Saturday 30 May 2009

KOMBE LA UJERUMANI: Werder Bremen 1 Bayer Leverkusen 0!!!!
Werder Bremen hatimaye wamemaliza msimu wao kwa kishindo kikubwa pale walipolibeba Kombe la Klabu huko Ujerumani baada ya kuwafunga Bayer 04 Leverkusen bao 1-0.
Werder Bremen hivi karibuni walivunjwa mioyo walipofungwa kwenye Fainali ya Kombe la UEFA na Klabu ya Ukraine Shakhtar Donetsk kwa bao 2-1 Fainali hiyo ikiwa ya mwisho kushindaniwa kwa jina la UEFA CUP.
Bao la ushindi la Werder Bremen lilifungwa na Mesut Ozil kwenye dakika ya 58.
Ni furaha kubwa kwa Werder Bremen kwa sababu pia nafasi waliyomalizia Bundesliga isingewaruhusu kucheza Ulaya kama wasingeshinda Kombe hilo.
Msimu ujao kuna mfumo mpya na jina jipya ambalo ni UEFA EUROPA LEAGUE na kwa kuwa wametwaa Kombe hilo la Ujerumani wataingizwa kwenye hiyo UEFA EUROPA LEAGUE.
Juninho aondoka Lyon kwa machozi!!

Kiungo wa zamani wa Brazil, Juninho Pernambucano, ataondoka Klabu ya Lyon baada ya msimu huu kumalizika leo baada ya kukaa Klabu hiyo ya Ufaransa tangu 2001 na kuwasaidia kuchukua Ubingwa mara 7.
Mwenyekiti wa Lyon, Jean-Michel Aulas, amesema ingawa mkataba wa Juninho, mwenye umri wa miaka 34, utaisha msimu ujao lakini kwa yale yote aliyoifanyia Lyon wameamua kumruhusu aondoke mapema kama ‘mtu huru’.
Aulas alitamka: ‘Juninho anaondoka!’
Kauli hiyo ya Mwenyekiti ilimfanya Juninho alieketi pembeni yake kububujikwa machozi.
Juninho aliifungia Lyon goli lake la 100 Jumamosi iliyopita walipoifunga Caen 3-1.
Juninho aliichezea Brazil mechi 44 na kufunga goli 7.
SCOTLAND: Baada ya Ubingwa, leo Rangers wabeba Kombe la Scotland!!
Rangers leo wamelibeba Kombe la Scotland walipowafunga Falkirk katika Fainali iliyochezwa Hampden Park na hivyo kufanikiwa kuchukua Vikombe viwili msimu huu baada ya wiki iliyopita kushinda Ubingwa wa Scotland uliokuwa ukishikiliwa na Mahasimu wao wakubwa Celtic.
Bao la ushindi la Rangers lilipachikwa na Mchezaji Nacho Novo alieingia kama Mchezaji wa Akiba na dakika moja tu baada ya kipindi cha pili kuanza akafunga goli hilo kwa shuti la juu la mbali sana.
Chelsea wachukua FA CUP: Chelsea 2 Everton 1
Licha ya kufunga goli mapema mno na kuvunja ile rekodi ya Fainali ya FA Cup iliyowekwa mwaka 1895 na Mchezaji wa Aston Villa Bob Chatt aliefunga sekunde 30 tangu mechi ianze, Luis Saha aliifungia Everton bao sekunde 25 tu tangu mechi ianze lakini Chelsea waliibuka na kuitawala Fainali hii ya Kombe la FA na mwishowe kuwa washindi wa bao 2-1.
Rekodi nyingine iliyowekwa leo ni ile ya Ashley Cole kuweza kushinda Kombe la FA mara 5 na kuwapita Ryan Giggs, Roy Keane, Mark Hughes, David Seaman na Ray Parlour wote waliochukua Kombe hilo mara 4.
Wengine walioweza kushinda Kombe hili la FA mara 5 ni Charles Wollaston, Arthur Kinnaird na Jimmy Forrest lakini hawa wote waliweka rekodi hii Karne ya 19!!!
Ashley Cole alishinda Kombe lake la kwanza akiwa na Arsenal walipowafunga Chelsea 2002 na kulitetea tena dhidi ya Southampton msimu uliofuata. Mwaka 2005 alishinda tena kwa matuta dhidi ya Manchester United na akahamia Chelsea na kuwafunga Man U 1-0 na leo ni kichwa cha Everton.
Chelsea walisawazisha bao lao kupitia Didier Drogba dakika ya 20 na mpaka mapumziko gemu ilikuwa 1-1.
Ndipo Frank Lampard alipoachia mkwaju nje ya boksi dakika ya 71 na kuwapa Chelsea Kombe la FA.
VIKOSI:
Chelsea: Cech, Bosingwa, Alex, Terry, Ashley Cole, Essien, Mikel, Lampard, Anelka, Drogba, Malouda. Akiba: Hilario, Ivanovic, Di Santo, Ballack, Kalou, Belletti, Mancienne.

Everton: Howard, Hibbert, Yobo, Lescott, Baines, Osman, Neville, Pienaar, Cahill, Fellaini, Saha. Akiba: Nash, Castillo, Vaughan, Jacobsen, Rodwell, Gosling, Baxter.

VETERANI NA SUPASTAA WA URENO FIGO KUSTAAFU SOKA KESHO!!!
Kiungo Luis Figo ametangaza rasmi kustaafu Soka kesho wakati Klabu yake Inter Milan, ambao ndio Mabingwa wa Italia, itakapokuwa nyumbani San Siro kucheza na Atalanta katika mechi ya mwisho ya msimu wa Serie A huku tayari Inter Milan washauchukua Ubingwa.
Figo alijiunga na Inter Milan mwaka 2005 na ameisaidia Klabu hiyo kunyakua Ubingwa wa Italia kwa mara 4 mfululizo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 ambae mwaka 2001 ndie alikuwa Mchezaji Bora Duniani alijitengenezea jina lake alipozichezea Barcelona na Real Madrid za Spain.
Figo alihama Barcelona na kwenda Real Madrid mwaka 2000 na mwaka 2002 alichukua Klabu Bingwa Ulaya akiwa na Real.
Katika mechi yake ya kwanza kurudi uwanjani Nou Camp akiichezea Real Madrid tangu ahame Barcelona, Mashabiki wa Barcelona walimrushia kichwa cha nguruwe.
Figo ndie Mchezaji anaeshikilia rekodi ya kuchezea Timu ya Taifa ya Ureno mechi nyingi kwa kucheza mechi 127 na kufunga magoli 32.
ATHARI NA HATARI YA ARSENAL KUSHIKA NAFASI YA 4 LIGI KUU!!!
Kwa kumaliza katika nafasi ya 4 katika msimamo wa LIGI KUU England, Arsenal wamefanikiwa kupata nafasi ya kucheza UEFA CHAMPIONS LEAGUE msimu ujao pamoja na Bingwa Manchester United, Mshindi wa pili Liverpool na Chelsea alieshika nafasi ya 3.
Lakini, wakati Manchester United, Liverpool na Chelsea wataingia kwenye hatua ya Makundi ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE, Arsenal inabidi aanze kwenye hatua ya Mtoano.
Katika misimu mitatu iliyopita, Arsenal ilimudu kukipita kikwazo hiki cha kucheza hatua ya Mtoano na kuingia hatua ya Makundi kwa kufaulu katika mechi za nyumbani na ugenini dhidi ya FC Twente, Sparta Prague na Dynamo Zagreb.
Lakini msimu ujao kuna hatari kubwa ya Arsenal kuteleza kwani UEFA wameubadilisha mfumo wa nani unaweza kukutana nae kwenye hatua hiyo ya awali ya Mtoano. Mfumo huu mpya unatoa uwezo mkubwa Arsenal kukutanishwa na Timu ‘kigogo’ ambayo kama Arsenal ilimaliza ligi ya kwao nafasi ya chini kidogo.
Mfumo huu, ulioshabikiwa sana na Rais wa UEFA, Michel Platini, una lengo la kuzisaidia zile Nchi ‘ndogo’ na ‘hafifu’ huko Ulaya ili ziweze kuingia hatua ya Makundi.
Mfumo huu mpya unaifanya Arsenal kuingizwa kwenya kapu moja pamoja na Timu zilizomaliza nafasi ya 4 huko Italy na Spain pamoja na Timu zilizomaliza nafasi ya 3 huko Ujerumani na Ufaransa. Hizi ni Nchi 5 zilizopewa upendeleo maalum wa kutoanza hatua ya awali kabisa ya Mtoano.
Timu zitakazoanza hatua ya awali kabisa ya Mtoano ni zile Timu zinazotoka Nchi 10 zilizoshika nafasi ya 2 kutoka Ureno, Uholanzi, Scotland, Turkey, Ukraine, Belgium, Greece, Czech Republic, na Romania pamoja na Timu ya 3 kutoka Urusi na zitapigiwa dro maalum ili kuzigawa katika mechi 5 zitakazochezwa nyumbani na ugenini kupata Washindi watano.
Washindi watano kutoka kundi la Nchi hizo 10 watajumuika na lile la kundi la Arsenal [yaani Timu kutoka England, Italy, Spain, Ujerumani na Ufaransa] kufanya jumla ya Timu 10 ambazo zitagawanywa Timu Bora 5 kapu moja na Timu ‘sio bora’ kapu jingine na itapigwa kura kupata nani kutoka Kapu Bora anacheza na Timu ipi kutoka Kapu la pili kwa mtindo wa nyumbani na ugenini na Washindi hao watano wataingizwa kwenye hatua ya Makundi.
Ingawa Arsenal, kufuatia rekodi yake nzuri ya miaka ya hivi karibuni kwenye Mashindano ya UEFA, ana hakika ya kuwekwa Kapu la Timu Bora lakini hata hizo Timu zitazokuwa Kapu la pili hazitakuwa Timu dhaifu na hii ndio athari na hatari kubwa inayoweza kumkuta Arsenal kwa kumaliza nafasi ya 4 kwenye
LIGI KUU England.
Makelele atoboa: ‘Ugomvi kati ya John Terry na Mourinho ulisababisha Mourinho atimuliwe Chelsea!!!’
Kiungo wa zamani wa Chelsea, Claude Makelele [36], amepasua kwenye Kitabu cha Maisha yake kilichochapishwa wiki hii na kuanza kuuzwa leo huko Ufaransa kuwa ugomvi kati ya aliekuwa Meneja wa Chelsea Jose Mourinho na Nahodha wa Chelsea, John Terry, ndio ulisababisha Mmiliki wa Chelsea, Mrusi Roman Abramovich amtimue Mourinho Septemba, 2007.
Claude Makelele, ambae alizaliwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kuhamia Ufaransa mwaka 1977, alikuwa pia Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Ufaransa, ameandika kwenye Kitabu chake kiitwacho ‘Tout Simplement’ kuwa baada ya John Terry kuwa anaumia mara kwa mara Jose Mourinho akaamua kumpumzisha kucheza na ndipo ugomvi mkubwa ukazuka kati yao.
Klabu ya Chelsea pamoja na John Terry mwenyewe wamekanusha taarifa hizo za kwenye Kitabu cha Claude Makelele kwa madai kuwa ukweli umepotoshwa.
Makelele anazungumzia kwenye Kitabu kwa kusema: ‘Nilipata habari za Mourinho kutoka kwa Drogba. Aliniambia kesho atafukuzwa! Nilishangaa sana! Nilidhani Mourinho hagusiki! Siku ya pili tukiwa Cobham, kwenye Uwanja wetu wa mazoezi, ilikuwa ni vurugu! Mapaparazi walijaa kila kona na hata helikopta zilikuwa zinaruka juu ya vichwa vyetu!’
Makelele anaendelea kwenye kitabu chake: ‘Wachezaji wengi walikuwa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo na nikakutana na Rui Faria, alikuwa ni Mkufunzi wetu wa Mazoezi ya Viungo nikamuuliza kuna nini? Akanijibu Kocha kafukuzwa! Nikamuuliza kwa nni na akasema Wachezaji wengi, akiwemo Terry, wamelalamika kwa Mmiliki kuhusu Mourinho!’
‘Ndio nikagundua, Mourinho alimwambia Terry.....’Makelele anaandika kitabuni. ‘......atabaki benchi kwa mechi kadhaa ili apone vizuri mgongo aliofanyiwa operesheni msimu uliopita kwani tangu wakati huo umekuwa ukimsumbua mara kwa mara. Terry akabisha na kusema yuko fiti. Mourinho akagoma kumchezesha na kumwambia kuanzia siku hiyo Walinzi wa Kati wa Chelsea watakuwa Ricardo Carvalho na Alex! Hapo ndipo ilipotangazwa vita rasmi!’
Makelele anaendelea: ‘Kwa Terry huo ulikuwa usaliti!! Msimu uliokwisha alichezea Klabu huku akiwa na maumivu makali! Terry alitegemea Mourinho angemwona anastahili kila nafasi ya kucheza kwa ushujaa wake. Mourinho alikuwa amechokoza vita mbaya sana! Ingekuwa Mchezaji wenyewe ni mimi au Ballack au Shevchenko hayo yangeisha!! Lakini ni Terry na huyo humgusi Chelsea!’
‘Terry akaenda kwa Mkurugenzi Mtendaji Peter Kenyon na kuomba uhamisho!.’ Makelele amezidi kuelezea kitabuni. ‘Abramovich akashtuka na kuchukua hatua haraka! Alijua Mashabiki na Wachezaji hawawezi kukubali John Terry aondoke! Badala yake Mourinho akaambiwa afungashe virago vyake!!!’
Jose Mourinho aliajiriwa Chelsea Juni 2004 na kufukuzwa tarehe 20 Septemba 2007. Katika kipindi hicho alichokuwa Chelsea aliweza kuchukua Ubingwa wa LIGI KUU England mara 2, Vikombe vya Carling mara 2 na FA Cup moja. Kwa sasa Mourinho ni Meneja wa Inter Milan kwa msimu mmoja sasa na juzi tu amefanikiwa kutwaa Ubingwa wa SERIE A ya Italia.
Kwa sasa Claude Makelele ni Mchezaji wa Klabu ya Ufaransa Paris St Germain.
FAINALI: Chelsea v Everton!!!!

Ni Fainali kati ya Meneja Guus Hiddink v Meneja David Moyes!!!

Ni Fainali ya Kombe Kongwe Duniani, Kombe la FA, na hii ni Fainali ya 128 katika historia yake na inazikutanisha Timu mbili zenye Mameneja wenye tofauti kubwa kati yao.
Mameneja hao, Guus Hiddink wa Chelsea na David Moyes wa Everton, leo Uwanjani Wembley, jijini London wataziongoza Timu zao kwenye kimbembe hicho.
Ni watu wawili, ingawa wote ni Mameneja wa Klabu za mpira, walio tofauti kabisa ukichukulia staili zao, uzoefu wao, mbinu zao na hata rasilimali zilizopo kwenye Klabu zao!
Guus Hiddink:
Mafanikio yake: PSV EINDHOVEN [Ubingwa mara 6, Vikombe vingine mara 4, Kombe la Ulaya mara 1] REAL MADRID [Kombe la Mabara (Ubingwa wa Dunia) mara 1]
Guus Hiidink ni Mholanzi anaeamini Soka la Kiholanzi la kupasiana na kucheza kitimu. Yeye ni Balozi mzuri wa Soka Duniani kwani ameshafanya kazi yake pembe nyingi za Dunia.
Ameshafundisha kwao Uholanzi, Spain, Uturuki, Korea ya Kusini, Urusi [ambayo bado ndie Mwajiri wake wa kudumu], Australia na sasa England.
Baada ya mechi ya leo inaaminika Guus Hiddink ataiacha Chelsea na kurudi kwenye kazi yake ya kudumu kama Meneja wa Timu ya Taifa ya Urusi.
Ingawa anaondoka Chelsea, Mashabiki wengi wa Timu hiyo wametokea kumpenda sana kwa jinsi ya ubora wa kazi yake, ucheshi na utu wake. Katika mechi 21 chini yake, Chelsea imefungwa mechi moja tu!
David Moyes, Meneja wa Everton kuanzia 2002:
Mafaniko yake: PRESTON NORTH END [Iliyokuwa Daraja la 2 sasa linaitwa LIGI WANI, Mabingwa 1999-2000] EVERTON [Hajashinda Kombe lolote ila yeye binafsi amepewa Tuzo ya Meneja Bora wa LIGI KUU kwa miaka mitatu mfululizo hadi sasa]
Tangu ajiunge Everton mwaka 2002, hajashinda Kikombe chochote lakini amefanikiwa kuiinua Klabu isiyo na utajiri mkubwa na kuiwezesha kuwa miongoni mwa Klabu 6 Bora za LIGI KUU.
Kwa mafaniko hayo, ndio maana Mameneja wenzake kwenye Chama chao cha Mameneja [LMA=League Managers Association] kimemtunuku Tuzo ya Meneja Bora kwa misimu mitatu mfululizo sasa.
Msimu huu, David Moyes ameiwezesha Everton kutoka sare ya 0-0 na Chelsea katika mechi zote mbili za LIGI KUU England na pia kuifanya Everton ishike nafasi ya 5 kwenye ligi hiyo na hivyo kucheza Ulaya kwenye Mashindano mapya msimu ujao yatakayoitwa UEFA EUROPA LEAGUE .
Paolo Maldini kustaafu kesho!!!!

Kesho kwenye mechi ya SERIE A huko Italia kati ya wenyeji ACF Fiorentina na AC Milan, Nahodha wa AC Milan Paolo Maldini mwenye umri wa miaka 40 ataingia uwanjani akiwa amevaa Jezi yake Namba 3 kwa mara ya mwisho kwa vile yeye mwenyewe, baada ya kucheza misimu 25, anastaafu na kwa heshima na kumtukuza yeye binafsi Klabu ya AC milan imeamua Jezi Namba 3 nayo istaafishwe.
Katika kipindi cha miaka 25, Nahodha Paolo Maldini ambae pia alichezea Timu ya Taifa ya Italia na kuwa Nahodha pia, amefaulu kuchukua Vikombe 26 ikiwa pamoja na vile vya Klabu Bingwa Ulaya mara 5.
Ingawa kesho ni mechi yake ya mwisho, Paolo Maldini hataki kutoka uwanjani kwa kufungwa na Fiorentina kwani kufungwa kutamaanisha Fiorentina wanaipiku AC Milan na kutwaa nafasi ya 3 msimamo wa Ligi SERIE A na hivyo kucheza moja kwa moja hatua ya Makundi ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE msimu ujao.
Paolo Maldini, kama Baba yake mzazi Cesare Maldini, ndio Manahodha wa muda mrefu wa AC Milan na hata Baba yake aliwahi kulibeba Kombe la Klabu Bingwa Ulaya.
Mwenyewe Paolo Maldini anamsifia Nahodha wa AC Milan aliemrithi aliekuwa akiitwa Franco Baresi na kumsema huyo ndie alikuwa akimpa motisha kubwa sana.
Baresi ni mmoja wa Wachezaji wa Italia wenye jina kubwa na sifa kubwa.
Paolo Maldini anasema anakumbuka na kuyakumbuka matukio mawili na kuyaona ni bora maishani mwake ambayo ni pale mwaka 2003 katika Fainali ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE walipowabwaga Wapinzani wao wa Italia Juventus kwa matuta ya mabao 3-2 baada ya kutoka suluhu 0-0.
Lakini siku spesho moyoni mwake ni Mei 2001 walipowakung'uta Wapinzani wao wa Jadi FC Internazionale Milano, maarufu kama Inter Milan, mabao 6-0!!!
Paolo Maldini anasema: 'Hiyo ilikuwa spesho kwa Familia yangu!!! Baba yangu Mzazi ndie alikuwa akiongoza Benchi la AC Milan!!'
Kwa sasa Paolo Maldini anaishi kwa matumaini makubwa kuwa Mwanawe Christian Maldini anaechezea Timu ya Vijana ya AC Milan atafuata nyayo za Baba na Babu yake!!!
Pengine, hapo, ndipo Jezi Nambari 3 itatoka kwenye kustaafu na kurudi uwanjani!!!!
Steven Gerrard: 'Tukipata Wachezaji Wawili au Watatu tutawafikia Man U!!!!'
Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard, ametamka kuwa Liverpool ina upungufu wa Wachezaji Wawili au Watatu wazuri ili kufikia kiwango cha Mabingwa Manchester United.
Gerrard, alieiongoza Liverpool kushika nafasi ya pili LIGI KUU England na pia kufikia Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE msimu huu, anaamini Meneja wake Rafa Benitez ameweka mkakati wa kuziba upungufu huo.
Gerrard anasema: 'Nina hakika Rafa anashughulikia mapungufu! Ni muhimu kuziba kwani ukitazama Mabenchi ya Akiba ya Man U na Chelsea utashangaa kuona Wachezaji Mastaa na Bora sana hawachezi!'
Gerrard akaongeza: 'Tumecheza vyema msimu huu! Tumemaliza tukiwa na pointi 86 na mara nyingi pointi hizi zinakupa Ubingwa!! Lakini pongezi kubwa kwa Man U!!!!'
Republic of Ireland 1 Nigeria 1

Timu za Taifa za Republic of Ireland na Nigeria jana zilitoka suluhu ya bao 1-1 katika mechi ya kirafiki iliyochezwa Uwanja wa Klabu ya Fulham, Craven Cottage huko London.
Nigeria ndio walifunga kwanza kupitia Eneramo kwenye dakika ya 30 lakini Ireland wakasawazisha dakika ya 38 mfungaji akiwa Robbie Keane.
Timu zilikuwa: [Kwenye mabano ni Wachezaji wa Akiba walioingizwa na dakika ya mchezo]
Ireland: Shay Given [Keiren Westwood, 46], Kevin Foley [Paul McShane, 72], Richard Dunne, Sean St Ledger, Eddie Nolan, Damien Duff [Aiden McGeady, 46], Liam Miller, Keith Andrews [Glenn whela, 59], Liam Lawrence [Stephen Hunt, 81], Robbie Keane [Shane Long, 46], Leon Best.
Nigeria: Austin Ajide, Olubayo Adefemi, Sam Sodje [Obinna nWaneri, 78], Yusuf Mohamed, Seyi Olofinjana, Sone Alouko [Nsofor Victor Obinna, 60], Kalu Uche, Dele Adeteye, John Utaka, Joseph Akpala [Peter Osaze Odemwingie, 60], Mike Eneramo.
Scholes adokeza huenda akaenda Stoke City kuwa Kocha-Mchezaji!!!
Veterani na Kiungo maarufu wa Manchester United, Paul Scholes, miaka 34, amedokeza kuwa huenda akaenda Klabu ya Stoke City mkataba wake na Manchester United utakapoisha mwakani.
Scholes alianza kuchezea Manchestet United tangu akiwa mdogo.
Scholes anategemewa kumalizia masomo yake ya Ukocha majira ya sasa ya joto wakati msimu wa ligi umemalizika.
Scholes alianza kuchukua mafunzo ya Ukocha, kama ilivyo desturi ya Wachezaji wengi wakongwe wa Man U kama vile Ole Gunnar Solskjaer, Giggs na Neville, misimu kadhaa ya nyuma.
LEO FAINALI YA KOMBE LA UJERUMANI: Werder Bremen v Bayer 04 Leverkusen!!!

Ndani ya Uwanja uitwao Olympiastadion huko Munich, leo Werder Bremen na Bayer 04 Leverkusen zinapambana kwenye Fainali ya kugombea Kombe la Ujerumani linaloshindaniwa na Klabu za Ujerumani.
Werder Bremen ambao wiki moja iliyopita walibwagwa 2-1 kwenye Fainali ya UEFA CUP na Timu ya Ukraine Shakhtar Donetsk watataka kushinda Kombe hili ili kupata nafasi ya kucheza kwenye mashindano mapya ya Ulaya yatayoanza msimu ujao ambayo ndiyo yatachukua nafasi ya UEFA CUP.
Mashindano hayo yatajulikana kama UEFA EUROPA LEAGUE.
Kwa Bayer 04 Leverkusen hali ni kama ya Werder Bremen kwani wao walimaliza Bundesliga wakiwa nafasi ya 9 huku Werder Bremen nafasi ya 10 na nafasi pekee ya kuweza kucheza Ulaya ni kushinda Kombe hili la Ujerumani.
Kwa Wachezaji wawili wa Werder Bremen, Frank Baumann na Diego [pichani] hii ni nafasi yao ya mwisho kwani Baumann anastaafu na Diego, ambae ni Mbrazil, amenunuliwa na Juventus ya Italia.

Friday 29 May 2009

FAINALI: CHELSEA v EVERTON
Wembley Stadium, London Jumamosi 30 Mei 2009 saa 11 jioni [bongo taimu]
Timu za LIGI KUU England Chelsea na Everton zinakutana Fainali ya Kombe la FA hapo kesho Jumamosi 30 Mei 2009 uwanjani Wembley.
Mbali ya kunyakua Kombe hilo ambalo ndilo linalosemekana ni la zamani sana kuanzwa kushindaniwa kwenye soka Duniani kupita Kombe lolote lile, mshindi ataibuka na kitika cha fedha Pauni Milioni 2 taslimu na atakaeshindwa atapata Pauni Milioni moja.
Mara ya mwisho kwa Everton kucheza Fainali ilikuwa mwaka 1995 walipoifunga Manchester United 1-0 na kuchukua Kombe hilo.
Chelsea nao wa walicheza Fainali mara ya mwisho mwaka 2007 na pia kuifunga Manchester United 1-0 na kunyakua Kombe hilo.
Hii itakuwa ni Fainali ya 128 ya FA Cup na ni mara ya 75 kuchezewa Uwanja wa Wembley.
Msimu huu jumla ya mechi 925 zilichezwa kushindaniwa Kombe hili na jumla ya magoli 3035 yalifungwa. Mechi iliyotoa magoli mengi ni ile ya Mildenhall Town 8 Felixstowe & Walton United 0.
Fainali ya kesho ya Chelsea v Everton ni ya 20 kwa Timu hizi mbili na Chelsea amechukua Kombe mara 4 na Everton mara 5.
Mbele ya Mashabiki 90,000, Chelsea watashuka uwanjani wakiwa na jezi za njano mwili mzima na Everton watakuwa na uzi wao ule ule wa kawaida wa kibuluu, bukta nyeupe na stokingi nyeupe.
Chelsea msimu huu wamemaliza nafasi ya 3 na Everton nafasi ya 5 kwenye LIGI KUU.
Vikosi vinategemewa:
Chelsea [Mfumo, pengine 4-3-3]: Cech, Bosingwa, Alex, Terry, A. Cole, Essien, Mikel, Lampard, Malouda, Drogba, Anelka.
Everton [Mfumo, pengine 4-4-1-1]: Howard, Hibbert, Yobo, Lescott, Baines, Osman, Neville, Cahill, Pienaar, Fellaini, Saha.
Refa: Howard Webb
Mkataba wa Torres waboreshwa!!!
Mkataba wa Fernando Torres umeboreshwa na Klabu yake ya Liverpool na vilevile kuongezewa kipengele cha kuurefusha hadi msimu wa mwaka 2013/14.
Mshambuliaji huyu kutoka Spain alichukuliwa na Liverpool toka Atletico Madrid na mpaka sasa ameifungia Liverpool mabao 50.
Mpaka sasa Dirk Kuyt, Daniel Agger, Steven Gerrard na Meneja Rafa Benitez wamesaini mikataba mipya.
Dwight Yorke kumwagwa na Sunderland!!
Mkongwe Dwight Yorke ni miongoni mwa Wachezaji 7 ambao wataachwa na Klabu ya Sunderland ambayo inataka kujijenga upya baada ya kunusurika kushushwa Daraja.
Wengine ni david Connolly, Arnau Riera, Darren Ward, Nick Colgan, Peter Hartley na Niall McArdle.
Steven Ireland asaini mkataba mpya Man City
Kiungo wa Manchester City, Steven Ireland, amesaini mkataba mpya wa miaka mitano utakaomweka hapo hadi mwaka 2014.
Ireland ndie Mchezaji aling'ara sana Man City msimu huu.

Thursday 28 May 2009

MBINU HAZIKUWA NZURI-MAN U WAKUBALI!

Baada ya kuchapwa 2-0 na kupokonywa Kombe la Klabu Bingwa la Ulaya na Barcelona, Manchester United wamekekubali kabisa mbinu zao zilikuwa ovyo na Timu haikucheza kabisa kwenye kiwango kinachotakiwa. Meneja wao Sir Alex Ferguason alisema: 'Messi hakuwa tatizo! Xavi na Iniesta walimiliki mpira usiku mzima! Hatukucheza vizuri hata kidogo!' Ronaldo nae alikubali: 'Huu ndio mpira. Mnashinda ua kufungwa! Wao walicheza vizuri lakini sisi mbinu zetu hazikuwa nzuri!' Ferdinand: 'Lazima uwasifie Barcelona! Wamecheza vizuri sana!' Kipa Edwin van der Sar nae alisema: 'Lile goli la kwanza liliwapa imani na wakaanza kucheza mpira wao wa kawaida! Tumefungwa! Msimu ujao inabidi turudi upya na sisi tuna uwezo huo!'


Ferguson akiri: 'Tumefungwa na Timu Bora!!'
Sir Alex Ferguson amekubali Manchester United imefungwa na Timu bora na ametamka sisi tuna Timu changa na tutaanza upya.
Barcelona wameshinda Kombe la Klabu Bingwa Ulaya baada ya kuwapiga waliokuwa Mabingwa Watetezi wa Kombe hilo Manchester United bao 2-0.
Hata Rio Ferdinard amekiri kwamba Barcelona wamestahili kuwa Mabingwa kwa vile Man U hawakucheza vizuri.

Wednesday 27 May 2009

BIGI MECHI: Barcelona waunyaka Ubingwa!!!

Barcelona 2 Man U 0


Barcelona wamewabwaga Mabingwa Watetezi Manchester United kwa bao 2-0 na kulichukua Kombe la Klabu Bingwa Ulaya.


Mabao ya Barcelona yalifungwa na Samuel Eto'o dakika ya 10 na la pili alifunga Lionel Messi kipindi cha pili


Barcelona: Valdes, Puyol, Toure, Pique, Sylvinho, Busquets, Iniesta, Xavi, Messi, Eto'o, Henry. Akiba: Pinto, Caceres, Gudjohnsen, Krkic, Keita, Rodriguez, Muniesa.
Man Utd: Van der Sar, O'Shea, Vidic, Ferdinand, Evra, Carrick, Anderson, Giggs, Park, Ronaldo, Rooney. Akiba: Kuszczak, Berbatov, Nani, Scholes, Rafael, Evans, evez.


BIGI MECHI: MANCHESTER UNITED v BARCELONA
Leo, kuanzia saa tatu dakika arobaini na tano usiku bongo taimu, dunia nzima iko ndani ya Roma, Italia kwenye Stadio Olimpico kushuhudia Mabingwa Watetezi ambao pia ndio Mabingwa wa Dunia, Manchester United ya England, wakivaana na Mabingwa wa Spain, Barcelona, kugombea Kombe la Klabu Bingwa ya Ulaya linaloitwa UEFA CHAMPIONS LEAGUE CUP. Ni mechi inayowakutanisha Mameneja wawili wenye tofauti ya miaka 29 kati yao.
Pep Guardiola, Meneja wa Barcelona, ana umri wa miaka 38 na huu ndio msimu wake wa kwanza kuongoza katika soka.
Sir Alex Ferguson, Meneja wa Manchester United, ana miaka 67 na huu ni msimu wake wa 23 akiwa na Man U.
Wakati Pep Guardiola amewahi kulitwaa Kombe hili la Klabu Bingwa Ulaya alipokuwa Mchezaji wa Barcelona mwaka 1992, Sir Alex Ferguson leo anajaribu kulichukua kwa mara ya 3 akiwa kama Meneja wa Manchester United. Ferguson alitwaa Kombe hili mwaka 1999 huko Nou Camp, nyumbani kwa Barcelona, walipowafunga Bayern Munich bao 2-1 na mwaka jana huko Moscow, Urusi walipowabwaga Chelsea.
Ingawa Mameneja hawa wana tofauti kubwa kati yao, kitu kimoja kinachofanana kati yao ni ile falsafa yao ya jinsi ya kusakata soka. Wote ni waumini wa staili ya soka ya pasi za haraka, bila ya kudhoofisha defensi zao na kushambulia kwa haraka.
Ingawa kila Timu imesheheni Mastaa wenye vipaji vya kila aina vinavyosifika na kutambulika dunia nzima, wataalam kadhaa wametoa maoni yao na kubainisha kuwa mechi ya leo itakuwa na mvuto katika sehemu tatu zitakazohusu vita binafsi kati ya Wachezaji wa pande hizo mbili kama ifuatavywo:
-Rio Ferdinand v Samuel Eto'o
Ferdinand ana nguvu, spidi na ni mwepesi kuusoma mchezo na bila shaka atakabiliana vyema na kutakuwa na ushindani mkubwa kati yake na Samuel Eto'o ambae amefunga magoli 35 kwenye La Liga huko Spain.
-Lionel Messi v Patrice Evra
Barcelona sio timu inayotegemea Mchezaji mmoja lakini, bila shaka, Lionel Messi ni mmoja wa Wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu sana duniani. Kawaida, Barcelona humpanga Messi winga ya kulia ili awe anaingia ndani kwa kutumia mguu wake bora wa shoto na kupiga chenga au kubadilishana pasi fupi na wenzake. Itabidi Evra awe makini dakika zote 90 kama alivyofanya kwenye mechi za Nusu Fainali za msimu uliopita alipomudu kumzima Messi na Man U kuibuka washindi.
-Cristiano Ronaldo v Sylvinho
Barcelona wana pengo kubwa kwenye defensi baada ya kufungiwa Mafulubeki wao wote wawili Dani Alvez na Eric Abidal. Hivyo, pengine, itabidi achezeshwe Beki wa zamani wa Arsenal Sylvinho ambae ni wazi sasa jua linamchwea. Itakuwa si ajabu kwa Sir Alex Ferguson kumpanga Cristiano Ronaldo winga ya kushoto ili apate mwanya kwa Beki huyu 'mchovu.'
Vikosi:
Manchester United [Mfumo, pengine, 4-3-3]:
Van der Sar, O'Shea, Ferdinand, Vidic, Evra, Carrick, Giggs, Anderson, Park, Ronaldo, Rooney.
Barcelona [Mfumo, pengine, 4-1-4-1]:
Valdes, Puyol, Pique, Toure, Sylvinho, Busquets, Henry, Xavi, Iniesta, Messi, Eto'o
Refa: Massimo Busacca kutoka Switzerland
NANI KASEMA NINI?
Sir Alex Ferguson: 'Mara nyingi tumeona mechi doro zinazochezwa kwa timu kujihami mno! Soka siku zote linataka liwe la kuvutia. Manchester United na Barcelona wanaweza kucheza soka tamu na la kuvutia!! Kila timu ina wachezaji wenye vipaji sana!! Leo tunacheza na timu bora yenye historia kubwa sana!! Niliwaona ile mechi yao waliyowafunga Real Madrid 6-2 na nikasema 'Mungu wangu!! Tunacheza nao hawa!!' Lakini hawa wanafungika!!'
Pep Gurdiola: 'Hii ni siku muhimu sana katika maisha yangu ya uchezaji na na kama kocha! Tuna staili yetu ya kucheza lakini kuna staili nyingi za uchezaji!! Hivyo hatujioni ni bora! Itabidi tutilie mkazo mbinu zetu tu! Lakini kama tutashindwa kumudu 'miguvu' ya Manchester United basi tutazama!!'
Lionel Messi: 'Kama tukicheza kama tulivyocheza msimu wote basi tuna nafasi! Man U na sisi tunacheza staili moja, wote tunamiliki mpira! Lakini wao ni Mabingwa Watetezi hivyo wako mbele yetu!'
Rio Ferdinand: 'Tukijihami mno kwenye mechi hii ni hatari kwetu kwani wana vipaji vikubwa!! Tuna uwezo mkubwa wa kujilinda na kushambulia!! Ni ngumu kumdhibiti Messi, ni mchezaji mzuri sana lakini tushammudu kabla!!'
Jordi Cruyff [Mtoto wa Johan Cruyff na ambae alichezea timu zote mbili Man U na Barcelona]: 'Ferguson ni mbweha mjanja sana na lazima atawashangaza watu kwa upangaji timu na mfumo wake na kuwafunga Barca!! Nilipokuwa Old Trafford alikuwa akifanya maamuzi ya ajabu na yenye mafanikio makubwa!! Anaweza kumchezesha Mchezaji ambae hategemewi kabisa na kila mara uamuzi huo hufanikiwa!! Ni Mcheza kamari mahiri!!!'
Marcel Desailly: 'Kila Timu ina Wachezaji bora lakini Barca wako mbele kiduchu!! Kama wakiweza kusimama imara kwenye ngome watashinda!!'
Nahodha wa Chelsea, John Terry: 'Naweza kuwasha TV hafutaimu au mwisho wa mchezo kujua matokeo! Sitatizama mechi, ntawaogesha wanangu na kulala mapema!!!'
MWISHONI:
Shabiki aliyekubuhu wa Barcelona: 'MANCHESTER UNITED WANAWEZA KUSHINDA!!! LAKINI NI JUU YA DAMU, JASHO NA MACHOZI YA BARCELONA YOTE!!!'
Sir Alex Ferguson alipoambiwa Manchester United leo wanavaa jezi nyeupe tupu kama Real Madrid ili kuwakera Barcelona alicheka na kusema: 'Tunafurahia jezi hii lakini sisi ni bora sana kuliko Real Madrid!!!'
Anderson aahidi kukimbia uchi akifunga goli!!!
Chipukizi wa Brazil, Anderson, ameahidi atavua jezi na kukimbia uchi akifunga goli kwenye Fainali ya leo kati ya Klabu yake Manchester United na Barcelona itakayochezwa Stadio Olimpico kugombea UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
Anderson hajawahi kufunga bao kwenye mechi yeyote ya Manchester United na mpaka sasa ameshacheza mechi 73 tangu ajiunge kutoka FC Porto mwaka 2007.
Goli pekee alilofunga ni lile la penalti katika Fainali ya msimu uliopita ambayo Man U waliwabwaga Chelsea kwa mikwaju ya penalti tano tano na kutwaa Kombe la UEFA CHAMPIONS LEAGUE huko Moscow, Urusi.
Shabiki wa Man U achomwa kisu huko Roma!!! Wengine wawili wakamatwa!!!
Vibweka vya Fainali ya leo huko Roma, Italia kati ya Mabingwa Watetezi Manchester United na Barcelona vimeanza kupamba moto baada ya taarifa kupatikana kuwa Shabiki mmoja wa Man U, Greg Wheldon, 34, amechomwa visu mapajani na matakoni nje ya hoteli yake iliyo karibu na Vatican.

Genge la Wahuni wa huko Italia lijulikanalo kama 'Ultras' ndio wanaaminika wamefanya unyama huo kwani wana staili ya kuchoma watu visu mapajani na matakoni.
Shabiki huyo alipelekwa hospitali alfajiri ya leo na kuruhusiwa kutoka baadae na Msemaji wa Hospitali iliyomtibu amesema majeraha yake si ya ‘kutisha’.
Maelfu ya Mashabiki wa Manchester United wameivamia Roma kushuhudia Fainali ya leo.
Wakati huo huo, Msemaji wa Polisi, Marcello Cardona, amethibitisha kuwa Mashabiki wawili wa Man U ambao ni Baba na Mwanawe wako lupango baaada ya kuwa njwii na kuwashambulia wapita njia katika eneo la Campo de Fiori ambalo linapendwa na Watalii.
Uuzwaji wa pombe jirani na Stadio Olimpico umepigwa marufuku kuanzia jana jioni hadi kesho asubuhi.

BUTI ZA ROONEY ZAIBIWA!!!!!
Buti za kuchezea soka za Wayne Rooney wa Manchester United zilizosafirishwa kwa ndege na Kampuni ya Nike hadi Roma, Italia zimeibiwa baada ya kupokelewa Uwanja wa Ndege huko Roma.
Inasemekana kuna mtu alisaini kuzipokea buti hizo spesheli aina ya Nike T90 na baada ya hapo zikatoweka.
Kwa sasa, Nike wanahaha kumtumia buti nyingine ili ziwahi mechi ya leo.
Wigan yairuhusu Sunderland kuongea na Meneja Steve Bruce!
Klabu ya Sunderland imepewa idhini na Wigan kufungua majadiliano ya kumchukua Meneja wa Wigan Steve Bruce.
Sunderland kwa sasa haina Meneja baada ya Meneja wao Ricky Sbragia kuitema Klabu mara tu baada ya Sunderland kunusurika kuteremshwa daraja siku ya Jumapili licha ya kufungwa na Chelsea 3-2.

Timu zilizoshuka ni Newcastle, Middlesbrough na West Brom.
Sbragia alirithi cheo hicho Desemba 2008 baada ya Roy Keane kubwaga manyanga mwenyewe.
Ferguson, Vidic ndio Meneja na Mchezaji Bora wa LIGI KUU England msimu huu 08/09!!!!

Mwanawe Ferguson, Darren, atwaa Umeneja Bora LIGI WANI!!
Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, na Mchezaji wake, Nemanja Vidic, wamepewa Tuzo ya Meneja Bora
na Mchezaji Bora wa LIGI KUU England msimu huu wa mwaka 2008/9.
Vilevile mtoto wake Ferguson aitwae Darren Ferguson, ambae ni Meneja wa Peterborough Timu iliyokuwa Daraja liitwalo LIGI WANI [LEAGUE 1] ameshinda Tuzo ya Meneja Bora kwa Daraja hilo baada ya kuweza kuipandisha Peterborough hadi Daraja la juu Coca Cola Championship.
LIGI WANI ni Daraja la chini ya Coca Cola Championship ambayo ipo chini ya LIGI KUU.
Ferguson na Vidic wamepewa Tuzo hizo kwa kutambua mchango wao mkubwa msimu huu ulioiwezesha Manchester United kutwaa Ubingwa wa LIGI KUU kwa mara ya 3 mfululizo.
Hii ni mara ya 9 kwa Ferguson kushinda Tuzo hii na ni mara ya kwanza kwa Vidic.
Jopo la Wawakilishi kutoka FA, Vyombo vya Habari na Mashabiki ndio waliotoa uamuzi wa kuwazawadia Ferguson na Vidic.
Meneja Mkuu Bayern atoboa Man U imewauliza kuhusu Ribery!!!
Meneja Mkuu wa Klabu ya Bayern Munich, Uli Hoeness, ametoboa kuwa Manchester United imewafuata kuulizia kuhusu Mchezaji wao Franck Ribery wa Ufaransa.
Inaaminika mbali ya Man U, Klabu kubwa kadhaa za Ulaya zinamuwania Ribery ambae bado ana miaka miwili kwenye mkataba wake na Bayern Munich. Miongoni mwa Klabu hizo ni Barcelona na Real Madrid.

Tuesday 26 May 2009

KITIMTIM ROMA KESHO!!!
Manchester United v Barcelona Stadio Olimpico Saa 3 dak 45 usiku Bongo Taimu
Kesho ndio kimbembe cha mwisho cha Klabu Bingwa Ulaya wakati Mabingwa Watetezi Manchester United watakapoingia Uwanjani Olimpico huko Roma, Italia kutetea taji lao kwa kupambana na Timu ngumu ya Barcleona katika Fainali ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
Hii ni mara ya 10 kwa Klabu hizi kukutana katika Mashindano mbalimbali ya Klabu za Ulaya huku Manchester United akiongoza kwa kushinda mechi 3, Barcelona ameshinda mara 2 na mechi 4 ziliisha droo. Klabu hizi zimewahi kukutana kwenye Fainali ya mwaka 1991 ya Kombe la Mabingwa wa Kikombe cha Nchi [European Cup Winners Cup] na Manchester United aliibuka mshindi kwa bao 2-1.
Msimu uliokwisha, kwenye Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE, Barcelona alitoka suluhu 0-0 kwake Nou Camp na Manchester United na marudiano yaliyofanyika Old Trafford, nyumbani kwa Manchester United, wenyeji waliibuka washindi kwa bao moja alilofunga Paul Scholes na Manchester United akatinga Fainali na kumtoa Chelsea.
==Safari ya kwenda Roma: Manchester United FC
Manchester United walianzia KUNDI E na walishinda mechi 2 katika mechi 6 za Kundi hili na kumaliza wakiwa vinara. Man U walitoka suluhu mbili na Villareal na kuwafunga Aalborg BK bao 3-0 na Celtic kwa idadi hiyo hiyo.
Katika Raundi ya Kwanza ya Mtoano, Man U walitoka suluhu 0-0 na Timu ya Jose Mourinho, Inter Milan, katika mechi ya kwanza huko Italia na kushinda 2-0 kwenye marudiano Old Trafford.
Kwenye Robo Fainali, Man U walikutana na FC Porto ya Ureno na mechi ya kwanza ndani ya Old Trafford mechi ilikwisha 2-2. Lakini katika mechi ya marudiano huko Ureno, Mreno Cristiano Ronaldo aliwatungua Wareno wenzake kwa kigongo cha mita 35 na kuiingiza Man U Nusu Fainali.
Nusu Fainali ilikuwa ni mechi kati ya Timu mbili toka England, yaani Manchester United v Arsenal, na mechi ya kwanza, iliyochezwa Old Trafford, Manchester United walishinda bao 1-0 kwa goli la Beki John O’Shea.
Marudiano huko nyumbani kwa Arsenal, Emirates Stadium, Manchester United waliibuka kidedea kwa ushindi mtamu wa mabao 3-1 kwa mabao yaliyofungwa na Ji-Sung Park bao moja na Ronaldo mabao mawili.
==Safari ya kwenda Roma: FC Barcelona
Barcelona walikuwa KUNDI C na walianza mechi zao kwa makeke makubwa kwa kuzikung’uta Sporting Clube de Portugal mabao 3-1, FC Basel ya Uswisi mabao 5-0 na pia kwenye mechi ya marudiano wakaibamiza Sporting Clube de Portugal mabao 5-2 huko huko kwao Lisbon, Ureno. Huku wakishajijua wamemaliza Kundi lao kama vinara, Barca walifungwa 3-2 na FC Shakhtar Donetsk.
Katika Raundi ya Kwanza ya Mtoano, Barca walitoka suluhu 1-1 na Olympique Lyonnais, maarufu kama Lyon, huko Ufaransa na marudiano huko Nou Camp waliichabanga Lyon mabao 5-2.
Robo Fainali, Barca walikutana na Wakongwe wa Ujerumani Bayern Munich na kuibamiza 4-0 ndani ya Nou Camp na marudiano huko Ujerumani yalikuwa 1-1.
Kwenye Nusu Fainali, Barca walipambana na Chelsea ya England.
Mechi ya kwanza huko Nou Camp ilikuwa 0-0 na mechi ya pili ikahamia Stamford Bridge, London nyumbani kwa Chelsea na huko ndiko ikazuka VITA KUU YA DARAJANI.
Huku wakiongoza kwa bao moja, bao tamu alilofunga Michael Essien, na licha ya Refa kutoka Norway Tom Henning Ovrebo kuwanyima Chelsea penalti kadha wa kadha za dhahiri, huku Uwanja mzima wa Stamford Bridge wakiamini Chelsea watatinga Fainali, katika dakika ya tatu ya muda wa nyongeza wa majeruhi Iniesta aliachia shuti lililomshinda Kipa Petr Cech na kutinga wavuni kuifanya mechi imalizike 1-1 na Barcelona kuingia Fainali kwa goli la ugenini.

Ndipo kasheshe la kina Drogba na wenzake likaanza na sasa wako kizimbani kwenye Mahakama za UEFA!!!!!
BAADA YA KWISHA LIGI KUU ENGLAND, ZIJUE KLABU ZITAKAZOCHEZA ULAYA MSIMU UJAO 2009/10
Kwa kumaliza nafasi nne za juu Klabu za Manchester United, Liverpool, Chelsea na Arsenal zitaiwakilisha England katika UEFA CHAMPIONS LEAGUE msimu ujao wa 2009/10.
Manchester United, Liverpool na Chelsea zitaingia moja kwa moja kwenye hatua ya MAKUNDI ambayo inachezwa kwa mtindo wa Ligi wa mechi za nyumbani na ugenini.
Arsenal, kwa kumaliza nafasi ya 4 kwenye LIGI KUU, atacheza UEFA CHAMPIONS LEAGUE kwenye hatua ya awali ya Mtoano na anaweza kupangiwa Klabu ya Nchi yeyote ile bila kubagua Nchi kubwa au Klabu kubwa kama ilivyokuwa zamani ambapo Timu kubwa zilikuwa zikitenganishwa kwenye awamu hii.
Klabu zilizomaliza nafasi ya 5 hadi ya 7 msimu ujao zitacheza kwenye mashindano mapya yatakayojulikana kama UEFA EUROPA LEAGUE. Mshindano haya yalikuwa yakiitwa UEFA CUP na msimu ujao mfumo wake utafanana na UEFA CHAMPIONS LEAGUE kwani Klabu zitapangwa kwenye Makundi na kucheza mtindo wa Ligi kwa mechi za nyumbani na ugenini.
Timu zitakazowakilisha England kwenye UEFA EUROPA LEAGUE ni Everton, Aston Villa na Fulham.
ZAWADI ZA KILA TIMU ZA LIGI KUU ENGLAND ZATANGAZWA!!!
Wasimamizi wa LIGI KUU England wametangaza zawadi ya kitita babu kubwa ambazo kila Klabu itaopoa kufuatana na nafasi iliyoshika kwenye msimamo wa Ligi hiyo.
Mbali ya zawadi hiyo ya Bulungutu kubwa, kila Klabu itapewa Pauni Milioni 23.6 ikiwa ni haki yao ya maonyesho ya mechi kwenye TV na pia nyongeza ya Pauni Milioni 5 kwa kila Klabu pamoja na kitita kingine ambacho kitategemea Klabu ilionyeshwa laivu mara ngapi.
Zawadi zinazotokana na Msimamo wa Ligi ni kama ifuatavywo [Fedha ni Pauni za Uingereza na ni Milioni]:
-1. Man U: 15.2
-2. Liverpool: 14.5
-3. Chelsea: 13.7
-4. Arsenal: 12.9
-5. Everton: 12.2
-6. Aston Villa: 11.4
-7. Fulham: 10.7
-8. Tottenham: 9.9
-9. West Ham: 9.1
-10. Man City: 8.4
-11. Wigan: 7.6
-12. Stoke: 6.9
-13. Bolton: 6.1
-14. Portsmouth 5.3
-15. Blackburn 4.6
-16. Sunderland 3.8
-17. Hull 3
-18. Newcastle 2.3
-19. Middlesbrough 1.5
-20. West Brom 0.8
Roma yaanza kujidhibiti kwa uvamizi!!!

Masanga marufuku kuanzia Jumanne hadi Alhamisi!!!!


Viongozi wa Jiji la Roma, Italia wameanza kujizatiti kukabiliana na uvamizi wa Washabiki zaidi ya 67,000 wanaotarajiwa kutua mjini humo ili kushuhudia Fainali ya Kombe la Klabu Bingwa Ulaya, lijulikanalo rasmi kama UEFA CHAMPIONS LEAGUE, litakalochezwa ndani ya Stadio Olimpico kati ya Mabingwa Watetezi wa Kombe hilo Manchester United na Barcelona.
Inasadikiwa zaidi ya Mashabiki 30,000 watatoka Uingereza na 20,000 watatoka Spain na ili kukabiliana na vurugu zinazoweza kutokea kati ya pande hizo Viongozi wa Roma wamezuia uuzwaji wa pombe kwa kutumia glasi katika maeneo yanayozunguka Stadio Olimpico kuanzia Jumanne jioni hadi Alhamisi asubuhi na pia usafiri wa sehemu mbalimbali Jijini humo umewekewa vizuizi kadhaa.
Vilevile, uuzwaji wa pombe kwa njia ya 'tekiawei' umepigwa marufuku.
Polisi wametangaza vita maalum kukabiliana na tiketi za bandia kwani inaaminika kuna Mashabiki zaidi ya 5,000 hawana tiketi na watatua Roma ili kubahatisha kupata tiketi dakika za mwisho kitu ambacho kitachochea uhalifu wa tiketi za bandia.
Hadi sasa Polisi wamethibitisha kukamata lundo la tiketi feki. Mkuu wa Polisi wa Roma Giuseppe Pecoraro amethibitisha: 'Tiketi zimekwisha! Zilizobaki zinazouzwa ni feki!!'
Na ili kudhibiti usalama, Polisi wa Italia watasaidiwa na Maafisa kadhaa wa vyeo vya juu kutoka England na Spain.
Mourinho aula zaidi inter Milan!!!
Jose Mourinho ameongezewa mkataba hadi mwaka 2012 na Klabu yake ya Inter Milan mara tu baada ya kuiwezesha Klabu hiyo ya Serie A Italia kutwaa Ubingwa wa Italia kwa mara ya 4 mfululizo.
Huu ni msimu wake wa kwanza kwenye Klabu hiyo.
Mourinho, ambae kabla ya kwenda Inter Milan alikuwa Meneja wa Chelsea, atamaliza mkataba wake tarehe 30 Juni 2012.
Hatua hii imezima ule mvumi mkubwa kuwa Mourinho ataenda Real Madrid msimu ujao.
Sunderland yagoma kumsajili Cisse kwa mkataba wa kudumu!!
Klabu ya Sunderland, ambayo juzi ilikuwa chupuchupu kuteremshwa Daraja, imetangaza kuwa Mshambuliaji toka Ufaransa, Djibril Cisse, hatopewa mkataba wa kudumu Klabuni hapo.
Cisse alijiunga Sunderland kwa mkopo kutoka Klabu ya Marseille ya Ufaransa huku kukiwa na kipengele kwenye mkopo huo kuwa Sunderland inaweza kumsaini kwa mkataba wa kudumu endapo itaafiki.
Lakini, Mwenyekiti wa Sunderland, Niall Quinn, ametangaza kupitia tovuti ya Klabu hiyo kuwa hawatomchukua Cisse ambae msimu huu alichezea Klabu hiyo mechi 38 na kuifungia mabao 11.
Gordon Strachan atimka Celtic!!!
Meneja wa Celtic, Gordon Strachan, amejiuzulu mara tu baada ya kuutema Ubingwa wa Scotland hapo juzi baada ya Mahasimu wao wakubwa Rangers kuutwaa Ubingwa huo.
Strachan aliiongoza Celtic kutwaa Ubingwa wa Scotland kwa misimu mitatu iliyopita.
Viera arudi kundini Ufaransa!!!
Kiungo veterani wa Ufaransa, Patrick Vieira [32], anaechezea Klabu Bingwa ya Italia Inter Milan, amerudishwa tena kwenye Timu ya Taifa ya Ufaransa na Kocha Raymond Domenech baada ya kukosa mechi 15 zilizopita za Ufaransa kwa kuwa majeruhi.
Ufaransa inategemewa kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Nigeria hapo Juni 2 na siku tatu baadae watacheza na Uturuki.
Kikosi kamili cha Ufaransa na Klabu wanazotoka:
Makipa: Cedric Carrasso (Toulouse), Hugo Lloris (Olympique Lyon), Steve Mandanda (Olympique Marseille).
Walinzi: Eric Abidal (Barcelona), Jean-Alain Boumsong (Olympique Lyon), Patrice Evra (Manchester United), Rod Fanni (Stade Rennes), Philippe Mexes (AS Roma), Bacary Sagna (Arsenal), Sebastien Squillaci (Sevilla), Julien Escude (Sevilla).
Viungo: Patrick Vieira (Inter Milan), Abou Diaby (Arsenal), Alou Diarra (Girondins Bordeaux), Lassana Diarra (Real Madrid), Yoann Gourcuff (Girondins Bordeaux), Jeremy Toulalan (Olympique Lyon), Florent Malouda (Chelsea).
Washambuliaji: Nicolas Anelka (Chelsea), Karim Benzema (Olympique Lyon), Andre-Pierre Gignac (Toulouse), Thierry Henry (Barcelona), Franck Ribery (Bayern Munich), Sidney Govou (Olympique Lyon), Loic Remy (Nice)

Monday 25 May 2009

Burnley watua LIGI KUU England!!!!! Waitungua Sheffield United 1-0!!!
BURNLEY, WOLVES NA BIRMINGHAM KUZIBADILI NEWCASTLE, MIDDLESBROUGH NA WEST BROM LIGI KUU MSIMU UJAO!!!!

Baada ya miaka 33 ya kutokucheza Daraja la juu kabisa la Soka huko England, leo huko Wembley Stadium, London, Timu ya Burnley imeifunga Sheffield United bao 1-0 na kufanikiwa kuingia LIGI KUU.
Goli lililoipeleka Burnley LIGI KUU lilifungwa na Wade Elliot dakika ya 13.
Hii ilikuwa ni Fainali ya Mtoano maalum wa kuipata Timu ya tatu itayoungana na Wolves na Birmingham zilizoingia moja kwa moja LIGI KUU kwa kuwa zilimaliza Ligi ya Coca Cola Championship nafasi za kwanza na ya pili.
Timu za Wolves, Birmingham na Burnley zinapanda Daraja kwenda LIGI KUU kuchukua nafasi za Newcastle, Middlesbrough na West Bromwich Albion zilizoshushwa na sasa zitacheza Coca Cola Championship msimu ujao.
Veterani Neville aitwa tena Timu ya Taifa England!!!!
Meneja wa England, Fabio Capello, katika hatua ya kushangaza amemuita kwenye Kikosi cha England Nahodha wa Manchester United Gary Neville [34] kwa ajili ya mechi za mchujo wa kuingia Fainali za Kombe la Dunia ambazo England itacheza na Kazakhstan Juni 6 na siku nne baadae watacheza na Andorra.
Gary Neville, ambae mara ya mwisho alichezea England Oktoba 2007 wakati England ilipofungwa na Urusi kwenye mchujo wa kuingia EURO 2008, amekuwa akiandamwa na kuumia mara kwa mara na kuifanya hata namba yake Klabuni kwake Manchester United isiwe ya kudumu.
Pia, Capello amemchukua tena aliyekuwa Kipa nambari wani wa England, Paul Robinson wa Blackburn baada ya Makipa wa sasa Nambari moja na mbili, David James wa Portsmouth na Ben Foster wa Manchester United kuumia. Robinson atasaidiwa na Makipa Scott Carson wa West Brom na Robert Green wa West Ham.
Kikosi kamili na Klabu wanazotoka ni kama ifuatavyo:
Scott Carson (West Bromwich Albion), Robert Green (West Ham United), Paul Robinson (Blackburn Rovers)
Wayne Bridge (Manchester City), Ashley Cole (Chelsea), Rio Ferdinand (Manchester United), Glen Johnson (Portsmouth), Joleon Lescott (Everton), Gary Neville (Manchester United), John Terry (Chelsea), Matthew Upson (West Ham United)
Gareth Barry (Aston Villa), David Beckham (AC Milan mkopo kutoka LA Galaxy), Michael Carrick (Manchester United), Steven Gerrard (Liverpool), Frank Lampard (Chelsea), Theo Walcott (Arsenal), Shaun Wright-Phillips (Manchester City), Ashley Young (Aston Villa)
Carlton Cole (West Ham United), Peter Crouch (Portsmouth), Jermain Defoe (Tottenham Hotspur), Emile Heskey (Aston Villa), Wayne Rooney (Manchester United)

REFA ALIECHEZESHA NUSU FAINALI YA MWAKA JANA HUKO NOU CAMP YA BARCELONA V MAN U KUCHEZESHA FAINALI JUMATANO!!!!

UEFA imemtangaza Refa kutoka Switzerland, Massimo Busacca [pichani], kuwa ndio Mwamuzi wa Fainali ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE huko Roma, Italia siku ya Jumatano kati ya Mabingwa Watetezi wa Kombe hilo Manchester United na Barcelona itakayochezwa ndani ya Stadio Olimpico. Busacca, miaka 40, atasaidiwa na Matthias Arnet na Francesco Buragina pia kutoka Switzerland na Mwamuzi wa nne ambae ni wa Akiba ni Claudio Circhetta nae pia kutoka Switzerland.
Wadau wanaweza kumkumbuka Refa huyu ndie aliechezesha pambano la mechi ya kwanza ya Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE msimu uliopita huko Nou Camp kati ya Barcelona na Manchester United, mechi iliyoisha 0-0, na katika mechi hiyo aliwapa penalti Manchester United kipindi cha kwanza lakini Ronaldo alikosa.
Lakini baadae, kipindi hicho hicho cha kwanza, aliwanyima Manchester United penalti ya wazi kabisa baada ya Ronaldo kuangushwa ndani ya boksi na baada ya mechi Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson alisema: 'Dunia nzima pamoja na Mkewe wanajua ile ni penalti!! Lakini kwenye mechi kama hizi ukipata penalti moja ni majaliwa, mbili ni maajabu makubwa!!!'
Hata hivyo, Busacca ameshachezesha mechi ya Manchester United msimu huu na ni ile mechi ya marudiano ya Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE kule Porto ambayo Man U waliwabwaga nje FC Porto kwa kuwafunga 1-0 nyumbani kwake.

Baada ya Balaa la kushushwa Daraja.......Shearer akataa kuthibitisha kama atabaki Newcastle

................Southgate ategemea Wachezaji kuikimbia Middlesbrough!!

==Baada ya kupona Balaa la kushushwa Daraja Sbragia wa Sunderland abwaga manyanga!!!!
Meneja wa Newcastle, Alan Shearer, baada ya Timu yake kushushwa Daraja walipofungwa na Aston Villa hapo jana, amekataa kujibu maswali yeyote kuhusu nini hatima yake.
Shearer alijibu maswali hayo kwa kusema: 'Ntakutana na Mmiliki wa Klabu wiki hii na ntamwambia nin kilienda sawa na nini kilienda vibaya lakini sasa si wakati wa kusema nini cha baadae!!'
Mwenzake wa Middlesbrough, Gareth Southgate, amekiri kuwa kutakuwa na wimbi la Wachezaji watakaohama kwa vile hawataki kucheza Daraja la chini.
'Bila shaka kutakuwa na mabadiliko makubwa kwa Wachezaji,' Southgate alisema. 'Watu watakuwa na ajenda binafsi! Kama Klabu itabidi tuuze Wachezaji ili tupate pesa za kusonga mbele. Na inabidi tubadilishe hali.'
Na katika hali ya kushangaza, ingawa Sunderland ilinusurika kuporomoka Daraja ingawa ilifungwa na Chelsea mabao 3-2, Meneja wake Ricky Sbragia, mara baada ya mechi, alitangaza kujiuzulu.
Sbragia alitamka: 'Nahisi Klabu inabidi imlete Meneja mwenye jina kubwa!! Niliichukua Klabu hii wakati mgumu sana!!!'
Sbragia aliteuliwa kuwa Meneja mwezi Desemba 2008 mara tu baada ya Roy Keane kubwaga manyanga mwenyewe bila kutegemewa.

Wolves, Birmingham na Sheffield United AU Burnley kuchukua nafasi za Newcastle, Middlesbrough na West Brom LIGI KUU msimu ujao!!!

==LEO ITAJULIKANA NI SHEFFIELD UNITED AU BURNLEY!!!
Leo saa 11 jioni bongo taimu Timu mbili za Daraja la Coca Cola Championship, Burnley na Sheffield United, zitapigana ndani ya Uwanja wa Wembley, jijini London kutafuta Timu moja ipi itaungana na Wolverhamton Wanderers, aliemaliza Ligi hiyo nafasi ya kwanza, na Birmingham, aliemaliza wa pili, kucheza LIGI KUU England msimu ujao.
Sheffield United na Burnley zilishinda mechi zao za awali za Mtoano kwa Sheffield United kuwatoa Preston kwa jumla ya mabao 2-1 katika mechi mbili na Burnley waliwanyuka Reading jumla ya bao 3-0 katika mechi mbili.
Katika mfumo wa Ligi ya Coca Cola Championship Timu mbili za kwanza huingia LIGI KUU moja kwa moja na Timu zilizo nafasi ya 3 hadi ya 6 hucheza Mtoano maalum ili kupata Timu moja itakayoungana na hizo Timu mbili za kwanza kupanda kwenda LIGI KUU.
Katika mechi mbili za Ligi, Burnley ilshinda mechi zote kwa kuifunga Sheffield United nyumbani kwake mabao 3-2 katika mechi ya kwanza na marudiano yalikuwa nyumbani kwa Burnley na walishinda tena bao 1-0.
Mbali ya umuhimu wa kupanda Daraja kwenda LIGI KUU, Timu zinazokuwa LIGI KUU hunufaika kwa kuingiza pesa nyingi sana na ndio maana mechi hii imebatizwa jina la 'MECHI MOJA YA KLABU YENYE THAMANI SANA DUNIANI!!' kwa vile mshindi akichezea LIGI KUU ataingiza MAPATO YA WASTANI wa zaidi ya Pauni Milioni 60 kwa msimu!!
Burnley mara ya mwisho kuchezea Darala la juu kabisa ilikuwa miaka 33 iliyopita na mwaka huu wana matumaini makubwa sana ya kufaulu kupanda hasa baada ya kuzitoa Timu za LIGI KUU kwenye Carling Cup msimu huu kama vile Arsenal, Chelsea na West Brom lakini wakatolewa Nusu Fainali na Tottenham ingawa walishinda mechi ya kwanza ya Nusu Fainali hiyo.
Sheffield United waliporomoshwa toka LIGI KUU misimu miwili iliyopita katika mechi ya mwisho katika lile sakata maarufu la Carlos Tevez kuichezea West Ham na kuiokoa West Ham kushushwa kwa kuifungia bao walipocheza na Manchester United mechi ya mwisho ya Ligi.
Refa katika mechi ya leo ni Mike Dean.

Sunday 24 May 2009

NEWCASTLE, MIDDLESBROUGH WAUNGANA NA WEST BROM KUSHUKA DARAJA!!!
  • TIMU ZOTE ZILIZOKUWA ZIKIPIGANIA KUTOSHUKA DARAJA ZAFUNGWA LAKINI HULL CITY NA SUNDERLAND WANUSURIKA!!!!!!!

Timu zote zilizokuwa kwenye VITA KUU ya kuepuka kushuka Daraja zimefungwa katika mechi zao za mwisho za LIGI KUU England leo lakini ni Newcastle na Middlesbrough ndio walioungana na West Bromwich Albion kushushwa Daraja na msimu ujao watacheza Daraja la chini liitwalo Coca Cola Championship.

MATOKEO YA MECHI YA TIMU ZILIZOKUWA ZIKIPIGANIA KUPONA KUSHUSHWA NI:

Sunderland 2 Chelsea 3

Hull City 0 Manchester United 1

Aston Villa 1 Newcastle 0

West Ham 2 Middlesbrough 1

BAADA YA MECHI ZA MWISHO ZA LEO MSIMAMO KWA TIMU ZA CHINI NI:

[TIMU ZA NAFASI YA 18 HADI 20 HUSHUSHWA]

-Nafasi ya 16: Sunderland pointi 36

-Nafasi ya 17: Hull City pointi 35

-Nafasi ya 18: Newcastle pointi 34

-Nafasi ya 19: Middlesbrough pointi 32

-Nafasi ya 20: West Brom pointi 31

MATOKEO KAMILI MECHI ZA LEO:

Arsenal 4 v Stoke 1

Aston Villa 1 v Newcastle 0

Blackburn 0 v West Brom 0

Fulham 0 v Everton 2

Hull 0 v Man U 1

Liverpool 3 v Tottenham 1

Man City 1 v Bolton 0

Sunderland 2 v Chelsea 3

West Ham 2 v Middlesbrough 1

Wigan 1 v Portsmouth 0

SCOTLAND: Rangers wachukua Ubingwa wa LIGI KUU Scotland!!
Kwa mara ya kwanza tangu 2005 leo Rangers wamenyakua ubingwa wa Ligi Kuu ya Scotland baada ya kuwafunga Dundee United mabao 3-0 katika mechi ya mwisho ya msimu na hivyo kuwabwaga Wapinzani wao wa Jadi Celtic katika kinyang'anyiro hicho.
Celtic wamekuwa Mabingwa wa Scotland mara 3 mfululizo tangu mwaka 2006 na hata leo kama Rangers wangeteleza na wao Celtic kushinda basi wangeweza kuutwaa tena.
Hata hivyo Celtic katika mechi yao ya mwisho ya leo wameambulia sare ya 0-0 na Hearts.
LEO NI LEO: KUZAMA AU KUZUKA!!!
Ni WAWILI gani kati ya Sunderland, Hull City, Newcastle na Middlesbrough kuungana na West Brom kushuka DARAJA???
Tamati ya LIGI KUU England ni leo jioni wakati Timu zote 20 zitashuka Viwanja mbalimbali kucheza mechi zao za mwisho kuanzia saa 12 jioni saa za kibongo huku tayari Bingwa Manchester United alitawazwa tangu wiki iliyopita na kuacha kimbembe kikubwa cha Timu zipi mbili zitaungana na West Bromwich Albion kucheza ‘mchangani’ Ligi ya chini iitwayo Coca Cola Championship msimu ujao.
Ingawa macho ya wengi yako kwenye ‘VITA KUU’ ya nani atashushwa Daraja lakini kimahesabu hata nafasi za pili na za tatu zinaweza kugeuka ikiwa leo Liverpool, alie nafasi ya 2, akifungwa na Tottenham na Chelsea, alie nafasi ya 3, akamfunga Sunderland mabao mengi ili kuifuta tofauti ya magoli bora ya Liverpool ya magoli matano aliyokuwa nayo.
Nafasi ya 4 ni ya Arsenal na hakuna anaeweza kumpiku.
Kwa kumaliza nafasi 3 za juu, Timu za Manchester United, Liverpool na Chelsea zinaingia moja kwa moja kwenye hatua ya Makundi ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE msimu ujao.
Arsenal, kwa kumaliza nafasi ya 4, pia anaingia UEFA CHAMPIONS LEAGUE msimu ujao lakini itabidi aanzie Raundi ya Mwanzo ya Mtoano na hatari ya mfumo wa msimu ujao ni kuwa anaweza kupangiwa Timu yeyote ile tofauti na misimu ya nyuma ambapo Timu Bora zilitenganishwa.
Ingawa Sunderland wako nafasi ya 16 wakiwa na pointi 36 lakini wakifungwa watashushwa ikiwa Newcastle na Hull City watashinda.Ikiwa Newcastle watashinda na Hull City kutoka droo basi Sunderland [IKIWA HATOFUNGWA ZAIDI YA BAO 5] na Newcastle watapona na badala yake Hull City wataporomoka.
Middlesbrough ndie anayeomba maajabu yatokee!!
Ili Middlesbrough apone itabidi kwanza ashinde mechi yake na kuomba Hull City na Newcastle wafungwe lakini nani atashushwa kati ya Middlesbrough na Hull City itategemea Middlesbrough kafunga bao ngapi na Hull City kafungwa ngapi.
Hizo, kwa ufupi, ndizo hesabu kali za nani atasalimika kubaki LIGI KUU.
Msimamo kwa Timu za chini zilizo kwenye VITA KUU ya KUJINUSURU KUSHUSHWA DARAJA ni [West Bromwich tayari kaporomoka]: [TIMU ZA NAFASI YA 18 HADI 20 HUSHUSHWA]

-Nafasi ya 16: Sunderland pointi 36 [tofauti ya magoli -19]
-Nafasi ya 17: Hull City pointi 35 [tofauti ya magoli -24]
-Nafasi ya 18: Newcastle pointi 34 [tofauti ya magoli -18]
-Nafasi ya 19: Middlesbrough pointi 32 [tofauti ya magoli -28]
-Nafasi ya 20: West Brom pointi 31 [tofauti ya magoli -31]
MECHI ZA MOTO ZA TIMU ZA CHINI:
Aston Villa v Newcastle
Hull v Man U
Sunderland v Chelsea
West Ham v Middlesbrough
RATIBA KAMILI:
Jumapili, 24 Mei 2009
[saa 12 jioni]
Arsenal v Stoke
Aston Villa v Newcastle
Blackburn v West Brom
Fulham v Everton
Hull v Man U
Liverpool v Tottenham
Man City v Bolton
Sunderland v Chelsea
West Ham v Middlesbrough
Wigan v Portsmouth
KASKAZINI MASHARIKI YA ENGLAND YAGUBIKWA NA MAJONZI!!!!
· Ni woga wa Timu za Mijini kwao KUSHUSHWA DARAJA!!!!
· Ni miji ya Hull, Middlesbrough, Sunderland na Newcastle!!!!
Wiki yote iliyopita Dereva mmoja wa Basi la Abiria linalofanya safari kati ya miji iliyoko Kaskazini Mashariki ya England, miji ya Hull, Middlesbrough, Sunderland na Newcastle, ambayo yote iko eneo moja lakini kwa bahati mbaya, imeunganishwa katika VITA KUBWA ya kunusuru Klabu zao kuporomoka kutoka LIGI KUU England, amekuwa akifanya kazi yake kama kawaida lakini kitu pekee anachokisikia wiki nzima miongoni mwa abiria wanaosafiri kwenye basi lake ni huzuni, matumaini na stori nyingi kuhusu Klabu za Hull City, Middlesbrough, Sunderland na Newcastle.
Safari yake kila asubuhi huanzia Hull na kuelekea kaskazini kwenda Middlesbrough halafu Sunderland na kumalizikia Newcastle.
‘Ni majonzi na masikitiko eneo lote!’ Dereva huyo anasema. ‘Binafsi nafikiria Hull City watashushwa pamoja na Middlesbrough hata kama Man U wataleta Kikosi cha pili Hull hawezi kuwafunga!! Nadhani Newcastle atapata pointi yake moja anusurike!’
Kila kona ya Miji hiyo minne, gumzo ni nani atapona?
Homa hii ya kunusuru Klabu zao imeingia mpaka ndani ya Klabu zenyewe na Gazeti moja la mjini Hull limeripoti Klabu ya Hull imempiga marufuku Shabiki wake mmoja mwenye tiketi ya msimu mzima kuingia KC Stadium kutoingia uwanjani humo baada ya kugundulika anatoa matusi mengi Timu yake Hull City inapocheza.
Lakini nani amlaumu Shabiki huyo ikiwa Hull City katika mechi 10 za mwisho ilizocheza uwanjani kwake KC Stadium haijashinda hata mechi moja??
Hilo ndilo kasheshe lililoikumba Miji ya Kaskazini Mashariki ya England!!!!
Powered By Blogger