Saturday 6 June 2009

KAZAKHSTAN 0 ENGLAND 4
England ikicheza ugenini Uwanja wa Almaty Central huko Almaty, Kazakhstan wamewafunga wenyeji wao Kazakhstan mabao 4-0 kwenye mechi ya Kundi la 6 la Nchi za Ulaya kugombea nafasi za kuingia Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwaka ujao 2010.
Mabao ya England yalifungwa na Gareth Barry na Emile Heskey kwenye kipindi cha kwanza na kipindi cha pili Wayne Rooney akapachika la 3 kisha Frank Lampard akafunga bao la 4 kwa njia ya penalti baada ya Heskey kuchezewa faulo.
England Jumatano ijayo nyumbani kwao Wembley, London watacheza mechi nyingine ya Kundi lao na Andorra.

England ndie anaeongoza Kundi hilo kwa kuwa na pointi 18 akifuatiwa na Croatia, anaecheza baadae leo na Ukraine, akiwa na pointi 10.
KIKOSI CHA ENGLAND: Green, Johnson, Terry, Upson, A Cole, Walcott, Barry, Lampard, Gerrard, Rooney, Heskey.AKIBA: Robinson, Lescott, Bridge, Defoe, Wright-Phillips, Beckham, Crouch.
MATOKEO KOMBE LA DUNIA:
NCHI ZA ASIA:
NORTH KOREA 0 IRAN 0
UZBEKISTAN 0 JAPAN 1
NCHI ZA AFRIKA:
ZAMBIA 1 RWANDA 0
MALAWI 0 BURKINA FASO 1
GABON 3 TOGO 0
Rais wa Real sasa ataka urafiki na Man U!!!!
Rais wa Real Madrid Florentino Perez amedai yeye anajali zaidi urafiki na Manchester United kuliko kumsaini Ronaldo.
Perez amesema: ‘Ikitokea siku moja Ronaldo atakuja kucheza Real basi hiyo itakuwa fahari kwetu! Lakini ikibidi nichague urafiki na Manchester United au kumsaini Ronaldo, ntachagua urafiki na Man U! Na ieleweke sijasema Ronaldo atakuja Bernabeu!’
Perez akaongeza: ‘Ntazungumza na Sir Alex Ferguson na David Gill [Mkurugenzi Mtendaji wa Man U] ili kudumisha urafiki!’’
Wenger-Defensi lazima iimarike!!!
Bosi wa Arsenal Arsene Wenger amekiri kuwa ana nia ya kuimarisha safu yake ya ulinzi kipindi hiki cha usajili kwani Defensi yao ilikuwa inavuja sana na iliruhusu mabao 37 katika LIGI KUU na wakamaliza nafasi ya 4 kwenye ligi hiyo wakiwa pointi 18 nyuma ya Mabingwa Manchester United.
Kwa sasa Wenger yuko Uchina akisaka Wachezaji na amesema: ‘Msimu ulioisha tulianza ligi pole pole lakini tukaimarika kadri muda ulivyosogea. Tuna Timu changa na itakuwa nzuri tu ingawa inabidi tuimarishe Defensi’

Friday 5 June 2009

Gattuso ndani ya Italia Bondeni!!
Kiungo wa AC Milan Gennaro Gattuso ametajwa na Meneja wa Italia Marcello Lippi kuwa ni mmoja wa Wachezaji 23 wa Italia watakaoshuka Bondeni, huko Afrika Kusini, kushindania Kombe la Mabara la FIFA wiki ijayo wakiwa Kundi moja pamoja na Watetezi wa Kombe hilo Brazil, USA na Mabingwa wa Afrika Egypt.
Gattuso hajacheza karibu msimu mzima baada ya kuumia goti lakini kwa mshangao wa wengi yupo Kikosini pamoja na Fulbeki chipukizi Davide Santon [18] wa Inter Milan na Mshambuliaji aliekulia Manchester United Giuseppe Rossi anaechezea Villarreal.
Mwingine ambae uteuzi wake ni wa kushangaza ni Andrea Dossena wa Liverpool.
KIKOSI KAMILI:
Gianluigi Buffon (Juventus), Marco Amelia (Palermo), Morgan De Sanctis (Galatasaray); Fabio Cannavaro (Juventus), Giorgio Chiellini (Juventus), Gianluca Zambrotta (Milan) Fabio Grosso (Lyon), Davide Santon (Inter), Alessandro Gamberini (Fiorentina), Nicola Legrottaglie (Juventus), Andrea Dossena (Liverpool); Mauro Camoranesi (Juventus), Gennaro Gattuso (Milan), Angelo Palombo (Sampdoria), Riccardo Montolivo (Fiorentina), Daniele De Rossi (Roma), Andrea Pirlo (Milan); Alberto Gilardino (Fiorentina), Vincenzo Iaquinta (Juventus), Fabio Quagliarella (Napoli), Luca Toni (Bayern Munich), Giuseppe Rossi (Villarreal), Pepe (Udinese)
KOMBE LA MABARA
Kombe la Mabara la FIFA, jina rasmi 2009 FIFA Confederations Cup, litakaloanza Afrika Kusini tarehe 14 Juni 2009 na kumalizika Juni 28, ni Mashindano ya 8 ya Kombe hili na kawaida huchezwa kwa Mwenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia mwaka mmoja kabla Fainali hizo kuanza ikiwa kama matayarisho maalum na pia kutangaza Fainali za Kombe la Dunia.
Bingwa Mtetezi wa Kombe hilo ni Brazil alielinyakua mwaka 2005 huko Ujerumani.
Timu ambazo zitakazoshiriki safari hii huko Afrika Kusini ni:
-Afrika Kusini: kama Mwenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia 2010.
-Italia: Bingwa wa Kombe la Dunia mwaka 2006
-USA: Bingwa wa Nchi za Marekani ya Kaskazini, Kati na Carribean mwaka 2007
-Brazil: Bingwa wa Marekani Kusini mwaka 2007 [Copa America 2007]
-Iraq: Bingwa wa Asia mwaka 2007
-Egypt: Bingwa wa Afrika mwaka 2008
-Spain: Bingwa wa Ulaya mwaka 2008
-New Zealand: Bingwa wa Bara la Baharini [Oceania]
Viwanja:
Miji minne ya Afrika Kusini ndio itakuwa Wenyeji wa mechi za Kombe la Mabara 2009:
-Johannesburg: Kiwanja cha Coca Cola Park [Uwezo Watazamaji 62,567]
-Pretoria: Kiwanja cha Loftus Versfeld [Uwezo Watazamaji 50,000]
-Bloemfontan: Kiwanja cha Free State [Uwezo Watazamaji 48,000]
-Rustenberg: Kiwanja cha Royal Bafokeng [Uwezo Watazamaji 42,000]
Makundi
Timu zimegawanywa kwenye Makundi mawili na:
-KUNDI A: Afrika Kusini, Spain, Iraq na New Zealand
-KUNDI B: USA, Italia, Brazil na Egypt
RATIBA: [saa za bongo]
-Jumapili 14 Juni 2009
KUNDI A:
Afrika Kusini v Iraq [saa 11 jioni]
New Zealand v Spain [saa 3 na nusu usiku]
-Jumatatu 15 Juni 2009
KUNDI B
Brazil v Egypt [saa 11 jioni]
USA v Italy [saa 3 na nusu usiku]
-Jumatano 17 Juni 2009
KUNDI A
Spain v Iraq [saa 11 jioni]
Afrika Kusini v New Zealand [saa 3 na nusu]
-Alhamisi 18 Juni 2009
KUNDI B
USA v Brazil [saa 11 jioni]
Egypt v Italia [saa 3 na nusu usiku]
-Jumamosi 20 Juni 2009
KUNDI A [Mechi zote zinaanza pamoja saa 3 na nusu usiku]
Iraq v New Zealand
Afrika Kusini v Spain
-Jumapili 21 Juni 2009
KUNDI B [Mechi zote zinaanza pamoja saa 3 na nusu usiku]
Italia v Brazil
Egypt v USA
NUSU FAINALI:
Jumatano Juni 24: MSHINDI KUNDI A v MSHINDI WA PILI KUNDI B
Alhamisi Juni 25: MSHINDI KUNDI B v MSHINDI WA PILI KUNDI A
Jumapili 28 Juni: FAINALI

Thursday 4 June 2009

Bongo 2 New Zealand 1
Jana Taifa Stars waliifunga New Zealand mabao 2-1 kwenye mechi ya kirafiki iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
New Zealand wako njiani kwenda Afrika Kusini kushiriki Kombe la Mabara la FIFA litakaloanza Juni 14 na kushirikisha Nchi Bingwa wa Mabara yote Duniani pamoja na Mwenyeji Afrika Kusini na Bingwa wa Dunia Italia. Nchi nyingine kwenye Mashindano hayo ya FIFA ya kuwapa uhondo Washabiki kabla ya Fainali Kombe la Dunia mwakani ni Brazil, Egypt, Spain, USA na Iraq
Mabao ya Bongo yalifungwa na Jerry Tegete na Mwinyi Kazimoto.
Baada ya mechi, Kocha wa New Zealand aliipa bigi faivu Stars kwa mchezo murua na kusema Tanzania imepanda kisoka.
Nae Maximo, Kocha wa Bongo, alifurahishwa na bidii za Wachezaji wake na kuwataka wasilegeze uzi katika mazoezi.
Ufaransa yafungwa na Nigeria na kuzomewa!!!
Kocha wa Ufaransa Raymond Domenech amelalamika baada ya Wachezaji wa Ufaransa kuzomewa na Mashabiki katika mechi ya kirafiki na Nigeria waliyotunguliwa bao 1-0 hapo juzi.
Domenech amevisema vitendo hivyo ni ubaguzi kwa vile vililenga kwa baadhi ya Wachezaji hasa Wachezaji wanaochezea Lyon kwa vile mechi ilichezwa Uwanja wa Klabu ya St Etienne ambayo ni pinzani na Lyon.
Wachezaji Karim Benzema na Sidney Govou, wote wa Lyon, ndio waliozomewa mno na Mashabiki hao na Domenech, ambae zamani alikuwa Mchezaji wa Lyon, amekiita kitendo hicho ni usaliti na ubaguzi mkubwa.
Ufaransa wanacheza mechi nyingine ya kirafiki dhidi ya Uturuki Ijumaa kwenye Uwanja wa Lyon kwani mechi zao za mchujo kuingia Fainali Kombe la Dunia Afrika Kusini 2010 mwezi Agosti watakapocheza na Faroe Islands na Septemba watacheza na Romania.
Real mimacho kwa Kaka na Ronaldo
Rais wa Real Madrid Florentino Perez, bila kupoteza wakati tangu alipothibitishwa Rais hapo Jumatatu,, ameanza kampeni zake kwenye vyombo vya habari kwa kutangaza anafanyia kazi ‘kuwabeba’ Kaka na Cristiano Ronaldo ili watue Bernabeu.
Inadaiwa kwa sasa Real Madrid wako mazungumzoni na AC Milan ili wamnunue Kaka lakini habari hizo hizo zinasema hamna mazungumzo ya aina yeyote kati ya Real Madrid na Manchester United ambao msimu uliopita walikataa katakata hata kufikiria kumuuza Ronaldo na ilifika hatua ya wao kuwashitaki Real Madrid FIFA kwa kujaribu kumrubuni Ronaldo kinyume cha taratibu.
Perez amekaririwa akisema: ‘Kaka, Ronaldo na Messi ndio bora duniani! Nitafanyia kazi kuwaleta Kaka na Ronaldo Real!! '
Juzi Jumanne ziliibuka habari kuwa Chelsea wanataka kuiteka nyara dili ya Kaka kwa kutoa ofa ya kitita cha Pauni Milioni 73.3 kumnunua Kaka kutoka AC Milan dau ambalo liliipiku ofa ya Real Madrid ya Pauni Milioni 56 lakini baadae Chelsea wakakanusha taarifa hizo.
Perez akaongeza: ‘Ikiwa Chelsea hawamo kwenye kinyang’anyiro ni nafuu kwetu! Tuna uhusiano mzuri na AC Milan na mimi ni rafiki na Adriano Galliani [Meneja Mkuu AC Milan] na hii itarahisisha kazi yangu.’
Hata hivyo Mmiliki wa AC Milan, Silvio Berlusconi, ambae pia ndie Waziri Mkuu wa Italia, amekanusha taarifa zote za Kaka kwenda Real Madrid na amesema: ‘Hamna uamuzi. Ntakutana na Kaka Jumatatu kasha ntawaambieni nini kitajiri.’
LIGI KUU kuonyesha mechi China, Afrika na India bure!!!
Wamiliki wa LIGI KUU England, wakati wanajitayarisha kwa Mkutano wao Mkuu wa Mwaka, wamedokeza kuwa kuna mipango ya kubadilisha jinsi makubaliano ya kupeperusha matangazo ya mechi laivu yanavyofikiwa na pia kutoa ofa ya kuonyesha baadhi ya mechi zake za laivu bure kwa Watangazaji wa TV China, Afrika na India wenye Stesheni zinazotangaza bure.
Kikao cha Mkutano huo wa mwaka kinachoanza leo kitasimamiwa na Mkurugenzi Mkuu wa LIGI KUU, Richard Scudamore, na Mkuu wake wa Habari na Matangazo, Phil Lines, ndie atatoa mapendekezo hayo mapya.
Hatua hii inakuja kwa kile walichokiita kukabiliana na hatari ya kushindwa na Kampuni za Kimarekani katika vita ya matangazo ya michezo kwenye TV.
Ingawa LIGI KUU imezalisha zaidi ya Pauni Bilioni 2 kwa matangazo ya Msimu wa 2010/11 ambayo tayari yashauzwa na mechi zake za msimu uliopita wa 2008/9 kushuhudiwa katika nyumba Milioni 662 dunia nzima, Wasimamizi hao wa LIGI KUU wamekiri kuwa walifanya kosa kubwa huko China kwa kukubaliana na Kampuni binafsi ya TV iitwayo WinTV ambayo haina soko kubwa kwenye Nchi hiyo yenye Watu wengi sana wakati NBA, Chama cha Mpira wa Vikapu cha Marekani, na Ligi nyingine za Soka kama vile Bundesliga, zinaonyeshwa kwenye TV ya Serikali ya China CCTV ambayo hutazamwa na watu wengi sana huko.
Hiyo ndio sababu kubwa inayowafanya LIGI KUU kutoa ofa ya kuonyesha baadhi ya mechi laivu bure katika Nchi za China na India, zenye watu wengi sana, na Bara la Afrika ambako LIGI KUU ndio nambari wani.

Wednesday 3 June 2009

Carvalho: ‘Ni mwaka mbaya sana kwangu!!’
Ricardo Carvalho, Sentahafu wa Chelsea, amesema yuko tayari kuhama Chelsea baada ya kuteseka msimu mzima uliopita kwa kuumia mara kwa mara na kuuita mwaka huo ‘ni mbaya sana kwake!’
Mlinzi huyo toka Ureno mwenye umri wa miaka 31 amezungumza akiwa kwenye Kambi ya Timu ya Taifa ya Ureno inayojitayarisha kwa mechi za mchujo kuwania nafasi za kuingia Fainali Kombe la Dunia huko Afrika Kusini 2010.
‘Nimekuwa na mafanikio mazuri Chelsea kwa miaka minne,’ Carvalho alisema. ‘Lakini mie niko tayari kwa yeyote atakaenitaka!’
Carvalho amecheza zaidi ya mechi 100 akiwa Chelsea tangu alipotua hapo pamoja na Meneja Jose Mourinho wote wakitokea FC Porto ya Ureno mwaka 2004.
Lakini msimu uliokwisha juzi, msimu wa mwaka 2008/9, Carvalho ameichezea Chelsea mechi 18 tu.
Nahodha West Ham aukataa mkataba mpya!!
Lucas Neill, Nahodha wa West Ham, amekataa kusaini mkataba unaomuongezea mwaka mmoja.
Neill [31], anaetoka Australia, amegoma kusaini mkataba huo wa mwaka mmoja kwa madai kuwa unashusha hadhi na thamani yake kama Mchezaji na Nahodha wa West Ham.
Neill kwa sasa yuko na Timu yake ya Taifa ya Australia itakayocheza mechi 3 dhidi ya Qatar, Bahrain na Japan za mchujo za Kundi la Asia ili kuwania nafasi kuingia Fainali ya Kombe la Dunia Afrika Kusini 2010 na Australia inahitaji pointi moja tu katika mechi hizo 3 ili kutua Afrika Kusini.
Lucas Neill alinunuliwa na West Ham Januari 2007 kutoka Blackburn kwa thamani ya Pauni Milioni 1 na nusu.
Hata hivyo inaelekea West Ham wana nia ya kujijenga upya chini ya Meneja Gianfranco Zola kwani Tovuti ya Klabu hiyo imetaja majina ya Wachezaji 12 tu watakaobaki kwa msimu ujao na nao ni Herita Ilunga, Jack Collison, Mark Noble, Savio Nsereko, Freddie Sears, Junior Stanislas, Marek Stech, James Tomkins, Dean Ashton, Valon Behrami, Carlton Cole na Scott Parker.
Klabu hiyo pia imesema Wachezaji Diego Tristan, Lee Bowyer, Walter Lopez, Kyel Reid, Tony Stokes na Jimmy Walker wote wako huru kuondoka hapo.
Steve Bruce athibitishwa Bosi mpya Sunderland!!!!

Mchezaji wa zamani wa Manchester United, Steve Bruce [48], amethibitishwa na Klabu ya Sunderland kuwa ndie Meneja mpya na amesaini mkataba wa miaka mitatu.
Steve Bruce anachukua nafasi ya Ricky Sbragia alieachia ngazi siku ya mwisho ya msimu wa LIGI KUU England mara tu baada ya Sunderland kupuruchuka kushushwa Daraja.
Sbragia alirithi cheo hicho toka kwa Nahodha wa zamani wa Manchester United Roy Keane aliebwaga manyanga mwenyewe Desemba mwaka jana.
Steve Bruce ameshawahi kuwa Meneja kwenye Klabu za Sheffield United, Huddersfiled, Crystal Palace, Birmingham na Wigan alikokuweko kwa vipindi viwili tofauti na ndiko alikotokea na kuhamia Sunderland.
Owen Hargreaves huenda asiendelee kucheza?
Kuna taarifa ambazo hazijathibitishwa na Klabu ya Manchester United lakini zinapamba moto kwenye Vyombo vya Habari kuwa Owen Hargreaves [28] wa Manchester United ambae alifanyiwa operesheni mbili kwenye kila goti lake huenda asirudi tena uwanjani na nyingine zinadai hata akirudi basi hawezi kucheza kwa muda mrefu.
Owen Hargreaves alisajiliwa kutoka Klabu kongwe ya Ujerumani Bayern Munich Julai 2007 kwa dau la Pauni Milioni 17 na amemudu kuanza mechi 25 tu hapo Man U.
Hargreaves mara ya mwisho aliichezea Man U Septemba 21, 2008 ilipotoka sare 1-1 na Chelsea huko Stamford Bridge kwenye mechi ya LIGI KUU na mwezi Novemba akapelekwa Marekani kufanyiwa operesheni ya goti lake la kulia kwa Mpasuaji stadi Daktari Richard Steadman na Januari akafanyiwa tena operesheni goti jingine la kushoto.
Daktari Steadman ameshawapasua kwa mafanikio makubwa sana Mastaa mbalimbali duniani akiwemo Mcheza Gofu maarufu Tiger Woods, Wanasoka Michael Owen, Alan Shearer na Ruud van Nistelrooy.
Tarehe 27 Mei 2009 kabla ya kuanza Fainali ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE huko Roma, Italia kati ya Manchester United na Barcelona, Owen Hargreaves alionekana akipiga danadana mpira huku Wachezaji wa Man U wakipasha moto.
Birmingham yamchukua Benitez
Timu mpya kwenye LIGI KUU England msimu ujao Birmingham City imevunja rekodi yao ya dau la uhamisho kwa kumsajili Mshambuliaji kutoka Ecuador Christian Benitez kutoka Klabu ya Mexico Santos Laguna.
Ingawa ada ya uhamisho haikutajwa lakini inaaminika ni zaidi ya Pauni Milioni 6.25 Klabu hiyo ililipa kumchukua Emile Heskey mwaka 2004 na hizo zikiwa ni fedha nyingi sana kwa wao kulipa kwa Mchezaji yeyote.
Benitez, 23, alifunga magoli 31 katika mechi za Ligi huko Mexico na ni Mtoto wa aliewahi kuwa Mfungaji Bora wa Nchi ya Ecuador, Ermen Benitez.
Christian Benitez alicheza Kombe la Dunia akiwakilisha Ecuador mwaka 2006 huko Ujerumani.

Nani aupinga uvumi kuwa Man U watambwaga!!!
Winga kutoka Ureno, Nani, anaechezea Manchester United amepuuza uvumi uliotapakaa kuwa Klabu yake inafikiria kumuuza kabla msimu mpya haujaanza.
Nani alijiunga kutoka Sporting Lisbon mwaka 2007 kwa ada ya Pauni Milioni 17 lakini hana namba ya kudumu Kikosini mwa Man U na mwenyewe amezipinga tetesi hizo kwa kutamka: ‘Maisha yangu ya baadae ni Man U! Nimetwaa Mataji mawili sasa na ni fahari kubwa kuwa na Klabu kubwa kama hii! Siondoki na wala siendi kokote kwa mkopo! Ntamaliza mkataba wangu hapa!’
MDHAMINI MPYA KWENYE JEZI ZA MAN U ATOA DAU LITAKALOWEKA REKODI YA DUNIA !!!
Manchester United wamepata Mdhamini mpya badala ya AIG, Kampuni ya Bima ya Kimarekani iliyodhoofika mno kutokana na mporomoko wa soko la dunia, ambayo jina lake lipo kifuani mwa jezi za Man U.
Mkataba wa Man U na AIG utamalizika Juni 2010 na AIG ilishatamka mapema hawatuongeza tena mkataba kwa sababu hali yao ni mbaya kiuchumi. AIG walikuwa wakiilipa Man U Pauni Milioni 14 kwa mwaka kwa kuweka jina la AIG kifuani mwa jezi.
Sasa Manchester United wamekubaliani na Kampuni kubwa ya huko Chicago, Marekani iitwayo Aon inayoshughulika na Mambo ya Fedha na Aon watawalipa Man U Pauni Milioni 20 kwa mwaka kwa mkataba wa miaka minne na hili ni dau kubwa kabisa kwa Klabu yeyote duniani kulipwa na Mdhamini.
Wadhamini wakubwa wanaozilipa Klabu kubwa duniani kwa majina yao kuonekana kwenye jezi ni:
-Bayern Munich - £17 Milioni kwa mwaka na T-Home, Kampuni ya Mawasiliano ya Simu.
-Real Madrid - £15 Milioni kwa mwaka na Kampuni ya Austria ya Kamari Bwin.com.
-Juventus - £15m kwa mwaka na Kampuni ya Libya ya mafuta Tamoil.
-Chelsea - £10 kwa mwaka na Kampuni ya Elektroniki ya Korea Samsung.
-Liverpool - £8m kwa mwaka na Kampuni ya Bia Carlsberg.
-Manchester City - £8 kwa mwaka na Kampuni ya Ndege ya huko Falme ya Nchi za Kiarabu Etihad Airways.

Tuesday 2 June 2009

NI RASMI: MAN CITY WAMCHUKUA NAHODHA WA VILLA BARRY!!!
Manchester City wamemnunua Kiungo na Nahodha wa Aston Villa, Gareth Barry [28], kwa kitita cha Pauni Milioni 12 na amesaini mkataba wa miaka mitano.
Barry, ambae amechezea England mechi 29, msimu uliokwisha alibakia kidogo tu kuhamia Liverpool lakini kukawa na mvutano kuhusu dau la uhamisho na dili ikavunjika.
Wamiliki wa Manchester City, Abu Dhabi United Group, mali ya Koo ya Kifalme ya Abu Dhabi ambao ni sehemu ya Nchi Tajiri sana ya Falme ya Nchi za Kiarabu, inaaminika watamwaga ‘vijisenti’ kipindi hiki ili kupata Wachezaji wengi ili kuimarisha Timu yao. Barry, ameichezea Villa jumla ya mechi 443 tangu mwaka 1997, kwa sasa yuko kambini na Timu ya Taifa ya England inayojitayarisha kwa mechi za mchujo wa kuwania kucheza Fainali Kombe la Dunia huko Afrika Kusini 2010 watakapocheza na Kazakhstan Jumamosi na Andorra siku nne baadae
RIO NJE ENGLAND!!!
Beki wa Manchester United, Rio Ferdinand, ametolewa kwenye Kikosi cha England kinachokwenda kucheza na Kazakhstan siku ya Jumamosi katika mechi ya mchujo wa kugombea kuingia Fainali Kombe la Dunia mwaka 2010 huko Afrika Kusini baada ya kusumbuliwa na misuli ya mguu.
Nafasi yake amepewa Beki wa Bolton, Gary Cahill, ambae huchezea Timu ya Taifa ya England ya Vijana wa chini ya miaka 21.
Hata hivyo, habari toka kambini kwa England zimesema Rio Ferdinand kama atapata afueni huenda akacheza mechi ijayo ya Kombe la Dunia itakayochezwa Jumatano ijayo na Andorra Uwanjani Wembley, London.

Huyu ni Mchezaji wa pili wa Manchester United kutoka kwenye Kikosi cha England baada ya Michael Carrick ambae nae ni majeruhi.
Haya kumekucha........mara baada ya kuukwaa Uraisi Real, Perez kishawavamia Alonso na Ronaldo!!!!
Kama ilivyotabiriwa na hata haijapita hata siku moja, Rais mpya wa Real Madrid, Florentino Perez, ameshaanza kubwabwaja na kudai Cristiano Ronaldo wa Manchester United na Xabi Alonso wa Liverpool [pichani]wanawavutia sana na ni Wachezaji wanaofaa Real Madrid.
Ingawa Perez hajatamka na kuweka bayana kama Real Madrid watatoa ofa rasmi kwa Klabu husika za Ronaldo na Alonso lakini kauli zake zinadokeza nia wanayo.
Perez alitamka: ‘Kuna dili nyingine zinachukua siku chache, nyingine miezi! Lakini tuna muda hadi Agosti 31.’
Agosti 31 ndio siku ya mwisho dirisha la uhamisho Wachezaji kufungwa.
Blackburn Rovers wamsaini Mchezaji kutoka Bondeni!!!!!
Elrio van Heerden, Mchezaji wa Kimataifa wa Afrika Kusini, anaechezea Klabu ya Ubelgiji ya Club Brugge ambako alikaa kwa miaka mitatu amesaini mkataba wa miaka miwili na Klabu ya Blackburn Rovers inayocheza LIGI KUU England.
Heerden, 25, alikuwa kambini na Timu ya Afrika Kusini inayojitayarisha kwa Kombe la Mabara lakini akaruhusiwa kwenda England kusaini mkataba na huyu ndie Mchezaji wa kwanza kwa Meneja wa Blackburn Rovers Sam Allardyce kumsajili majira haya ya joto ambako Timu za LIGI KUU zinasubiri msimu kuanza upya mwezi wa Agosti.
Heerden atajumuika na Mchezaji mwingine kutoka Afrika Kusini, Benni McCarthy, hapo Ewood Park lakini Mchezaji mwingine wa Afrika Kusini aliekuwepo hapo Blackburn Rovers Aaaron Mokoena amehama hivi karibuni kwenda Portsmouth
Nahodha wa Villa Barry afanya mazungumzo na Man City!!
Kiungo na Nahodha wa Aston Villa, Gareth Barry, amepewa baraka na Klabu yake kuongea na Manchester City ili kufikia muafaka ahamie Man City.
Barry, 28, msimu uliokwisha alibakia kidogo kuhamia Liverpool lakini kukawa na mvutano kuhusu dau la uhamisho na dili ikavunjika.
Ingawa Villa imefanikiwa kuingia na kucheza Ulaya msimu ujao ambako watacheza kwenye Mashindano mapya yatakayojulikana kama UEFA EUROPA LEAGUE na Man City hawachezi Ulaya kwa kumaliza nafasi duni kwenye LIGI KUU, inaaminika mvuto pekee unaomfanya Barry kuhama Villa Klabu aliyoichezea tangu 1997 ni dau kubwa huko Man City.
Barry, ambae ameichezea Villa jumla ya mechi 443, kwa sasa yuko kambini na Timu ya Taifa ya England inayojitayarisha kwa mechi za mchujo wa kuwania kucheza Fainali Kombe la Dunia huko Afrika Kusini 2010 watakapocheza na Kazakhstan Jumamosi na Andorra siku nne baadae.

Perez kuapishwa Rais wa Real Madrid leo, Pellegrini ateuliwa Kocha!
Florentino Perez leo ataapishwa kama Rais mpya wa Klabu ya Spain Real Madrid na sasa dunia isubiri tu ngonjera za kuchukuliwa Christiano Ronaldo, Cesc Fabregas, Xavi Alonso na Mastaa kadhaa kwenda huko Spain.
Florentino Perez, miaka 62, ni tajiri mwenye shughuli za Ujenzi, na aliwahi kuwa Rais wa Real kati ya mwaka 2000 na 2006 na katika kipindi hicho aliweza kuwasajili Zinedine Zidane, Ronaldo, Luis Figo and David Beckham. Vilevile, alimudu kutwaa La Liga mara 2, UEFA CHAMPIONS LEAGUE mara moja na Real kubatizwa jina la ‘Galacticos!’
Mara tu baada ya kutangazwa Perez Rais, Real Madrid ikatoa tamko rasmi kuwa aliekuwa Bosi wa Villareal Manuel Pellegrini [pichani], anaetoka Chile, ndie Kocha mpya.
Pellegrini, 55, atakuwa Meneja wa 8 kwa Real Madrid katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Fabregas ataka Alonso asainiwe Arsenal!!
Nahodha wa Arsenal, Cesc Fabregas, ameitaka Klabu yake Arsenal imsajili Kiungo wa Liverpool Xabi Alonso ambaye ni Mhispania mwenzake.
Fabregas amesema: ‘Tumepoteza Wachezaji wakubwa na Meneja anajua hilo. Lakini tunaweza kusaini Wachezaji wakubwa! Tunahitaji mtu kwenye Kiungo atakaeleta ushindani na kutupa mwelekeo mwingine! Alonso ni bora na anafunga magoli!’

Monday 1 June 2009

KOMBE LA DUNIA AFRIKA KUSINI 2010
MECHI ZA MCHUJO MAKUNDI YA NCHI ZA ULAYA
Jumamosi, 6 Juni 2009
Albania v Portugal,
Azerbaijan v Wales,
Belarus v Andorra,
Bulgaria v Rep of Ireland,
Croatia v Ukraine,
Cyprus v Montenegro,
Finland v Liechtenstein,
FYR Macedonia v Norway,
Iceland v Netherlands,
Kazakhstan v England,
Lithuania v Romania,
Serbia v Austria,
Slovakia v San Marino,
Sweden v Denmark,
Jumatano, 10 Juni 2009
England v Andorra,
Faroe Islands v Serbia,
Finland v Russia,
FYR Macedonia v Iceland,
Netherlands v Norway,
Sweden v Malta,
Ukraine v Kazakhstan,
MECHI ZA MCHUJO MAKUNDI YA NCHI ZA MAREKANI YA KUSINI
Jumamosi, 6 Juni 2009
Uruguay v Brazil
Bolivia v Venezuela
Argentina v Colombia
Paraguay v Chile
Peru v Ecuador
Jumapili, 7 Juni 2009
Peru v Ecuador
Jumatano, 10 Juni 2009
Ecuador v Argentina
Colombia v Peru
Venezuela v Uruguay
Chile v Bolivia
Brazil v Paraguay
ANCELOTTI BOSI MPYA CHELSEA!!!
Klabu ya Chelsea imemwajiri Mtaliana Carlo Ancelotti [49] kuwa Meneja mpya wa Klabu hiyo na amepewa mkataba wa miaka mitatu.
Jana Ancelotti aliiwezesha Klabu yake AC Milan kushika nafasi ya 3 kwenye Ligi ya Serie A huko Italia na hivyo kuweza kucheza UEFA CHAMPIONS LEAGUE msimu ujao na mara baada ya mechi ya jana kumalizika akatangaza kuachia ngazi AC Milan.
Ancelotti sasa ni Meneja wa 5 hapo Chelsea katika kipindi cha miezi 21 iliyopita na waliomtangulia ni Claudio Ranieri, Jose Mourinho, Avram Grant, Luis Filipe Scolari na Guus Hiddink.
Carlo Ancelotti ataanza rasmi kazi yake Julai 1.

UEFA yatangaza majaribio ya Waamuzi Watano kwenye mechi!!!

UEFA, Chama cha Soka cha Ulaya, kimetangaza kuwa msimu ujao kwenye Mashindano mapya ya UEFA EUROPA LEAGUE ambayo yalikuwa yakiitwa UEFA CUP majaribio ya kuwa na Waamuzi watano kwenye mechi moja yatafanyika.
Mbali ya Refa na Wasaidizi wake wawili Washika Vibendera wanaokaa pembeni mwa Uwanja kutakuwa na Wasaidizi wengine wawili wa ziada watakaokaa nyuma ya goli kila mmoja.
Waamuzi hawa watano watakuwa wakiwasiliana kwa kutumia redio.
Majaribio ya Waamuzi watano yalifanyika kwenye mechi za Nchi za Ulaya ya Vijana wa chini ya miaka 19 yaliyozikutanisha Nchi za Slovenia, Cyprus na Hungary na UEFA kuridhika na mafanikio yake na sasa wanataka kuyapeleka ngazi ya juu zaidi.

Sunday 31 May 2009

MMILIKI NEWCASTLE ATAKA KUTIMKA!!

Mike Ashley anaemiliki Klabu ya Newcastle amesema anatafuta mnunuzi wa Klabu hiyo mapema iwezekanavywo. Ashley hivi juzi aliwaomba radhi Mashabiki kwa makosa yaliyofanyika Misimu miwili iliyopita mpaka yakasababisha timu kuporomoka Daraja. Ashley amekiri: 'Ni balaa kubwa kwa kila mtu! Nimepoteza pesa zangu na nilifanya maamuzi mabovu! Sasa nataka kuiuza Klabu na Washauri watateuliwa hivi karibuni!'
Mike Ashley amekiri ilikuwa ni kosa kubwa kwake aliponunua asilimia mia ya hisa za Klabu hiyo. Ashley anasema: 'Hilo ni kosa! Najuta kwa sababu mie sie mtaalam wa soka! Mie ni Shabiki tajiri tu!'

HIDDINK ABEBA FA CUP NA KUIAGA CHELSEA!!
Guus Hiddink, Mdachi aliyeletwa na Roman Abramovich ili kuiokoa Chelsea Februari mwaka huu baada ya kufukuzwa Kocha wa Dunia, Mbrazil, Luis Felipe Scolari, ametimiza ahadi yake na kuibebesha Chelsea Kombe la FA.
Hiddink amekubali: 'Hili ni Kombe muhimu na ni historia kuchukua! Nimefanya kazi na watu wema! Wachezaji wazuri kabisa!'
Nahodha wa Chelsea, John Terry, akaungama: 'Ni miaka miwili hatuna Kombe! Timu nzima tumempa zawadi! Tumewaona Man U wanachukua Vikombe kaja yeye tumepata!'
Frank Lampard akamalizia kwa kutoa kauli ya wenzake kwamba: GUS HIDDINK ni MTU MKUBWA, MTUKUFU NA KOMBE HILI ANASTAHILI YEYE!!
Powered By Blogger