Saturday 12 September 2009

LIGI KUU ENGLAND: Jumamosi Septemba 12, 2009.
MATOKEO KWA UFUPI:
Arsenal yakung’utwa tena jijini Manchester, Chelsea, Liverpool zapeta!!!
Blackburn 3 v Wolverhampton 1
Blackburn: Robinson, Jacobsen, Samba, Givet, Chimbonda, Andrews, Grella, Diouf, Dunn, Pedersen, Roberts. Akiba: Brown, Emerton, Nelsen, Salgado, Kalinic, Di Santo, Hoilett.
Wolverhampton: Hennessey, Stearman, Berra, Mancienne, Hill, Halford, Henry, Milijas, Jarvis, Doyle, Keogh. Akiba: Hahnemann, Elokobi, Edwards, Surman, David Jones, Vokes, Maierhofer.
Stoke 1 v Chelsea 2
Magoli: Stoke: Faye. Chelsea: Drogba, Malouda
Stoke: Sorensen, Wilkinson, Huth, Abdoulaye Faye, Shawcross, Collins, Delap, Whitehead, Whelan, Beattie, Kitson. Akiba: Simonsen, Higginbotham, Lawrence, Fuller, Pugh, Sanli, Etherington.
Chelsea: Cech, Bosingwa, Ivanovic, Terry, Ashley Cole, Mikel, Ballack, Malouda, Lampard, Kalou, Drogba. Akiba: Hilario, Essien, Carvalho, Sturridge, Belletti, Anelka, Hutchinson.
Portsmouth 2 v Bolton 3
Portsmouth: James, Vanden Borre, Kaboul, Ben-Haim, Belhadj, Mokoena, Brown, O'Hara, Boateng, Smith, Piquionne. Akiba: Begovic, Mullins, Williamson, Utaka, Webber, Kanu, Yebda.
Bolton: Jaaskelainen, Ricketts, Knight, Cahill, Samuel, Steinsson, Cohen, Mark Davies, Muamba, Taylor, Kevin Davies. Akiba: Al Habsi, Robinson, Klasnic, McCann, Lee, Basham, Andrew O'Brien.
Liverpool 4 v Burnley 0
Magoli: Yossi Benayoun, bao 3. Kuyt bao 1.
Liverpool: Reina, Johnson, Skrtel, Carragher, Insua, Gerrard, Lucas, Kuyt, Benayoun, Riera, Torres. Akiba: Cavalieri, Voronin, Kyrgiakos, Ngog, Spearing, Degen, Dossena.
Burnley: Jensen, Mears, Carlisle, Bikey, Jordan, Alexander, Blake, McCann, Elliott, Steven Fletcher, Paterson. Akiba: Penny, McDonald, Gudjonsson, Nugent, Thompson, Guerrero, Eagles.
Man City 4 v Arsenal 2
Magoli: Man City: Almunia [kajifunga mwenyewe], Bellamy, Adebayor, Wright-Phillips. Arsenal: Rosicky, Van Persie
Man City: Given, Richards, Toure, Lescott, Bridge, Wright-Phillips, Ireland, Barry, De Jong, Adebayor, Bellamy. Akiba: Taylor, Onuoha, Zabaleta, Sylvinho, Petrov, Vidal, Weiss.
Arsenal: Almunia, Sagna, Vermaelen, Gallas, Clichy, Bendtner, Song Billong, Fabregas, Denilson, Diaby, van Persie. Akiba: Mannone, Rosicky, Eduardo, Ramsey, Silvestre, Eboue, Gibbs.
Sunderland 4 v Hull 1
Sunderland: Gordon, Bardsley, Turner, Ferdinand, Richardson, Malbranque, Cana, Cattermole, Reid, Bent, Campbell. Akiba: Carson, Nosworthy, Mensah, Murphy, Henderson, Jones, Da Silva.
Hull: Myhill, Zayatte, McShane, Sonko, Dawson, Ghilas, Kilbane, Olofinjana, Hunt, Geovanni, Fagan. Akiba: Duke, Barmby, Altidore, Mendy, Halmosi, Boateng, Vennegoor of Hesselink.
Wigan 1 v West Ham 0
Wigan: Kirkland, Melchiot, Boyce, Bramble, Figueroa, Thomas, Koumas, Gomez, Diame, N'Zogbia, Rodallega. Akiba: Pollitt, Edman, Cho, Scharner, Scotland, Sinclair, King.
West Ham: Green, Faubert, Upson, Tomkins, Gabbidon, Kovac, Noble, Parker, Stanislas, Cole, Hines. Akiba: Kurucz, Spector, Behrami, Da Costa, Nouble, Collison, Diamanti.
FIFA yaizuia Chelsea kuwarudisha hata Wachezaji wao waliowatoa kwa mkopo!!
FIFA imewaambia Chelsea hawaruhisiwi kuwarudisha Wachezaji wao waliowatoa kwa Klabu nyingine kwa mkopo wa msimu mzima kufuatia kifungo chao cha kutosajili Wachezaji kwa vipindi viwili vya usajili ikimaanisha hawawezi kusajili hadi mwaka 2011 adhabu ambayo wamepewa baada ya kumchukua Chipukizi Gael Kakuta kutoka FC Lens ya Ufaransa kinyume cha taratibu.
Ingawa Chelsea wana nia ya kukata rufaa kupinga adhabu hiyo, Meneja wao Carlo Ancelotti alitaka kupunguza makali ya adhabu hiyo kwa kuwarudisha Wachezaji wao Klabuni waliowatoa kwa mkopo akiwemo Mchezaji wa Timu ya Vijana ya England wa chini ya miaka 21 Michael Mancienne kutoka Wolves, Scott Sinclair toka Wigan na Muargentina Franco di Santo kutoka Blackburn.
FIFA imetoa ufafanuzi kuwa ni Di Santo pekee anaeweza kurudi Stamford Bridge kwa vile mkopo wake ni nusu msimu lakini Sinclair haruhusiwi kurudi kwa vile mkopo wake ni wa msimu mzima na kuhusu Mancienne, ingawa mkopo wake ni wa msimu mzima, FIFA itatoa uamuzi baadae kuhusu kipengele cha mkataba ambacho kinatamka anaweza kurudi Chelsea kwa dharura.
Mpaka sasa Chelsea wanangoja kupokea kutoka FIFA adhabu yao rasmi ndani ya siku 10 zijazo na kisha wanatakiwa ndani ya siku 21 kukata rufaa.
Chelsea wametaka kuwarudisha Wachezaji hao iliowatoa kwa mkopo ili wawe kava ya akina Didier Drogba, Michael Essien, John Obi Mikel na Salomon Kalou ambao itawakosa mwezi Januari 2010 kwani wote wanategemewa kuwakilisha Nchi zao kwenye mashindano ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika huko Angola.
Hata hivyo Januari 2010, Chelsea wanategemea majeruhi wao wa muda mrefu Paulo Ferreira na Joe Cole kurudi uwanjani baada ya kupona magoti waliyoumia.
Adebayor atoboa nini ugomvi wake na Bendtner!!!
Kisa ni viatu!!!
Januari 22, 2008, kwenye mechi ya Kombe la Carling, ulimwengu wa soka ulipigwa butaa baada ya kushuhudia Wachezaji wa Timu moja wakigombana na mmoja kumtwanga kichwa mwenziwe na kumpasua.
Tukio hilo liliihusu Arsenal walipocheza na Tottenham na Wachezaji hao ni Emmanuel Adebayor alipomvisha mwenziwe Nicklas Bendtner ‘ndoo!”
Wakati leo Adebayor na Bendtner watakutana uso kwa uso, safari hii wakiwa Timu pinzani, Adebayor akiwa Manchester City na Nicklas Bendtner akiwa bado yuko Arsenal, Adebayor ametoa bayana nini chanzo cha ugomvi huo.
Adebayor ametoboa kuwa mwanzo kabisa wa mfarakano wao ni viatu!
Adebayor amesema Klabuni Arsenal kulikuwa na sheria kuwa Mchezaji yeyote haruhusiwi kuingia kwenye Chumba cha kubadilishia Jezi na viatu vyake binafsi vya nyumbani.
Adebayor akapasua: “Kila siku Bendtner alivunja sheria hiyo na kuingia Chumbani humo na viatu vyake binafsi vya nyumbani! Nikamwambia tuheshimiane na vua viatu! Hapo ndipo uhasama ukaanza!”
Kuhusu siku aliyompiga kichwa Bendtner kwenye mechi, Adebayor ameeleza: “Alininyooshea kidole! Huwezi kumnyooshea mtu kidole!”
Kuhusu mechi ya leo kati ya Man City na Arsenal, Adebayor amesema: “Naiheshimu Arsenal na namuheshimu Wenger kama Meneja! Alex Song na Emmanuel Eboue sio marafiki- ni ndugu! Tumefanya vitu vingi pamoja na wao! Lakini sasa niko Man City na wao si marafiki wa Man City! Sasa leo kati ya saa 11 na saa 1 tutakuwa si ndugu! Baada ya mechi udugu utarudi!”
Na Bendtner je? Bila shaka uhasama wa viatu unaendelea!
Mjomba wa Berbatov alikuwa na wasiwasi kwake kujiunga na “Mashetani Wekundu!”
Mjomba wake Dimitar Berbatov ambae ni Padri anaepunga watu Mashetani alipatwa na wasiwasi mkubwa na kumkataza asijiunge na “Mashetani Wekundu!”
Berbatov anasema: “Mjomba wangu huko kwetu Bulgaria ni Padre anaepunga watu Mashetani na kufukuza pepo mbaya sasa aliposikia najiunga na Manchester United ambao jina la utani ni “Mashetani Wekundu” alinikataza nisifuate Mashetani!”
Lakini baadae, Mjomba huyo huyo, amemshukuru Berbatov kwa kuihama Tottenham na kwenda Manchester United na Berbatov anasema: “Ameniambia Kanisa lake limepata Waumini wengi zaidi! Bulgaria watu ni wehu kwa mpira na sasa Kanisa linajaa kwa vile nipo Manchester United! Lakini, kitu kizuri ni kuwa wanaenda huko kusikiliza na kujifunza kutoka kwa Padre!”
Kwa Berbatov, ingawa kwa sasa ni tajiri na mtu maarufu sana, Familia yake inabaki muhimu sana kwake na mwenyewe anadai aliamua kuihama Tottenham kwenda Man U alipokuwa akilima kabeji na viazi bustanini kwa Babu yake na ndipo Babu yake huyo akamshauri ajiunge na Man U.
Berbatov anasema: “Mafaninkio yangu ni kwa sababu ya Mama yangu. Sala zake, upendo wake na msaada wake ndio umenifikisha hapa! Najua hata nikimfanyia kitu chochte kikubwa hakiwezi kulipa msaada wake! Babu na Bibi yangu ni watu muhimu pia! Nikiwa likizo huwa nakuwa bustanini kwa Babu na yeye ni mtu mwenye hekima sana! Tunalima na ananipa mawaidha na ni yeye alieniambia nijiunge na Man U!”
Leo jioni, Berbatov anarudi uwanjani White Hart Lane nyumbani kwa Klabu yake ya zamani Tottenham na ametamka: “Nilifurahia wakati wangu nilipokuwa Spurs na Mashabiki walinipenda! Lakini ukisikia Klabu kama Man U inakutaka na unapata nafasi ya kucheza UEFA CHAMPIONS LEAGUE, haiwezekani ukasema hapana!”
Defoe na Redknapp wazoa Tuzo za mwezi
Mshambuliaji wa Tottenham Jermain Defoe na Meneja wake Harry Redknapp wameshinda Tuzo ya Barclays ya Mchezaji Bora na Meneja Bora wa mwezi ikiwa ni Tuzo ya kwanza kutolewa kwa msimu huu mpya wa 2009/10.
Tuzo hizi hutolewa kila mwezi na Wadhamini wa Ligi Kuu England, Barclays.
Defoe na Redknapp wamejishindia Tuzo hizo baada ya Timu yao Tottenham Hotspur kuanza vizuri sana kwenye Ligi Kuu na kushinda mechi zote 4 katika 4 walizocheza.
Hii ni mara ya kwanza kwa Defoe kushinda Tuzo hiyo wakati kwa Redknapp ni mara ya 6.
Mpaka sasa Tottenham wako nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu baada ya kuzifunga Liverpool 2-1, Hull City 5-1, West Ham 2-1 na Birmingham City 2-1.
Leo, Tottenham wana mtihani mkubwa uwanjani kwao White Hart Lane watakapopambana na Mabingwa Watetezi Manchester United.
Man City v Arsenal LEO:

Wenger akiri: “Ni muhimu kumsimamisha Adebayor!”
Arsene Wenger amekiri kuwa ili Timu yake Arsenal iambulie chochote kwenye mechi ya leo ya Ligi Kuu England watakapocheza City of Manchester City Stadium na wenyeji Manchester City ni muhimu kumkaba Emmanuel Adebayor alieihama Arsenal na kwenda Man City msimu huu kwa vile ndie anaeng’ara sana kwa sasa.
Adebayor msimu huu, katika mechi 3 za Man City Ligi Kuu ambazo wameshinda zote, amefunga goli katika kila mechi.
Wenger vilevile ameongeza kuwa katika miaka ya hivi karibuni Mchezaji pekee ambae kiwango chake kilipanda juu sana kwa muda mfupi ni Adebayor ambae alimnunua kutoka Monaco mwaka 2006.
Wenger amesema: “Tulimchukua kutoka Monaco akiwa hana namba huko na alipokuja kwetu kiwango chake kilipanda sana! Tunafurahia yote aliyotufanyia Arsenal na nadhani Klabu zote mbili, Arsenal na Man City, zimeridhika! Sisi tumepata pesa nzuri na wao wamepata Straika bora!”
Mbali ya Adebayor, Man City pia imemchukua msimu huu Mlinzi Kolo Toure kutoka Arsenal ambae pia anang’ara na Timu yake mpya akiiongoza ngome ambayo katika mechi zao 3 za Ligi Kuu hawajafungwa hata goli moja.
Katika mechi ya leo, Man City itawakosa nyota wao Robinho na Tevez ambao wote waliumia katika mechi moja wakati Nchi zao Brazil na Argentina zilipokutana kwenye mechi ya Kombe la Dunia Jumamosi iliyopita huko Rosario City, Argentina na Brazil kushinda 3-1.
Arsenal watamkosa majeruhi Andriy Arshavin lakini Nahodha wao Cesc Fabregas na Tomas Rosicky wapo fiti na huenda wakacheza.
Mechi kama hii msimu uliokwisha, Man City walishinda bao 3-0.
Refa katika mechi ya leo ni Mark Clattenburg.

Friday 11 September 2009

Kijue Kikosi cha Man U kilichosajiliwa UEFA CHAMPIONS LEAGUE
Kila Timu inayoshiriki UEFA CHAMPIONS LEAGUE inatakiwa isajili Wachezaji 25 lakini idadi hiyo inaweza ikaongezeka kwa kutumia Sheria ya UEFA inayoruhusu Vilabu kusajili Wachezaji waliozaliwa tarehe 1 Januari 1988 au baada ya hapo na ambao wamechezea Klabu hiyo mfululizo kwa zaidi ya miaka miwili tangu walipotimiza miaka 15.
Kwa kutumia kipengele hicho, Kikosi cha Man U kwenye UEFA kina jumla ya Wachezaji 35.
Wachezaji 25 waliosajiliwa: Edwin van der Sar, Gary Neville, Patrice Evra, Owen Hargreaves, Rio Ferdinand, Wes Brown, Michael Owen, Dimitar Berbatov, Wayne Rooney, Ryan Giggs, Ben Foster, Ji-sung Park, Nemanja Vidic, Michael Carrick, Nani, Paul Scholes, Fabio, Rafael, John O’Shea, Darren Fletcher, Antonio Valencia, Gabriel Obertan, Federico Macheda, Darron Gibson, Tomasz Kuszczak.
Wachezaji walioongezwa kwa kipengele maalum cha Sheria za UEFA:
Anderson, Danny Welbeck, Jonny Evans, Corry Evans, Sam Hewson, David Gray, Craig Cathcart, Ron-Robert Zieler, James Chester, Ben Amos
LIGI KUU England: Mechi za Wikiendi hii na taarifa zake mbalimbali
Emmanuel Adebayor atakuwa kivutio kikubwa wakati Klabu yake ya zamani Arsenal itakapotua City of Manchester Stadium kucheza na Wenyeji Manchester City hapo kesho.
Adebayor, akiwa na Man City msimu huu, amefunga bao katika mechi zote 3 za Ligi Kuu walizocheza na kushinda zote.
Katika mechi hizo 3, ngome ya Man City haijaruhusu hata bao moja na inaongozwa na Mchezaji mwingine alietoka Arsenal, Kolo Toure.
Tottenham ni Klabu nyingine ambayo haijapoteza mechi msimu huu baada ya kushinda mechi zao zote 4 ikiwa na ile waliyoipiga Liverpool bao 2-1 siku ya ufunguzi wa mechi za Ligi Kuu lakini kesho wana mtihani mkubwa pale watakapowakaribisha Mabingwa watetezi Manchester United Uwanjani White Hart Lane.
Chelsea, ambao ndio vinara wa Ligi baada ya mechi 4 na kushinda zote, kesho wapo safarini hadi Uwanja wa Britannia kupambana na Stoke City.
Liverpool, ambao tayari katika mechi 4 wamepoteza mbili, watakwaana na Wababe wa Manchester United na Everton, Timu iliyopanda Daraja Burnley uwanjani Anfield. Hata hivyo, Burnley, wakicheza ugenini, hawajashinda wala kutoka droo na hawajafunga hata goli moja katika mechi zao mbili walizocheza huko ugenini.
Huko katikati ya England, mjini Birmingham, kutakuwa na kindumbwendumbwe cha Watoto wa mji mmoja kukutana na mechi hii, kwa sababu za usalama, itachezwa saa 6 mchana kwa saa za Uingereza na kuwakutanisha Birmingham City na Aston Villa Uwanjani St Andrews. Villa ndio wanaoonekana wenye nguvu baada ya kushinda mechi zote 4 zilizopita kati yao ukiwemo ushindi wa mabao 5-1 Uwanjani Villa Park mwaka jana.
Fulham wanawakaribisha Everton uwanjani Craven Cottage siku ya Jumapili huku Klabu zote zikitaka ushindi hasa baada ya kutoanza vizuri Ligi msimu huu. Fulham wameshinda mechi moja tu walipowafunga Portsmouth siku ya ufunguzi na wenzao Everton walifungwa mechi zao zote 2 za kwanza na kushinda ya 3 walipoiua Wigan.
Portsmouth hawana pointi hata moja hadi sasa baada ya mechi 4 na wawakaribisha Bolton ambao nao pia wanasuasua baada ya kupoteza mechi zao zote 3.
Blackburn Rovers , mpaka sasa wamecheza mechi 3 na kutoka droo moja na kufungwa mbili, wanawakaribisha Wolves uwanjani Ewood Park. Wolves wameanza msimu huu kwa kuwafunga Wigan, kutoka droo na Hull City na kufungwa na West Ham na Man City.
Sunderland, walioshinda mechi 2 na kufungwa 2, watakuwa nyumbani Stadium of Light kucheza na Hull City ambao wamecheza mechi 4 na kushinda moja, droo moja na kufungwa 2.
Wigan watakuwa wenyeji wa West Ham kwao DW Stadium msimu uliokwisha ilikuwa ikiitwa KC Stadium.
Wigan wameshacheza mechi 4, wameshinda moja na kufungwa 3 wakati West Ham wana mechi 3 na wameshinda moja, droo moja na kufungwa moja.
Ramos ni Kocha wa CSKA Moscow
Kocha wa zamani wa Tottenham na Real Madrid Juande Ramos ameteuliwa Meneja wa CSKA Moscow na kumbadili Mbrazil Zico.
Ramos, baada ya kutimuliwa Tottenham Oktoba, 2008, alipata kazi Real Madrid ya mkataba wa miezi 6 ulioisha mwishoni mwa msimu uliokwisha.
CSKA Moscow wako Kundi moja pamoja na Manchester United kwenye UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
Germany Mabingwa Ulaya kwa Mabibi!!
Waitandika England 6-2 Fainali ya UEFA!!
Jana huko Helsinki, Finland, Timu ya Taifa ya Wanawake ya Germany iliwapiga England mabao 6-2 na kunyakua Ubingwa wa Ulaya hii ikiwa ni mara yao ya 5 kuchukua Ubingwa huo.
Ujerumani ilikuwa ya kwanza kupata mabao ya haraka haraka yaliyofungwa na Prinz dakika ya 20 na Behringer dakika ya 22.
England wakakomboa moja dakika ya 24 likifungwa na Carney.
Kipindi cha pili ndipo mvua ya magoli ikaanguka na Germany wakapachika bao la 3 dakika ya 51kupitia Kulig na England wakafunga bao lao la pili na la mwisho dakika ya 55 Mfungaji akiwa Smith.
Germany wakaongeza bao 3 nyingine kupitia Grings, dakika ya 62 na 73, na Prinz akapachika bao lake la pili na la 6 kwa Germany dakika ya 76.

Mechi za Vilabu zarudi tena!!
Baada ya mikiki na hekaheka, furaha kwa baadhi na huzuni kwa wengine katika Nchi zao mbalimbli zilizokuwa zikiwania kuingia Fainali Kombe la Dunia huko Afrika Kusini 2010, sasa tunarudi kwenye michuano ya Klabu kwenye LIGI KUU England, UEFA CHAMPIONS LIGI na EUROPA LIGI.
Ifuatayo ni Ratiba ya Wiki moja kuanzia Jumamosi hii hadi Jumapili, Septemba 20.
LIGI KUU ENGLAND:
Jumamosi, 12 Septemba 2009
[mechi zote saa 11 jioni saa za bongo isipokuwa ikitajwa]
Blackburn v Wolverhampton
Liverpool v Burnley
Man City v Arsenal
Portsmouth v Bolton
Stoke v Chelsea
Sunderland v Hull
Tottenham v Man Utd [saa 1 na nusu usiku]
Wigan v West Ham
Jumapili, 13 Septemba 2009
Birmingham v Aston Villa [saa 8 mchana]
Fulham v Everton [saa 12 na robo]
UEFA CHAMPIONS LEAGUE:
[mechi zote saa 3 dak 45 usiku bongo taimu]
Jumanne, 15 Septemba 2009
Atletico Madrid v Apoel Nicosia
Besiktas v Man U
Chelsea v FC Porto
FC Zurich v Real Madrid
Juventus v Bordeaux
Maccabi Haifa v Bayern Munich
Marseille v AC Milan
Wolfsburg v CSKA Moscow
Jumatano, 16 Septemba 2009
Dynamo Kiev v Rubin Kzan
Inter Milan v Barcelona
Liverpool v Debrecen
Lyon v Fiorentina
Olympiakos v AZ Alkmaar
Sevilla v Unirea Urziceni
Standard Liege v Arsenal
VfB Stuttgart v Rangers
EUROPA LIGI:
[Kuna jumla ya mechi 24 na hapa zinatajwa mechi zinazohusu Timu za Uingereza tu. Ratiba kamili tutaiweka baadae].
Alhamisi, 17 Septemba 2009
Hapoel Tel Aviv FC V Celtic
PFC CSKA Sofia v Fulham
Everton v AEK Athens
LIGI KUU ENGLAND:
[saa za bongo]
Jumamosi, 19 Septemba 2009
[saa 8 dak 45 mchana]
Burnley v Sunderland
[saa 11 jioni]
Bolton v Stoke
Hull v Birmingham
[saa 1 na nusu usiku]
West Ham v Liverpool
Jumapili, 20 Septemba 2009
[saa 9 na nusu mchana]
Man U v Man C
[saa 10 jioni]
Wolves v Fulham
[saa 11 jioni]
Everton v Blackburn
[saa 12 jioni]
Chelsea v Tottenham


Thursday 10 September 2009

Sweden wapendekeza Wachezaji wasipeane mikono ili kujikinga na Homa ya Mafua ya ‘KITI MOTO’!!!
Chama cha Soka cha Sweden kimetoa pendekezo Wachezaji wasipeane mikono kabla na baada ya mechi ili iwe kinga ya kutoeneza ugonjwa wa Mafua ya ‘Kiti moto’.
Huko Sweden kuliripotiwa Wachezaji kadhaa wa Timu moja waliugua ugonjwa huo ingawa hawakuwa wanatoka Klabu kubwa na wote inasemekana walipona.
Mwezi Julai Mchezaji wa Manchester City, Micah Richards, aliupata ugonjwa huo alipokuwa vakesheni nje ya Uingereza lakini akapona baada ya kupata matibabu na kukaa karantini siku kadhaa.
Mwezi Mei, Klabu za Mexico, Chivas Guadalajara na San Luis, ilibidi zijitoe kwenye Kombe la Klabu za Marekani ya Kusini, Copa Libertadores, baada ya kutokea mlipuko wa ugonjwa huo huko Mexico.
Sir Alex Ferguson aitetea Man U!
Sir Alex Ferguson ameutetea msimamo wa Klabu yake Manchester United kuhusu kuwasaini Vijana Wadogo toka nje ya Uingereza na kudai wao wanaburuzwa kwenye mgogoro huo kwa sababu wao ni klabu kubwa.
Kufuatia kufungiwa kwa Chelsea na FIFA kutosajili Wachezaji hadi 2011 baada ya kupatikana na hatia ya kukiuka taratibu walipomsaini Chipukizi Gael Kakuta kutoka FC Lens ya Ufaransa, Manchester United nao wakajikuta wakituhumiwa na Klabu nyingine ya Ufaransa Le Havre kuhusu kumsajili Bwana Mdogo Pogba.
Wakati huo huo Klabu ya Italia Fiorentina imewasiliana na FIFA kuhusu Man U kumchukua Kijana Michele Fornasier na kudai imempora ingawa Man U imesema Fiorentina haina mkataba na kijana huyo.
Ferguson amesema: “Siku zote watatuingiza kwenye migogoro kwa sababu tu ni Man U! Sasa kumekuwa na mtindo wa kurukia treni bila kujua iendako!”
Ferguson amesisitiza Man U haiwezi kutoa pesa kwa Wazazi wa Wachezaji kama inavyodaiwa na amesema itabidi Le Havre wajibu kwa nini walitoa tuhuma hizo zisizo msingi.
Ferguson akaongeza: “Tuhuma hizi zimeletwa na Mkurugenzi mmoja wa Le Havre mwenye kinyongo na sasa itabidi afute usemi huo! Sisi tunasajili kisheria. Klabu nyingine hufanya mambo kichinichini lakini sisi tunajiamini ni wakweli!”
Argentina wako njia panda kwenda Bondeni!
Argentina wako hatarini kukosa kucheza Fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu 1970 baada ya kufungwa na Paraguay 1-0 leo alfajiri.
Kikosi cha Diego Maradona wapo nafasi ya 5 wakiwa pointi moja nyuma ya Ecuador huku kumesalia mechi 2 kwa kila timu na ni Timu 4 za juu ndizo zinazoingia moja kwa moja Fainali huku ya 5 ikicheza na Mshindi wa 4 toka Kundi la Nchi za Marekani ya Kati, Kaskazini na Caribean.
Wakati Argentina wanaweweseka, Brazil, inayoongoza Kundi la Nchi za Marekani ya Kusini, ikichezesha Kikosi ‘dhaifu’ bila ya Kaka, Lucio na Fabiano waliokuwa na Kadi na pia Robinho aliekuwa majeruhi, waliifunga Chile 4-2 huku Mshambuliaji Nilmar akifunga bao 3 mguuni kwake na moja kufungwa na Baptista.
Ingawa Chile walifungwa bado wako nafasi ya 3.
Katika mechi nyingine, Ecuador waliifunga Bolivia 3-1 kwa magoli ya Edison Mendez, Antonio Valencia [wa Man U] na Cristian Benitez [Birmingham].
Uruguay wamejipa pia matumaini baada ya ushindi wa 3-1 juu ya Colombia na Venezuela wakaichabanga Peru 3-1.
Kipigo cha Argentina ni cha 4 katika mechi 5 za mwisho walizocheza kwenye Kundi lao hilo na presha inazidi kumbana Maradona.
Lakini mwenyewe Diego Maradona ametamka: “Mpaka tone langu la mwisho la damu, ntapigana kuifanya Argentina iingie Fainali! Hatupo nje ya Kombe la Dunia! Siogopi kusakamwa na siogopi mtu! Ntaendelea bila kujali nani ananiponda!”
Mechi zilizobaki za Argentina ni dhidi ya Peru na Uruguay.
Msimamo wa KUNDI hilo ni:
-Brazil pointi 33
-Paraguay pointi 30
-Chile pointi 27
-Ecuador pointi 23
-Argentina pointi 22
-Uruguay pointi 21
-Venezuela pointi 21
-Colombia pointi 20
-Bolivia pointi 12
-Peru pointi 10
MATOKEO KOMBE LA DUNIA: MAREKANI YA KUSINI
Jumatano, 9 Septemba 2009
Bolivia 1 v Ecuador 3
Uruguay 3 v Colombia 1
Paraguay 1 v Argentina 0
Venezuela 3 v Peru 1
Brazil 4 v Chile 2

MATOKEO KOMBE LA DUNIA: AFRIKA
Jumatano 9 Septemba 2009
Cameroun 2 Gabon 1
Magoli Cameroun Wafungaji Jean Makoun, dakika ya 25 na Samuel Etoo dakika ya 64.
Goli la Gabon Mfungaji Daniel cousin dakika ya 90.
BAIBAI MARADONA?
Argentina chali kwa mara ya pili mfululizo!!!!
Paraguay 1 Argentina 0, Paraguay waingia Fainali!!!
Paraguay leo alfajiri wameungana na Brazil kutoka Nchi za Marekani ya Kusini kuingia Fainali za Kombe la Dunia baada ya kuwapa kipigo cha bao 1-0 Argentina kwenye mechi iliyochezwa Paraguay.

Jumamosi, Argentina wakiwa nyumbani Rosario City, walipigwa bao 3-1 na Mahasimu wao wakubwa Brazil.
Bao la Paraguay lilifungwa na Haedo dakika ya 28.
Kwa kipigo hiki cha pili mfululizo ambacho mbali ya kuhatarisha sana nafasi ya Argentina kucheza Fainali huku zikiwa zimebaki mechi 2 tu kwenye Kundi lao, hata kibarua cha Kocha Diego Maradona sasa kina walakini mkubwa.
England, Spain zabingiria Bondeni!!
Mashine za Germany, Italia zanguruma kuelekea Bondeni!!
Ufaransa bado kimbembe!!
England waliitandika Croatia mabao 5-1 Uwanjani Wembley na kutinga Fainali Kombe la Dunia mwakani huko Afrika Kusini.
Mabao ya England yalifungwa na Frank Lampard, bao 2, Steven Gerrard, 2, na Wayne Rooney. Bao la Croatia lilifungwa na Eduardo.
Spain nao waliwapiga Estonia mabao 3-0 na wapinzani wao Bosnia-Herzegovina na Uturuki kutoka suluhu na hivyo kuwapa mwanya Spain kufuzu kuingia Fainali za Kombe la Dunia.

Mambo kwa Ufaransa ni magumu kwani jana wakiwa ugenini walitoka suluhu 1-1 na Serbia ambao wanaongoza Kundi lao kwa pointi 4 mbele ya Ufaransa huku mechi zimebaki 2.
MATOKEO KAMILI MECHI ZA ULAYA ZA JANA:
Jumatano, 9 Septemba 2009
Albania 1 v Denmark 1,
Andorra 1 v Kazakhstan 3,
Armenia 2 v Belgium 1,
Belarus 0 v Ukraine 0,
Bosnia-Herzegovina 1 v Turkey 1,
Czech Republic 7 v San Marino 0,
England 5 v Croatia 0,
Faroe Islands 2 v Lithuania 1,
Germany 4 v Azerbaijan 0,
Hungary 0 v Portugal 1,
Israel 7 v Luxembourg 0,
Italy 2 v Bulgaria 0,
Latvia 2 v Switzerland 2,
Liechtenstein 1 v Finland 1,
Malta 0 v Sweden 1,
Moldova 1 v Greece 1,
Montenegro 1 v Cyprus 1,
Northern Ireland 0 v Slovakia 2,
Norway 2 v FYR Macedonia 1,
Romania 1 v Austria 1,
Scotland 0 v Netherlands 1,
Serbia 1 v France 1,
Slovenia 3 v Poland 0,
Spain 3 v Estonia 0,
Wales 1 v Russia 3,

KOMBE LA DUNIA ASIA: Bahrain yaitoa Saudi Arabia, kupambana na New Zealand na mshindi ataenda Bondeni!!
Jana, Kisiwa kidogo cha Bahrain kiliwatoa Saudi Arabia nishai wakiwa nyumbani kwa kulazimisha suluhu ya 2-2 na kusonga mbele kwa magoli ya ugenini, baada ya mechi ya kwanza huko Bahrain kuwa 0-0 Jumamosi iliyopita, na hivyo mwezi ujao watacheza na New Zealand ili kupata mshindi atakaenda Fainali Kombe la Dunia huko Afrika Kusini 2010.
Saudi Arabia walipata bao la pili dakika za majeruhi, dakika ya 94, na kuongoza 2-1 na huku uwanja mzima ukishanglia ushindi wao mkubwa, Bahrain walipata kona na kusawazisha na mechi ikaisha sekunde chache baadae ikiuacha uwanja mzima umepigwa butaa kwani furaha ndani ya sekunde iligeuka huzuni.
Man U yaja juu, yasema hatuwezi kukaa kimya tukitukanwa!!
Mkurugenzi Mkuu wa Manchester United, David Gill, amesema ni ‘matusi’ kuambiwa kuwa wametoa pesa kwa Wazazi wa Paul Pogba ili wamsaini.
Mara baada ya Chelsea kufungiwa na FIFA kusaini wachezaji hadi 2011 kwa kumchukua kinyume cha taratibu Chipukizi Gael Kakuta aiekuwa Klabu ya FC Lens ya Ufaransa, Le Havre nayo pia ya Ufaransa ikaibuka na madai kama hayo wakidai wameporwa Kijana wao Pogba kinyume cha taratibu.
Gill amesema: “Hatuwatishi lakini hatukubali jina zuri la Manchester United lichafuliwe. Sisi tumefuata sheria zote.”
Jumatatu, Man U ilitoa onyo kwa Le Havre kwamba itawashitaki wakiendelea kutoa madai yao.

Wednesday 9 September 2009

KOMBE LA DUNIA: England na Serbia wanachungulia Fainali!!
England na Serbia watatinga Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwakani wakishinda mechi zao za leo Jumatano Septemba 9 na Spain, Denmark na Slovakia pia wanaweza kujihakikishia kucheza Fainali ikiwa, kwanza, watashinda na kisha mechi nyingine katika Makundi yao yaangukia upande wao na kuwasaidia.
England na Serbia zinaweza kufanya idadi ya Timu zilizotinga Fainali kufikia 10 ikiwa England itawafunga Croatia nyumbani Wembley Stadium katika KUNDI la 6 na Serbia wakiwafunga Ufaransa mbele ya Mashabiki wa Serbia kwenye Uwanja wa Marakana mjini Belgrade.
Mpaka sasa Timu zilizo Fainali ni Wenyeji Afrika Kusini, Uholanzi, Brazil, Ghana, Japana, Korea Kaskazini, Korea Kaskazini na Australia.
Huko Ulaya Washindi 9 wa kila Kundi wataenda Fainali na Timu 8 Bora zitakazoshika nafasi ya pili zitafanyiwa dro ili kuwe na mechi 4 na washindi wa mechi hizo wataingia Fainali.
Mabingwa wa Ulaya Spain wataingia Fainali wakiwafunga Estonia na wakati huo huo Turkey iwafunge Bosnia. Lakini hata Spain wakitoka droo na Turkey akishinda, Spain atenda Fainali.
Denmark atatinga Fainali ikiwa tu ataifunga Albania huku Portugal waifunge Hungary na Malta wasifungwe na Sweden.
Na kwa Slovakia, itabidi kwanza waombe Slovenia na Poland watoke suluhu kisha wao waifunge Ireland nyumbani kwao Belfast ndipo wataingia Fainali.
Mutu aomba atoe pesa kwenye Mifuko ya Hisani badala ya kuilipa Chelsea Pauni Milioni 15!!!!
**ASEMA HANA UWEZO KULIPA FAINI HIYO ILIYOWEKWA NA FIFA!
Adrian Mutu ametoa pendekezo ni bora achangie kwenye Mifuko ya Hisani au kwenye Mifuko yoyote inayowasaidia watu badala ya kuilipa Chelsea fidia ya Pauni Milioni 15 kama ilivyoamuliwa na FIFA na kuungwa mkono na CAS [Mahakama ya Usuluhishi Michezoni].
Mshambuliaji huyo kutoka Rumania alieigharimu Chelsea Pauni Milioni 15 mwaka 2003 alifukuzwa Chelsea mwaka mmoja baadae baada ya kugundulika anatumia cocaine na kufungiwa miezi 7 kutocheza soka.
FIFA iliamua Mutu ailipe Chelsea Pauni Milioni 15 ikiwa ni fidia lakini Mutu alikata rufaa kupinga uamuzi huo kwa Korti ya Usuluhishi Michezoni [CAS= Court of Arbitration for Sport].
Uamuzi wa CAS ulitolewa Julai mwaka huu na Mutu amebakiza muda wa wiki moja tu kukata Rufaa kwa Mahakama Kuu ya Uswisi ambayo ndiyo pekee yenye haki ya kusikiliza na kuamua maamuzi yanayotolewa na CAS.
Hatua ya Mutu ipo kwenye barua aliyowaandikia Chelsea, Kamati ya Nidhamu ya FIFA na Rais wa FIFA, Sepp Blatter.
Katika barua hiyo, Mutu ameandika: “Siwezi kulipa kiasi hicho. Si suala la kuamua bali la kuelewa na kufahamu misingi ya kutokuwa na uwezo. Napendekeza nitoe mchango mkubwa utakaoamuliwa ili kuwasaidia Vijana wenye matatizo ya madawa ya kulevya na pia kutoa kiwango hicho hicho kwa Mfuko wa Hisani watakauchagua Chelsea wa mjini London na Nchini kwangu Romania.”
Baada ya kutimuliwa Chelsea, Mutu alijiunga na Juventus Januari 2005 kama Mchezaji huru na hivyo Chelsea kutopata hata senti na msimu mmoja baadae akaenda Fiorentina ambako yuko mpaka leo.
David Gill wa Man U achaguliwa Chama cha Klabu Ulaya [ECA]!
Mkurugenzi Mkuu wa Manchester United, David Gill, amechaguliwa kwenye Bodi ya Chama cha Klabu Ulaya, ECA, [European Club Association] pamoja na Rais wa Real Madrid, Florentino Perez kwa kipindi cha miaka miwili.
ECA ina Bodi hiyo yenye Wawakilishi 15 na hupeleka Wajumbe wake kwenye Kamati za UEFA na kushirikiana na kutoa ushauri kuhusu masuala ya Soka huko Ulaya.
ECA inaundwa kutokana na Klabu 144 toka Nchi 53 za Ulaya na hupigania haki za Vilabu hivyo huko Ulaya.

Tuesday 8 September 2009

KOMBE LA DUNIA: MAREKANI YA KUSINI
RATIBA: Jumatano, 9 Septemba 2009
Bolivia v Ecuador
Uruguay v Colombia
Paraguay v Argentina
Venezuela v Peru
Brazil v Chile
KOMBE LA DUNIA: NCHI ZA ULAYA
RATIBA: Jumatano, 9 Septemba 2009
Albania v Denmark,
Andorra v Kazakhstan,
Armenia v Belgium,
Belarus v Ukraine,
Bosnia-Herzegovina v Turkey,
Czech Republic v San Marino,
England v Croatia,
Faroe Islands v Lithuania,
Germany v Azerbaijan,
Hungary v Portugal,
Israel v Luxembourg,
Italy v Bulgaria,
Latvia v Switzerland,
Liechtenstein v Finland,
Malta v Sweden,
Moldova v Greece,
Montenegro v Cyprus,
Northern Ireland v Slovakia,
Norway v FYR Macedonia,
Romania v Austria,
Scotland v Netherlands,
Serbia v France,
Slovenia v Poland,
Spain v Estonia,
Wales v Russia,

Rafa awaonya Mawinga wake Babel na Riera
Ryan Babel alitoka hadharani hivi karibuni na kusema bora aende kucheza kwao Uholanzi Timu ya Ajax ili ajihakikishie kuchukuliwa Timu ya Taifa ya Uholanzi ili acheze Fainali za Kombe la Dunia kwa sababu akiwa Liverpool hana namba ya kudumu na hilo limemfanya asichukuliwe Timu ya Uholanzi katika mechi za hivi karibuni.
Babel hakutajwa kwenye Kikosi cha Uholanzi kilichochaguliwa kucheza mechi za Kombe la Dunia Jumatano iliyopita ila aliitwa baadae baada ya Mshambuliaji mmoja kuumia.
Inaelekea kauli ya Babel imemtibua Kocha Rafa Benitez ambae alitoka na kudai kuwa Babel na Riera wote wanalilia kucheza na wote wanacheza pozisheni moja hivyo kuna ushindani mkubwa.
Benitez anasema: “Ujumbe ni rahisi tu. Kiwanjani kila Mchezaji lazima adhihirishe ana uwezo. Babel anajua hawezi kuhama kwa sasa. Ni lazima afanye kazi turidhike. Ni Mchezaji mzuri na ana kipaji. Ni muhimu tuongee nae na tuone anapata maendeleo gani.”
Sasa balaa la Wafaransa lawakumba Man City kwa kumpora Chipukizi!
Klabu ya Ufaransa Rennes imethibitisha kuwa wameishitaki Manchester City kwa FIFA kwa kumpora Chipukizi Jeremy Helan mwanzoni mwa mwaka huu.
Mwaka 2008, Kijana huyo Helan, miaka 17, alitakiwa na Manchester United lakini Rennes wakagoma kumtoa na ndipo Man City wakajikita na kumchukua ingawa Rennes walidai wana mkataba na Helan kuwa atasaini mkataba mwingine kama Mchezaji wa Kulipwa akifikisha miaka 17.
Huko Ufaransa hairuhsiwi mtoto chini ya miaka 18 kusaini mkataba wa kuwa Mchezaji wa Kulipwa wakati England wanaruhusiwa wakifikisha miaka 17.
Hivi juzi tu FIFA imeifungia Chelsea hadi 2011 kutosajili Mchezaji baada ya kupatikana na hatia ya kumpora Chipukizi Gael Kakuta kutoka FC Lens ya Ufaransa.
Siku mbili baadae ikaibuka Klabu nyingine ya Ufaransa Le Havre na kudai Manchester United imewapora Kijana wao Pogba kwa kuwarubuni Wazazi wake na kuwapa fedha taslimu na nyumba.
Hata hivyo, ingawa Le Havre imedai imepeleka mashtaka FIFA, FIFA imesema haijapokea chochote na wakati huo huo Manchester United imewataka Le Havre waache madai hayo au la watawashitaki.
Ingawa Rennes imepeleka kesi FIFA na wao pia wamepelekwa Mahakamani na upande wa Chipukizi Helan wakivutana kuhusu nini kilisainiwa wakati Helan alipojiunga na Rennes.
Kipa Paddy Kenny afungiwa Miezi 9 kwa kutumia madawa!!
Kipa wa Sheffield United inayocheza Daraja la Championship, chini tu ya Ligi Kuu, Paddy Kenny, miaka 31, amefungiwa kutocheza soka kwa miezi 9 kuanzia Julai 22, 2009 kwa kupatikana na hatia ya kutumia dawa ‘Ephedrine’ ambayo ipo kwenye listi ya dawa zinazokatazwa kwa Wanasoka kwani huongeza nguvu.
Paddy Kenny aligundulika kutumia dawa hiyo ambayo kawaida hutumika kutibu kifua hasa afueni kwenye pumu katika mechi Sheffield United walipocheza na Preston kwenye mechi maalum za mtoano kutafuta Timu kupanda Daraja kuingia Ligi Kuu.
Paddy Kenny amekiri kutumia dawa hiyo lakini alijitetea kuwa alikuwa akiumwa kifua.
Kamati ya Sheria ya FA, Chama cha Soka England, imesema imeridhika na utetezi wa Kenny Paddy kuwa hakutumia ‘Ephedrine’ kuongeza nguvu na ndio maana hawakumpa adhabu kali ya kifungo cha miaka miwili lakini ni wajibu wao kutoa adhabu ili iwe fundisho kwa Wachezaji wa Kulipwa kutotumia dawa bila ya maelekezo ya Madaktari wa Klabu zao.
Klabu ya Sheffield United imelalamika kuwa Kamati hiyo kwa sababu imekubali Kipa huyo hakutumia dawa hiyo kuongeza nguvu walitegemea adhabu ndogo zaidi au onyo au msamaha.
MAN U WAIONYA LE HAVRE!
Manchester United imeionya Klabu ya Le Havre ya Ufaransa kuwa watachukua hatua za kisheria ikiwa Klabu hiyo haitaacha kutoa madai kwamba waliwapa pesa Wazazi wa Chipukizi Paul Pogba, miaka 16, ili kijana huyo asaini kwao.
Rais wa Le Havre, Jean-Pierre Louvel, amedai kuwa Manchester United iliwapa Wazazi wa Pogba, Baba na Mama, Pauni 87,000 kila mmoja pamoja na nyumba ya kuishi mjini Manchester.
Louvel aliendelea na madai yake kwa kusema kuwa wameshapeleka malalimiko yao FIFA.
Wiki iliyopita, FIFA iliifungia Chelsea hadi mwaka 2011 kutosajili Mchezaji yeyote baada ya kupatikana na hatia ya kumchukua Mchezaji chipukizi Gael Kakuta kutoka FC Lenz ya Ufaransa kinyume cha taratibu.
Manchester United imesema imefuata taratibu zote za UEFA na FIFA na kwamba uhamisho huo ikiwa pamoja na Mikataba yake, ilipitiwa na kupasishwa na FA, Chama cha Soka England, pamoja na uongozi wa Ligi Kuu England. Vilevile, Man U walisisitiza kuwa kufuatana na kanuni za Klabu yao pamoja na sheria za soka wao hawawezi kutoa fedha au kuwanunulia nyumba Wzazi wa Mchezaji.
Hata hivyo, inasemekana Chama cha Soka cha Ufaransa, kufuatia shinikizo la Le Havre, bado hakijatoa Cheti cha Kimataifa cha Uhamisho na ndio maana FIFA hawajaubariki uhamisho huo.
Maradona aandamwa baada ya Brazil kuwachoma mkuki moyoni!!!
*Wengi waponda mbinu zake kwenye kipigo cha 3-1 na Brazil!
Tangu walipokuwa Wachezaji, Dunga na Maradona, walikuwa dunia tofauti. Dunga alikuwa mpiganaji anaehaha uwanja mzima akitafuta ushindi kwa kila hali wakati Diego Maradona alikuwa ni Mshambuliaji alieamini mashambulizi ya ufundi wa hali ya juu ndio njia bora.
Lakini, Jumamosi iliyopita, Argentina ya Maradona, iliyoahidi kushambulia mechi yote, ilijikuta ikibamizwa na Brazil iliyosimama ngangari kwa bao 3-1 na kufanya mategemeo ya Argentina kuingia Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini kuwa kwenye hatihati huku wakiwa wamebakiwa na mechi 3 tu.
Ingawa falsafa ya Dunga kuhusu uchezaji wa Brazil haumpi Mashabiki wengi kwani Kikosi chake si ile Brazil inayocheza ‘soka tamu’ kama la enzi za kina Pele, Bebeto, Romario, Zico na hata Ronaldo, lakini ni Brazil ya Dunga ndiyo iliyobeba Copa America na Kombe la Mabara hivi juzi na sasa kutinga Fainali Kombe la Dunia huku wana mechi 3 mkononi!
Juu ya yote, ni Brazil ya Dunga iliyomudu kuwapiga mahasimu wao wakubwa Argentina mara 3 tangu mwaka 2006!
Bila shaka Maradona, muumini wa mashambulizi mfululizo, atakerwa sana na timu yake jinsi ilivyoshindwa kuleta hatari golini mwa Brazil na, bila shaka pia, udhaifu wa Argentina kwenye ngome utampa Maradona kero kubwa zaidi kwani, kwenye kipindi cha kwanza walipachikwa na Brazil bao 2 zote zikitokana na frikiki za Elano walizoshindwa kuzilinda na badala yake, kwa goli la kwanza, kumwacha Luisao akipiga kichwa akiwa pekee bila kuwepo ulinzi wowote na bao la pili lilifungwa tena kwa frikiki waliyoshindwa kujihami nayo vizuri na mpira kumfikia Fabiano aliefunga kilaini.
Magazeti ya huko Argentina, baada ya mechi hiyo, yameweka vichwa vya habari vikubwa wakiiponda Timu ya Maradona na kuiita sio timu huku mengine yakidai Maradona ameshindwa kuibadili Argentina.
Fadhaa ya wengi Argentina inaangukia kwa Mchezaji wao Bora ambae wengi wanaamini kuwa ndie bora kuliko wote kwa sasa duniani , Lionel Messi, ambae anang’ara sana akiwa na Klabu yake FC Barcelona lakini akiwa na jezi ya Argentina hupwaya sana na siku ya mechi na Brazil alijikuta yuko mpweke sana katikati ya ngome imara ya Brazil.
Nalo Gazeti moja huko Argentina, mbali ya kumponda Maradona, pia lilimcharukia Messi na kunyooshea kidole maamuzi yake mabovu uwanjani na uchoyo wa kutoa pasi kwa wenzake.
Argentina wako nafasi ya 4 ambayo ndiyo nafasi ya mwisho kwa Timu kufuzu kuingia Fainali za Kombe la Dunia moja kwa moja na Timu iliyo nafasi ya 5 itabidi icheze na Timu itayomaliza nafasi ya 4 toka Kundi la Nchi za Marekani ya Kati, Kaskazini na Caribean ili kupata timu moja kwenda Fainali.
Lakini, nyuma tu ya Argentina, wakiwa pointi mbili nyuma, ni Ecuador na Colombia na wote bado wapo kwenye kinyang’anyiro cha kugombea nafasi hiyo ya 4 na ya 5.
Hivyo njia kwa Argentina si nyeupe kwani Jumatano wanakwenda ugenini kucheza na timu ngumu ya Paraguay walio nafasi ya pili nyuma ya Brazil.
Kisha mwezi Oktoba watacheza na Peru nyumbani na kumaliza ugenini na Uruguay.

Monday 7 September 2009

Bilic adai wamegundua udhaifu wa England!
Kocha wa Croatia, Slaven Bilic, ambayo Timu yake inakutana na England Jumatano Uwanjani Wembley kwenye mechi muhimu ya mtoano ya kuwania kuingia Fainali Kombe la Dunia, amedai kuwa wamegundua udhaifu wa Timu ya England na watatumia mwanya huo siku hiyo ya Jumatano.
Mpaka sasa, England, walio chini ya Kocha toka Italia, Fabio Capello, wanaongoza Kundi lao kwa kushinda mechi 7 katika 7 walizocheza na wako mbele ya timu ya pili Croatia kwa pointi 4 na pia wana mechi moja mkononi.
England wakiifunga Croatia hiyo Jumatano watatinga Fainali Afrika Kusini.
Croatia, walio nafasi ya pili Kundi hili, wamewazidi Timu ya 3, Ukraine, pointi 3 lakini Ukraine wana mechi moja mkononi.
Hivyo, ni muhimu sana Croatia kuifunga England ingawa itakuwa mechi ngumu kwao hasa kwa vile katika mechi ya kwanza kati ya timu hizo, England waliwaumbua Croatia kwa kuwapigia bao 4-1 nyumbani kwao mjni Zagreb.
Hata hivyo, Croatia wanapata matumaini hasa wakikumbuka Novemba, 2007, Uwanjani Wembley, walipowafunga England 3-2 na kuwang’oa England kuingia Fainali za EURO 2008.
Slaven Bilic, enzi za Uchezaji wake alichezea West Ham mwaka 1996 na 1997 kisha kwenda kucheza Everton mwaka 1997 hadi 2000, amesema: “England kwa sasa ni Timu tofauti. Wana uzuri wao lakini kuna kitu kimepungua kwao. Sasa wanaukosa ule “Uingereza” ambao uliifanya iwe ngumu kufungika zamani! Lakini, tunajua nini hasa wanakikosa na siwezi kuwaambia ni nini! Ni siri yetu!”
Ghana watinga Bondeni, Nchi ya kwanza Afrika kuingia Fainali Kombe la Dunia 2010!!!
Ghana ni Nchi ya kwanza ya Afrika kufanikiwa kuingia Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwaka 2010 baada ya kuifunga Sudan bao 2-0 mjini Accra hapo jana.
Nchi nyingine inayonyemelea kujiunga na Ghana ni Ivory Coast, ambao juzi waliikung’uta Burkina Faso 5-0, na sasa wanahitaji pointi moja tu kutinga Fainali.
Afrika kuna Makundi matano na Mshindi wa kila Kundi ndie atacheza Fainali huko Afrika Kusini wakati Timu 3 za juu kila Kundi zitacheza Kombe la Mataifa ya Afrika huko Angola mwakani.
MATOKEO KOMBE LA DUNIA:
MECHI ZA: Jumapili Septemba 6,
Togo 1 v Morocco 1
Mozambique 1 v Kenya 0
Nigeria 2 v Tunisia 2
Algeria 1 v Zambia 0
Ghana 2 v Sudan 0
Benin 1 v Mali 1

Sunday 6 September 2009

NANI AMEFUZU KUSHUKA BONDENI?
-BRAZIL: Wamefanikiwa kuingia Fainali kutoka Kundi la Nchi za Marekani ya Kusini leo alfajiri baada ya kuwafunga Mahasimu wao wakubwa Argentina waliokuwa kwao Rosario City kwa mabao 3-1.
Brazil ni Nchi pekee duniani kucheza Fainali zote za Kombe la Dunia.
Kocha wa Brazil Dunga amesema: “Ni furaha. Tumeifunga Timu ngumu yenye Mchezaji, Messi, ambae pengine kwa sasa ndie Bora kuliko wote! Tumewafunga Argentina kwao na wao hawajafungwa nyumbani kwenye michuano hii!”
-KOREA KASKAZINI: Hapo Juni 17, baada ya Iran kushindwa kuifunga Korea Kusini, Korea Kaskazini walihitaji suluhu tu na Saudi Arabia kwenye mechi iliyochezwa Riyadh siku hiyo hiyo.
Korea Kaskazini walipata suluhu ya 0-0 na kutinga Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini ikiwa ni mara ya kwanza tangu walipofikia Robo Fainali ya Kombe la Dunia mwaka 1966 iliyochezwa Uingereza na kutolewa na Portugal, ikiwa na Mchezaji hatari wakati huo, Eusebio, kwa mabao 5-3 ingawa walikuwa wakiongoza 3-0 hadi mapumziko.
-UHOLANZI: Juni 6, Uholanzi ilimudu kuwa Nchi ya kwanza kutoka Ulaya kutinga Fainali za Kombe la Dunia baada ya kuwafunga Iceland ugenini mabao 2-1 na mpaka hapo walikuwa wameshinda mechi zao zote kwenye Kundi lao.
-KOREA KUSINI: Kwa kuweza kuingia Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwakani, Korea Kusini sasa wametimiza kucheza Fainali yao ya 7 mfululizo. Waliingia Fainali Juni 6 walipowafunga Falme ya Nchi za Kiarabu mabao 2-0 mjini Dubai.
-AUSTRALIA: Australia walipata ubwete kutinga Fainali za Kombe la Dunia waliposhinda mechi zao zote 6 bila kufungwa hata goli na waliupata uhakika huo baada ya kutoka suluhu 0-0 na Qatar mjini Doha hapo Juni 6, 2009.
-JAPAN: Japan ilikuwa Nchi ya kwanza kupata tiketi ya kwenda Afrika Kusini walipoifunga Uzbekistan kwao mjini Tashkent bao 1-0. Hiyo pia ilikuwa Juni 6.
KOMBE LA DUNIA: Argentina 1 Brazil 3
Brazil wamewanyuka Mahasimu wao wakubwa Argentina 3-1 wakiwa nyumbani kwao Rosario City katika mechi muhimu ya Kombe la Dunia na kutinga Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwaka 2010 na kuwaacha Argentina wamesambaratika na kutojua hatima yao.
Mabao ya Brazil yalifungwa na Luisao, dakika ya 29, Faabiano bao 2 dakika ya 34 na 69.
Bao la Argentina lilifungwa dakika ya 67.
Argentina: Andujar; Zanetti, Dominguez, Otamendi, Heinze; Maxi, Mascherano, Veron, Datolo; Messi, Tevez. Akiba: Carrizo, Papa, Gago, Milito, Schiavi, Coloccini, Aguero.
Brazil: Julio Cesar; Maicon, Lucio, Luisao, Andre Santos;
Silva, Felipe Melo; Elano, Kaka; Robinho, Luis Fabiano. Akiba: Victor, Dani Alves, Miranda, Lucas, Ramires, Julio Baptista,
Adriano.
Refa: Julian Oscar Ruiz Acosta (Colombia
MATOKEO KOMBE LA DUNIA: AFRIKA
MECHI ZA: Jumamosi Septemba 5, 2009-09-05
Gabon 0 v Cameroon 2
Togo v Morocco [mechi inachezwa leo]
Mozambique v Kenya [mechi inachezwa leo]
Nigeriav Tunisia [mechi inachezwa leo]
Rwanda 0 v Egypt 1
Algeria v Zambia [mechi inachezwa leo]
Ghana v Sudan [mechi inachezwa leo]
Benin v Mali [mechi inachezwa leo]
Malawi 2 v Guinea 1
Ivory Coast 5 v Burkina Faso 0
MATOKEO KOMBE LA DUNIA: ULAYA
Jumamosi, 5 Septemba 2009
Armenia 0 v Bosnia-Herzegovina 2,
Austria 3 v Faroe Islands 1,
Azerbaijan 1 v Finland 2,
Bulgaria 4 v Montenegro 1,
Croatia 1 v Belarus 0,
Cyprus 1 v Rep of Ireland 2,
Denmark 1 v Portugal 1,
France 1 v Romania 1,
Georgia 0 v Italy 2,
Hungary 1 v Sweden 2,
Iceland 1 v Norway 1,
Israel 0 v Latvia 1,
Moldova 0 v Luxembourg 0,
Poland 1v Northern Ireland 1,
Russia 3 v Liechtenstein 0,
Scotland 2 v FYR Macedonia 0,
Slovakia 2 v Czech Republic 2,
Spain 5 v Belgium 0,
Switzerland 2 v Greece 0,
Turkey 4 v Estonia 2,
Ukraine 5 v Andorra 0,
MATOKEO KOMBE LA DUNIA NCHI ZA MAREKANI YA KUSINI
Jumamosi, 5 Septemba 2009-09-05
Colombia 2 v Ecuador 0
Peru 1 v Uruguay 0
Paraguay 1 v Bolivia 0
Argentina 1 v Brazil 3
KOMBE LA DUNIA: Baharain 0 Saudi Arabia 0
Bahrain na Saudi Arabia jana zilitoka suluhu 0-0 mjini Manama, Bahrain na Timu hizi zitarudiana Jumatano ijayo Nchini Saudi Arabia.
Mshindi atakutana na New Zealand mwezi Oktoba na Novemba ili kupata Timu moja itakayoingia Fainali Kombe la Dunia.
MECHI YA KIRAFIKI: England 2 Slovenia 1
Kwenye Uwanja wa Wembley, England wameifunga Slovenia mabao 2-1 katika mechi ya kirafiki.
England Jumatano, hapohapo Wembley, watacheza na Croatia kwenye mechi ya Kombe la Dunia na endapo England watashinda basi watatinga Fainali huko Afrika Kusini mwaka 2010.
Mabao ya England yalifungwa na Frank Lampard kwa penalti baada ya Wayne Rooney kuangushwa na la pili na Jermain
Defoe.
Powered By Blogger