Saturday 29 November 2008

ARSENAL WATHIBITISHA 'VIJISENTI' VYA KUNUNUA WACHEZAJI VIPO!!!!

Mwenyekiti wa Klabu ya Arsenal Peter Hill-Wood aliezuka hivi juzi kumtetea Meneja wake Arsenal amethibitisha Meneja huyo atapewa pesa ili kununua Wachezaji awatakao pindi dirisha la uhamisho litakapofunguka mwezi Januari.
Arsenal kwa sasa wako nafasi ya 5 kwenye msimamo wa ligi wakiwa nyuma ya vinara Chelsea, Liverpool, Manchester United na Aston Villa huku wakiwa nyuma ya Chelsea, timu ambayo wanacheza nayo kesho Jumapili, kwa pointi 10.
Wenger huwa anapenda kutafuta na kukuza chipukizi na ni nadra sana ananunua Wachezaji wa bei mbaya lakini Klabu hiyo haijatwaa Kombe lolote lile tangu 2005 na mashabiki wameshaanza shinikizo kwake ili aingie sokoni kutafuta Wachezaji bora.
Mwenyekiti Hill-Wood aliiambia Arsenal TV: 'Wenger atapewa pesa za kununua Wachezaji. Yeye ni mtulivu katika kununua Wachezaji na hawezi kununua tu ili mradi mashabiki au magazeti yanataka!'
Mwishoni mwa msimu uliokwisha Arsenal iliwapoteza Wachezaji Mathieu Flamini, Alexander Hleb, Gilberto Silva na Philippe Senderos (kwa mkopo) waliohama na Samir Nasri, Aaron Ramsey, Amaury Bischoff na Mikael Silvestre wakanunuliwa.

NEWCASTLE WAMWONGEZA MKATABA MENEJA JOE KINNEAR!!

Joe Kinnear amesaini mkataba wa kuendelea kuwa Meneja wa Newcastle hadi mwisho wa msimu huu.
Kinnear alitua Newcastle mwezi Septemba baada ya Kevin Keagan kubwaga manyanga na aliwekwa hapo kama mtu wa muda tu kwa mkataba wa mwezi hadi mwezi hadi klabu itakapouzwa lakini kumekuwa na ugumu mkubwa kupata mnunuzi.
Kabla ya kuja Newcastle, Joe Kinnear, alikuwa akifundisha Nottingham Forest hadi 2004 na tangu wakati huo mpaka Septemba 2008 alipotua Newcastle alikuwa hana kibarua chochote.

WINGA ZORAN TOSIC KUTUA MAN U JANUARI!!

Mabingwa wa Uingereza na Ulaya, Manchester United, wamefanikiwa kupata kibali cha kufanya kazi kwa Winga chipukizi wa Kimataifa wa Serbia Zoran Tosic [21] ambae ilibidi aombewe kibali hicho kwa sababu alikuwa hajacheza asilimia 70 ya mechi zilizochezwa na Timu ya Taifa ya Serbia za hivi karibuni.
Meneja wa Man U, Sir Alex Ferguson, aliongoza jopo la maofisa wengine wa Mabingwa hao kwenda kutoa utetezi kwenye Tume inayotoa vibali vya kazi mjini Sheffield na sasa Winga huyo anaechezea Klabu ya Serbia Patizan Belgrade yuko huru kujiunga na Man U ifikapo Januari wakati dirisha la uhamisho litakapofunguka.
Zoran Tosic, aliechezea Timu ya Taifa ya Serbia mara 12, atakuwa Mserbia wa pili kwenye timu ya Man U, mwingine akiwa Beki mahiri Nemanja Vidic.
MECHI ZA MIAMBA KESHO: Man City v Man U & Chelsea v Arsenal

Tambo na vita ya kisaikolijia vyatawala!!!

Leo kwenye LIGI KUU UINGEREZA kuna mechi 5 zinazochezwa lakini ni uhakika mkubwa kwamba macho ya washabiki wote wa soka la Uingereza pamoja na mioyo yao itakuwa kwenye mechi za kesho za miamba Chelsea watakapowakaribisha Arsenal Stamford Bridge na Manchester City atakapokuwa mwenyeji wa jirani zake wanaoishi maili 8 tu toka City of Manchester Stadium, Mabingwa wa LIGI KUU, Manchester United.
Tayari tambo, majigambo na kauli za kuwaumiza wapinzani kisaikolojia zishaanza kupeperushwa angani.
Wakati juzi nyota wa Man U Wayne Rooney alisema watawaonyesha Man City nani Wafalme wa Manchester, Meneja wa Man U, Sir Alex Ferguson amekaririwa akitamka Man City, mbali ya sasa kutangazwa ni Klabu tajiri duniani hasa baada ya kununuliwa na Koo ya Kifalme ya Abu Dhabi ambayo ni sehemu ya nchi tajiri sana duniani, Falme ya Nchi za Kiaarabu, si tishio na si lolote wala chochote na ndio maana wako nafasi ya 11 kwenye ligi.
Hata hivyo Sir Alex Ferguson amemsifia staa wa Man City Mbrazil Robinho ambae amesema ana kipaji cha hali ya juu.
Man U wanategemewa kumkaribisha tena Mshambuliaji Dimitar Berbatov aliekosa mechi mbili kwa kuwa na maumivu.
Mark Hughes, Meneja wa Man City, ambae aliwahi kuwa mchezaji chini ya Sir Alex Ferguson, amekiri mechi itakuwa ngumu kwani Man U ni timu bora.
Nae Meneja wa Chelsea Luis Felipe Scolari hakuikandya Arsenal na badala yake amesema hata Arsenal inaweza kuwa bingwa mbali ya kuwa pointi 10 nyuma ya wao Chelsea wanaoongoza ligi.
Scolari amedai bingwa wa ligi anapatika mwisho wa ligi na si sasa.
Bosi wa Arsenal Arsene Wenger ambae timu yake haina mwendo mzuri kwenye ligi amekaririwa akisema: 'Watu wameshatufuta kwenye ligi hii. Ni kweli huwezi kusema utachukua ubingwa wakati uko pointi 10 nyuma lakini unaweza kusema njia pekee ya kurudi kwenye kinyang'anyiro ni kuamini unaweza kuwa bingwa! Ndio maana tutaingia kwenye mechi Jumapili tukijiamini tunaweza kuwafunga! Hicho ni kitu pekee unataka wachezaji wako wafanye.'

Katika mechi hiyo Arsenal watapata nguvu kidogo hasa baada ya mastaa wao majeruhi Adebayor, Sagna na Samir Nasri kupona huku Chelsea watamkosa Mshambuliaji Didier Drogba alie kifungoni kwa mechi 3 pamoja na Beki Ricardo Carvalho, Essien na Belletti walio majeruhi.

MECHI ZA WIKIENDI HII:

Jumamosi, 29 Novemba 2008

[saa 12 jioni bongo taimu]

Aston Villa v Fulham

Middlesbrough v Newcastle

Stoke v Hull

Sunderland v Bolton

Wigan v West Brom

Jumapili, 30 Novemba 2008

Chelsea v Arsenal [saa 1 usiku]

Man City v Man U [saa 10 na nusu jioni]
[saa 12 jioni]

Portsmouth v Blackburn

Tottenham v Everton

Jumatatu, 1 Decemba 2008

Liverpool v West Ham [saa 5 usiku]

Friday 28 November 2008

PORTSMOUTH 2 AC MILAN 2

Portsmouth wakiongoza bao 2-0 hadi dakika ya 84 kwa mabao yaliyofungwa na Younes Kaboul na Kanu walijikuta wakiumwaga ushindi baada ya kumruhusu Ronaldinho, alieingia mwishoni kipindi cha pili, kufunga kwa frikiki na Inzaghi kuwaliza dakika ya mwisho ya mchezo.
UEFA CUP:

NEC NIJMEGEN 0 TOTTENHAM 1

Bao lililofungwa na Jamie O'Hara dakika ya 14 limewapa ushindi wa bao 1-0 Tottenham wakicheza ugenini Uholanzi dhidi ya NEC Nijmegen.
Bao hilo lilipatikana baada ya Mshambuliaji chipukizi Frazier Campbell ambae yuko Tottenham kwa mkopo akitokea Manchester United kuunganisha krosi ya Gareth Bale iliyogonga mwamba na kumaliziwa na O'Hara.

SCHALKE 04 0 MAN CITY 2

Magoli yaliyofungwa na Benjani Mwaruwaru, raia wa Zimbabwe, na Steven Ireland yamewapa ushindi wa mabao 2-0 Manchester City waliocheza ugenini na Schalke 04 ya Ujerumani.

Thursday 27 November 2008

MWENYEKITI WA ARSENAL AINGIA VITANI KUMTETEA WENGER!

Mwenyekiti wa Klabu ya Arsenal Peter Hill-Wood [kulia] ameziita taarifa kwamba wamepoteza imani kwa Meneja wao Arsene Wenger aliedumu miaka 12 sasa kuwa ni 'upumbavu'.
Kwa mara nyingine tena msimu huu Arsenal imeonekana dhaifu na kukosa uwezo wa kupigania Ubingwa wa LIGI KUU UINGEREZA kwani mpaka sasa baada ya kucheza mechi 14 imeshafungwa mechi 5 na Mapaparazi washaanza kushika bango kwamba ikiwa kikosi cha Wenger kisiposhinda Kombe lolote msimu huu basi mwanzo wa mwisho wa Mfaransa huyo umewadia.
Mara ya mwisho Arsenal kushinda LIGI KUU ilikuwa msimu wa 2003/04 ambao hawakufungwa hata mechi moja! Na Kombe lao la mwisho kuchukua ni la FA mwaka 2005 baada ya kutoka suluhu 0-0 na Man U na kushinda kwa penalti 5-4.
Lakini, Mwenyekiti wa Arsenal Peter Hill-Wood amezishambulia ripoti hizo na kusema Wenger amefanya mengi hapo na haiwezekani kamwe Bodi ya Wakurugenzi imgeuke.
'Ndio amefanya mengi sana na namuunga mkono.' Alisistiza Mwenyekiti huyo. 'Katika miaka 12 hapa amefanya kazi kubwa! Sasa tupo theluthi moja tu ya msimu na ndio tumepata matokeo matatu au manne mabaya. Ni upumbavu kuzungumzia yeye!'
Rooney awabeza Man City: 'SISI NDIO WAFALME WA MANCHESTER'

Wayne Rooney wa Manchester United [pichani kushoto] amewasha utambi kwa kuwabeza wapinzani wao wa jadi Manchester City kabla ya patashika yao ya Jumapili itakayochezwa City of Manchester Stadium nyumbani kwa Man City.
Rooney ametamba: 'Tutawaonyesha kwamba sisi ni Wafalme wa Manchester!'
Msimu uliokwisha Rooney hakucheza mechi zote mbili timu hizi zilipopambana kwani ya kwanza alikuwa kavunjika kidole na ya pili alikuwa kafungiwa mechi moja.
Mechi zote hizo mbili ziliisha kwa ushindi wa Man City.
Mpaka sasa msimu huu, Man U ambae ni Bingwa mtetezi wa LIGI KUU yuko nafasi ya 3 huku Man City akiwa wa 11 na akiwa pointi 4 tu juu ya timu 3 za mwisho kwenye msimamo wa ligi.
Man City hivi karibuni wamenunuliwa na Koo ya Kifalme kutoka Abu Dhabi ambayo ni sehemu ya Falme ya Nchi za Kiarabu, nchi ambayo ni moja ya nchi tajiri sana duniani, na matajiri hao walionyesha kucha zao pale walipomnyakua staa wa Brazil Robinho [pichani kulia] toka Klabu kiburi ya Real Madrid dakika za mwisho kabla dirisha la usajili halijafungwa mwishoni mwa mwezi Agosti kwa uhamisho wa Pauni milioni 32.5 ambayo ni rekodi kwa Uingereza.
Ingawa Man City wana staa Robinho akisaidiwa na Wabrazil wengine Jo na Elano ambao wote wapo Timu ya Taifa ya Brazil, mwendo wao kwenye LIGI KUU ni wa kusuasua na wa kutoridhisha ingawa mechi yao ya mwisho walicharuka pale walipoinyuka Arsenal mabao 3-0.
Ballack atamba kuua matumaini ya Arsenal kuwa Bingwa!

Wapinzani wa mjini London wanakutana Stamford Bridge Jumapili na ushindi kwa wenyeji Chelsea utawafanya waongoze LIGI KUU UINGEREZA huku wamewatupa Arsenal pointi 13 nyuma.
Chelsea walitoka sare ya 0-0 na Newcastle hapo kwao Stamford Bridge wiki iliyokwisha kwenye mechi ya LIGI KUU wakati Arsenal alikula kipigo chake cha pili mfululizo kwenye LIGI KUU aliposhindiliwa 3-0 na Manchester City mjini Manchester uwanjani City of Manchester.
Kabla ya kipigo hicho, Arsenal aliadhiriwa kwa mabao 2-0 mbele ya mashabiki wake nyumbani kwake Emirates Stadium alipofungwa na Aston Villa pia kwenye mechi ya LIGI KUU kikiwa ni kipigo chake cha 5 msimu huu ambao mpaka sasa washacheza mechi 14.
Arsenal kwa sasa wanaenda mrama hata nje ya uwanja kwa migogoro ambayo imesababisha Nahodha William Gallas avuliwe madaraka na kiungo kijana mdogo wa miaka 21 Cesc Fabregas apewe madaraka hayo huku mashabiki nje ya uwanja wakianza kunung'unika waziwazi kitu ambacho hakijatokea katika utawala wa Meneja Arsene Wenger wa miaka 12 sasa.
Michael Barrack, Mjerumani kiungo wa Chelsea ambae majuzi tu alitamka Ubingwa msimu huu ni vita kati ya timu yake Chelsea na Man U, ametamba: 'Kwa sasa tunaongoza ligi na wao Arsenal wako nyuma yetu pointi 10. Kwa sasa wao si timu ngumu na nzuri kwani wana matatizo makubwa! Nia yetu ni kuwafunga na kuwaacha kwa pointi 13. Kila mtu hapa Chelsea ana njaa ya Ubingwa na hii unaihisi kwenye mazoezi!'
WAFUNGAJI BORA LIGI KUU UINGEREZA:
Nicholas Anelka wa Chelsea ndie anaeongoza kwa kufunga mabao mengi LIGI KUU kwa kufunga mabao 12 na nafasi ya pili imeshikiliwa na Wachezaji watatu waliofunga mabao 8 kila mmoja. Wachezaji hao ni Mfungaji Bora msimu uliopita Cristiano Ronaldo wa Man U ambao ndio Mabingwa LIGI KUU, Robinho wa Man City na Amr Zaki, Mmisri anaechezea Wigan.
Nafasi ya tatu imeshikwa na Agbonlahor wa Aston Villa na Darren Bent wa Tottenham kwa mabao 7 kila mmoja.
Nafasi ya 4 ni ya Defoe [Portsmouth], Geovanni [Hull City] na Ireland [Man City] wenye mabao 6 kila mmoja.
Nafasi ya 5 imeshikwa na Wachezaji 6 wenye bao 5 kila mmoja yaani Adebayor [Arsenal], Carew [Aston Villa], Cisse [Sunderland], Crouch [Portsmouth], Fuller [Stoke] na Kuyt [Liverpool].
UEFA CUP: MECHI ZA LEO Alhamisi, 27 Novemba 2008

Leo timu 3 zilizoko LIGI KUU UINGEREZA zitajimwaga viwanja mbalimbali kugombea Kombe la UEFA.

Timu hizo ni Tottenham, Portsmouth na Manchester City ambazo zipo Makundi tofauti.

Portsmouth atakuwa nyumbani akicheza na AC Milan huku Tottenham na Manchester City watakuwa ugenini. Tottenham atacheza Uholanzi na Klabu ya NEC Nijmegen na Man City yuko Ujerumani kupambana na Schalke 04.

Braga v Wolfsburg,

Club Brugge v St Etienne,

CSKA Moscow v Lech Poznan,

Deportivo La Coruna v Feyenoord,

Dinamo Zagreb v Spartak Moscow,


Galatasaray v FC Metalist Kharkiv,

Hamburg v Ajax,

MSK Zilina v Slavia Prague,

NEC v Tottenham,

Olympiacos v Benfica,

Partizan Belgrade v Standard Liege,

Portsmouth v AC Milan,

PSG v Racing Santander,


Rosenborg Trondheim BK v Valencia,

Sampdoria v VfB Stuttgart,

Schalke 04 v Man City,
Liverpool asonga mbele, Chelsea bado asota!!!!

Timu 13 zishaingia Raundi ya Mtoano ya jumla ya Timu 16.

Tatu zilizobaki ni ama Panathinaikos au Anorthosis Famagusta na mbili kati ya Chelsea, AS Roma au Bordeaux!!!

Kufuatia mechi za jana za UEFA CHAMPIONS LEAGUE, Timu za Liverpool, Mabingwa wa Italia Inter Milan na Atletico Madrid ya Spain wameungana na Timu nyingine 10 kuingia Raundi nyingine ya Mtoano ya Kombe hilo linalotoa Klabu Bingwa Ulaya.
Raundi inayokuja ya Mtoano itakuwa na jumla ya Timu 16 na droo yake kuamua timu ipi inakutana na ipi itafanyika tarehe 19 Desemba 2008 na mechi zenyewe za Raundi hiyo zitachezwa tarehe 24 na 25 Februari 2009 na marudiano tarehe 10 na 11 Machi 2009 kwa mtindo wa nyumbani na ugenini huku timu zitazoshinda Raundi hiyo zitaingia Robo Fainali.
Mpaka sasa Timu zilizofuzu kuingia Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ni pamoja na hizo zilizofuzu jana, yaani Liverpool, Inter Milan, Atletico Madrid, zitakazojumuika na Mabingwa Watetezi wa Kombe hili, Manchester United pamoja na Villareal toka Kundi E, Barcelona na Sporting Lisbon kutoka Kundi C, Lyon na Bayern Munich Kundi F, Arsenal na FC Porto Kundi G na Juventus na Real Madrid Kundi H.
Timu nyingine 3 zitakazokamilisha idadi ya Timu 16 moja itatoka Kundi B ambako tayari Inter Milan kashafuzu ingawa jana alipigwa 1-0 nyumbani kwake na Panathinaikos.
Nafasi moja ya kusonga mbele na kujumuika na Inter Milan toka Kundi hili itaamuliwa katika mechi ya mwisho hapo tarehe 9 Desemba 2008 wakati Panathinaikos atacheza na Anorthosis Famagusta na mshindi ndie ataendelea.
Nafasi mbili za mwisho kukamilisha jumla ya Timu 16 ni za Timu za Kundi A ambamo kukiwa kumesalia mechi moja kwa kila Timu, AS Roma, ambae jana aliifunga CFR Cluj ya Romania mabao 3-1, anaongoza Kundi hili akiwa na pointi 9, Chelsea, ambae jana alitoka dro ya 1-1 na Bordeaux, ni wa pili akiwa na pointi 8 na Bordeaux wa tatu akiwa na pointi 7 huku CFR Cluj wa mwisho akiwa na pointi 4.
Katika mechi za mwisho, AS Roma anamkaribisha Bordeaux na Chelsea atakuwa nyumbani Stamford Bridge kupambana na CFR Cluj.

Wednesday 26 November 2008

MAREFA WATAKAOCHEZESHA MECHI ZA LIGI KUU WIKENDI HII WATAJWA

Refa Mike Dean anaeongoza kutembeza Kadi nyingi kuchezesha pambano la Chelsea na Arsenal!!

Marefa ambao watachezesha mechi za LIGI KUU UINGEREZA wikendi hii zikiwemo 'mechi kubwa' mbili yaani ile ya Chelsea v Arsenal na patashika ya wakazi wa mji mmoja wa Manchester, Manchester City v Manchester United, wametajwa.
Refa Mike Dean [pichani], ambae ndie anashika hatamu katika ile listi ya Marefa waliotoa Kadi nyingi msimu huu akiwa ametoa Kadi Nyekundu 5 na Njano 50 katika mechi 11 alizochezesha, atasimamia pambano la Chelsea na Arsenal huko Stamford Bridge litakalochezwa Jumapili tarehe 30 Novemba 2008.
Nae Refa ambae kwa sasa anasifika kuwa bora huko Uingereza, Howard Webb, ndie atakaechezesha patashika ya huko Manchester inayowakutanisha wakazi wa mji mmoja wa Manchester, Manchseter City itakapowakaribisha Mabingwa wa Uingereza, Manchester United, uwanjani kwake City of Manchester Stadium siku ya Jumapili tarehe 30 Novemba 2008.

Listi kamili ya Marefa na mechi watakazochesha wikendi hii ni:

Aston Villa v Fulham - Mike Jones

Middlesbrough v Newcastle United - Alan Wiley

Stoke City v Hull City - Keith Stroud

Sunderland v Bolton Wanderers - Chris Foy

Wigan Athletic v West Bromwich Albion - Phil Dowd

Chelsea v Arsenal - Mike Dean

Manchester City v Manchester United - Howard Webb

Portsmouth v Blackburn Rovers - Mark Halsey

Tottenham Hotspur v Everton - Steve Bennett

Liverpool v West Ham United - Pater Walton
LEO KIMBEMBE KWA Chelsea na Liverpool!

Baada ya Mabingwa wa Ulaya Manchester United na Arsenal jana kufuzu kusonga mbele na kuingia Raundi inayofuata ya UEFA Champions League, leo ni zamu ya Klabu nyingine za Uingereza, Chelsea na Liverpool, kucheza na kujihakikishia kusonga mbele.
Liverpool watajihakikishia nafasi ya kusonga mbele endapo watawafunga Marseille ya Ufaransa katika mechi inayochezwa leo usiku nyumbani kwake Anfield.
Lakini Liverpool vilevile anaweza kusonga mbele kwa droo ikiwa Atletico Madrid hatofungwa na PSV Eindhoven katika mechi nyingine ya Kundi lao Kundi D, mechi ambayo itachezwa kwenye Uwanja wa Atletico Madrid uitwao Vicente Calderon ambao Watazamaji leo hawaruhusiwi kuingia kutokana na Atletico Madrid kuadhibiwa na UEFA.
Nao Chelsea, ingawa wanaongoza Kundi A lakini wako kwenye wakati mgumu kufuatia kipigo chao kwenye Kundi hili kwenye mechi yao ya mwisho walipobamizwa 3-1 na AS Roma.
Leo Chelsea wanasafiri hadi Ufaransa kupambana na Bordeaux timu ambayo waliichabanga mabao 4-0 katika mechi yao ya kwanza iliyochezwa Stamford Bridge.
Chelsea atasonga mbele tu endapo atashinda leo. Matokeo yoyote mengine yatawafanya wasote na itawalazimu washinde mechi yao ya mwisho dhidi ya Klabu ya Romania CFR Cluj.
Bordeaux kwa sasa wako pointi moja nyuma ya Chelsea na wamefungana na AS Roma ambao leo wako safarini kuelekea Romania kupambana na CFR Cluj timu ambayo iliwashangaza wengi pale ilipowafunga Roma mabao 2-1 nyumbani kwao!
Mechi nyingine zenye mvuto ni zile za Kundi B ambalo timu zake zote 4 zina nafasi ya kusonga mbele.
Inter Milan, Timu inayoongozwa na Jose Mourinho, Meneja wa zamani wa Chelsea, inaongoza Kundi hili na leo wanahitaji sare tu katika mechi yao dhidi ya Panathinaikos, mechi inayochezwa Milan.
Klabu ya Cyprus, Anorthosis Famagusta, ambayo ilitoka droo ya 3-3 na Inter Milan, inashika nafasi ya pili na itafuzu kusonga mbele endapo leo watawafunga Werder Bremen ya Ujerumani na Panathinaikos wafungwe na Inter Milan.
Katika Kundi C, Barcelona na Sporting Lisbon, wote washafuzu kusonga mbele na kinachogombewa kwa sasa ni nani atakuwa wa kwanza kwenye Kundi hili kitu ambacho kinaweza kuamuliwa leo wakati Sporting Lisbon watakapowakaribisha Barcelona leo usiku.
Mechi nyingine ya Kundi hili ni kati ya Shakhtar Donetsk na Basle ambayo itaamua nani ni mshindi wa tatu na hivyo kucheza UEFA CUP.
Ferguson: 'Rooney ameniomba radhi kwa kudanganya kaangushwa ndani ya boksi!'

Meneja wa Mabingwa wa Ulaya Manchester United Sir Alex Ferguson amesema Mchezaji wake Wayne Rooney alimtaka radhi kwa kugushi kachezewa rafu ndani ya penalti boksi na kujiangusha ili apate penalti katika mechi ambayo timu yake ilitoka suluhu 0-0 na Villareal jana kwanye mechi ya UEFA Champions League iliyochezwa uwanjani Estadio El Madrigal nchini Spain.
'Ameniomba radhi na kusema hakukusudia.' Ferguson alisema. 'Nadhani alikuwa amemtizama sana Robert Pires [mchezaji wa zamani wa Arsenal na sasa yuko Villareal]. Lakini, yeye ameomba radhi na huyo Pires hana hata haya, haombi radhi!'
Ferguson vilevile alizungumzia kuhusu rafu mfululizo anazofanyiwa Cristiano Ronaldo.
Alitamka: 'Ni mbinu za timu pinzani kumzuia mchezaji bora. Lakini Refa wa jana kutoka Italia Roberto Rosetti alikuwa mzuri na mkali kwa timu zote!'
Refa Roberto Rosetti alimpa Kadi Nyekundu Mchezaji wa Villareal Joan Capdevila na kumtoa nje kwa kumshindilia Ronaldo njumu juu ya goti zilizoacha alama pajani.

Wenger akiri ushindi finyu umewapa ahueni!!

Arsene Wenger amekiri ushindi finyu walioupata Arsenal jana ambao umewasaidia kufuzu kuingia Raundi inayofuata ya UEFA Champions League baada ya kuwachomeka Dynamo Kiev bao 1-0 unwanjani Emirates kwa bao la dakika ya 87 lililofungwa na Nicklas Bendtner umewapa ahueni kidogo kufuatia vipigo mfululizo kwenye LIGI KUU UINGEREZA hali iliyosababisha mtafaruku uliomfanya amtimue Nahodha wake William Gallas na kumpa Cesc Fabregas utepe huo.
Wenger alipumua kwa kusema: 'Ushindi huu umetutuliza kidogo! Gallas alicheza kwa moyo wote na Kepteni mpya Fabregas alihaha kila dakika!'

MATOKEO MECHI ZA JANA UEFA CHAMPIONS LEAGUE:


Group E:

AaB Aalborg 2-1 Celtic

Villarreal 0-0 Man Utd

Group F:

Bayern Munich 3-0 Steaua Bucharest

Fiorentina 1-2 Lyon

Group G:

Arsenal 1-0 Dynamo Kiev

Fenerbahce 1-2 FC Porto

Group H:

BATE Borisov 0-1 Real Madrid

Zenit St Petersburg 0-0 Juventus

Arsenal na Manchester United wasonga mbele kwenda Raundi nyingine!!

Timu za Arsenal na Manchester United zimefanikiwa kusonga mbele kutoka kwenye makundi yao huku bado wakiwa na mechi moja mkononi.
Arsenal aliifunga Dynamo Kiev uwanjani kwake Emirates kwa bao 1-0, bao lililofungwa na Nicklas Bendtner kwenye dakika ya 87.

Manchester United walitoka suluhu ya 0-0 na Villareal ugenini huko Spain na hivyo kujihakikishia wanasonga mbele pamoja na Villareal.

Timu nyingine ambazo tayari zimefuzu kuingia raundi inayofuata ni pamoja na Real Madrid, Juventus, FC Porto, Lyon na Bayern Munich.

MECHI ZA LEO: Jumatano, 26 Novemba 2008 [saa 4 dak 45 usiku]

Anorthosis Famagusta v Werder Bremen,

Atletico Madrid v PSV,

Bordeaux v Chelsea

CFR 1907 Cluj-Napoca v Roma,

Inter Milan v Panathinaikos,

Liverpool v Marseille,

Shakhtar Donetsk v Basle,

Sporting v Barcelona,

Tuesday 25 November 2008

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: MECHI ZA LEO

Group E:

AaB Aalborg v Celtic

Villarreal v Man Utd

Group F:

Bayern Munich v Steaua Bucharest

Fiorentina v Lyon

Group G:

Arsenal v Dynamo Kiev

Fenerbahce v FC Porto

Group H:

BATE Borisov v Real Madrid

Zenit St Petersburg 0-0 Juventus

[MECHI IMEANZA SAA 2 NA NUSU USIKU NA MPAKA SASA 0-0]

UEFA CHAMPIONS LEAGUE:


Villareal v Manchester United

Mabingwa watetezi Man U leo usiku wanashuka uwanjani Estadio El Madrigal kupambana na wenyeji wao Villareal katika mechi ya KUNDI E ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
Kipa nambari wani wa Mabingwa hao, Edwin Van der Sar, ameachwa kwa kile Meneja Sir Alex Ferguson amekiita kumpumzisha na kutoa nafasi kwa Makipa wengine yaani Ben Foster au Kuszczak.
Man U na Villareal, ambao wote wana pointi 8, wanahitaji pointi moja tu ili kusonga mbele.
Leo Man U watakutana na Mchezaji wao wa zamani Mtaliana Giuseppe Rossi ambae kwa sasa ni Mshambuliaji wa kutumainiwa wa Villareal.
Mechi nyingine katika Kundi hili ambayo pia inachezwa leo ni kati ya Aalborg na Celtic. Timu hizi zina pointi 2 kila moja.
Kikosi cha Man U kilichosafiri kwenda huko Madrid, Spain ni:
Foster, Kuszczak, Rafael, O'Shea, Ferdinand, Vidic, Evans, Evra, Ronaldo, Park, Anderson, Fletcher, Carrick, Giggs, Nani, Rooney, Tevez, Possebon, Gibson, Manucho.

Arsenal v Dynamo Kiev

Baada ya vipigo viwili mfululizo kwenye LIGI KUU UINGEREZA vya mabao 2-0 na Aston Villa na 3-0 na Man City, leo Arsenal wanaingia uwanjani kwao Emirates Stadium huku wakiwa na Kepteni mpya, Cesc Fabregas, kupambana na Dynamo Kiev katika mechi ya KUNDI G ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
Mechi nyingine katika Kundi hili inayochezwa leo ni kati ya Fenebahce v FC Porto.
Mpaka sasa katika Kundi hili, Arsenal anaongoza akiwa na pointi 8 akifuata FC Porto pointi 6, Dynamo Kiev pointi 5 na Fenerbahce pointi 2.
Timu ya Arsenal itatokana na Wachezaji:
Almunia, Hoyte, Gallas, Silvestre, Clichy, Ramsey, Fabregas, Denilson, Vela, Van Persie, Bendtner, Fabianski, Song, Djourou, Wilshere, Gibbs, Lansbury, Simpson.
Wigan wajinasua toka chini!

Wigan, wakicheza kwao JJB Stadium, wameipachika Everton 1-0 kupitia bao lilofungwa na Henri Camara na kujikwamua kutoka nn'gwe ya kushuka daraja na kuchupa hadi nafasi ya 15.
Camara, anaetoka Senegal, aliingizwa dakika ya 46 kumbadilisha Kapo, alifunga kwenye dakika ya 51 kufuatia pasi ya Luis Antonio Valencia.
Meneja wa Wigan, Steve Bruce [pichani], aliekuwa sentahafu wa Man U wakati Sir Alex Ferguson ni Meneja wa Man U, alizungumza baada ya mechi: 'Mara nyingine soka ni mchezo wa ajabu! Tumecheza vibaya na tumeshinda!'

Timu zilikuwa:

Wigan: Kirkland, Taylor, Bramble, Scharner, Figueroa, Valencia, Brown, Palacios, Cattermole, Kapo (Camara 46), Heskey.
Akiba [hawakucheza]:Pollitt, Kilbane, Koumas, De Ridder, Cywka, Routledge.
Goli: Camara 51.

Everton: Howard, Neville (Baines 85), Yobo, Jagielka, Lescott, Cahill, Fellaini, Arteta, Osman, Saha (Anichebe 65), Yakubu.
Akiba [hawakucheza]: Nash, Castillo, Rodwell, Jutkiewicz, Gosling.
Watazamaji: 18,344
Refa: Rob Styles

Monday 24 November 2008

Wenger amtetea Gallas!

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, amesimama kidete na kumtetea William Gallas, Mchezaji aliemvua madaraka ya Ukepteni wa timu hiyo, kwa kusema: 'Sijuti kumchagua Nahodha. Yeye aliyaweka matatizo yote ya timu moyoni mwake! Alifanya kazi ya Unahodha kwenye mazingira magumu ya kuandamwa na mapaparazi. Inafika hatua hatutaki presha ihujumu timu!'
Arsenal imemteua kijana Cesc Fabregas [21] kuwa Nahodha mpya wa timu [pichani kulia Fabregas na Gallas wakiwa mazoezini leo].
Wenger vilevile alikanusha madai ya magazeti kuwa dirisha la uhamisho likifunguliwa Januari basi Gallas atauzwa kwa kutamka: 'Ni maoni yao, siwezi kuyazuia. Namheshimu sana William kama mtu na mchezaji na uhusiano wetu hauyumbi kwa haya! Kwangu, yeye ni mchezaji thabiti kwa klabu. Hii inaweza kuwa mwanzo mpya kwake na kumfanya awe mchezaji bora zaidi!'
Wenger akaongeza: 'Kepteni ni sauti ya klabu nje. Lakini yeye ni mmoja tu wa viongozi ndani ya chumba cha kubadilisha jezi wachezaji. Siamini hata chembe Nahodha pekee ndio mtu pekee wa kuongoza Wachezaji!'
Wenger alimalizia kwa kugusia Arsenal inavyoyumba uwanjani: 'Kwa Waandishi Habari, kila kitu ni ama balaa au bora! Hawajui ukweli huwa katikati! Si kila kitu ni kiama na mateso tu! Hii ni nafasi nzuri kwetu kuonyesha tunaijali, kuipenda klabu na kudhihirisha uwezo wetu!'
RONALDO APAA KWENDA EL MADRIGAL!

Mchezaji Bora Uingereza, Ulaya na kwa Wachezaji wa Kulipwa, Cristiano Ronaldo, amepaa pamoja na kikosi cha Manchester United kwenda Madrid, Spain kupambana na Villareal kwenye mechi ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE uwanjani El Madrigal.

Ronaldo aliumizwa Jumamosi Man U ilipocheza na Aston Villa kwenye mechi ya LIGI KUU ambayo iliisha suluhu ya 0-0.

Katika mechi yote hiyo Ronaldo alionekana anawindwa na Aston Villa waliokuwa wakitumia miguvu, rafu na kila staili ya mchezo wa raga ili kumsimamisha.

Ilibidi Ronaldo apumzishwe kipindi cha pili cha mechi hiyo na baadae Meneja wa Man U Sir Alex Ferguson aligusa kwamba huenda Ronaldo asiwemo kwenye kikosi kitakachoenda Spain.

Wachezaji ambao hawamo kwenye kikosi kilichosafiri ni Kipa Edwin Van der Sar [ anaepumzishwa], Dimitar Berbatov, Wes Brown, Gary Neville, chipukizi Danny Welbeck, Paul Scholes na Owen Hargreaves [ambao wote ni majeruhi].

Man U na Villareal wote wana pointi 8 ingawa Man U inaongoza KUNDI hili kwa magoli.

Kila timu inahitaji pointi moja tu kuhakikisha iinaingia raundi inayofuata.
FABREGAS NAHODHA MPYA ARSENAL!

Kijana mdogo wa miaka 21, raia wa Spain, Cesc Fabregas, anaechezea kama kiungo, leo ametangazwa kuwa ndie Nahodha mpya wa Klabu ya Arsenal kuchukua nafasi ya William Gallas alievuliwa cheo hicho majuzi baada ya kubatuka hadharani kuhusu mpasuko ndani ya klabu.
Kufuatia kitendo hicho, Gallas alitemwa kwenye kikosi cha Arsenal kilichocheza LIGI KUU Jumamosi huko Manchester na Manchester City mechi ambayo Arsenal, ikiongozwa na Nahodha wa muda, Kipa Manuel Almunia, ilichabangwa mabao 3-0.
Uteuzi wa Fabregas umethibitishwa na Meneja Arsene Wenger alietamka: 'Fabregas ndie Nahodha wa kudumu. Sina haja ya kueleza kwa nini!'
Akaongeza: 'Gallas atacheza mechi ya kesho ila Kepteni ni Fabregas. Nimetoa uamuzi huu.'
Alipobanwa na kuhojiwa kama alifanya makosa kwa kumteua Gallas kama Nahodha, Wenger alisema: 'Hapana, sijutii kumfanya yeye Kepteni.'
FIFA CLUB WORLD CUP JAPAN 2008 & FIFA CONFEDERATIONS CUP SOUTH AFRICA 2009:

Wadau wengi wa Soka wanasubiri kwa hamu mashindano makubwa ya kandanda yanayoandaliwa na FIFA ambayo yanakuja hivi karibuni.
Mwezi ujao, Desemba 2008, huko Japan, Klabu Bingwa za Mabara mbalimbali hapa duniani watajimwaga kuwania Ubingwa wa Klabu Duniani ambao rasmi unaitwa FIFA Club World Cup Japan 2008. Mashindano haya yatafunguliwa rasmi Desemba 11 huko Uwanja wa Taifa mjini Tokyo, Japan na Fainali itachezwa Uwanja wa Kimataifa wa Yokohama mjini Yokohama, Japan tarehe 21 Desemba 2008.
Mwakani, mwezi Juni, huko Afrika Kusini, ambao ndio wenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2010, watakuwa wenyeji wa Kombe la Mabara ambalo rasmi hujulikana kama FIFA Confederations Cup South Africa 2009 ambalo hushindaniwa na Timu za Taifa ambazo ni Bingwa wa Mabara. Kawaida Kombe hili huchezwa kwa mwenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia zinazofuatia ikiwa kama ni fungua pazia na vilevile kutesti maandalizi ya Fainali za Kombe la Dunia.

Kwenye FIFA Club World Cup Japan 2008, Klabu zitakazocheza ni:

-Klabu Bingwa ya Asia: Gamba Osaka kutoka Japan

-Klabu Bingwa ya Afrika: Al Ahly ya Misri

-Klabu Bingwa ya Marekani ya Kati: Pachuca toka Mexico

-Klabu Bingwa ya Marekani ya Kusini: Liga de Quito toka Ecuador

-Klabu Bingwa ya Nchi za Baharini: Waitakere United toka New Zealand

-Klabu Bingwa ya Ulaya: Manchester United toka Uingereza

-Mshindi wa Pili wa Klabu Bingwa ya Asia: Adelaide United toka Australia [Timu hii imeingizwa kwa sababu Klabu Bingwa ya Asia inatoka Japan ambao ndio wenyeji wa mashindano].

Kwenye FIFA Confederations Cup South Africa 2009, nchi zitakazoshiriki zimegawanywa makundi mawili kama ifuatavyo:

KUNDI A

-South Africa [Mwenyeji]

-Iraq [Bingwa wa Asia]

-New Zealand [Bingwa wa Nchi za Bahari]

-Spain [Bingwa wa Ulaya]

KUNDI B

-USA [Bingwa wa Marekani ya Kaskazini]

-Italy [Bingwa wa Dunia]

-Brazil [Bingwa wa Marekani ya Kusini]

-Egypt [Bingwa wa Afrika]

RATIBA YA FIFA CLUB WORLD CUP JAPAN 2008:

-11 Desemba 2008: MECHI YA 1: Adelaide United v Waitakere United

-13 Desemba 2008: MECHI YA 2: Al Ahly v Pachuca

-14 Desemba 2008: MECHI YA 3: MSHINDI MECHI YA 1 v Gamba Osaka

-17 Desemba 2008: MECHI YA 4: MSHINDI MECHI YA 2 v Liga de Quito

-18 Desemba 2008:
MECHI YA 5: MSHINDI MECHI YA 3 v Manchester United

-21 Desemba 2008: FAINALI: MSHINDI MECHI YA 4 v MSHINDI MECHI YA 5

RATIBA YA FIFA CONFEDERATIONS CUP SOUTH AFRICA 2009:

-14 Juni 2009: KUNDI A: South Africa v Iraq

-14 Juni 2009: KUNDI B: Brazil v Egypt
[RATIBA KAMILI TUTAITOA BAADAE]
MECHI YA LEO YA LIGI KUU 24 Novemba 2008:
Wigan v Everton
Uwanja: JJB Saa: 5 usiku bongo taimu


Kufuatia mechi zilizochezwa wikiendi hii iliyopita, hakuna hata timu moja kati ya timu zilizoko kwenye nusu ya juu katika msimamo wa LIGI KUU iliyoshinda na leo usiku Everton ambao wako nafasi ya 7 kwenye msimamo wa ligi wanashuka uwanjani ugenini kucheza na Wigan ambao wanashikilia nafasi ya 18 ikiwa ni tinu ya tatu toka chini.
Wigan wameshinda mechi moja tu ya ligi kati ya 7 walizocheza mwisho huku Everton hawajafungwa katika mechi 5 zilizopita.
Timu zitatokana na Wachezaji wafuatao:
Wigan:
Kirkland, Pollitt, Melchiot, Bramble, Scharner, Figueroa, Taylor, Kilbane, De Ridder, Valencia, Palacios, Brown, Cattermole, Koumas, Kapo, Heskey, Zaki, Camara, Cywka, Kupisz, Routledge.
Everton: Howard, Neville, Yobo, Jagielka, Lescott, Arteta, Cahill, Rodwell, Vaughan, Pienaar, Fellaini, Osman, Yakubu, Saha, Hibbert, Anichebe, Baines, Nash, Castillo, Jutkiewicz, Gosling.
Refa: Rob Styles
BALLACK: 'Msimu huu Bingwa ni Chelsea au Man U'

Michael Ballack wa Chelsea amesisitiza Ubingwa wa LIGI KUU msimu huu ni vita kati ya Klabu yake na Mabingwa Watetezi Manchester United.
Ballack amewapuuza Liverpool ingawa ndio kwa sasa ni vinara wa pamoja na Chelsea kwenye msimamo wa ligi huku timu zote hizo zimefungana kwa kuwa na pointi 33 baada ya mechi 14 huku Man U wako nafasi ya tatu wakiwa na pointi 25 kwa mechi 13.
Timu zote hizo tatu za juu zilitoka sare ya 0-0 kwenye mechi zao za ligi za wikiendi hii iliyopita na kwa sasa Chelsea anaongoza ligi kwa tofauti ya magoli.
Ballack ametamka:'Kila mtu anazungumzia juu ya Vigogo wanne wa ligi yaani Chelsea, Liverpool, Man U na Arsenal lakini kwa sasa Arsenal wamepoteza mwelekeo na wako nyuma sana! Liverpool wazuri lakini wao ni timu ya kucheza Ulaya tu kwenye LIGI YA MABINGWA YA UEFA kwa sababu wao mkazo wao ni mechi moja au mbili tu hawana ubavu wa kuhimili mechi nyingi! Ukitazama matokeo na vikosi vilivyopo Chelsea na Man U utajua timu hizo ndizo ngumu na ziko tafu kupita zote!'
Gallas huenda akarudishwa kikosini kwenye mechi ya kesho na Dynamo Kyiv

Aliekuwa Nahodha wa Arsenal, William Gallas, ambae alivuliwa Unahodha na kutemwa kwenye kikosi kilichoenda Manchester kupambana na Manchester City Jumamosi na hatimaye kupata kipigo cha 3-0 huko, huenda akarudi uwanjani kama Mchezaji wa kawaida kesho kwenye mechi ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE dhidi ya Dynamo Kyiv itakayochezwa Emirates Stadium.
Inaaminika utepe wa Nahodha utaenda kwa Kipa Manuel Almunia kama ilivyokuwa kwenye mechi ya juzi na Man City au huenda akapewa Beki wa pembeni Gael Clichy.
Gallas alipata adhabu hizo baada ya kutoboa siri za mgogoro ndani ya Arsenal hadharani kitendo ambacho kimeiudhi Klabu.
Baada ya kipigo cha Jumamosi huko Manchester, Meneja Arsene Wenger aligoma kuzungumzia ishu ya Gallas ingawa alidokeza bado anaamini Mchezaji huyo ana nafasi kubwa kuendelea kuchezea Arsenal.
Siku ya Jumapili, Gallas alijumuika na Wachezaji wengine wenzake wa kikosi cha kwanza katika mazoezi ya kujitayarisha na mechi ya Dynamo Kyiv.
MECHI ZA JANA LIGI KUU:

Tottenham 1 Blackburn 0

Jana Tottenham, ikicheza kwake White Hart Lane, ilijikwamua kutoka kwenye klabu tatu za chini katika msimamo wa ligi baada ya kuifunga Blackburn Rovers bao 1-0 katika mechi ambayo Beki wa pembeni kushoto Martin OLsson alitolewa nje kwenye dakika ya 39 baada ya kulambwa Kadi yake ya pili ya Njano na Refa Howard Webb.
Winga Aaron Lennon wa Tottenham ndie aliekuwa Mchezaji Bora wa mechi hii na alimtesa sana mkabaji wake Martin Olsson na alimudu kumpora mpira kwenye dakika ya 9 na kuingia nao ndani ya boksi kisha kupiga vii murua iliyounganishwa utamu na Mshambuliaji Mrusi Roman Pavlyuchenko na kutinga wavuni.
Winga Aaron Lennon aliendelea kumtesa Beki kutoka Sweden Martin Olsson na kumsababisha apewe Kadi ya Njano dakika ya 26 iliyofuatiwa na nyingine ya pili dakika ya 39 na hivyo kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.

Tottenham: Gomes, Corluka, Woodgate, King, Assou-Ekotto, Bentley (O'Hara 86), Jenas, Huddlestone, Lennon, Pavlyuchenko (Campbell 74), Bent.
Akiba [Hawakucheza]: Cesar, Bale, Zokora, Gunter, Dawson.
Kadi: Bentley, Jenas.
Goli: Pavlyuchenko

Blackburn: Robinson, Ooijer, Samba, Nelsen, Olsson, Emerton (Derbyshire 71), Andrews, Mokoena, Pedersen (Treacy 81), McCarthy (Simpson 46), Roque Santa Cruz.
Akiba [hawakucheza]: Brown, Kerimoglu, Fowler, Roberts.
Kadi Nyekundu: Olsson
Kadi: Olsson, Ooijer, Andrews.
Watazamaji: 35,903
Refa: Howard Webb

Sunderland 0 West Ham 1

Goli lililofungwa na Valon Behrami [pichani wa kushoto] katika dakika ya 20 limewapa West Ham ushindi wao wa kwanza katika mechi 8 zilizopita.
Bao hio lilifungwa baada ya kumbabatiza Mchezaji wa Sunderland Kenwyne Jones na kumchuuza Kipa Marton Fulop.
Sunderland , wakiwa nyumbani Stadium of Light, walicheza chini ya kiwango na kukosa nafasi kadhaa za dhahiri kupitia kwa Mshambuliaji wao wa Kifaransa Djibril Cisse.
Na ili kudhihirisha haikuwa siku yao hata Refa Mike Dean aliwanyima penalti za wazi pale Washambuliaji wao Djibril Cisse na Kenwyne Jones walipoangushwa ndani ya boksi.
Kipigo hiki ni cha 4 kwa timu ya Sunderland inayoongozwa na Meneja Roy Keane wakiwa nyumbani kwao msimu huu na cha 3 mfululizo.

Sunderland: Fulop, Bardsley, Nosworthy, Ferdinand, Collins, Malbranque (Edwards 66), Whitehead, Reid (Murphy 66), Richardson, Jones (Diouf 81), Cisse.
Akiba [hawakucheza]: Colgan, Tainio, Colback, Henderson.
Kadi: Reid, Bardsley.

West Ham: Green, Neill, Collins, Upson, Ilunga, Faubert (Boa Morte 76), Parker, Bowyer (Mullins 61), Behrami, Bellamy (Di Michele 87), Cole.
Akiba [hawakucheza]: Lastuvka, Davenport, Collison, Sears.
Kadi: Bowyer.
Goli: Behrami 20.
Watazamaji: 35,222.
Refa: Mike Dean

Sunday 23 November 2008

Baada ya patashika LIGI KUU jana, wasemavyo Mameneja:

Kufuatia kipigo cha 3-0 mikononi mwa Man City, Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, atamka: 'Ni ushindi unaowakweza Man City. Kisaikolojia timu yangu haikuwa na tatizo kwani tulipigana sana. Tulikosa ukomavu wa kutawala mchezo. Sidhani Man City walitengeneza nafasi nyingi. Nadhani tulitawala mchezo. Hatuna sababu ya kuhamanika ingawa tumefungwa. Tutabadilika!'
Alipobanwa kuhusu utata wa Nahodha wake Gallas alietimuliwa, Wenger alifoka: ' Kwa nini tutoe stetimenti? Tunaweza tukawa na Nahodha na tukambadili bila ya kuvalia njuga suala hilo. Tushawahi kuwa na matatizo. Lakini daima tuna nguvu ya kukabiliana na kila kitu na safari hii tutakabiliana kwa nguvu tena!'

Nae Mark Hughes wa Man City alisema: 'Nadhani ni mara ya pili tunawafunga Arsenal kwenye LIGI KUU kwa hiyo ni ushindi mzuri! Tulikuwa na plani kwa mechi hiyo na tulimudu kuvunja staili yao ya uchezaji. Ila nashangazwa na Wenger kwa kudai hatukustahili ushindi!'

Baada ya suluhu ya 0-0 na Newcastle kwenye ngome yao ya Stamford Bridge, Luis Felipe Scolari, Meneja wa Chelsea amenung'unika: ' Tumecheza asilimia 70 ya mechi upande wao wa kiwanja na kujaribu kufunga mara 10! Wao hawakujaribu chochote! Nani kashinda leo? Ni Newcastle kwani walikuja kutafuta suluhu na wamepata!'
Bosi wa Newcastle, Joe Kinnear, alijibu mapigo: 'Ni mafanikio mazuri na ni mechi tuliyocheza vizuri kupita zote! Kipa wetu Shay Givens alituokoa sana lakini pia kitimu tulifanikiwa. Sidhani Chelsea walitengeneza nafasi yoyote ya wazi ya kufunga! Tumetoka sare na Mabingwa Man U na sasa Chelsea, sidhani mambo ni mabaya!'

Baada ya kuzimwaga pointi mbili nyumbani Anfield, Bosi wa Liverpool, Rafa Benitez, alalama:' Ni siku mbaya, hatukuwa na nguvu na hatukucheza pasi vizuri! Tulipomaliza mechi na kurudi vyumbani, tukagundua Chelsea katoka dro na Arsenal kabamizwa! Matokeo hayo yangekuwa mazuri kwetu kama tungeshinda mechi hii!'

Baada ya mechi za wapinzani wake jana huku akisubiri timu yake Man U ishuke dimbani uwanjani Villa Park kupambana na timu ngumu ya Aston Villa ambayo wiki iliyopita iliikung'uta Arsenal mabao 2-0, Meneja Sir Alex Ferguson alipohojiwa alisema:'Baadhi ya matokeo ya leo yanashangaza lakini si mazuri kwetu endapo tutashindwa kupata pointi 3 leo! Hayo yanafanya mechi hii na Villa kuwa tamu sana!'
Baada ya mechi hiyo ambayo walitoka suluhu ya 0-0 na Aston Villa ambayo wameongeza pengo na Arsenal kuwa pointi 2 na kubaki nyuma ya Chelsea na Liverpool kwa pointi 8 ingawa wana mechi moja mkononi, Sir Alex Ferguson alisema: 'Nadhani tulikuwa timu bora katika mechi yote ukiondoa kipindi cha dakika 15 za kwanza baada ya mapumziko walipotusumbua kwa frikiki na kona. Nimefurahishwa na juhudi zetu dhidi ya timu iliyokuwa ikijihami kutetea maisha yao.'
"
Powered By Blogger