Saturday 11 October 2008

ENGLAND WAISHINDILIA KAZAKHSTAN 5-1

Timu ya Taifa ya Uingereza ndani ya Uwanja wa kwao Wembley mjini London wamewabamiza Kazakhstan mabao 5-1 katika mechi ya Kundi la 6 la Nchi za Ulaya kuwania nafasi za kuingia FAINALI KOMBE LA DUNIA AFRIKA KUSINI 2010.
Magoli ya England yalifungwa na Nahodha Rio Ferdinand dakika ya 52 na dakika ya 64 Kazakhstan walijifunga wenyewe kufanya gemu iwe 2-0 lakini kosa kubwa la Beki Ashley Cole wa England liliwapa zawadi Kazakhstan kupata bao.
Lakini kifaru Wayne Rooney akawapatia England mabao mawili katika dakika za 76 na 86.
Jermaine Defoe akamalizia bao la 5 kwenye dakika ya 90.
Aliechaguliwa nyota wa mechi ni Wayne Rooney ingawa kwa mashabiki wengi David Beckham alieingizwa kipindi cha pili ndie alikuwa nyota wao kwani walimshangilia kupita kifani.
Kwa mechi ya leo David Beckham amefikisha mechi 106 kuchezea Timu ya Taifa ya Uingereza sawa na Sir Bobby Charlton na wote kwa pamoja sasa wanashika nafasi ya tatu kwa kuichezea England mechi nyingi.
Nafasi ya kwanza inashikwa na Kipa Peter Shilton aliechezea mechi 125 na ya pili inashikwa na Bobby Moore aliekuwa Nahodha wa England pale waliponyakua Ubingwa wa Dunia mwaka 1966 kwa kucheza mechi 108.
VIWANJA MBALIMBALI DUNIANI LEO KUTIMUA VUMBI KUTAFUTA WATAKAOINGIA FAINALI KOMBE LA DUNIA AFRIKA KUSINI 2010

Wikiendi hii, yaani leo Jumamosi na kesho Jumapili, dunia nzima itakuwa kwenye harakati ya kutafuta Nchi zitakazoingia FAINALI KOMBE LA DUNIA AFRIKA KUSINI 2010.

Mechi hizi za wikiendi hii zitafuatiwa na mechi nyingine zitakazochezwa Jumatano.

Baadhi ya mechi za 'moto' zitazochezwa leo na kesho ni kama zifuatazo:

ULAYA: [LEO JUMAMOSI]

Bulgaria v Italy, [Kundi la 8, saa 3:15]

England v Kazakhstan, [Kundi la 6, saa 1:15]

Germany v Russia, [Kundi la 4, saa 3:45]

Romania v France, [Kundi la 7, saa 2:15]

Scotland v Norway, [Kundi la 9, saa 11:00]

Sweden v Portugal, [Kundi la 1, saa 3:00]

MAREKANI KUSINI:

Jumamosi 11 Oktoba 2008

Bolivia v Peru

Argentina v Uruguay

Colombia v Paraguay

Jumapili 12 Oktoba 2008

Venezuela v Brazil

Ecuador v Chile

AFRIKA: [LEO JUMAMOSI]

Tanzania v Cape Verde

Malawi v Congo DRC

Rwanda v Ethiopia

Namibia v Zimbabwe

Ivory Coast v Madagascar

Botswana v Mozambique

Ghana v Lesotho

Cameroon v Mauritius

Tunisia v Seychelles

Nigeria v Sierra Leone

Senegal v Gambia

Morocco v Mauritania

BOSI WA HULL CITY, PHIL BROWN, NDIE MENEJA BORA SEPTEMBA!!

Phil Brown, Meneja wa Hull City, timu iliyopanda daraja msimu huu kuingia LIGI KUU, ameshinda tuzo ya kuwa MENEJA BORA LIGI KUU UINGEREZA kwa mwezi wa Septemba.
Timu ya Phil Brown, Hull City ilianza mwezi Septemba kwa kuwafunga Newcastle 2-1, wakatoka suluhu ya 2-2 na Everton, kisha wakaonyesha maajabu makubwa pale walipowafunga vigogo Arsenal kwa bao 2-1 tena Arsenal wakiwa nyumbani kwao Emirates Stadium.
Jumapili iliyopita, Hull City waliendeleza wimbi la ushindi pale waliposhinda ugenini kwa bao 1-0 dhidi ya Tottenham.
Tuzo hii ya Meneja Bora wa Mwezi hutolewa na Wadhamini wa LIGI KUU BARCLAYS.
Mshindi huteuliwa na bodi yenye wawakilishi kutoka FA, Vyombo vya Habari na Mashabiki.

NAE ASHLEY YOUNG APATA TUZO YA MCHEZAJI BORA MWEZI SEPTEMBA

Winga wa Aston Villa Ashley Young ametuzwa kuwa MCHEZAJI BORA WA LIGI KUU kwa mwezi wa Septemba na hii ni mara yake ya pili kwa mwaka huu kwani msimu uliopita alipata tuzo hii mwezi Aprili.
Winga huyu mwenye miaka 23 alifunga mabao mawili na kuwatengenezea wenzake kufunga mabao mawili kwa mwezi Septemba na kuifanya Timu yake Aston Villa kushinda mechi 3 mfululizo kwa mwezi Septemba.
Ashley Young sasa ameingia orodha ya Wachezaji wachache waliomudu kushinda tuzo hii zaidi ya mara moja. Wengine walioko kwenye orodha hiyo ni Cristiano Ronaldo, Wayne Rooney na Steven Gerrard.

Friday 10 October 2008

CHELSEA WADAI MABILIONI MAHAKAMANI KUHUSU UHAMISHO WA MIKEL OBI

Klabu ya Chelsea imeishitaki Klabu ya FC Lyn Oslo ya Norway pamoja na aliekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Klabu hiyo Morgen Andersen kuhusu uhamisho wa Mchezaji Jon Mikel Obi wakidai warudishiwe Pauni Milioni 16 walizolipia uhamisho wake kwa sababu walidanganywa kuwa Mikel Obi alikuwa na mkataba na Klabu hiyo.
Mashtaka haya yanafuatia kupatikana na hatia kwa Mkurugenzi Mkuu huyo wa zamani wa Klabu hiyo ya Norway,Morgen Andersen, kwenye Mahakama ya Norway kwamba aligushi mikataba kuhusu Mchezaji huyo Jon Mikel Obi.
Mwezi Juni, 2006, Chelsea waliilipa Klabu ya FC Lyn Oslo Pauni Milioni 4 na Manchester United Pauni Milioni 12 kwa ajili ya uhamisho wa Mikel Obi. Wakati huo Jon Mikel Obi alikuwa tayari ameshasaini mkataba kujiunga na Manchester United ingawa baadae Obi aligoma kwenda Man U akidai mapenzi yake yako Chelsea na ndipo Man U wakalifikisha suala hilo FIFA na baadae Chelsea wakakubali kuilipa Man U.
Chelsea imetoa tamko rasmi kuhusu sakata hili kwa kusema: 'Wakati wa uhamisho wa Obi, Chelsea, Lyn na Man U tulikubaliana kulipia malipo ya Pauni Milioni 16 na kwamba huo ndio utakuwa mwisho wa sakata la Mchezaji Obi. Lakini, kwa sababu sasa Mahakama imedhihirisha kwamba kiongozi wa Klabu ya Lyn alidanganya basi sisi tunawadai wao pesa zetu!'
Chelsea ilimalizia tamko hili kwa kusema waziwazi mashtaka yao yanawahusu Klabu ya Lyn na Mkurugenzi Mkuu wao Morgan Andersen pekee na sio Manchester United.
NAHODHA WA ENGLAND JOHN TERRY HUENDA ASICHEZE JUMAMOSI!

Nahodha wa Timu ya Taifa John Terry huenda asicheze mechi ya Jumamosi dhidi ya Kazakhstan ya Kundi la 6 la Nchi za Ulaya ya mitoano ya Kombe la Dunia kuwania nafasi za kuingia Fainali zitazochezwa Afrika Kusini mwaka 2010 kwa sababu anaumwa mgongo.
John Terry hakufanya mazoezi ya Timu ya England hapo jana na nafasi yake kwenye mechi hiyo huenda ikachukuliwa na mmoja kati ya Matthew Upson, Wes Brown au Joleon Lescott.
Endapo hatocheza basi Unahodha wakati wa mechi utachukuliwa na Rio Ferdinand ambae ni Naibu Nahodha wa England.

FLETCHER ATEULIWA NAHODHA SCOTLAND

Nae Mchezaji mwenzake Rio Ferdinand kwenye Klabu ya Manchester United, Darren Fletcher ameteuliwa kuwa Nahodha wa Timu ya Taifa ya Scotland kwenye mechi ya Jumamosi dhidi ya Norway ya mitoano ya kuwania nafasi za kuingia Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwaka 2010.
Darren Fletcher amechukua nafasi ya Nahodha wa siku zote Barry Ferguson ambae ameumia enka na Naibu wake Stephen McManus amefungiwa mechi kwa kuwa na adhabu ya kadi.
Darren Fletcher, mwenye umri wa miaka 24, ni mara ya nne kuteuliwa kuwa Nahodha wa Nchi yake Scotland.

Thursday 9 October 2008


RIO AIPONDA FIFA KWA KUPUUZIA UBAGUZI WA RANGI VIWANJANI

Staa wa Manchester United na Naibu Nahodha wa Timu ya England, Rio Ferdinand, ameishutumu vikali FIFA kwa kutokuwa na msimamo thabiti wa kutokomeza ubaguzi wa rangi hasa kwenye mechi za soka.
Rio alisema FIFA imekuwa ikizipiga faini hafifu Nchi na Klabu zenye Mashabiki Wabaguzi lakini haiendi mbali zaidi kwa kuchukua hatua kali za kuwafungia au kupiga marufuku Wabaguzi kuingia michezoni.
Hivi karibuni Mchezaji wa England Emily Heskey aliletewa vituko vya kibaguzi huko Zagreb, Croatia wakati England ilipoifunga Croatia 4-1 kwenye mechi ya mtoano wa Kombe la Dunia na FIFA ikaipiga faini Croatia na kuipa onyo kali.
Vilevile huko Uingereza, kwenye Uwanja wa Fratton Park nyumbani kwa Portsmouth, Mchezaji Sol Campbell wa Portsmouth aliletewa vituko vya kibaguzi na Washabiki wa Tottenham kwenye mechi ya LIGI KUU ambayo Tottenham ilifungwa 2-0.
Sol Campbell aliwahi kuichezea Tottenham huko nyuma. Suala hili lipo kwenye uchunguzi wa Polisi.

Wednesday 8 October 2008


UEFA CUP: Portsmouth kukutana na AC Milan

Portsmouth wamepangiwa timu ngumu ya AC Milan kwenye Kombe la UEFA wakati Aston Villa, Tottenham na Manchester City nao watakuwa na wapinzani wazito.
Aston Villa watacheza na Ajax na Hamburg wakati Tottenham watakabiliwa na Spartak Moscow na Udinese.
Lakini Manchester City, ambao watacheza na Schalke O4, Paris St Germain, Racing Santander na Timu ya Bosi wa zamani wa England Steve McClaren, FC Twente, ndio wenye mtihani mgumu zaidi.
Kila timu iko kwenye Kundi la Timu 5 na watacheza mechi 2 nyumbani na 2 ugenini na wapinzani tofauti.
Timu 3 toka kila Kundi zitasonga mbele.
Fainali ya UEFA CUP itafanyika mjini Istanbull, Uturuki tarehe 20 Mei 2009.

KUNDI A: Schalke 04 Paris St Germain MANCHESTER CITY Racing Santander FC Twente

KUNDI B: Benfica Olympiakos Galatasaray Hertha Berlin Metalist Kharkiv

KUNDI C: Sevilla Stuttgart Sampdoria Partizan Belgrade Standard Liege

KUNDI D: TOTTENHAM Spartak Moscow Udinese Dinamo Zagreb NEC Nijmegen

KUNDI E: AC Milan Heerenveen SC Braga PORTSMOUTH Vfl Wolfsburg

KUNDI F: Hamburg Ajax Slavia Prague ASTON VILLA MSK Zilina

KUNDI G: Valencia Club Brugge Rosenborg FC Copenhagen Saint-Etienne

KUNDI H: CSKA Moscow Deportiva La Coruna Feyenoord Nancy Lech Poznan

Monday 6 October 2008

KWA MAPENZI YA EVERTON, AMPACHIKA BINTI YAKE KICHANGA JINA EVA-TONI-ANN: ukilitamka unamaanisha wewe ni shabiki wa kutupwa wa EVERTON!!!

Kabinti kachanga kilichozaliwa ndani ya Familia ya Mashabiki wenda wazimu wa Klabu ya Everton iliopo jijini Liverpool huko Uingereza kilijikuta kikibatizwa majina matatu yaliyounganishwa yaani EVA-TONI-ANN na ukiyatamka basi unakuwa unataja EVERTONIAN na hiyo inamaanisha wewe ni Shabiki wa kutupwa wa Klabu ya Everton!
Baba mtoto huyo EVA-TONI-ANN aitwae Danny Pierce amesema hiyo ilikuwa ndoto yake tangu yuko mtoto shuleni alipoapa akipata binti basi atampa majina hayo kuonyesha mapenzi thabiti kwa Timu yake Everton.
Lakini ndoto hiyo haikutimia pale alipozaa watoto wawili wa kike wa kwanza na mkewe Bibi Claire Cooper aligomea jina hilo la Eva-Toni-Ann.
Lakini baada ya kukerwa sana na mumewe, Claire alikiri jina hilo lilianza kumwingia akilini ingawa alikuwa bado halipendi.
Pale alipozaliwa binti huyo mpya ikapigwa kura.
Wakaandika majina tofauti kwenye karatasi na kuvitia vikaratasi hivyo ndani ya kofia likiwemo lile la Eva-Toni-Ann.
Baba mtu Danny akatoa karatasi ndani ya kofia na liliposomwa jina lilikuwa ni Eva-Toni-Ann! Ilipokuja zamu ya Binti yao wa kwanza kuokota karatasi ndani ya kofia hiyo likatoka jina Eva-Toni-Ann!
Mamu mtu nae ilipofika zamu yake jina likawa hilo hilo Eva-Toni-Ann!
Baba wa mtoto huyo Eva-Toni-Ann anakiri kama angezaliwa dume basi angemwita Duncan- akimaanisha Duncan Ferguson aliyekuwa Mchezaji veterani na mahiri wa Everton.

Danny anasema hata Babu yake mtoto huyo Eva-Toni-Ann alikuwa ni mpenzi wa Everton na alifurahia jina hilo ingawa hakuishi muda mrefu tangu azaliwe mjukuu wake kwani alifariki kwa kuungua moto nyumbani kwake!

Danny anakiri hata Mashabiki wa Watani wao Klabu ya Liverpool wanakiri jina hilo ni maridadi sana!
MITOANO KOMBE LA DUNIA: KUNDI LA NCHI ZA MAREKANI KUSINI NA RATIBA YAO YA WIKIENDI HII

Timu za Taifa za Nchi za Marekani Kusini zinaingia tena dimbani kuanzia Jumamosi hii katika mapambano ya Kundi lao ambalo lina Nchi 10. Mpaka sasa kila Nchi ishacheza mechi 8 na ikifika Jumatano ya tarehe 15 Oktoba 2008 watakuwa wameshavuka nusu ya mechi wanazotakiwa kucheza na hivyo kuleta picha kidogo nani anaweza akaingia FAINALI huko AFRIKA KUSINI mwaka 2010.

Baada ya mechi 8 kwa kila timu, Paraguay yuko kileleni akiwa na pointi 17 akifuatiwa na Brazil mwenye pointi 13 sawa na Argentina na Chile lakini Brazil yuko mbele kwa kufunga magoli mengi. Uruguay ana pointi 12, Colombia 10, Ecuador 9, Venezuela na Peru wana 7 kila mmoja na mkiani yuko Bolivia mwenye 5.
Timu nne za juu za Kundi hili zitaingia moja kwa moja FAINALI huko AFRiKA KUSINI mwaka 2010.

Timu ya 5 itakwenda kupambana na mshindi wa Kundi la Oceania ili kupata timu moja kati ya hizo itakayoingia FAINALI hizo.

RATIBA:

Jumamosi 11 Oktoba 2008

Bolivia v Peru

Argentina v Uruguay

Colombia v Paraguay


Jumapili 12 Oktoba 2008

Venezuela v Brazil

Ecuador v Chile

Jumanne 14 Oktoba 2008

Bolivia v Uruguay


Jumatano 15 Oktoba 2008

Paraguay v Peru

Chile v Argentina

Venezuela v Ecuador

Brazil v Colombia

UEFA KUFANYA DRO YA UEFA CUP KESHO

Klabu za Uingereza Tottenham, Manchester City, Portsmouth na Aston Villa kesho zitajua ni wapinzani gani watakuwa nao kwenye Makundi ya kugombea Kombe la UEFA [UEFA CUP]. Kwa taratibu za UEFA CUP timu za nchi moja haziwezi kuwekwa kwenye Kundi moja hivyo timu hizi za Uingereza haziwezi kukutana kwenye hatua hii ya Makundi.
Klabu 40 za Ulaya zimegawanywa katika Vikapu vitano na dro itafanyika ili kupata Makundi manane ya timu 5 kila moja. Katika kila Kundi timu moja itacheza mechi 2 nyumbani na 2 ugenini na wapinzani tofauti.
Timu 3 za juu za kila Kundi zitaingia hatua inayofuata ya mtoano itakayojumuisha timu 8 zitakazochukua nafasi ya tatu katika Makundi ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE.

VIKAPU VYA DRO VIMEGAWANYWA IFUATAVYO:

KAPU LA 1: AC Milan, Sevilla, Valencia, Benfica, Schalke 04, CSKA Moscow, TOTTENHAM, Hamburg.

KAPU LA 2: VfB Stuttgart, Ajax, Olympiacos, Deportivo La Coruna, Club Brugge, Spartak Moscow, Paris SG, Heerenveen.

KAPU LA 3: Rosenborg, Udinese, Feyenoord, SC Braga, Slavia Prague, MANCHESTER CITY, Galatasaray, Sampdoria.

KAPU LA 4: Hertha Berlin, Partizan Belgrade, Nancy, PORTSMOUTH, ASTON VILLA, Racing Santander, FC Copenhagen, Dinamo Zagreb.

KAPU LA 5: Saint-Etienne, VfL Wolfsburg, Standard Liege, FC Twente, NEC Nijmegen, Metalist
Michael Owen kaachwa tena Timu ya Taifa ya England!!

Meneja wa England Fabio Capello hakumchagua Michael Owen kwenye kikosi chake cha Wachezaji 23 wa Timu ya Taifa ya England kitakachocheza mechi za mtoano za Kundi la 6 la Nchi za Ulaya ambalo lina timu za Croatia, Ukraine, Belarus, Kazakhstan na Andorra.
Wengi walitegemea Owen ataitwa baada ya kupona lakini ameachwa na badala yake Peter Crouch amechukuliwa.
England Jumamosi inayokuja tarehe 11 Oktoba inacheza na Kazakhstan Uwanja wa nyumbani Wembley na Jumatano tarehe 15 Oktoba 2008 watakuwa ugenini kupambana na Belarus.

Kikosi kamili cha England [kwenye mabano Klabu wanazochezea]:

James (Portsmouth), Green (West Ham), Carson (West Brom); Brown (Manchester United), Johnson (Portsmouth), Terry (Chelsea), Ferdinand (Manchester United), Lescott (Everton), Upson (West Ham), A Cole (Chelsea), Bridge (Chelsea); Beckham (Los Angeles Galaxy), Walcott (Arsenal), Barry (Aston Villa), Jenas (Tottenham), Lampard (Chelsea), Gerrard (Liverpool), Downing (Middlesbrough), Wright-Phillips (Manchester City); Heskey (Wigan), Crouch (Portsmouth), Rooney (Manchester United), Defoe (Portsmouth).
KOMBE LA DUNIA: MECHI ZA MAKUNDI YA ULAYA

Timu za Mataifa ya Ulaya siku ya Jumamosi tarehe 11 Oktoba na Jumatano tarehe 15 Oktoba 2008 zitajimwaga viwanja mbalimbali katika mechi za Makundi ya Nchi za Ulaya kuwania nafasi za kuingia Fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika huko Afrika Kusini mwaka 2010.
Nchi hizi za Ulaya zimegawanywa Makundi 9 na bingwa wa kila Kundi anaingia moja kwa moja Fainali hizo. Washindi wa pili Wanane Bora kutoka kwenye Makundi hayo 9 watagawanywa mechi 4 za mtoano za nyumbani na ugenini ili kupata timu nyingine nne zitakazoenda Fainali.
Uingereza ambayo ipo Kundi la 6 pamoja na Croatia, Ukraine, Belarus, Kazakhstan na Andorra inaongoza Kundi hilo ikiwa na pointi 6 baada ya kushinda mechi zake mbili za kwanza ilipozifunga Andorra 2-0 na Croatia 4-1.
Uingereza Jumamosi inacheza na Kazakhstan Uwanja wa nyumbani Wembley na Jumatano watakuwa ugenini kupambana na Belarus.

RATIBA: Jumamosi, 11 Oktoba 2008 [saa zilizotajwa ni zabongo]

Belgium v Armenia, [Kundi la 5, saa 3:45]

Bulgaria v Italy, Kundi la 8, saa 3:15]

Denmark v Malta, [Kundi la 1, saa 3:15]

England v Kazakhstan, Kundi la 6, saa 1:15]

Estonia v Spain, [Kundi la 5, saa 3:45]

Faroe Islands v Austria, [Kundi la 7, saa 12:00]

Finland v Azerbaijan, [Kundi la 4, saa 11:00]

Georgia v Cyprus, [Kundi la 8, saa 1:30]

Germany v Russia, [Kundi la 4, saa 3:45]

Greece v Moldova, [Kundi la 2, saa 3:30]

Holland v Iceland, [Kundi la 9, saa 3:45]

Hungary v Albania, [Kundi la 1, saa 2:45]

Luxembourg v Israel, [Kundi la 2, saa 3:15]

Poland v Czech Republic, [Kundi la 3, 1saa 3:30]

Romania v France, [Kundi la 7, saa 2:15]

San Marino v Slovakia, [Kundi la 3, saa 3:30]

Scotland v Norway, [Kundi la 9, saa 11:00]

Serbia v Lithuania, [Kundi la 7, saa 3:15]

Slovenia v Northern Ireland, [Kundi la 3, saa 3:45]

Sweden v Portugal, [Kundi la 1, saa 3:00]

Switzerland v Latvia, [Kundi la 2, saa 12:45]

Turkey v Bosnia-Herzegovina, [Kundi la 5, saa 3:00]

Ukraine v Croatia, [Kundi la 6, saa 4:00]

Wales v Liechtenstein, [Kundi la 4, saa 1:30]


LIGI KUU UINGEREZA KUSIMAMA KUPISHA KOMBE LA DUNIA WIKIENDI HII!!

Michuano ya LIGI KUU UINGEREZA itasimama wikiendi hii ili kupisha mechi za mtoano wa kutafuta Nchi za kuingia FAINALI KOMBE LA DUNIA AFRIKA KUSINI 2010.

Mechi mbalimbali za Kimataifa zitachezwa Jumamosi hii tarehe 11 Oktoba na Jumtano ijayo tarehe 15 Oktoba 2008.

LIGI KU UINGEREZA itaendelea tena Jumamosi ya terehe 18 Oktoba 2008.

Sunday 5 October 2008

MATOKEO MECHI ZA LEO Jumapili, Oktoba 5

West Ham 1 Bolton 3


Chelsea 2 Aston Villa 0


Manchester City 2 Liverpool 3


Portsmouth 2 Stoke City 1


Tottenham 0 Hull City 1
Powered By Blogger