Thursday 4 September 2008

UINGEREZA YAPOROMOKA KWENYE LISTI YA FIFA YA TIMU ZA TAIFA BORA!!!!!


-Tanzania iko nafasi ya 117!!!


Wakati nchi zikiwa zinaingia kwenye mitoano wikiendi hii ya kutafuta timu zitazocheza Fainali Kombe la Dunia huko bondeni Afrika Kusini mwaka 2010 Timu ya Taifa ya Spain ndiyo timu bora duniani kwa miezi mitatu mfululizo kufuatia listi iliyotolewa na FIFA.
Uingereza imeporomoka nafasi moja na kushika nafasi ya 15 ikiwa chini ya Cameroun ambayo ndio timu inayoshika nafasi ya juu kabisa kutoka Afrika ikiwa ipo nafasi ya 14 kwa ubora duniani.
Ghana pia iko kwenye ishirini bora ikishikilia nafasi ya 20.
Timu ya Taifa ya Tanzania iko nafasi ya 117 huku jirani zetu Rwanda, Kenya na Uganda wakiwa juu yetu wakifuatana kwa kushika nafasi ya 85 kwa Rwanda, 86 kwa Kenya na 87 kwa Uganda.
Katika Afrika timu iliyokuwa chini kabisa ni Jamhuri ya Afrika ya Kati ikiwa nafasi ya 199.
Timu ya mwisho kabisa duniani ni American Samoa ambayo iko nafasi ya 200 huku ikifungana na nchi nyingine kadhaa.
NAFASI 20 ZA JUU NI IFUATAVYWO [KWENYE MABANO NAFASI ZA AWALI]:
1. Spain (1), 2. Italy (3), 3. Germany (2), 4. Netherlands (4), 5. Croatia (5), 6. Brazil (6), 7. Argentina (7), 8. Czech Republic (8), 9. Portugal (9), 10. Turkey (13)11. France (12), 12. Russia (10), 13. Romania (11), 14. Cameroon (15), 15. England (14), 16. Scotland (16), 16. Bulgaria (17), 18. Greece (18), 19. Israel (20), 20. Ghana (19)

Wednesday 3 September 2008


MANCHESTER UNITED WATEUA MSAIDIZI WA FERGUSON

Tangu aondoke Carlos Queiroz kwenda kuwa Meneja wa Ureno, nafasi ya Meneja Msaidizi ilikuwa tupu na leo klabu imetangaza pengo hilo linazibwa na Mchezaji wa zamani na mtumishi wa siku nyingi hapo klabuni Mike Phelan [pichani na Ferguson].

Kabla ya uteuzi huu, Mike Phelan alikuwa na wadhifa wa Mwalimu wa kikosi cha kwanza cha Man U.

Sasa nafasi ya Mwalimu wa kikosi cha kwanza amepewa Mholanzi Rene Meulensteen ambae alikuwa na wadhifa wa mwendelezaji wa ufundi na vipaji hapo Man U.

MENEJA WA WEST HAM ALAN CURBISHLEY AACHIA NGAZI!
Alan Curbishley amekuwa Meneja wa kwanza wa klabu ya Ligi Kuu Uingereza kuachia ngazi wakati leo alipotangaza kujiuzulu kufuatia kutoridhika na mwenendo wa klabu kuuza wachezaji bila kumhusisha kikamilifu.
Siku chache zilizopita West Ham walimuuza mdogo wake Rio Ferdinand, mlinzi Anton Ferdinand kwa Klabu ya Sunderland na pia mchezaji mwingine George Mc Cartney bila ridhaa yake.
Wakati huohuo, Kevin Keagan, Meneja wa Newcastle yuko kwenye mvutano mkubwa na wamiliki wa klabu hiyo ambao walitaka kuwauza wachezaji bila ridhaa yake. Wachezaji wanaohusishwa na mfarakano huu, ingawa hawajauzwa, ni Michael Owen na Joey Burton.
WIKIENDI HII HAMNA MECHI LIGI KUU!!!
-Jumamosi ni mechi za kimataifa za kuwania nafasi KOMBE LA DUNIA itakayofanyika mwaka 2010 huko bondeni AFRIKA KUSINI!!!
Wikiendi hii kutakuwa hamna mechi za LIGI KUU UINGEREZA na badala yake Timu za Taifa za Nchi mbalimbali zitacheza mechi za mchujo za kutafuta Timu zitakazoingia Fainali ya Kombe la Dunia 2010 ambayo itachezwa Afrika Kusini.

Mechi hizi za Timu za Taifa zitachezwa Jumamosi tarehe 6 Septemba 2008 na kufuatiwa na nyingine Jumatano tarehe 10 Septemba 2008.
Jumamosi Timu ya Taifa ya UINGEREZA inacheza ugenini na Andorra na Jumatano watacheza na Croatia pia ugenini.
LIGI KUU itaendelea tena kuchezwa wikiendi inayofuata yaani Jumamosi tarehe 13 Septemba 2008.
Mechi kubwa itakayochezwa wikiendi hiyo ni kati ya Liverpool v Man U kwenye Uwanja wa Anfield saa 9 dakika 45 mchana [bongo time].
Mechi nyingine za kuvutia ni Blackburn v Arsenal huku Man City wakicheza na Chelsea.

Tuesday 2 September 2008

BERBATOV YUKO MAN U!
ROBINHO YUKO MAN C!

Amini usiamini Dimitar Berbatov katua MAN U na Robinho yuko MAN C!

Monday 1 September 2008

WAKATI LEO MABILIONI YABADILISHANA MIKONO KUNUNUA WACHEZAJI HUKO ROMANIA MCHEZAJI AUZWA KWA KILO 15 ZA NYAMA!!!!
Leo ni siku ya mwisho ya kuhamisha Wachezaji na tayari kuna kupigana vikumbo vya dakika za mwisho ili kupata Wachezaji lakini taarifa zilizotoka Bucharest, Romania toka Gazeti la Michezo Pro Sport linadai Mchezaji wa Klabu ya Daraja la Pili UT Arad ameuzwa kwa Klabu ya Daraja la Nne Regal Horia kwa malipo ya kilo 15 za nyama!
Lakini, kwa bahati mbaya, Regal Horia, imepata pigo kwani mara baada ya kumnunua Mchezaji huyo aitwae Marius Ciora anaecheza kama mlinzi aliamua kustaafu soka ili aende Spain kufanya kazi kama Mkulima!!!
Sasa, Msemaji wa Klabu ya Regal Horia, analalama: 'Tumekasirika! Tumekula hasara mara mbili! Kwanza tumepoteza mchezaji bora na pili timu yetu itakosa mboga ya wiki nzima!'
PRIMERA LIGA:
VIGOGO REAL MADRID NA BARCELONA WAANZA LIGI KWA VIPIGO!!!!
Jana mechi za kwanza za ligi huko Spain ijulikanayo kama PRIMERA LIGA zilichezwa huku vigogo Barcelona na Real Madrid wakikung'utwa kwenye mechi hizo za kwanza.
Real Madrid walisafiri hadi nyumbani kwa Deportivo la Coruna bila ya nyota Robinho anaelilia kuhamia Chelsea na kupigwa mabao 2-1.
Nao Barcelona wakicheza nyumbani kwao walifungwa na timu iliyopanda daraja msimu huu Numancia kwa bao 1-0!
Nyota wa Barcelona Samuel Eto'o na Lionel Messi wote walipiga mashuti yaliyogonga mwamba!
SIKU YA MWISHO UHAMISHO WACHEZAJI:
Pavlyuchenko na Corluka waingia Spurs!!!
Mshambuliaji Mrusi Roman Pavlyuchenko [26] na Mlinzi wa Croatia Vedran Corluka [22] wamesaini mikataba ya kujiunga na Tottenham Hotspurs leo ikiwa ndio siku ya mwisho ya kuhamisha Wachezaji.
Pavlyuchenko ni Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Urusi iliyofana sana EURO 2008 na ametokea Klabu ya Spartak Moscow ya huko Urusi.
Nae Corluka ni Mchezaji wa Taifa wa Croatia na ameshaichezea Croatia mara 24. Klabu yake ilikuwa ni Manchester City aliyojiunga nayo mwaka 2007.


Aston Villa 0-0 Liverpool
Jana Timu ya Aston Villa ilitoka suluhu na Liverpool ya 0-0 katika mechi iliyochezwa nyumbani kwa Villa uwanjani Villa Park.
Liverpool ilipata pigo pale nyota wao na mshambuliaji tegemezi Fernando Torres alipolazimika kutoka kwenye dakika ya 30 baada ya kuumia.
Ingawa kila timu ilipata nafasi mbili tatu nzuri kila timu ilionekana dhahiri wanalinda wasifungwe tu.

Sunderland 0-3 Man City
Sunderland waliadhiriwa uwanjani kwao baada ya kubamizwa mabao 3-0 na Manchester City iliomchezesha mchezaji wao wa zamani Shaun Wright-Phillips aliehamia Chelsea na kurudi tena Man City juzi na jana ikawa mechi yake ya kwanza tangu arudi na aling'ara kupita kiasi baada ya kupachika bao 2.
Bao la kwanza la Man City lilifungwa na Stephen Ireland.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
HUKO SCOTLAND: Celtic 2 Rangers 4
Na huko Scotland timu zenye uhasama wa jadi Celtic na Rangers jana zilikutana kwa mara ya kwanza msimu huu kwenye LIGI KUU ya Scotland kwenye uwanja wa Celtic Park nyumbani kwa timu ya Celtic.
Katika mechi hiyo iliyokuwa mshikemshike timu zote zilibaki na wachezaji 10 baada ya kila timu kulimwa kadi nyekundu kwa mchezaji wake mmoja kufuatia matukio tofauti huku wengine kadhaa wakipata za njano.
Hadi mwisho Celtic 2 Rangers 4.

Sunday 31 August 2008

Chelsea 1-1 Tottenham
wabanwa na Spurs nyumbani Stamford Bridge!!!
Tottenham wamepata pointi yao ya kwanza ya LIGI KUU baada ya kufungwa katika mechi zao mbili za kwanza kwa kulazimisha sare ya 1-1 walipocheza ugenini kwenye Uwanja wa Stamford Bridge nyumbani kwa Chelsea.
Chelsea wlikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 28 lililofungwa na Belletti baada ya kona.
Spurs wakasawazisha kwenye dakika za majeruhi za kipindi cha kwanza wakati Darren Bent alipopachika bao.
SASA REAL YAMEWAKUTA!!!!!!
ROBINHO ALIA: 'Niacheni nijiunge na Chelsea!'
Leo mbele ya Waandishi wa habari Mbrazil Robinho ambae ni mchezaji wa Real Madrid amekitangaza kilio chake na kudai aachiwe ajiunge Chelsea kabla ya kesho ambayo ni siku ya mwisho ya uhamisho wa wachezaji.
Robinho ambae ameonyesha kutofurahishwa na kubaki Real Madrid ameachwa kwenye kikosi cha timu hiyo kitakachocheza mechi ya kwanza ya msimu wa Primera Liga leo huko Spain zidi ya Deportivo la Coruna.
Robinho amedai kwamba tangu Mei alibembeleza mkataba wake uboreshwe lakini alipuuzwa kwa sababu Real walikuwa na uhakika wa kumsaini Cristiano Ronaldo.
Hata hivyo Robinho ameihakikishia Real kuwa endapo hatahama basi ataichezea klabu kwa moyo mmoja.
Raundi ya Tatu ya Carling Cup yapangwa
Ratiba ya Raundi ya Tatu kuwania Kombe la Carling imetolewa na mechi hizi zimepangwa kuanzia tarehe 22 Septemba 2008.

Mara nyingi Timu za LIGI KUU UINGEREZA hutumia mechi za mashindano haya kuwachezesha Wachezaji wao chipukizi au wale wanaokaa kwenye benchi la akiba ili kuwapa uzoefu wa mechi.
Wanaoshikilia Kombe hilo ni Timu ya Totenham Hotspurs na wamepangiwa mechi ugenini dhidi ya Newcastle.
RATIBA ni kama ifuatavywo [TIMU INAYOTAJWA KWANZA IKO NYUMBANI]:
Arsenal v Sheffield United

Brighton & Hove or Man City v Derby

Burnley v Fulham

Portsmouth v Chelsea

Blackburn Rovers v Everton

Rotherham United v Southampton

Swansea City v Cardiff City

Ipswich Town v Wigan Athletic

Stoke City v Reading

Leeds United v Hartlepool United

Watford v West Ham United

Manchester United v Middlesbrough

Liverpool v Crewe Alexandra

Aston Villa v Queens Park Rangers

Sunderland v Northampton Town

Newcastle United v Tottenham Hotspurs

MATOKEO LIGI KUU UINGEREZA:
JUMAMOSI, 30 Agosti 2008
ARSENAL 3-0 NEWCASTLE
BOLTON 0-0 WEST BROM
EVERTON 0-3 PORTSMOUTH
HULL 0-5 WIGAN
MIDDLESBROUGH 2-1 STOKE CITY
WEST HAM 4-1 BLACKBURN
MECHI ZA LEO:
JUMAPILI, 31 Agosti 2008
[SAA 9 NA NUSU MCHANA BONGO TIME]
CHELSEA V TOTTENHAM HOTSPURS
[LAIVU DSTV SS3]
[SAA 11 JIONI BONGO TIME]
SUNDERLAND V MAN CITY
[LAIVU GTV EXTRA]
[SAA 12 JIONI BONGO TIME]
ASTON VILLA V LIVERPOOL
[LAIVU GTV GS1 & DSTV SS3]
Powered By Blogger