli.
Colombia nae ananyemelea akiwa na pointi 20.
ULAYA
WALIOFUZU: England, Spain na Uholanzi
Ni England, Spain na Uholanzi ambazo tayari zimeingia Fainali.
Yapo Makundi 9 na Washindi wa kila Kundi wanatinga Fainali huku Washindi wa Pili Bora wa nane watawekewa droo maalum ili kupanga mechi 4 zitakazochezwa nyumbani na ugenini ili kupata Timu 4 zitakazoenda Fainali.
KUNDI 1: Lipo wazi ingawa Denmark anaeongoza anahitaji pointi 2 toka mechi 2 ngumu dhidi ya Mahasimu wao Sweden na Hungary ili afuzu. Kundi hili lina Ureno pia ambao mpaka sasa wanasuasua ingawa mechi zao zilizobaki wanacheza na Hungary nyumbani [baada ya kuifunga huko Hungary] na Timu dhaifu Albania.
KUNDI 2: Uswisi wako mbele kwa pointi 3 na wana mechi laini kidogo na wachovu Luxemborg. Inaelekea Greece na Latvia zinagombea nafasi ya pili.
KUNDI 3: Slovakia wana hali nzuri kwani wanahitaji kushinda au Slovenia wafungwe ili wafuzu. Czech Republic bado wana nafasi ya kupata nafasi ya pili na hata Poland, kimahesabu, bado ana nafasi hiyo.
KUNDI 4: Ni Germany au Urusi ndie atakaefuzu kuingia Fainali moja kwa moja na Timu hizi zinapambana uso kwa uso huko Urusi katika pambano litakalotoa sura nani Mshindi wa kwanza ingawa Germany ndie alie nafasi nzuri kwani yuko mbele kwa pointi moja.
KUNDI 5: Spain ameshanyakua nafasi ya kwanza Kundi hili na hivyo kuingia Fainali na vita iliyobaki ni nani Mshindi wa Pili ili aende kwenye mtoano wa kuingia Fainali. Kukiwa na mechi 2 zilizobaki, Bosnia-Herzegovina ana nafasi nzuri kwani yuko mbele ya Uturuki kwa pointi 4.
KUNDI 6: England tayari yuko Fainali na wa pili ni Croatia lakini ikiwa Ukraine atashinda mechi zake 2 zilizobaki basi atanyakua nafasi ya pili.
KUNDI 7: Serbia anahitaji ushindi kwenye mechi moja tu kati ya 2 ili afuzu. Ufaransa nae anahitaji kushinda mechi moja ili angalau amalize wa pili ingawa pia Austria nae bado anayo matumaini.
KUNDI 8: Mabingwa Watetezi wa Dunia, Italy, wanahitaji suluhu tu ugenini na Republic of Ireland ili watinge huko Afrika Kusini mwakani kutetea taji lao.
KUNDI 9: Uholanzi walishinda mechi zao zote kwenye Kundi hili na kuingia Fainali na Norway ndie atakaemaliza nafasi ya pili lakini nafasi yao kuingia Fainali kwa kapu la Washindi wa Pili liko finyu kwani wao, katika Washindi wa Pili toka Makundi 9, ni wa mwisho na ni Timu 8 tu ndizo zinazochukuliwa kwenye droo maalum.

Thursday 8 October 2009

LISTI YA MAMENEJA MATAJIRI ENGLAND YATAJWA!!
Mchezaji na Nahodha wa zamani wa Manchester United, Roy Keane, ambae sasa ni Meneja wa Timu inayosuasua mkiani Daraja la Coca Cola Championship, Ipswich Town, anashikilia nafasi ya pili katika Listi ya Mameneja Matajiri huko England.
Roy Keane amethaminiwa kuwa na utajiri wa Pauni Milioni 27.
Anaeshika nambari wani ni Fabio Capello mwenye Pauni Milioni 30.
Sir Alex Ferguson wa Manchester United ni wa tatu akiwa na Pauni Milioni 22.
Listi ya Mameneja Matajiri 10 ni:
-Fabio Capello [England] Pauni Milioni 30
-Roy Keane [Ipswich] Pauni Milioni 27
-Sir Alex Ferguson [Manchester United] Pauni Milioni 22
-Carlo Ancelotti [Chelsea] 17
-Sven-Goran Eriksson [Notts County]
-Arsene Wenger [Arsenal] 15
-Harry Redknapp [Tottenham] 10
-Rafael Benitez [Liverpool] 9
-Martin O’Nell [Aston Villa] 9
-Mark Hughes [Man City] 8
FIFA yairuhusu Man U kumsajili Kinda Pogba!!!
Manchester United imeruhusiwa na FIFA kumsajili Kijana mdogo wa miaka 16 Paul Pogba baada ya Klabu ya Ufaransa Le Havre awali kuweka pingamizi kuwa Man U imempora Mchezaji huyo.
Mwezi Septemba Chelsea ilifungiwa na FIFA kwa kumrubuni na kumsaini kinyume cha sheria Gael Kakuta mwaka 2007 na hivyo kupewa adhabu ya kutosajili Mchezaji yeyote hadi 2011.
Lakini Jaji aliyeteuliwa na FIFA kuipitia kesi ya Le Havre na Manchester United kuhusu Paul Pogba aliamua kuwa kwa sababu Pogba ni mdogo haiwezekani kisheria Le Havre wawe na mkataba na Pogba kuichezea Klabu hiyo ya Ufaransa kama Mchezaji wa Kulipwa.
Uamuzi huo wa FIFA umewaruhusu Manchester United kumsajili Pogba kwenye Chuo chao cha Soka.
Mwezi uliokwisha Manchester United iliwatishia kuwashitaki Le Havre kwa kuwachafulia jina lao kwa madai kuwa wamemwiba Pogba.
FIFA U-20 WORLD CUP EGYPT 2009
Brazil, UAE na Germany zajikita Robo Fainali!!
MATOKEO MECHI ZA JANA Jumatano, Oktoba 7:
Brazil 3 v Uruguay 1
Venezuela 1 v UAE 2
Germany 3 v Nigeria 2
ROBO FAINALI:
09/10/09: South Korea v Ghana
09/10/09: Italy v Hungary
10/10/09: Brazil v Germany
10/10/09: UAE v Costa Rica

Wednesday 7 October 2009

Grant arudi Portsmouth!!
Aliekuwa Kocha wa Chelsea, Avram Grant, ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Soka wa Portsmouth na atakuwa akishirikiana na Meneja Paul Hart kuinasua Klabu hiyo iliyo mkiani Ligi Kuu England.
Grant aliwahi kuwa Portsmouth mwaka 2006 kama Mkurugenzi wa Soka wakati huo Meneja akiwa ni Harry Redknapp lakini alihamia Chelsea Septemba 2007 Jose Mourinho alipoondoka Chelsea.
Grant aliifikisha Chelsea Fainali ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE mwaka jana mwezi Mei na ikatolewa na Manchester United kwa penalti na baada ya mechi hiyo akatimuliwa Chelsea.
Mahakama Uswisi yasimamisha ulipaji Fidia wa Mutu kwa Chelsea
Mahakama huko Uswisi imesimamisha kwa muda kulipwa kwa Fidia aliyotakiwa Adrian Mutu kuilipa Chelsea na FIFA baada ya kufungiwa alipokutwa na chembechembe za Kokeni na kisha kufukuzwa Chelsea.
Mutu aliamriwa na FIFA kulipa Pauni Milioni 15 na adhabu hiyo iliungwa mkono na Mahakama ya Usuluhishi Michezoni [CAS ambako Mutu alikata rufaa.
Wakala wa Mutu, Victor Becali, amethibitisha uamuzi wa Mahakami hiyo wa kusimamisha ulipwaji fidia hadi Novemba ili isikilize Kesi ya Mutu.
Mutu mwenyewe amesema hana pesa za kulipa fidia hiyo.
Wenyeji Misri nje Kombe la Dunia!!!
Wenyeji Misri jana wamebwagwa nje ya Kombe la Dunia la Vijana wa Chini ya Miaka 20 baada ya kufungwa 2-0 na Costa Rica ambao sasa wameingia Robo Fainali na watacheza na Mshindi kati ya UAE na Venezuela wanaokutana leo.
Ghana nao wamesonga mbele na kuingia Robo fainali baada ya kuifunga South Africa 2-1 katika muda wa nyongeza baada ya mechi kwisha dakika 90 mabao yakiwa 1-1.
Hungary na Czech Republic zilitoka suluhu 2-2 hadi muda wa nyongeza na penalti tano tano zikawapa ushindi wa penalti 4-3.
MECHI ZA LEO Jumatano, Oktoba 7:
Brazil v Uruguay
Venezuela v UAE
Germany v Nigeria
ROBO FAINALI:
09/10/09: South Korea v Ghana
09/10/09: Italy v Hungary
10/10/09: Brazil AU Uruguay v Germany AU Nigeria
10/10/09: Venezuela AU UAE v Costa Rica
Van der Sar arudi golini baada ya kuumia 
Kipa wa Manchester United Edwin van der Sar jana alimaliza dakika 90 za mechi ya Vikosi vya Akiba kati ya Manchester United na Everton ambayo Man U walishinda kwa bao 1-0 mfungaji akiwa Federico Macheda.
Kipa huyo Mdachi mwenye umri wa miaka 38 hajaonekana Uwanjani tangu Agosti 5 alipocheza mechi ya kugombea Kombe la Audi huko Ujerumani na Bayern Munich na kuvunjika mifupa miwili ya mkono wa kushoto.
Kutokuwepo kwa Van der Sar kulimpa nafasi Kipa Ben Foster kucheza lakini Kipa huyo wa akiba ameonekana kupwaya sana na amekuwa akitoa zawadi ya magoli.
Foster alikuwa lawamani kwa goli lililofungwa na Gareth Barry katika mechi na Manchester City na pia siku ya mechi ya Sunderland bao la pili la Mshambuliaji Kenwyne Jones linasemwa kuwa ni kosa lake.
Foster hakuchaguliwa kwenye Timu ya Taifa ya England itayocheza mechi za Kombe la Dunia Jumamosi hii na Jumatano ijayo dhidi ya Ukraine na Belarus ingawa kuachwa kwake kunasemekana ni kuugua kifua.
Van der Sar anatarajiwa kurudi golini kwenye mechi ya Ligi Kuu tarehe 17 Oktoba Man U watakapokwaana na Bolton.

Tuesday 6 October 2009

Refa Mstaafu amponda Fergie!!!
Fergie atakiwa na FA kujieleza!!
Jeff Winter ambae amestaafu baada ya kuwa mmoja wa Marefa wa Ligi Kuu England amemponda Sir Alex Ferguson kwa kauli yake aliyoitoa mara baada ya dro ya 2-2 ya mechi ya Ligi Kuu kati ya Manchester United na Sunderland alipomsema Refa aliechezesha mechi hiyo Alan Wiley kuwa hayuko ‘fiti’.
Jeff Winter amesema kauli za Ferguson ni za uburuzaji na kiwoga na pia amedai Ferguson alitoa kauli hizo ili kuficha ukweli kuwa Timu yake Man U ilicheza vibaya mechi hiyo.
Winter amesema: “Nadhani safari hii Ferguson amezidisha na hili linaweza kuwaathiri Manchester United na huenda Marefa wakaungana na kuikomoa Timu hiyo kwenye mechi zao!”
Klabu ya Manchester United imekataa kuzungumza lolote kuhusu kauli za Refa huyo wa zamani.
Wakati huohuo, FA imemtaka Sir Alex Ferguson atoe ufafanuzi kuhusu kauli yake kwamba Refa Alan Wiley hayuko fiti
Mmiliki wa Portsmouth auza hisa zake wiki 6 tu baada ya kuzinunua!!
Sulaiman al-Fahim, ambae aliinunua Portsmouth wiki 6 zilizopita, ameamua kuuza aslimia 90 ya hisa hizo kwa Tajiri kutoka Saudi Arabia Ali al-Faraj.
Uamuzi huo umekuja huku Klabu ya Portsmouth ikishindwa kuwalipa Wachezaji wake mishahara.
Sulaiman al-Fahim ndie alishiriki kuinunua Klabu ya Manchester City kwa ajili ya Koo mojawapo ya Kifalme ya huko Abu Dhabi, Falme ya Nchi za Kiarabu.
Mmiliki wa Liverpool George Gillett amlaumu Rafael Benítez kwa matokeo mabaya!!!
George Gillett, mmoja wa Wamarekani wawili ambao ndio Wamiliki wa Liverpool amedai Rafael Benitez ndie alaumiwe kwa matokeo mabaya ya Liverpool ambao juzi walifungwa na Chelsea mabao 2-0 kwenye Ligi Kuu. Gillett amedai yeye na Mmiliki mwenzake Tom Hicks wametoa dau la kutosha kuifanya Liverpool ipate Wachezaji bora na kuhakikisha mafanikio lakini kama hilo linaonekana haliwezekani basi wa kulaumiwa ni Benitez.
Gillettte amesema: “Sisi tumewekeza pesa nyingi kupita hata Klabu za Arsenal, Chelsea na Manchester United!”
FIFA U-20 WORLD CUP EGYPT 2009
Spain na Paraguay zatinga Robo Fainali.
Jana Italia na South Korea zimekuwa Timu za kwanza kuingia Robo Fainali ya Kombe la Dunia la Vijana Chini ya Miaka 20 baada ya kuzichabanga Timu zilizopewa nafasi kubwa kufanya vizuri Spain na Paraguay.
Spain ilipigwa 3-1 na Italy na South Korea iliikung’uta Paraguay 3-0.
Raundi ya Pili inaendelea leo kwa mechi zifuatavywo:
MECHI ZA LEO Jumanne, Oktoba 6:
Ghana v South Africa
Egypt v Costa Rica
Hungary v Czech Republic
LIGI KUU ENGLAND: Kusimama hadi Oktoba 17 kupisha Mechi za Kimataifa za Kombe la Dunia
Ligi Kuu itasimama baada ya mechi yaJumatatu baina ya Aston Villa v Man City ili kuruhusu Mechi za Kimataifa za kuwania nafasi za kuingia Fainali Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwaka 2010.
Mechi hizo za Kimataifa za Nchi mbalimbali zinatarajiwa kuchezwa wikiendi ya Oktoba 10 na katikati ya wiki yaani Jumatano Oktoba 14.
Ligi Kuu itarudia tena Jumamosi Oktoba 17 na Ratiba ni kama ifuatavywo:
Jumamosi, Oktoba 17
Aston Villa v Chelsea [saa 8 na dak 45 mchana]
[saa 11 jioni]
Arsenal v Birmingham
Everton v Wolverhampton
Man United v Bolton
Portsmouth v Tottenham
Soke City v West Ham
Sunderland v Liverpool
Jumapili, Oktoba 18
[saa 9 mchana]
Blackburn v Burnley
Wigan v Man City
Jumatatu, Oktoba 19
[saa 4 usiku]
Fulham v Hull City
KOMBE LA DUNIA
Afrika:
Oktoba 10:
Zambia v Egypt
Malawi v Ivory Coast
Cameroun v Togo
Gabon v Morocco
Oktoba 11:
Benin v Ghana
Nigeria v Mozambique
Tunisia v Kenya
Guinea v Burkina Faso
Mali v Sudan
Algeria v Rwanda
Ulaya:
Oktoba 10:
Finland v Wales
Luxemborg v Switzerland
Belarus v Kazakhstan
Russia v Germany
Estonia v Bosnia-Herzegovina
Montenegro v Georgia
Ukraine v England
Denmark v Sweden
Liechtenstein v Azerbaijan
Republic of Ireland v Italy
Czech Republic v Poland
Slovakia v Slovenia
Austria v Lithuania
Serbia v Romania
Portugal v Hungary
Belgium v Turkey
Israel v Moldova
Armenia v Spain
France v Faroe Islands
Greece v Latvia
Marekani ya Kusini:
Oktoba 11:
Colombia v Chile
Ecuador v Uruguay
Venezuela v Paraguay
Argentina v Peru
Bolivia v Brazil
Oktoba 14:
Peru v Bolivia
Paraguay v Colombia
Brazil v Venezuela
Chile v Ecuador
Uruguay v Argentina
LIGI KUU ENGLAND: Aston Villa 1 Man City 1
Wenye mechi pekee ya Ligi Kuu iliyochezwa Villa Park, Wenyeji Aston Villa na Manchester City zilitoka suluhu ya bao 1-1.
Mpaka hafutaimu, Villa walikuwa mbele kwa bao 1-0 Mfungaji akiwa Richard Dunne kwa kichwa baada ya kona.
Dunne alikuwa Mchezaji na Nahodha wa Man City kabla ya kuhamia Villa msimu huu.
Kipindi cha pili Man City walisawazisha kupitia Craig Bellamy baada ya pasi ya Adebayor.

Sunday 4 October 2009

ZE BIGI MECHI: Chelsea 2 Liverpool 0
Hadi mapumziko mechi ilikuwa ngumu na suluhu lakini ushirikiano mwema kati ya Washambuliaji hatari wa Chelsea Didier Drogba aliempa pande tamu Nicolas Anelka dakika ya 59 na kupachika bao la kwanza ndio uliwafungulia njia Chelsea wakiwa nyumbani Stamford Bridge na kuwanyuka Liverpool 2-0 na kuchukua uongozi wa Ligi Kuu England.
Alikuwa tena Didier Drogba aliefanya kazi ya punda kwa kupigana na Mabeki wawili wa Liverpool katika dakika ya 91 na kuingia nao mpira ndani ya boksi na kuupenyeza kumfanya Malouda afunge bao la pili.
Chelsea wako kileleni wakiwa na pointi 21 na Mabingwa Watetezi Manchester United ni wa pili wakiwa na pointi 19.
West Ham 2 Fulham 2
Goli la dakika za majeruhi la Junior Stanislas limewapa West Ham suluhu ya bao 2-2 dhidi ya mtu 10 Fulham na kuwafanya wapate pointi ya kwanza Uwanja wa nyumbani Upton Park tangu ligi ianze.
Carlton Cole aliwapa uongozi West Ham dakika ya 16 na pengine walitegemea ubwete hasa baada ya Fulham kupata pigo kwa Mchezaji wao kutoka Afrika Kusini aliekuwa akicheza mechi yake ya kwanza, Kagisho Dikgacoi, kupewa Kadi Nyekundu na Refa Phil Dowd baada ya kuvaana na Scott Parker wa West Ham huku mpira ukiwa haupo kwao.
Refa Phil Dowd aliwapa Dikgacoi na Parker Kadi za Njano lakini ghafla akabadili uamuzi baada ya kuwasiliana na Msaidizi wake na kumpa Nyekundu Dikgacoi.
Kipindi cha pili Fulham walisawazisha dakika ya 47 kwa penalti iliyopigwa na Danny Murphy na kuongeza bao kupitia Gera dakika ya 57.
Everton 1 Stoke City 1
Robert Huth aliwapa uongozi Stoke daki ya 50 kufuatia kona lakini Leon Osman alisawazisha kwa Everton dakika ya 55 kwa bomba murua.
Arsenal 6 Blackburn 2
Leo Arsenal imeibamiza Blackburn Rovers mabao 6-2 katika mechi ya Ligi Kuu England iliyochezwa Uwanja wa Emirates.
Hadi mapumziko Arsenal walikuwa mbele kwa mabao 3-2.
Mabao ya Arsenal yalifungwa na Vermaelen dakika ya 17, Van Persie dakika ya 33, Arshavin, 37, Fabregas 57, Walcott 75 na Bendtner, 89.
Mabao ya Blackburn yalifungwa na Nzonzi dakika ya 4 na David Dunn dakika ya 30.
Kwa ushindi wa leo Arsenal wako nafasi ya 4 wakiwa na pointi 15 kwa mechi 7.
Mechi ya Wababe wa Scotland: Rangers 2 Celtic 1
Leo, Rangers imeibwaga Celtic 2-1 katika "dabi" iliyochezwa Uwanjani kwa Rangers Ibrox Stadium mjini Glasgow katika mechi ya Ligi Kuu ya Scotland.
Ni Mshambuliaji Kenny Miller wa Rangers ndie aliekuwa shujaa baada ya kupachika bao 2 katika dakika ya 8 na 16.
Bao la Celtic lilifungwa kwa penalti dakika ya 25 na McGeady.
Celtic bado anaongoza Ligi hiyo kwa kuwa na pointi 16 huku Rangers wana 15 kwa mechi 7 kwa kila Timu.
Steve Bruce ajutia kuibwaga nafasi kuwafunga Man U!!
Bosi wa Sunderland aliewahi kuwa Nahodha wa Manchester United, Steve Bruce, amesikitishwa na Timu yake kuipoteza nafasi ya kuifunga Manchester United Old Trafford pale walipojifunga wenyewe dakika za majeruhi na kufanya mechi hiyo iishe 2-2.
Beki wa Sunderland, Anton Ferdinand, mdogo wake Rio Ferdinand wa Man U, aliukwamisha mpira wavuni katika harakati za kuokoa katika dakika ya 92 na kuipa Man U dro ya 2-2.
Katika mechi hiyo ya jana, Sunderland waliongoza mara mbili kwa magoli ya Darren Bent na Kenwyne Jones lakini Man U walisawazisha.
“Inasikitisha!” Bruce alisema. “Sizijui takwimu zinasemaje lakini hii ni kawaida ya Man U kusawazisha au kushinda dakika za majeruhi! Hata kama hawachezi vizuri, huwa wanapata matokeo mazuri! Nadhani Ayatollah mwenyewe hukaa na kuwatazama!”
Beckham kurudi tena San Siro Januari
David Beckham amefichua kwamba yuko mbioni kukamilisha makubaliano ya yeye kurudi kuichezea tena AC Milan mwezi Januari mwakani wakati msimu wa Soka huko Marekani utakaposimama ili kuweka hai mategemeo yake ya kuichezea England kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwaka 2010.
Kocha wa England Fabio Capello ameshatamka kuwa ni lazima Beckham arudi kucheza Ulaya ili achaguliwe England.
Msimu uliokwisha Beckham aliichezea AC Milan kwa mkopo na hilo lilimwezesha kuendelea kuichezea England.
Ingawa kuna Klabu nyingi zinamtaka, akiwamo Harry Redknapp wa Tottenham, Beckham mwenyewe amesema hawezi kurudi kucheza England.
Beckham anatamka: “Siku zote nimesema, baada ya kuondoka Man United siwezi kurudi England kuchezea Klabu nyingine! Hiyo ni ngumu kwangu!”
Kwa sasa Beckham anachezea LA Galaxy kwenye Ligi ya Marekani ijulikanayo kama MLS .
Roy Keane awa mbogo kwa Maripota!!!
Meneja wa Ipswich, ambae alikuwa Nahodha wa Manchester United, Roy Keane, ambae Timu yake ipo mkiani kwenye Ligi ya Coca Cola Championship, amewafokea Waandishi mara baada ya mechi ambayo Ipswich ilifungwa 2-1 na Barsnley hapo jana.
Alipohojiwa na Mwandishi mmoja kama atabaki kuendelea kuwa Meneja baada ya Timu yake kutoshinda hata mchezo mmoja katika 10 waliyocheza tangu Ligi ianze, Keane alijibu: “Sitaki kujibu swali hilo”
Alipoendelea kuulizwa je jibu hilo linamaanisha ndio au hapana, Keane alisema: “Chukulia unavyopenda.” Na kutimka toka chumba cha mahojiano.
Fergie: “Refa Wiley hayuko fiti!”
Sir Alex Ferguson amemshambulia Refa Alan Wiley aliechezesha mechi ya jana iliyoisha 2-2 kati ya Timu yake Manchester United na Sunderland kwenye Ligi Kuu na kunusurika kufungwa kwa kusawazisha kwa bao la kujifunga mwenyewe kwa Beki Anton Ferdinand katika dakika za majeruhi.
Ferguson amedai Wiley hakuongeza muda sahihi kwenye dakika za majeruhi kwa vile hakuhesabu muda mpira uliposimama baada ya Man U kusawazisha na kuacha muda ubaki dakika zilezile 4 zilizoonyeshwa baada ya dakika 90 kwisha.
Goli la Man U la kusawazisha lilifungwa katika dakika hizo 4 za nyongeza.
Ferguson alisema: “Refa amenisikitisha. Hakuongeza muda wowote juu ya dakika zile 4 ingawa mpira ulisimama tulipofunga ndani ya dakika hizo 4. Alikuwa akitembea uwanjani badala ya kukimbia. Dhahiri alionyesha hayuko fiti. Kasi ya mchezo ilitaka Refa aliefiti. Angalia Marefa wa nje. Wako fiti kam Mbwa wa mwenye Bucha! Refa alikuwa akichukua sekunde 30 kumpa Mchezaji Kadi na kumwandika! Bila shaka alikuwa akipumzika wakati huo!”
Hata hivyo, Ferguson alikiri Man U ilicheza mpira mbovu sana na alikerwa na goli la pili walilofungwa. Ferguson alisema: “Ni goli laini! Pasi zetu zilikuwa mbovu! Hatukucheza vizuri!”
MATOKEO LIGI ZA ULAYA:
BUNDESLIGA:
Ijumaa, Oktoba 2:
Schalke 04 2 v Eintracht Frankfurt 0
Jumamosi, Oktoba 3
Bayer 04 Leverkusen 4 v FC Nurnberg 0
Bayern Munich 0 v FC Koln 0
Hannover 5 v SC Freiburg 2
VFL Bochum 1 v VfL Wolfsburg 1
FSV Mainz 2 v TSG Hoffeinheim 1
Borussia Munchen Gldbach 0 v VB Borussia Dortmund 1
ITALIA SERIE A:
Jumamosi, Oktoba 3
As Bari 0 v Catania 0
Inter Milan 2 v Udinese 1
SPAIN LA LIGA:
Jumamosi, Oktoba 3:
Cd Tenerife 0 v Deportivo La Coruna 1
FC Bacerlona 1 v UD Almeria 0
Atletico de Madrid 2 v Real Zaragoza 0
FIFA U-20 WORLD CUP EGYPT 2009
Raundi ya Pili yakamilika!
MATOKEO MECHI ZA JANA:
Costa Rica 2 Czech Republic 3
Australia 1 Brazil 3
Hungary 2 UAE 0
South Africa 2 Honduras 0
RATIBA RAUNDI YA PILI:
Jumatatu Oktoba 5:
Spain v Italy
Paraguay v Korea Republic
Jumanne, Oktoba 6:
Ghana v South Africa
Egypt v Costa Rica
Hungary v Czech Republic
Jumatano, Oktoba 7:
Brazil v Uruguay
Venezuela v UAE
Germany v Nigeria
Powered By Blogger