Saturday 22 August 2009

Man United wainyuka Wigan 5-0!!
Baada ya kupoteza mechi yao siku ya Jumatano walipofungwa bila kutegemewa na Timu ngeni iliyopanda Daraja msimu huu Burnley kwa bao 1-0, leo Sir Alex Ferguson amefanya mabadiliko ya Wachezaji 7 na kuibuka na ushindi mnono wa 5-0 walipoifunga Wigan ugenini.
Mabao ya Manchester United, yote yakipatikana kipindi cha pili, yalifungwa na Rooney mabao mawili na kumfanya afikishe mabao 101 akiwa na Man U, Berbatov, Michael Owen na Nani.
Vikosi vilikuwa:
Wigan: Kirkland, Melchiot, Scharner, Bramble, Figueroa, N'Zogbia, Thomas, Brown (Scotland 62), Koumas (Sinclair 62), Gomez, Rodallega.
Akiba hawakucheza: Pollitt, Edman, Watson, Boyce, King.
Man Utd: Foster, O'Shea, Jonathan Evans, Brown (Neville 71), Evra, Park, Anderson (Valencia 59), Carrick, Giggs, Owen (Berbatov 63), Rooney.
Akiba hawakucheza: Kuszczak, Scholes, Gibson, De Laet.
Refa: Howard Webb
Arsenal waendeleza ushindi!!!
Arsenal wakiwa kwao Emirates Stadium leo wamepata ushindi wao wa pili mfululizo katika LIGI KUU England walipoifunga Portsmouth 4-1.
Diaby alipachika mabao mawili, dakika ya 18 na 21, Gallas moja dakika ya 51, Ramsey dakika ya 68 na bao la Portsmouth lilifungwa na Younus Kabul.
Vikosi vilikuwa:
Arsenal: Almunia, Sagna, Gallas, Vermaelen, Clichy, Fabregas (Ramsey 72), Song Billong, Denilson, Bendtner (Eboue 63), van Persie (Eduardo 72), Arshavin.
Akiba hawakucheza: Mannone, Silvestre, Gibbs, Merida.
Portsmouth: James, Kaboul, Wilson, Distin, Belhadj, Vanden Borre (Utaka 46), Diop (Basinas 42), Mokoena, Mullins, Kranjcar, Piquionne (Kanu 79).
Akiba hawakucheza: Begovic, Hughes, Nugent, Ward.
Refa: Steve Benett
Matokeo mechi nyingine:
Hull City 1 Bolton 0
Man City 1 Wolves 0
Sunderland 2 Blackburn 0
Birmingham 0 Stoke 0
Mchezaji wa West Ham achomwa kisu, hali mbaya hospitalini!!!!
Beki wa West Ham Calum Davenport, umri miaka 26, na Mama yake mzazi walichomwa visu wakiwa nyumbani kwao na hali ya Mchezaji huyo imeelezwa kuwa ni mbaya na ilibidi afanyiwe upasuaji.
Hali ya Mama yake pia ni mbaya ingawa Madaktari wameridhishwa nayo.
Tukio hilo lilitokea Ijumaa usiku.
Liverpool wamsaini Mlinzi Kyrgiakos
Klabu ya Liverpool imekamilisha taratibu za kumsaini Beki wa Kimataifa wa Ugiriki Sotirios Kyrgiakos kutoka AEK Athens kwa ada ya Pauni Milioni 2.
Kyrgiakos, miaka 30, anaecheza kama Sentahafu, aliwahi kuichezea Rangers ya Scotland na amesaini mkataba wa miaka miwili.
Wakati huohuo, Beki wa Liverpool, Daniel Agger, atafanyiwa upasuaji wa mgongo na atakuwa nje ya uwanja kwa wiki 6.
Adriano arudishwa tena Timu ya Brazil
Mshambuliaji Adriano alieisusa Inter Milan na kugoma kurudi kwenye Timu hiyo na sasa yuko kwao Brazil akichezea Klabu ya Flamengo, ameitwa tena kwenye Kikosi cha Timu ya Taifa ya Brazil kitakachocheza na Wapinzani wao wakubwa Argentina Septemba 5 kwenye mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia. Siku 4 baadae Brazil watachuana na Chile kwenye mashindano hayo hayo.
Kikosi kamili:
Makipa: Julio Cesar (Inter Milan), Victor (Gremio);
Walinzi: Andre Santos (Fenerbahce), Daniel Alves (Barcelona), Maicon (Inter), Filipe (Deportivo La Coruna), Lucio (Inter), Luisao (Benfica), Miranda (Sao Paulo), Juan (AS Roma);
Viungo: Elano (Galatasaray), Felipe Melo (Juventus), Gilberto Silva (Panathinaikos), Josue (VfL Wolfsburg), Ramires (Benfica), Julio Baptista (AS Roma), Kaka (Real Madrid), Lucas (Liverpool);
Washambuliaji: Luis Fabiano (Sevilla), Nilmar (Villarreal), Robinho (Manchester City), Adriano (Flamengo

Friday 21 August 2009

Lampard: "Ni Messi tu anaweza kumbadili Ronaldo!"
Kiungo wa Chelsea Franck Lampard amesema Manchester United hawawezi kupata mbadala wa Cristiano Ronalndo labda wamchukue Messi.
Hata hivyo Lampard amesema anaamini pengo la Ronaldo litazibwa kwa Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson kuifanya Timu hiyo icheze "kitimu" badala ya kutegemea mtu mmoja na hivyo amekiri Man U itakuwa tishio.
Rio nje mwezi!!
Taarifa zinasema Beki kigogo wa Manchester United, Rio Ferdinand, atakuwa nje ya uwanja mwezi mzima baada ya kuumia musuli pajani mazoezini.
Hivyo Ferdinand ataikosa mechi ya Jumamosi hii dhidi ya Wigan na Jumamosi ijayo dhidi ya Arsenal.
EUROPA LEAGUE: Everton na Fulham zapeta mechi ya kwanza nyumbani, Villa yapigwa kimoja ugenini!!!
Kwenye mechi za kwanza za mchujo wa kuwania kuingia kwenye Makundi ya EUROPA LEAGUE Klabu za England Aston Villa, Everton na Fulham, zilizomaliza LIGI KUU England zikiwa nafasi za 5, 6 na 7 na hivyo kupata nafasi kucheza Ulaya, leo zilitupa karata zao na ni Aston Villa pekee waliocheza ugenini walifungwa bao 1-0 na Rapid Vienna ya Austria huku Everton na Fulham zikipata ushindi mnono kwao.
Everton waliibamiza Sigma Olomouc ya Urusi kwa mabao 4-0 mawili mguuni kwa Luis Saha na mengine mawili toka kwa Chipukizi Jack Rodwell.
Fulham waliinyuka Amkar Perm ya Urusi 3-1 kwa mabao ya Jonhson, Dempsey na Zamora.
Marudiano ya mechi hizi ni wiki ijayo.
Matokeo mengine ni:
Ajax 2 Bratislava 0
CSKA Sofia 0 Dinamo Moscow 0
FC Twente 3 FK Qabarag 1
Guingamp 1 Hamburg 5
MFK Kosice 3 Roma 3

Thursday 20 August 2009

Man U mashakani?
Mechi mbili tu ndani ya Msimu mpya wa Ligi zilizochezwa na Mabingwa Manchester United, zote zikiwa dhidi ya Timu zilizopanda Daraja msimu huu, moja waliyoifunga Birmingham 1-0 na ya pili kufungwa na Burnley 1-0, tayari baadhi ya watu wameanza kuchonga kuwa matokeo yote hayo ni sababu ya pengo kubwa la Ronaldo na ufa wa kukosekana kwa Carlos Tevez.
Ingawa katika mechi hizo mbili za kwanza za Ligi Man U wameonekana kupwaya kidogo, kuwa butu na kukosa spidi ya kuponyoka Mabeki, wengi wamesahau ile “desturi” ya Mabingwa hao kuanza Ligi kwa upole na matokeo mabovu lakini mwishowe hupamba moto na hatimaye kuibuka Mabingwa, mtindo uliowafanya wanyakue Ubingwa mara 11 katika Misimu 17 iliyopita ikiwemo kuwa Bingwa kwa Misimu mfululizo mitatu iliyopita.
Wengi pia hawakuona au wanasahau kuwa katika mechi hizo mbili za kwanza Man U imewakosa baadhi ya Vigogo wao ambao ni majeruhi. Listi hii wamo Kipa Edwin van der Sar, Mabeki Rio Ferdinand na Nemanja Vidic, Viungo Owen Hargreaves na Darren Fletcher.
Vilevile, Sir Alex Ferguson, Meneja wa Man U, alibadilisha Wachezaji 6 kutoka kile Kikosi kilichoifunga Birmingham katika mechi na Burnley.
Graeme Souness, Mchezaji na Meneja wa zamani wa Liverpool, anaeleza: “Ni kweli Ronaldo ni Mchezaji Bora Duniani alieibeba Man U kwa misimu miwili iliyopita lakini huweza ukapima pengo lake kwa sasa! Lakini, kama Michael Owen atakuwa fiti kwa muda mrefu atafunga goli nyingi tu! Najua ntaudhi watu wengi nikisema hili lakini ukweli ni kwamba Owen hajawahi kucheza Timu nzuri yenye Wachezaji wazuri kama Manchester United! Atakuwa mashine ya magoli tu!”
Juu ya yote kuna Mdau amedai bahati na hatima ya Timu zote huwa ni mzunguko unaoamuliwa na jinsi Wachezaji Bora wanapoingia au kuhama Timu.
Kitu cha mwisho kabisa alichokifanya Patrick Viera akiwa na Jezi ya Arsenal ni kuifungia Klabu hiyo bao la ushindi katika mikwaju ya penalti tano tano katika Fainali ya Kombe la FA mwaka 2005 na kuibebesha Arsenal Kombe hilo.
Kisha akahama- na tangu wakati huo Arsenal haijashinda Kombe lolote!!!
Alipoondoka David Beckham Old Trafford mwaka 2003, Manchester United hawakuchukua Ubingwa kwa miaka minne!!
Ni kweli Mchezaji Bora Duniani, Cristiano Ronaldo, amehama na haiwezekani kumpata mbadala, na, ingawa Manchester United, kama “desturi” yake imeonyesha kwa mara nyingi tena mwanzo wa kusuasua kwenye Ligi, utakuwa mwehu ukimpinga Sir Alex Ferguson kwani historia itakusuta!!!
Yeye ni gwiji wa kuleta marekebisho na mafanikio!!!
Mwana wa Sir Alex Ferguson matatani!!!!
Mtoto wa Sir Alex Ferguson, Darren Ferguson ambae ni Meneja wa Klabu ya soka ya Peterborough United, timu iliyo Daraja chini tu ya Ligi Kuu England liitwalo Coca Cola Championship, ameshitakiwa na FA, Chama cha Soka England, kwa kosa la kumtukana Refa mara tu baada ya mechi ya Ligi ambapo Timu yake ilifungwa bao 3-2 na West Bromwich Albion.
Darren Ferguson [pichani], aliepewa mpaka Jumanne ijayo kuwasilisha utetezi wake, alikasirishwa na kitendo cha Refa kuwanyima Peterborough bao la kusawazisha.
EUROPA LEAGUE: Leo Mechi za Mchujo kuwania kuingia hatua ya Ligi kwenye Makundi
Viwanja mbalimbali Ulaya vitawaka moto kwa Klabu maarufu kuchuana kutafuta Timu 48 zitakazoingia hatua ya Makundi ambapo Timu hizo zitagawanywa Makundi 12 ya Timu 4 kila moja na kucheza mtindo wa Ligi wa nyumbani na ugenini.
Baadhi ya Mechi za moto za leo ni:
Ajax v Bratislava
Athletic Bilbao v Tromso
Benfica v Vorskia Poltava
Brondby v Hertha Berlin
CSKA Sofia v Dinamo Moscow
Dinamo Zagreb v Hearts
Everton v Sigma Olomouc
FC Sion v Fenerbahce
FC Twente v FK Qarabag
Fulham v Amkar Perm
Galatasaray v Lev, Tallinn
Guingamp v Hamburg
Lazio v Elfsborg
MFK Kosice v Roma
Rapid Vienna v Aston Villa
Stabaek v Valencia
Werder Bremen v FC Aktobe

-
LIGI KUU ENGLAND: MAN U WABAMIZWA, LIVERPOOL, TOTTENHAM ZATOA VIPIGO & BIRMINGHAM YAJIKONGOJA!!!!
Katika mechi za Ligi Kuu zilizochezwa jana usiku, Mabingwa watetezi Manchester United, wakicheza soka bovu sana ambalo lilimkasirisha hata Meneja Sir Alex Ferguson, walichapwa na Burnley Timu iliyopanda Daraja msimu huu kwa mara ya kwanza katika muda wa miaka 33.
Burnley walipata ushindi wa bao 1-0 huku Man U wakikosa kufunga penalti aliyopiga Michael Carrick na kuokolewa na Kipa wa Burnley.
Mahasimu wa Man U, Liverpool, baada ya kupigwa 2-1 na Tottenham katika mechi ya kwanza ya Ligi, jana waliangusha mkong’oto kwa Stoke City wa mabao 4-0 wakiwa kwao Anfield.
Nao Tottenham wakicheza ugenini walipata ushindi wao wa pili mfululizo pale walipowapiga Hull City mabao 5-1. Na Birmingham waliipachika Portmouth bao 1-0.
LIGI KUU itaendelea wikiendi hii kwa Ratiba ifuatayo:
Jumamosi, Agosti 22
[Saa 11 jioni bongo taimu]
Arsenal v Portsmouth
Birmingham v Stoke City
Hull City v Bolton
Man City v Wolverhampton
Sunderland v Blackburn
Wigan v Man U
Jumapili, Agosti 23
[Saa 9 na nusu mchana]
West Ham v Tottenham
[Saa 11 jioni]
Burnley v Everton
[Saa 12 jioni]
Fulham v Chelsea

Jumatatu, Agosti 24
[Saa 4 usiku]
Liverpool v Aston Villa

Wednesday 19 August 2009

Moyes ambwaga Mchezaji wake Lescott!!
Meneja wa Everton, David Moyes, amemwondoa kutoka kwenye Kikosi cha Kwanza cha Everton Beki Joleon Lescott na kumtupa kwenye mazoezi ya Timu ya Akiba kwa kile alichokiita mwenendo usioridhisha wa Beki huyo hasa kufuatia kuomba kwake rasmi kuruhusiwa kuhamia Manchester City.
Lescott, aliekuwemo kwenye Timu ya Everton iliyobamizwa magoli 6-1 na Arsenal Uwanjani kwao Goodison Park siku ya Jumamosi kwenye mechi ya awali ya LIGI KUU kwa timu hizo mbili, amekuwa akiwindwa na Manchester City ambao tayari wameshatoa of mbili za Pauni Milioni 15 na nyingine ya Pauni Milioni 18 na zote zimekataliwa na Everton ambao hawataki kumuuza ingawa kuna tetesi kuwa endapo Manchester City watatoa Pauni Milioni 30 basi Everton watamuachia Mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 27 ambae pia huchezea England.
Moyes amekaririwa akisema: “Tumemtoa Kikosi cha Kwanza kwa sababu hana ari na atabaki huko hadi Dirisha la Uhamisho lifungwe Agosti 31 na hapo ndipo atafunua macho na kuanza kupata ari mpya. Kumtoa Kikosini hakuna maana tunamuuza! Yeye ni Mchezaji mzuri na tunaempenda sana!”
Inasemekana Moyes amekasirishwa sana na mwenzake Mark Hughes ambae ni Meneja wa Manchester City kwa jinsi anavyomrubuni Joleon Lescott.
Kesho Everton inapambana na Sigma Olomouc ya Czech Republic kwenye mpambano wa EUROPA LEAGUE.
KWA Ufupiiiii....................................:
-Salgado atua Ewood Park!!!
Michael Salgado, miaka 33, Veterani kutoka Spain, alieichezea Real Madrid kwa muda wa miaka 10 na kuiwezesha kutwaa Ubingwa wa Ulaya mara mbili na La Liga mara nne, amesaini mkataba wa miaka miwili na Klabu ya Blackburn Rovers inayoongozwa na Sam Allardyce anaesifika kwa kuwachota Wachezaji Wakongwe na kuwaibua upya kama alivyofanya na akina Jay Jay Okocha.
Salgado, alieiwakilisha Timu ya Taifa ya Spain mara 53, ametemwa na Real Madrid kabla msimu huu kuanza.
-Kipa wa zamani wa Arsenal kustaafu soka!!!
Jens Lehman, Kipa wa zamani wa Arsenal na Timu ya Taifa ya Ujerumani, ambae atafikisha umri wa miaka 40 Novemba mwaka huu, atastaafu kucheza soka mwishoni mwa msimu huu ulioanza majuzi.
Lehman, ambae kwa sasa ni Kipa wa Klabu iliyo Bundesliga VfB Stuttgart, ameidakia Timu ya Ujerumani mara 61 na kucheza Arsenal kati ya 2003 na 2008.
-Wakala wa Vidic akanusha Nemanja kwenda Barca!!!
Paolo Fabbri, Wakala wa Beki mahiri wa Mabingwa Manchester United, Nemanja Vidic, amekanusha taarifa zilizomnukuu yeye na kuzagaa sana leo hii kuwa ametamka Vidic ana nia ya kuhamia Spain Klabuni Barcelona.
Fabbri amesema yeye hakusema hayo ila anachojua ni kuwa Vidic anajisikia raha kuwa na Manchester United.
UEFA CHAMPIONS LEAGUE: Arsenal yaipiga Celtic 2-0 nyumbani kwao!!
Arsenal jana walianza vyema harakati zao za kutaka kuingia hatua ya Makundi ya UEFA Champions League baada ya kuibugiza Celtic ya Scotland hukohuko kwao Uwanjani Parkhead kwa mabao 2-0.
Timu hizi zitarudiana wiki ijayo Jumanne Emirates Stadium nyumbani kwa Arsenal.
Matokeo mechi nyingine za UEFA CHAMPIONS LEAGUE zilizochezwa jana ni: [kwenye mabano ni Nchi Timu zinazotoka]
FC Sheriff Tiraspol [Moldova] 0 Olympiacos [Greece] 2
Celtic [Scotland] 0 Arsenal [England] 2
Poli Aek Timisoara [Romania] 0 VfB Stuttgart [Germany] 2
FC Kobehavn [Denmark] 1 APOEL Nicosia FC [Cyprus] 0
Sporting Lisbon [Portugal] 2 Fiorentina [Italy] 2

LIGI KUU ENGLAND: Chelsea wachanja mbuga!
Jana Chelsea wameendeleza wimbi lao la ushindi baada ya kushinda ugenini walipoipiga Sunderland mabao 3-1 mabao yote matatu yakifungwa kipindi cha pili baada ya Sunderland kuongoza kwa bao lililofungwa na Darren Bent hadi mapumziko.
Mabao ya Chelsea yalifungwa na Ballack, Lampard [penalti] na Deco.
Katika mechi nyingine za LIGI KUU, Wigan wakiwa nyumbani walipachikwa kimoja na Wolverhampton timu iliyopanda Daraja msimu huu.
Mechi za leo LIGI KUU ni: [saa za bongo]
-SAA 3 DAK 45 usiku
Birmingham v Portsmouth
Burnley v Manchester United
Hull City v Tottenham
-SAA 5 usiku
Liverpool v Stoke City
Powered By Blogger