Saturday 4 April 2009

Liverpool wachomeka kigoli dakika za majeruhi, waongoza Ligi kwa pointi 2 ingawa Man U ana mechi 2 mkononi!!!!

Kigoli cha babu kilichofungwa na Myahudi Yossi Benayoun dakika ya 92 kimewapa ushindi Liverpool dhidi ya Fulham na hivyo kuwa na pointi 67 huku wamecheza mechi 31.
Mabingwa Man U wanaocheza kesho na Aston Villa uwanjani kwake Old Trafford ni wa pili wakiwa wamecheza mechi 29 na pointi 65 huku Chelsea akifuatia akiwa na pointi 64 kwa mechi 31.
Arsenal ni wa nne kwa mechi 31 na pointi 58.
MECHI ZA JUMAPILI, Aprili 5:
[saa 11 jioni]
Everton v Wigan
[saa 12 jioni]
Man U v Aston Villa
Shearer aanza na kipigo nyumbani: Newcastle 0 Chelsea 2!!!!
Adebayor arudi kikosini na kuipa ushindi Arsenal wa 2-0!!!

Nyota wa zamani wa Newcastle, Alan Shearer, alieletwa Newcastle ili kuinusuru kuporomoka daraja leo ameanza kazi kwa kipigo cha 2-0 nyumbani walipofungwa na Chelsea.
Hadi mapumziko jahazi la Newcastle lilikuwa likiselelea vizuri kwa sare ya 0-0 lakini mabao ya kipindi cha pili yaliyofungwa na Lampard na Malouda yaliwapa ushindi wa bao 2-0 Chelsea na kuwadidimiza chini Newcastle huku wakiwa wamebakiza mechi 7 kujinusuru.
Arsenal, wakiwakaribisha tena nyota wao waliokuwa majeruhi akina Fabregas, Walcott na Adebayor, waliibuka washindi wa mabao 2-0 yaliyofungwa na Adebayor.
MATOKEO MECHI NYINGINE ZA LEO:
Blackburn Rovers 2 Tottenham 1
Bolton 4 Middlesbrough 1
Hull City 0 Portsmouth o
West Bromwich 0 Stoke City 2
West Ham 2 Sunderland 0
Ligi Kuu leo: Shearer kuanza kibarua, Berbatov majeruhi, Fabregas uwanjani, Zaki matatani!!!

Baada ya kutochezwa kwa wiki mbili sasa ili kupisha mechi za Timu za Taifa kwenye michujo ya Kombe la Dunia, leo LIGI KUU England inarudi dimbani huku Newcastle, watakaocheza na Chelsea, wakiwa na Meneja mpya aliekuwa Mchezaji wao wa zamani, Alan Shearer, ambae amesimikwa hapo kwa kazi moja tu na nayo ni kuinusuru Newcastle isporomoke daraja.
Kwa sasa Newcastle iko nafasi ya 18 kwenye msimamo wa ligi ikiwa ni nafasi ya 3 toka mkiani na kawaida timu za mkiani, yaani nafasi ya 18, 19 na 20, hushushwa daraja.
Ingawa Newcastle wako nyumbani leo, uwanjani kwao St James Park, kazi yao ni ngumu sana kwani wanakumbana na Timu ngumu ya Chelsea iliyo nafasi ya 3 na ambayo bado ina matumaini makubwa ya kuwa Bingwa.
Nao Mabingwa wa LIGI KUU, Maanchester United, kesho watakuwa kwao Old Trafford huku wakiwa wamekumbwa na balaa la kuwakosa Wachezaji wao wakubwa kwenye mechi dhidi ya Aston Villa.
Wayne Rooney na Nemanja Vidic wamefungiwa kwa kuwa na Kadi Nyekundu na Berbatov ni majeruhi kwa kuumia enka.
Hivyo mbele watamtegemea Tevez tu ambae hali yake haijathibitishwa kwani aliwasili jana jioni akitokea Marekani Kusini alikokuwa na Timu yake ya Taifa ya Argentina.
Huko Wigan nako mambo si shwari kwani baada ya Mmisri Mido kumshutumu Mmisri mwenzake, Amr Zaki, wote wakiwa Wachezaji wa Wigan, Meneja wa Wigan Steve Bruce ametangaza kuwa watamchukulia hatua kali sana Zaki kwa kuchelewa kurudi kutoka Misri alikochezea Timu ya Taifa ya Misri iliyocheza kwenye dro ya 1-1 na Zambia kwenye mechi ya Kombe la Dunia.
Steve Bruce amesema hii ni mara ya nne kwa Zaki kuchelewa kurudi na kila mara amekuwa akipigwa faini lakini safari hii watampa adhabu kali sana.
Kesho Wigan ni wageni wa Everton.
Arsenal leo wanawakaribisha Manchester City Emirates Stadium na vilevile watamkaribisha Nahodha wao Cesc Fabregas aliekuwa nje ya uwanja kwa miezi mitatu baada ya kuumia.
Vilevile, Wachezaji wengine wa Arsenal walioumia na sasa kupona na leo watakuwa kikosini ni pamoja na Emmanuel Adebayor, Theo Walcott na Nicklas Bendtner.
Lakini Robin van Perise, Eduardo, Abou Diaby na Samir Nasri wote watakuwa nje kwa kuwa majeruhi.

Thursday 2 April 2009

LIGI KUU England ndani ya nyumba wikiendi hii!!

Baada ya mapumziko ya lazima ili kupisha michuano ya mchujo wa kutafuta Nchi zitakazocheza Fainali Kombe la Dunia huko Afrika Kusini 2010, sasa macho yetu yote yako ndani ya starehe yetu ya mikikimikiki ya LIGI KUU England itayoanza kuonekana wikiendi hii.
Vivutio vikubwa ni kuona jinsi Mabingwa wa LIGI KUU, Ulaya na Dunia, Manchester United, watakavyoibuka baada ya kufungwa mechi mbili mfululizo watakapochuana na Aston Villa Jumapili, Liverpool, wakiwa pointi moja nyuma ya Man U ingawa wamecheza mechi moja zaidi, wakiongeza kibano kwa Mabingwa hao kwa kushinda mechi yao dhidi ya Fulham Jumamosi na hivyo kuwapiku Man U kileleni japo kwa siku moja tu, pia kumuona 'Mkombozi' Alan Shearer [pichani] akiwa Meneja mpya wa Newcastle alieletwa mahsusi kuinusuru Timu hiyo kushuka daraja akianza kibarua hicho kigumu kwa kupambana na Chelsea na kwa Arsenal kumuona Nahodha wao Cesc Fabregas akirudi uwanjani kupambana na Man City baada ya miezi mitatu kuwa majeruhi.
Kwa Mabingwa Man U itabidi washuke uwanjani bila ya Nemanja Vidic, Paul Scholes na Wayne Rooney ambao wote wamefungiwa mechi hii kwa kupata Kadi Nyekundu mechi zilizokwisha.
RATIBA YA MECHI NI:
Kumbuka: Majira ya Joto yameanza rasmi huko Ulaya hivyo tofauti ya saa kati ya Uingereza na Bongo imepungua na sasa kuwa ni Masaa mawili tu.
Hivyo utaona mechi zinaanza saa moja kabla na vile ulivyozoea-mathalan mechi za saa 12 jioni, bongo taimu, sasa zitachezwa saa 11 jioni.
Jumamosi, Aprili 4, 2009
[saa 8.45 mchana]
Blackburn v Tottenham
[saa 11 jioni]
Arsenal v Man City
Bolton v Middlesbrough
Hull City v Portsmouth
Newcastle v Chelsea
West Brom v Stoke City
West Ham v Sunderland
Jumapili, Aprili 5, 2009
[saa 11 jioni]
Everton v Wigan
[saa 12 jioni]
Man U v Aston Villa
Argentina wapata kipigo kibaya!!! Wamebebeshwa mabao SITA!!!!!

Wapinzani wao wa jadi Brazil washinda 3-0!!!!

Kwenye mechi ya mchujo na kuwania nafasi ya kuingia Fainali za Kombe la Dunia 2010 kwa Nchi za Marekani Kusini, Argentina inayomilikiwa na Staa wao wa zamani Diego Armando Maradona, ilipata kipigo kibaya sana ambacho hawajahi kukipata kwa miaka 60 sasa pale walipofungwa mabao 6-1 na Bolivia.
Nchi nyingi huhofia kucheza na Bolivia huko kwao kwa sababu Nchi hiyo iko milimani na ipo zaidi ya Mita 3600 toka usawa wa bahari na kufanya hewa yake kuwa nyepesi na ngumu kupumua na hivyo kuzichosha timu ngeni.
FIFA iliwahi kupiga marufuku mechi za kimataifa kuchezwa huko lakini wimbi la malalamiko kutoka kwa Wadau wa Soka, akiwemo Maradona, walipinga hatua hiyo na Sepp Blatter wa FIFA akaamua kuufuta uamuzi huo na kuwaacha Wataalam kufanya utafiti kama kuna madhara kwa Wachezaji kucheza mechi kwenye Viwanja vya Bolivia ukitilia maanani matatizo ya pumzi kwa Wachezaji kutokana na kuwa juu sana toka usawa wa bahari.
Argentina, chini ya Meneja Maradona, iilicheza mechi 3 na kushinda zote bila kufungwa hata goli moja lakini mechi hiyo ya 4 na Bolivia walikumbana na kipigo cha mvua ya magoli.
Maradona mwenyewe alilia: 'Kila goli lilikuwa ni kuuchoma mkuki moyo wangu! Lazima tuwasifie Bolivia, walituzidi kila kitu!'
Na Brazil, wapinzani wa jadi wa Argentina, waliifunga Peru 3-0 kwa mabao yaliyopachikwa na Luis Fabiano, mabao mawili, na Felipe Melo, bao moja na hivyo kuwafanya wachupe hadi nafasi ya pili katika msimamo wa Kundi la Nchi za Marekani Kusini.
Huku kila Nchi ikiwa imeshacheza mechi 12 [zipo jumla Nchi 10 kwenye Kundi hili], Paraguay wanaongoza wakiwa na pointi 24, Brazil wa pili pointi 21, anafuata Chile pointi 20, Argentina pointi 19 na Uruguay pointi 17.
Timu nne za kwanza zitafuzu kuingia moja kwa moja Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwaka 2010.

England 2 Ukraine 1

Uwnjani kwao Wembley, England waliendeleza wimbi la ushindi kwa kushinda mechi yao ya 5 mfululizo kwenye Kundi lake pale walipowafunga Ukraine bao 2-1.
Mabao ya England yalifungwa na Peter Crouch dakika ya 29 [pichani] na John Terry dakika ya 85.
Bao la Ukraine lilifungwa na Andriy Shevchenko dakika ya 74.
England: James, Johnson, Ferdinand (Jagielka 88), Terry, Cole, Lennon (Beckham 57), Lampard, Barry, Gerrard, Rooney, Crouch (Wright-Phillips 79). Akiba hawakucheza: Foster, Lescott, Carrick, Agbonlahor.
Kadi: Barry, Johnson, Beckham.
Ukraine: Pyatov, Yarmash, Mykhalyk, Chigrinsky, Shevchuk, Aliev, Slyusar (Kalinichenko 88), Tymoschuk, Valyaev (Nazarenko 61), Voronin (Shevchenko 55), Milevskiy.
Akiba hawakucheza: Bogush, Kucher, Rusol, Seleznyov.
Kadi: Mykhalyk.
Watazamaji: 87,548
Refa: Claus Bo Larsen (Denmark).

MATOKEO MECHI NYINGINE ZA KOMBE LA DUNIA HUKO ULAYA:
Andorra 0 Croatia 2
Austria 2 Romania 1
Bosnia-Herzegovina 2 Belgium 1
Bulgaria 2 Cyprus 0
Czech 1 Slovakia 2
Denmark 3 Albania 0
France 1 Lithuania 0
Greece 2 Israel 1
Holland 4 Macedonia 0
Italy 1 Republic of Ireland 1
Poland 10 San Marino 0
Scotland 2 Ireland 1
Turkey 1 Spain 2

Wednesday 1 April 2009

Alan Shearer Bosi mpya Newcastle!!!!

Klabu ya Newcastle ambayo iko nafasi ya tatu toka chini kwenye msimamo wa LIGI KUU England na hivyo kuwamo hatarini kuporomoka daraja imemtangaza Mchezaji wake Nyota wa zamani Alan Shearer kuwa ni Meneja mpya ili kuchukua nafasi ya Joe Kinnear ambae ni mgonjwa.
Newcastle imebakisha mechi nane kwenye LIGI KUU na mechi yao inayofuata na itakayokuwa ya kwanza chini ya Alan Shearer ni Jumamosi dhidi ya Chelsea.

Mido akwaruzana na Zaki!!!

Wachezaji wa Misri, Mido na Zaki, ambao wote wako Klabu moja ya LIGI KUU England, Wigan, wamefarakana wakati wote wakiwa kwenye Timu yao ya Taifa, Misri, ambayo wikiendi iliyopita ilitoka sare 1-1 na Zambia kwenye mechi ya kuwania nafasi Fainali Kombe la Dunia 2010.
Mido ambae alikuwa benchi mechi hiyo amedai Zaki, aliecheza mechi hiyo na kuumia, ametangaza uongo kuwa Kocha wa Misri Hassan Shehata hakumpanga Mido kwa kuwa amegombana nae.
Taarifa hizo zimemuudhi sana Mido na ameibukia vyombo vya habari akimshutumu vikali Zaki

Monday 30 March 2009

Drogba asema walikuwa hawajui chochote kuhusu maafa mechi ilipokuwa ikichezwa!!!

Nahodha wa Timu ya Taifa ya Ivory Coast, Didier Drogba, amesema walikuwa hawajui kabisa kama kuna maafa wakati wakicheza mechi waliyowafunga Malawi 5-0 kwenye mchujo wa Kombe la Dunia 2010 Uwanjani kwao Houphouet-Boigny.
Watu 19 wanaaminika wamekufa huku zaidi ya 139 kujeruhiwa baada ya Mashabiki wasiokuwa na tiketi kuvamia na kutaka kuingia bure kupambana na Polisi waliofyatua mabomu ya machozi na kusababisha ukuta kuanguka.
Drogba alisema: 'Inasikitisha! Huwezi kuelewa!! Soka sio kitu chochote!! Tunazungumzia vifo vya watu 19!! Ikitokea kitu kama hiki ndio unajua jinsi watu walivyo na moyo na Nchi yao na Timu yao!!'
Kikosi kizima cha Ivory Coast, wakiwemo akina Salomon Kalou, Kolo Toure, Emmanuel Eboue, Didier Zokora, Ndri Romaric na Bakari Kone, wakibubujikwa machozi wameahidi kuifikisha Nchi yao Fainali Kombe la Dunia huko Afrika Kusini 2010 kama heshima kwa waliopoteza maisha yao.
Nae Rais wa FIFA, Sepp Blatter, aliehuzunika sana, ametuma rambirambi kwa kutamka: 'Naomba nitume huzuni, majonzi na rambirambi zangu kwa jamii ya soka ya Ivory Coast, na muhimu kwa familia, marafiki na wapendwa wote wa watu waliopoteza maisha.'

Rooney Mchezaji Bora England 2008!!!!

Wayne Rooney wa Manchester United amechaguliwa na mashabiki kuwa ndie MCHEZAJI BORA WA ENGLAND 2008 baada ya kura iliyofanyika kwenye tovuti rasmi ya FA, Chama cha Soka cha England, huku Gareth Barry akishika nafasi ya pili.
Mwaka 2008, Rooney aliichezea England mechi 8 kati ya 10 walizocheza na kufunga bao 5.
Gareth Barry alikuwa ndie Mchezaji pekee wa England aliecheza mechi zote hizo 10.
Washindi waliopita wa Tuzo hii ni:
2007-Steven Gerrard
2006-Owen Hargreaves
2005-Frank Lampard
2004-Frank Lampard
2003-David Beckham

Watazamaji wafa mechi ya Ivory Coast na Malawi!!

Katika mechi ya mchujo ya kuingia Fainali Kombe la Dunia 2010 iliyochezwa mjini Abidjan, Ivory Coast kati ya Ivory Coast iliyokuwa ikiongozwa na Didier Drogba, aliepachika bao 2, na Malawi ambapo wenyeji hao waliibuka na ushindi mnono wa mabao 5-0 lakini wamepata majonzi na huzuni kubwa pale Washabiki wao wapatao 19 walipofariki na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa.
Janga hilo lilitokea kabla mechi kuanza pale mashabiki wasiokuwa na tiketi walipotaka kuingia kwa nguvu huku Polisi wakifyatua mabomu ya machozi na ndipo ukuta ukaporomoka na kuleta maafa hayo.
Ingawa janga hilo lilitokea kabla ya mechi, pambano hilo halikuvunjwa na liliendelea kama ilivyopangwa.

MATOKEO MECHI ZA JUMAPILI
AFRIKA:
Mozambique 0 Nigeria o
Ghana 1 Benin o
MAREKANI YA KUSINI:
Ecuador 1 Brazil 1
Peru 1 Chile 3

MECHI ZENYE MVUTO ZA MAKUNDI YA ULAYA ZA MCHUJO WA KUINGIA FAINALI KOMBE LA DUNIA 2010
Jumatano Aprili 1
Denmark v Albania
England v Ukraine
France v Lithuania
Holland v Macedonia
Italy v Republic of Ireland
Turkey v Spain
Wales v Germany

Sunday 29 March 2009

MATOKEO MECHI ZA JANA MICHUJO YA KOMBE LA DUNIA 2010

ULAYA:
Abania 0 Hungary 1
Armenia 2 Estonia 2
Belgium 2 Bosnia-Hercegovina 4
Cyprus 2 Georgia 1
Germany 4 Liechtenstein 0
Holland 3 Scotland 0
Israel 1 Greece 1
Lithuania 0 France 1
Luxemborg 0 Latvia 4
Malta 0 Denmark 3
Moldova 0 Switzerland 2
Montenegro 0 Italy 2
Northern Ireland 3 Poland 2
Portugal 0 Sweden 0
Republic of Ireland 1 Bulgaria 1
Romania 2 Serbia 3
Russia 2 Azerbaijan 0
Slovenia 0 Czech Republic 0
Spain 1 Turkey 0
Wales 0 Finland 2
AFRIKA:
Rwanda 0 Algeria 0
Togo 1 Cameroun 0
Kenya 1 Tunisia 2
Burkina Faso 4 Guinea 2
Sudan 1 Mali 1
Morocco 1 Gabon 2
MAREKANI YA KUSINI:
Uruguay 2 Paraguay 0
Argentina 4 Venezuela 0
Colombia 2 Bolivia 0
MECHI ZA KIMATAIFA ZA KIRAFIKI:
England 4 Slovakia 0
South Africa 2 Norway 1
South Korea 2 Iraq 1
Powered By Blogger