Saturday 30 August 2008

PLANI YA UWANJA MPYA WA LIVERPOOL-ambao umekwama!!!!!
Wamiliki wa Liverpool ambao ni Wamarekani wawili Tom Hicks na George Gillett wamekwama katika mikakati yao ya kujenga uwanja mpya wa Klabu ya Liverpool katika eneo jingine liitwalo Stanley Park baada ya kushindwa kupata kibali cha plani za kupanua uwanja huo mpya ili kufikia uwezo wa kuchukua watazamaji 73,000 kwani vibali vya mwanzo walivyopata vya ujenzi wa kiwanja kipya vilikuwa vya plani ya ujenzi wa uwanja wenye chini ya uwezo huo.
Uwanja wao wa sasa uitwao Anfield una uwezo wa kuingiza watazamaji 45,362 tu.
Vilevile wamiliki hao wameshindwa kupata uwezo wa kifedha ili kuendeleza mradi huo ingawa hili limekuja baada ya wao kuwa na mfarakano mkubwa kati yao.
Wamiliki hao wa Kimarekani wakati wanainunua Klabu ahadi yao kubwa ilikuwa ni kujenga uwanja mkubwa ili kushindana na Manchester United na vilevile kuitangaza Liverpool vyema katika soko la dunia.


Manucho akaribia kushuka dimbani na MAN U
Mshambuliaji wa Angola Manucho ambae alisainiwa na Manchester United mwezi Januari mwaka huu kutoka Pedro Atletico ya Angola anakaribia kuvaa jezi ya timu hiyo baada ya kupata rasmi kibali cha kazi nchini Uingereza hivi majuzi ingawa hasa kitu kilicho mchelewesha kuanza kucheza mapema ni kuumia baada ya kuvunjika mfupa kwenye kidole cha mguu wa kulia. Manucho ambae aling’ara sana kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika mwezi Januari akiwa na Timu ya Taifa ya Angola mara baada ya kusaini mkataba na Man U alipelekwa Ugiriki kuchezea timu ya Panathanaikos kwa mkopo ili apate uzoefu na alikuwa na timu hiyo hadi msimu ulipoisha mwezi Mei.
Wadadisi wanahisi Manucho ataliziba vizuri pengo linaloachwa na Louis Saha anaehamia Everton.
MECHI ZA LEO:
JUMAMOSI, 30 AGOSTI 2008
[MECHI SAA 11 JIONI BONGO TIME]
BOLTON WANDERERS V WEST BROMWICH ALBION
[LAIVU GTV GS2]
EVERTON V PORTSMOUTH
[LAIVU DSTV SS3]
HULL CITY V WIGAN ATHLETIC
MANCHESTER UNITED V FULHAM
[IMEAHIRISHWA]
MIDDLESBROUGH V STOKE CITY
WEST HAM UNITED V BLACKBURN ROVERS
[LAIVU GTV GS1 & DSTV SS5]
[SAA MOJA NA NUSU USIKU BONGO TIME]
ARSENAL V NEWCASTLE
[LAIVU DSTV SS3]

Friday 29 August 2008


Man Utd 1-2 Zenit St Petersburg
Wakicheza mchezo hafifu na wa chini ya kiwango Mabingwa wa Ulaya Man U walifungwa 2-1 na Mabingwa wa Kombe la UEFA Zenit St Petersburg na hivyo Warusi hao kutwa UEFA Super Cup huko Monaco.
Pavel Pogrebnyak na Danny waliwafungia Zenit na Vidic akafunga bao la Man U.
Scholes alisawazisha bao kwa mkono na Refa akalikataa na kumlima Kadi ya njano ambayo ilikuwa ya pili kwake na hivyo kupewa nyekundu hapo hapo.
Man Utd:
Van der Sar, Neville, Ferdinand, Vidic, Evra, Fletcher, Anderson, Scholes, Nani, Rooney, Tevez.
AKIBA: Kuszczak, Brown, Park, O'Shea, Gibson, Campbell, Possebon.
GOLI: Vidic 73
KADI NYEKUNDU: Scholes 90
Zenit St Petersburg:
Malafeev, Krizanac, Aniukov, Puygrenier, Sirl, Zyryanov, Danny, Denisov, Tymoschuk, Pogrebniak, Dominguez.
AKIBA: Contofalsky, Radimov, Kim, Tekke, Arshavin, Shirokov, Faitzulin.
MAGOLI: Pogrebniak 44, Danny 59
Referee: Claus Bo Larsen (Denmark)
LEO NI UEFA SUPER CUP:
MAN U vs Zenit St Petersburg
UWANJA: STADE LOUIS II, MONACO
Leo saa 3 dakika 45 usiku [bongo time] MABINGWA WA ULAYA, Manchester United, watapambana na MABINGWA WA KOMBE LA UEFA, Zenit St Petrsburg ya Urusi kuwania UEFA SUPER CUP huko Monaco.
Watu wa bongo mechi wataiona moja kwa moja kupitia DSTV Supersport 3.

MAN U KUWA NA UZI MPYA MECHI ZA UGENINI UEFA!!!

Wakati huohuo, Man U msimu huu kwenye UEFA CHAMPIONS LEAGUE wakicheza mechi za ugenini watatumia uzi mpya [pichani] uliotengenezwa na NIKE mahsusi kusheherekea miaka 40 tangu Man U walipokuwa Klabu ya kwanza Uingereza kutwaa UBINGWA WA ULAYA.

Katika mechi ya Fainali iliyochezwa mjini London Uwanja wa Wembley tarehe 29 Mei 1968 Man U waliwafunga Benfica mabao 4-1 na kutwaa UBINGWA WA ULAYA.

Benfica wakati huo ilikuwa ikiongozwa na Eusebio fowadi hatari mzaliwa wa Msumbiji. Nao Man U walikuwemo kina Sir Bobby Charlton, Dennis Law, George Best nk.

Siku hiyo Man U walivaa jezi za bluu tupu.
RONALDO NI BORA ULAYA!!!!!

Cristiano Ronaldo jana alinyakua tuzo mbili za Ulaya, moja ikiwa ni FOWADI BORA ambayo alikabidhiwa na veterani Eusebio na ya pili ni MCHEZAJI BORA ULAYA.
Ronaldo ni mchezaji wa pili wa Manchester United kunyakua tuzo ya MCHEZAJI BORA kwani mwaka 1999 ambapo Man U pia walitwaa ubingwa wa Ulaya David Beckham alishinda tuzo hiyo.
Ronaldo ambae aliwafungia MABINGWA Man U mabao 42 katika msimu wa 2007/8 ndie alikuwa MFUNGAJI BORA wa UEFA CHAMPIONS LEAGUE kwa kufunga mabao 8.
Tuzo nyingine zilizobaki na kutolewa jana zilinyakuliwa na Wachezaji wa Chelsea. MLINZI BORA ni John Terry, KIUNGO BORA ni Frank Lampard na KIPA BORA ni Petr Cech.

UEFA CHAMPIONS LEAGUE:
MAKUNDI TAYARI!!
MCHEZAJI BORA NI CRISTIANO RONALDO!!!!!
Jana usiku UEFA ilitoa mpangilio wa Makundi manane katika LIGI ya KLABU BINGWA ULAYA.
Vilevile Mchezaji nyota wa Mabingwa wa ULAYA Manchester United CRISTIANO RONALDO alipata tuzo mbili, moja kuwa Fowadi Bora ULAYA na ya pili kuwa MCHEZAJI BORA WA ULAYA.
Makundi yamegawanywa ifuatavyo:

KUNDI A: CHELSEA, Roma, Bordeaux, CFR Cluj
KUNDI B: Inter Milan, Werder Bremen, Panathinaikos, Anorthosis Famagusta
KUNDI C: Barcelona, Sporting Lisbon, Basel, Shakhtar Donetsk
KUNDI D: LIVERPOOL, PSV Eindhoven, Marseille, Atletico Madrid
KUNDI E: MAN UTD, Villarreal, CELTIC, Aalborg
KUNDI F: Lyon, Bayern Munich, Steaua Bucharest, Fiorentina
KUNDI G: ARSENAL, Porto, Fenerbahce, Dynamo Kiev
KUNDI H: Real Madrid, Juventus, Zenit St Petersburg, Bate Borisov
MECHI ZITACHEZWA TAREHE:
16/17 September
30 September/1 October
21/22 October
4/5 November
25/26 November
9/10 December
RATIBA YA MECHI ZA KWANZA:
16 SEPTEMBA 2008
CHELSEA V BORDEAUX
ROMA V CFR
PANATHINAIKOS V INTER MILAN
BREMEN V ANORTHOSIS
BASEL V SHAKHTAR
BARCELONA V SPORTING LISBON
PSV V ATLETICO MADRID
MARSEILLE V LIVERPOOL
17 SEPTEMBA 2008
MAN U V VILLAREAL
CELTIC V AALBORG
STEAU BUCHAREST V BAYERN MUNICH
LYON V FIORENTINA
PORTO V FENERBAHCE
DYNAMO KIEV V ARSENAL
JUVENTUS V ZENIT
REAL MADRID V BATE

Thursday 28 August 2008


UEFA CHAMPIONS LEAGUE: DROO YA MAKUNDI LEO!
-WACHEZAJI BORA KUJULIKANA LEO PIA!!!
Leo saa moja usiku kutakuwepo na droo maalum ili kuzipanga Klabu 32 za Ulaya katika Makundi manane ya timu nne nne ili timu zicheze mtindo wa ligi ambayo itaanza kuchezwa tarehe 16 Septemba na kumalizika tarehe 10 Desemba.
Timu hizo 32 zimegawanywa katika Makapu manne ili kutenganisha timu ngumu na za nchi moja zisiwe katika kundi moja.
Hivyo timu za kapu moja haziwezi kuwa kundi moja.
Vilevile leo ndio atapatika MCHEZAJI BORA WA KLABU WA MSIMU WA 2007/8.
KAPU LA KWANZA
MANCHESTER UNITED
CHELSEA
LIVERPOOL
Barcelona
ARSENAL
Lyon
Inter Milan
Real Madrid
KAPU LA PILI
Bayern Munich
PSV Eindhoven
Villarreal
AS Roma
FC Porto
Werder Bremen
Sporting Lisbon
Juventus
KAPU LA TATU
Marseille
Zenit St Petersburg
Steaua Bucharest
Panathinaikos
Bordeaux
CELTIC
Basel
Fenerbahce
KAPU LA NNE
Shakhtar Donetsk
Fiorentina
Atletico Madrid
Dynamo Kiev
CFR Cluj
Aalborg
Anorthosis Famagusta
Bate Borisov
MECHI ZITACHEZWA TAREHE:
16/17 September
30 September/1 October
21/22 October
4/5 November
25/26 November
9/10 December
ARSENAL WAVUKA KILAINI!!

LIVERPOOL WAINGIA KWA MBINDE!!!

Arsenal wameingia kwenye kapu la droo ya makundi itakayofanyika kesho baada ya kuwazidi kila kitu FC Twente ya Uholanzi kwa mabao 4-0 kwenye Uwanja wa Emirates.
Magoli ya Arsenal yalifungwa na Samir Nasir, Gallas, Walcott na Bendtner.
Arsenal wanasonga mbele kwa jumla ya mabao 6-0.
Liverpool, wakiwa nyumbani Anfield, walihema na kutweta lakini mwishowe walipata bao la ushindi katika muda wa nyongeza dakika ya 118 kwa goli la Dirk Kuyt baada ya kwenda suluhu 0-0 katika dakika 90 za kawaida na hivyo kuwabwaga Standard Liege ya Belgium.
Kesho usiku, saa 1 saa za bongo, kuna droo ya kuchagua timu zipi zinakuwa kwenye makundi.

Wednesday 27 August 2008

LEO PATASHIKA KLABU BINGWA ULAYA:
Arsenal v FC Twente
Leo Arsenal wanashuka dimbani uwanjani kwao Emirates Stadium kurudiana na Klabu ya Uholanzi FC Twente ambayo iko chini ya Meneja wa zamani wa Uingereza Steve McClaren katika mechi ya marudiano ya mtoano wa Raundi ya Tatu ya mashindano ya LIGI ya Klabu Bingwa Ulaya maarufu kama UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
Katika mechi ya kwanza Arsenal ikicheza ugenini huko Uholanzi ilishinda kwa mabao 2-0 na hivyo leo sare ya aina yeyote ile au wakifungwa bao 1-0 basi wanasonga mbele katika hatua inayofuata ambayo ni ya makundi.
Leo Arsenal wanategemea kumchezesha mchezaji wao kiungo mahiri Cesc Fabregas ambae hajacheza tangu msimu uanze kwani alikuwa majeruhi.
Mchezaji wao mpya Mikael Silvestre waliempata kutoka Manchester United hawezi kucheza kwa sababu ni majeruhi.
Mechi hii inaanza kuchezwa saa 4 dakika 5 usiku saa za bongo.
Liverpool v Standard Liege
Baada ya kuendeshwa puta mechi ya kwanza iliyochezwa Ubelgiji ambayo Kipa wao Pepe Reina aliokoa penalti iliyowafanya Liverpool wanusurike ugenini kwa sare ya 0-0 leo Liverpool wanashuka ngomeni kwao Uwanja wa Anfield wakitafuta ushindi utakaowafanya siku ya Alhamisi wawemo kwenye kapu la timu nyingine za Ulaya zitakapoingia kwenye droo ya kupanga makundi ya LIGI ya KLABU BINGWA ULAYA maarufu kama UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
Mechi inaanza saa 4 dakika 5 saa za bongo na inaonyeshwa moja kwa moja na DSTV Supersport 3.


MECHI ZA WIKIENDI ZA LIGI KUU UINGEREZA
[PAMOJA NA KITUO CHA TV KITACHOONYESHA MECHI BONGO]

JUMAMOSI, 30 AGOSTI 2008

[MECHI SAA 11 JIONI BONGO TIME]

BOLTON WANDERERS V WEST BROMWICH ALBION
[LAIVU GTV GS2]
EVERTON V PORTSMOUTH
[LAIVU DSTV SS3]
HULL CITY V WIGAN ATHLETIC
MANCHESTER UNITED V FULHAM
[IMEAHIRISHWA KWANI MAN U WANACHEZA UEFA SUPER CUP IJUMAA 29 AGOST 2008]
MIDDLESBROUGH V STOKE CITY
WEST HAM UNITED V BLACKBURN ROVERS
[LAIVU GTV GS1 & DSTV SS5]

[SAA MOJA NA NUSU USIKU BONGO TIME]

ARSENAL V NEWCASTLE
[LAIVU DSTV SS3]

JUMAPILI, 31 AGOSTI 2008

[SAA 9 NA NUSU MCHANA BONGO TIME]

CHELSEA V TOTTENHAM HOTSPURS
[LAIVU DSTV SS3]
[SAA 11 JIONI BONGO TIME]
SUNDERLAND V MAN CITY
[LAIVU GTV EXTRA]

[SAA 12 JIONI BONGO TIME]

ASTON VILLA V LIVERPOOL
[LAIVU GTV GS1 & DSTV SS3]



MCHEZAJI BORA ULAYA KUJULIKANA KESHO!!!!!
-Makundi LIGI ya KLABU BINGWA ULAYA KUPANGWA!
Chama cha Mpira ULAYA, UEFA, kesho Alhamisi tarehe 28 Agosti 2008, kitatangaza washindi wa tuzo mbalimbali za Wachezaji Bora wa Klabu za Ulaya kwa msimu wa 2007/8 na vilevile itafanyika droo maalum ili kupanga Makundi ya Mashindano ya LIGI ya KLABU BINGWA ULAYA ya msimu huu 2008/9 ambayo itaanza tarehe 16 Septemba 2008.
Ijumaa tarehe 29 Agosti 2008, Mabingwa wa LIGI ya KLABU BINGWA ULAYA Manchester United watapambana na Mabingwa wa Kombe la UEFA Zenit St Petersburg ya Urusi kugombea UEFA Super Cup mjini Monaco kwenye Uwanja wa Stade Louis II.
Kati ya Wachezaji 20 waliomo kwenye listi ya mwisho ya Wachezaji Bora, wachezaji 17 wanatoka kwenye Klabu za LIGI KUU UINGEREZA.
Juu ya yote, mmoja kati ya hawa Wachezaji 20 Bora ndie atakaevikwa Taji la Mchezaji Bora wa Klabu wa Ulaya kwa msimu wa 2007/8.
Wachezaji wanaogombea tuzo na nafasi zao pamoja na Klabu watokazo ni kama ifuatavyo:
UEFA KIPA BORA WA MWAKA
-Manuel Almunia [ARSENAL]
-Petr Cech [CHELSEA]
-Manuel Nuer [FC SCHALKE 04]
-Pepe Reina [LIVERPOOL]
-Edwin van der Sar MANCHESTER UNITED]
UEFA MLINZI BORA WA MWAKA
-Jamie Carragher [LIVERPOOL]
-Rio Ferdinand [MANCHESTER UNITED]
-Carles Puyol [FC BARCELONA]
-John Terry [CHELSEA]
-Nemanja Vidic [MANCHESTER UNITED]
UEFA KIUNGO BORA WA MWAKA
-Michael Essien [CHELSEA]
-Cesc Fabregas [ARSENAL]
-Steven Gerrard [LIVERPOOL]
-Frank Lampard [CHELSEA]
-Paul Scholes [MANCHESTER UNITED]
UEFA MSHAMBULIAJI BORA WA MWAKA
-Didier Drogba [CHELSEA]
-Lionel Messi [FC BARCELONA]
-Cristiano Ronaldo [MANCHESTER UNITED]
-Wayne Rooney [MANCHESTER UNITED]
-Fernando Torres LIVERPOOL]

UHAMISHO LIGI KUU:
-Mdogo wake Rio njiani kwenda Sunderland, Senderos safarini AC Milan, Berbatov bado kanasa!!!
Wakati mdogo wake Rio Ferdinand, sentahafu wa West Ham Anton Ferdinand [23] akifanyiwa uchunguzi wa afya ili kukamilisha taratibu za kuhamia Sunderland na sentahafu wa Arsenal Philippe Senderos nae pia akipimwa afya ili ahamie kwa mkopo AC Milan, Dimitar Berbatov amekwama kuhamia Manchester United baada ya Klabu yake Tottenham Hotspurs kung’ang’ania waongezewe dau.
Mvutano huo umefikia hatua ya kuzorotesha uhusiano kati ya Berbatov na Tottenham kiasi cha klabu hiyo kumtema katika kikosi chake kilichofungwa na Sunderland wikiendi kwa bao 2-1.
Mchezaji huyo ameshadai kwa maandishi ili aruhusiwe kuhamia Man United.
Tayari Man U washatoa ofa mbili rasmi zilizokataliwa na Tottenham wanaotaka dau liwe Pauni milioni 30 wakati ofa waliyopewa ni Pauni milioni 25.
Tarehe ya mwisho ya kukamilisha usajili ni Jumatatu Septemba 1 na baada ya hapo mchezaji haruhusiwi kuhama hadi Januari 1, 2009.

Tuesday 26 August 2008

RAUNDI YA TATU ya Mtoano ya LIGI YA KLABU BINGWA ULAYA
Mechi za marudiano ya Raundi ya Tatu ya Mtoano ya LIGI YA KLABU BINGWA ULAYA zinachezwa leo na kesho.
Leo ni mechi moja tu kati ya Artmedia na Juventus.
Timu za LIGI KUU UINGEREZA Arsenal na Liverpool zitacheza kesho zote zikiwa viwanja vya nyumbani.
Arsenal alimfunga FC Twente ya Uholanzi kwa bao 2-0 na Liverpool ilitoka sare ya 0-0 na Standard Liege ya Ubelgiji katika mechi ya kwanza.
Washindi wa mechi hizi watajumuika na Mabingwa wa nchi pamoja na timu zilizoshika nafasi ya pili kwenye droo maalum itayofanyika Alhamisi tarehe 28 Agosti ili kupanga Makundi manane ambamo timu zitacheza kwa mtindo wa ligi.

MATOKEO YA MECHI YA KWANZA:
Vitoria Guimaraes 0 v Basel 0
Shakhtar 2 v Dinamo Zagreb 0
Schalke 1 v Atletico Madrid 0
Aalborg 2 v Kaunas 0
Barcelona 4 v Wisla Krakow 0
Levski Sofia 0 v BATE 1
Standard Liege 0 v LIVERPOOL 0
Partizan 2 v Fenerbahce 2
FC Twente 0 v ARSENAL 2
Spartak Moscow 1 v Dinamo Kiev 4
Juventus 4 v Artmedia 0
SK Brann 0 v Marseille 1
Fiorentina 2 v Slavia Prague 0
Galatasaray2 v Steaua Bucharest 2
Sparta Prague 1 v Panathinaikos 2




MABINGWA MAN U WASHINDA!!
portsmouth 0 man u 1
Darren Fletcher katika mechi ya pili mfululizo ndie mkombozi wa Man U baada ya kufunga bao la ushindi katika dakika ya 32 kwenye Uwanja wa Fratton Park nyumbani kwa Portsmouth.
Hiki ni kipigo cha pili mfululizo kwa Portsmouth.
Wiki iliyopita walipachikwa 4-0 na Chelsea huko Stamford Bridge.
Huu ni ushindi wa kwanza kwa Mabingwa wa LIGI KUU kwani wiki iliyopita walilazimishwa sare ya 1-1 na Newcastle uwanjani kwao Old Trafford.
Timu zilikuwa:
Portsmouth:
James, Kaboul, Campbell, Distin, Johnson, Diop, Davis (Utaka 66), Diarra, Armand Traore (Thomas 56), Crouch, Defoe.
AKIBA: Ashdown, Lauren, Hreidarsson, Mvuemba, Sahar.
KADI: Diop, Defoe.
Man Utd:
Van der Sar, Brown, Ferdinand, Vidic, O'Shea, Fletcher, Anderson (Possebon 76), Scholes, Evra, Rooney, Tevez.
AKIBA: Kuszczak, Neville, Fabio Da Silva, Rafael Da Silva, Gibson, Campbell.
KADI: Brown, Fletcher.
WATAZAMAJI: 20,540
REFA: Chris Foy (Merseyside).

Sunday 24 August 2008

LEO MAN CITY WAIBUKA!
washinda 3-0 nyumbani!!!!!
Baada ya kubandikwa magoli 4-2 wiki iliyokwisha walipocheza nyumbani kwa Aston Villa leo Manchester City wameibuka wakiwa uwanjani kwao City of Manchester Stadium na kuwatandika West Ham mabao 4-2.
Ushindi huu umesaidiwa sana na kadi nyekundu aliyopewa mchezaji wa West Ham Mark Nobles kipindi cha kwanza ingawa mpaka mwisho wa kipindi hicho bado mechi ilikuwa suluhu.
Katika kipindi cha pili Man City walipata bao la kwanza kupitia Daniel Sturridge na bao la pili na la tatu yalifungwa na Mbrazil Elano.
CHELSEA WASIKITISHA...lakini washinda 1-0!!!!
Bao la frikiki ya Mreno Deco kwenye dakika ya nne tu ya mchezo liliwapa Chelsea ushindi finyu wa 1-0 walipocheza na Wigan.
Baada ya goli hilo Wigan wakicheza nyumbani kwao walicharuka lakini walishindwa kurudisha ingawa mafowadi wao Mmisri Amr Zaki na Mwingereza Emile Heskey walihaha kila dakika.
Huu ni ushindi wa pili mfululizo kwa Chelsea baada ya kuwachabanga Portsmouth 4-0 wiki iliyopita wakati Wigan kwao ni kipigo cha pili mfululizo kwani walifungwa 2-1 na West Ham.
TUZO WACHEZAJI BORA WA KLABU ULAYA KUTOLEWA ALHAMISI 28 AGOSTI 2008!!!!
-ratiba ya KLABU BINGWA ULAYA kutolewa siku hiyo!!!
-MCHEZAJI BORA WA KLABU ULAYA KUJULIKANA siku hiyo!!!
-MAN U KUGOMBEA UEFA SUPER CUP siku inayofuata!!!!

Chama cha Mpira ULAYA, UEFA, siku ya Alhamisi tarehe 28 Agosti 2008, kitatangaza washindi wa tuzo mbalimbali za Wachezaji Bora wa Klabu za Ulaya kwa msimu wa 2007/8 na vilevile siku hiyo hiyo itafanyika droo maalum ili kupanga Makundi ya Mashindano ya LIGI ya KLABU BINGWA ULAYA ya msimu huu 2008/9 ambayo itaanza tarehe 16 Septemba 2008.
Siku inayofuata, yaani tarehe 29 Agosti 2008, Mabingwa wa LIGI ya KLABU BINGWA ULAYA Manchester United watapambana na Mabingwa wa Kombe la UEFA Zenit St Petersburg ya Urusi kugombea UEFA Super Cup mjini Monaco kwenye Uwanja wa Stade Louis II.
Kati ya Wachezaji 20 waliomo kwenye listi ya mwisho ya Wachezaji Bora, wachezaji 17 wanatoka kwenye Klabu za LIGI KUU UINGEREZA.
Hii inadhihirisha ubora wa LIGI KUU UINGEREZA katika Ulaya na Dunia.
Wachezaji 6 wanatoka kwa Mabingwa wa Ulaya Manchester United, watano Chelsea, wanne Liverpool na wawil Arsenal. Wachezaji wengine watatu waliobaki ni Kipa wa Schalke 04 Manuel Neuer, Mlinzi wa Barcelona Carles Puyol na Mchezaji mwenzake wa Barcelona Mshambuliaji Lionel Messi.
Majina ya Wachezaji wa Manchester United ni Edwin van der Sar, Rio Ferdinand, Nemanja Vidic, Paul Scholes, Wayne Rooney na Cristiano Ronaldo.
Wa Chelsea ni Peter Cech, John Terry, Michael Essien, Frank Lampard, Didier Drogba. Liverpool ni Pepe Reina, Jamie Carragher, Steven Gerrard na Fernando Torres. Arsenal ni Manuel Almunia na Cesc Fabregas.
Kila Mchezaji atakuwa anagombea nafasi Bora katika pozisheni anayochezea yaani kama ni Kipa basi Kipa Bora, Mlinzi zawadi ya Mlinzi Bora, Kiungo zawadi ya Kiungo Bora na Mshambuliaji tuzo ya Mshambuliaji Bora.
Juu ya yote, mmoja kati ya hawa Wachezaji 20 Bora ndie atakaevikwa Taji la Mchezaji Bora wa Klabu Ulaya kwa msimu wa 2007/8.
Wachezaji hawa 20 waliteuliwa kwa kupigiwa kura na Makocha wa Klabu 16 za Ulaya zilizoingia hatua ya mtoano ya Mashindano ya LIGI ya KLABU BINGWA ULAYA
ya msimu uliopita.
Shevchenko arudi AC Milan
Mshambuliaji wa Chelsea Andriy Shevchenko anarudi timu yake ya zamani ya Italia AC Milan kwa makubaliano ambayo yamewekwa siri.
Shevchenko [31] amabae ni raia wa Ukraine alihamia Chelsea mwaka 2006 kutokea AC Milan lakini ameshindwa kutamba kwenye LIGI KUU UINGEREZA ingawa huko AC Milan alikotoka ndie mfungaji anaeshikilia namba mbili katika wafungaji bora wa AC Milan kwenye historia. Alifunga magoli 127 katika mechi 208 alizocheza.
Akiwa Chelsea amefunga goli 9 tu katika mechi 47 alocheza.

DJIBRIL CISSE awaua Spurs!!!

ni mechi yake ya kwanza kwa Sunderland!!!
Mchezaji wa zamani wa Liverpool akichezaji mechi yake ya kwanza tangu ajiunge na Sunderland juzi kwa mkopo kutoka Klabu ya Marseille ya Ufaransa Djibril Cisse alifunga bao la ushindi katikA dakika ya 83 na kuiwezesha Sunderland kuibamiza Tottenham Hotspurs kwa bao 2-1.
Meneja wa Spurs Juande Ramos waliokuwa wakicheza nyumbani kwao Uwanja wa White Hart Lane aliamua kumwacha kwenye timu nyota na mfungaji wao bora Dimitar Berbatov kwa madai kuwa akili yake haijatulia na amekuwa akivuruga maandalizi ya timu kwani mchezaji huyo ameshatoa madai kwa maandishi aruhusiwe kuhamia Manchester United. Mpaka sasa Spurs wamegomea ofa ya Man U kwa mchezaji huyo wakitaka dau lipandishwe.
Awali kwenye dakika ya 55 mchezaji wa zamani wa Man U Kieron Richardson aliipatia Sunderland bao la kuongoza na Nahodha wa Spurs Jermaine Jenas ahasawazisha kwenye dakika ya 73.
TIMU ZILIKUWA:
Tottenham: Gomes, Zokora, King, Woodgate, Assou-Ekotto (Huddlestone 56), Modric, Lennon (Giovanni 56), Jenas, Bentley, Bale, Bent. AKIBA: Cesar, Gilberto, Gunter, Dawson, O’Hara.
Sunderland: Gordon, Bardsley, Nosworthy, Higginbotham, Collins, Malbranque, Whitehead, Reid (Miller 87), Richardson (Cisse 65), Diouf, Murphy. AKIBA: Ward, Chopra, Leadbitter, Healy, Stokes.
WAZAMAJI: 36,064
REFA: Mike Dean (Wirral).

MECHI ZA LEO JUMAPILI, 24 August 2008
mechi zote zipo laivu DSTV Supersport 3


[saa 9 na nusu mchana bongo time]
WIGAN v CHELSEA

[saa 12 jioni bongo time]
MAN CITY v WEST HAM UNITED


Powered By Blogger