Saturday 21 February 2009

Arsenal wabanwa mbavu!!! Bolton washinda!!

Arsenal wakiwa nyumbani Emirates na huku wakimchezesha staa kutoka Urusi, Andrei Arshavin kwa mara ya kwanza, walitoka suluhu ya 0-0 na Sunderland hii ikiwa ni mechi ya 3 mfululizo ya LIGI KUU wakitoka uwanjani bila kufunga goli.
Arsenal wanabaki nafasi ya 6 wakiwa pointi 5 nyuma ya Timu ya 5 Aston Villa.
Katika mechi nyingine zilizochezwa sambamba na hiyo ya Arsenal, Bolton waliwapiga West Ham 2-1, Middlesbrough v Wigan 0-0 na Stoke v Portsmouth iliisha bao 2-2.

Villa 0 Chelsea 1


Meneja wa Urusi, ambae sasa pia ni Meneja wa Chelsea hadi mwishoni mwa msimu Guus Hiddink, ameanza vyema kibarua chake baada ya Chelsea kuiengua Aston Villa kutoka nafasi ya 3 kwenye msimamo wa LIGI KUU walipoifunga bao 1-0 katika mechi iliyochezwa Villa Park nyumbani kwa Aston Villa.
Bao la ushindi la Chelsea liloifanya timu hiyo iwe na pointi 52 na kuchukua nafasi ya 3 na kuibwaga Aston Villa nyuma kushika nafasi ya 4 ikiwa na pointi 51 lilifungwa na Nicolas Anelka baada ya kupikiwa na Frank Lampard kwenye dakika ya 21.
Neville aongezewa mkataba mwaka mmoja

Nahodha na Veterani wa Manchester United, Garry Neville, ameongezewa mkataba wa mwaka mmoja na atabaki kwa Mabingwa hao hadi 2010.
Neville alianza kuchezea Man U tangu 1992 na kwa sasa ana umri wa miaka 34.

Kimbembe leo LIGI KUU England: Aston Villa v Chelsea!!

Timu zinazoshikilia nafasi ya tatu na ya nne kwenye msimamo wa LIGI KUU, Aston Villa na Chelsea, leo zinakutana Villa Park nyumbani kwa Aston Villa.
Aston Villa wako nafasi ya 3 wakiwa na pointi 51 na Chelsea wako nyuma yao tu wakiwa na pointi 49.
Kwenye mechi hii ya leo itakayochezeshwa na Refa Mark Halsey, Aston Villa huenda wakawakosa Wachezaji wao Emile Heskey na James Milner ambao wana maumivu.
Chelsea nao watamkosa Beki mahiri Ashley Cole ambae amefungiwa mechi hii kutokana na kuwa na Kadi.
Mechi hii ni kivutio kikubwa kwani Meneja wa Urusi Guus Hiddink alieteuliwa kuwa Meneja wa Chelsea hadi mwisho wa msimu ataiongoza Klabu hiyo kwa mara ya kwanza.

MECHI NYINGINE ZA LEO [Saa ni za bongo]:
Jumamosi Februari 21
[saa 9.45 mchana]
Aston Villa v Chelsea
[saa 12 jioni]
Arsenal v Sunderland
Bolton v West Ham
Middlesbrough v Wigan
Stoke v Portsmouth
[saa 2.30 usiku]
Man U v Blackburn

Friday 20 February 2009

UEFA CUP: Man City waambua droo huko Denmark, Tottenham wapigwa huko Ukraine!!!

Manchester City wameambulia sare ya 2-2 walipocheza na FC Copenhagen huko Denmark hapo jana na wenzao Tottenham walijikuta wakipigwa mabao mawili dakika 10 za mwisho walipokutana na Shakhtar Donetsk huko Ukraine.
Timu hizo zitarudiana Februari 26 na safari hii Man City na Tottenham watakuwa nyumbani.
Juzi Aston Villa akicheza kwake Villa Park alitoka suluhu 1-1 na CSKA Moscow na timu hizi zitarudiana huko Moscow tarehe 26 Februari.

KOMBE LA DUNIA SOUTH AFRICA 2010: Tiketi zaanza kuuzwa!!

Tiketi milioni 3 za kuingia kwenye mechi 64 za Fainali ya Kombe la Dunia litakalochezwa Juni 2010 huko Afrika Kusini zitaanza kuuzwa hivi karibuni na mchujo wa maombi ya ununuzi wa tiketi hizo utafanyika mwezi Aprili.
Tiketi za bei nafuu 120,000 zimetengwa kwa Wakazi wa Afrika Kusini na Mafundi 40,000 walioshiriki ujenzi wa Viwanja vitakavyochezewa mechi hizo wamepewa pasi za kuingia mechi bure.
Inategemewa Watu zaidi ya 400,000 watakwenda Afrika Kusini kushuhudia Fainali hizo.

Thursday 19 February 2009

LIGI KUU England: Man U 3 Fulham 0
Ndani ya uwanja wao Old Trafford, Mabingwa Manchester United wamezidi kupaa na kuwaacha timu ya pili Liverpool pointi 5 nyuma baada ya jana kushinda mechi yao ya kiporo walipoifunga Fulham mabao 3-0.
Mabao hayo yalifungwa na Paul Scholes, Dimitar Berbatov na Wayne Rooney.

MECHI ZIJAZO ZA LIGI KUU:

Jumamosi Februari 21
Arsenal v Sunderland
Aston Villa v Chelsea
Bolton v West Ham
Man U v Blackburn
Middlesbrough v Wigan
Stoke v Portsmouth
Jumapili Februari 22
Fulham v WBA
Liverpool v Man City
Newcastle v Everton
Jumatatu Februari 23
Hull City v Tottenham

Wednesday 18 February 2009

Ferguson ateta: 'Kwa kumfukuza Scolari, Chelsea wamejitia kitanzi!!'

Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, amedai hatua ya Chelsea kumfukuza Mbrazil Luiz Felipe Scolari na kumweka Guus Hiddink kama kiraka cha muda kunaisaidia sana Man U katika harakati zake za kutetea Ubingwa wake wa LIGI KUU England.
Ferguson amesema hakuamini jinsi Chelsea walivyochukua pupa ya kumtema mtu alieifanya Brazil kuwa Bingwa wa Kombe la Dunia na kuifikisha Portugal Fainali ya EURO 2004.
Ferguson alisisitiza hatua hiyo imeyaua matumaini ya Chelsea kutwaa Ubingwa wa LIGI KUU msimu huu na ikiwa Man U leo usiku watashinda mechi yao ya kiporo watakapocheza na Fulham Old Trafford watakuwa pointi 10 mbele ya Chelsea na pointi 5 mbele ya Liverpool timu ambayo iko nyuma tu ya Mabingwa hao.
'Niliamini siku zote ili kuwa mshindi kunahitaji utulivu na mipango ya muda mrefu ya Klabu,' Ferguson alisisitiza. 'Lakini, siku hizi, mara nyingi Klabu zikikumbwa na matatizo kidogo, busara hutupwa nje ya dirisha wakidhani Meneja mpya ataleta maajabu ya mafanikio ya haraka!!!'

Wenger akiri: 'Man U hawashikiki!!!'

Arsene Wenger, Meneja wa Arsenal timu iliyoselelea nafasi ya 5 kwenye LIGI KUU England, amekiri Man U ya sasa ni kiboko na hawakamatiki.
Wenger ameungama: 'Ingawa kwa sasa Arsenal tunachanja mbuga vizuri na tutapigana mpaka siku ya mwisho, ukweli ni kwamba Man U hawashikiki!! Wako pointi 12 mbele yetu na wakiwafunga Fulham watakuwa pointi 15 ikimaanisha inabidi wafungwe mechi 5 na sie tushinde 5 ili tuwakamate!!'

Tuesday 17 February 2009

LIGI KUU England: Kesho Man U v Fulham, Rooney ndani ya nyumba!

Mabingwa Manchester United kesho saa 5 usiku wanawakaribisha Fulham Old Trafford kucheza mechi yao ya kiporo ya LIGI KUU ambayo itawafanya wawe wamecheza mechi 25 ikiwa ni idadi sawa na timu nyingine.
Mechi hii ilikuwa ichezwe mwaka jana lakini ikaahirishwa kwa vile Man U walienda kucheza UEFA Super Cup walipopambana na Timu ya Urusi Zenit St Petersburg.
Mpaka sasa, Man U aliecheza mechi 24, anaongoza LIGI KUU kwa kuwa na pointi 56, Liverpool ni wa pili na amecheza mechi 25 na ana pointi 54, Aston Villa wa tatu pia mechi 25 pointi 51 huku akifuatiwa na Chelsea akiwa na pointi 49.
Arsenal ni wa 6 akiwa na pointi 44.
Man U wanategemea kumchezesha Mshambuliaji wao nyota Wayne Rooney ambae hajacheza mechi 7 sasa baada ya kuumia musuli ya nyuma ya paja.
Endapo Mabingwa hao watawafunga Fulham watakuwa mbele ya Timu ya pili Liverpool kwa pointi 5.

KOMBE LA FA: Eduardo arudi uwanjani kwa kishindo, Arsenal 4 Cardiff 0!!!

Mshambuliaji wa Arsenal, Eduardo kutoka Croatia ingawa ni mzaliwa wa Brazil, amerudi uwanjani kuichezea Arsenal kwenye mechi ya marudio Kombe la FA ya Raundi ya 4 mwaka mmoja tangu avunjike vibaya enka [tizama picha siku aliyoumizwa] na ameweza kupachika bao 2 katika ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Cardiff.

Timu hizi zilitoka sare ya 0-0 katika mechi ya kwanza iliyochezwa nyumbani kwa Cardiff, timu ya daraja la chini.

Mabao mengine ya Arsenal yalifungwa na Robbin van Persie na Bendtner.

Sasa Arsenal atapambana na Burnley kwenye Raundi ya 5 kwake Emirates Machi 7 au 8 na mshindi wa mechi hii atacheza na mshindi wa Sheffield United au Hull City kwenye Robo Fainali.

Sunday 15 February 2009

DROO YA ROBO FAINALI KOMBE LA FA: Mechi kuchezwa Tarehe 7 na 8 Machi 2009 [Timu inayotajwa kwanza iko nyumbani]

Vigogo watenganishwa!

Blackburn Rovers au Coventry City v Chelsea

Swansea City au Fulham v Manchester United

Cardiff City au Arsenal v Sheffield United au Hull City

Everton v West Ham United au Middlesbrough

KOMBE LA FA: Matokeo

Derby County 1 Man U 4

Everton 3 Aston Villa 1

Everton na Man United zimeingia Robo Fainali ya Kombe la FA baada ya kushinda mechi zao za Raundi ya 5 leo.
Everton alimfunga Aston Villa 3-1 wafungaji wakiwa Jack Rodwell, kijana wa miaka 17 aliepachika bao la kuongoza kwa Everton lakini Villa wakarudisha kwa penalti ya James Milner muda mfupi baadae.
Everton walipata bao la pili kwa penalti kupitia Mikel Arteta na Tim Cahill alipiga msumari wa mwisho kwa goli la tatu.
Manchester United wakicheza ugenini nyumbani kwa Derby County waliibuka na ushindi mzuri wa mabao 4-1.
Mabao ya Man U yalifungwa na Nani, Darron Gibson, Ronaldo na Danny Wellbeck. Bao la Derby lilipatikana kupitia Miles Addison.
LIGI KUU England: Portsmouth 2 Man City 0

Katika mechi ya kwanza baada ya kutimuliwa Meneja Tony Adams, Portsmouth imeweza kupata ushindi wake wa kwanza baada ya kucheza mechi 9 bila kushinda walipoifunga timu nyingine inayosuasua Man City kwa bao 2-0 kwenye mechi pekee ya LIGI KUU wikiendi hii.
Mabao hayo yote yalifungwa kipindi cha pili kupitia kwa Glen Johnson na Hermann Hreidarsson.

KOMBE LA FA:

Chelsea 3 Watford 1

Nicolas Anelka alifunga bao 3 mguuni kwake na kuiwezesha Chelsea kusonga Raundi ya 6 ya Kombe la FA walipowafunga Watford, Timu ya Daraja la chini, mabao 3-1 uwanjani kwao Stamford Bridge huku wakishuhudiwa na Meneja mpya Guus Hiddink aliekaa kwenye jukwaa la Watazamaji pamoja na Mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovich.
Chelsea wakiwa chini ya usimamizi wa Meneja Msaidizi Ray Wilkins kwa vile Guus Hiddink hajaanza kazi hiyo rasmi, walistushwa pale walipopachikwa bao na Priskin dakika ya 69 lakini mabao ya haraka ya Anelka kwenye dakika ya 75 na 77 na lile la 3 dakika ya 90 yaliwamaliza Watford.

Mechi nyingine zote za FA zilizochezwa jana zilimalizika suluhu kama ifuatavyo na timu hizi zitarudiana tarehe zinazoonyeshwa.

West Ham 1 Middlesbrough 1 [marudio Februari 24 huko Riverside nyumbani kwa Middlesbrough]

Sheffield United 1 Hull City 1 [marudio nyumbani kwa Hull Februari 26]

Swansea 1 Fulham 1 [marudio Craven Cottage nyumbani kwa Fulham Februari 24]
Powered By Blogger