Saturday 16 August 2008

TORRES AWAPA USHINDI LIVERPOOL
SUNDERLAND 0 LIVERPOOL 1
Katika mechi ambayo wapenzi wa Liverpool walisikitikia kiwango cha timu yao Fernando Torres aliwainua mioyo kwa kufunga dakika ya 83 na kuwapa ushindi wa bao 1-0!
Sunderland walipata nafasi nyingi lakini ubutu wao kwa kukosa mmaliziaji ndio uliowaua ingawa wachezaji wapya kama Diouf na Malbranque walicheza kufa na kupona.

TIMU ZILIKUWA:
Sunderland: Gordon, Chimbonda, Nosworthy, Collins, Bardsley, Malbranque (Edwards 73), Tainio (Whitehead 57), Reid, Richardson, Diouf (Chopra 81), Murphy.
Liverpool: Reina, Arbeloa, Carragher, Hyypia, Dossena, Kuyt, Gerrard, Plessis (Alonso 46), Benayoun (Aurelio 81), Keane (El Zhar 77), Torres.

MATOKEO MECHI ZILOZOCHEZWA SAA 11 JIONI [BONGO TIME].
Bolton 3 v Stoke 1
Everton 2 v Blackburn 3
Hull 2 v Fulham 1
West Ham 2 v Wigan 1
LIGI KUU UINGEREZA YAANZA!!!
ARSENAL 1 WBA 0
Mchezaji mpya Samir Nasri alifunga goli katika dakika ya 4 tu ya mchezo na kuwapa Arsenal ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu iliyopanda daraja West Bromwich Albion katika mechi ya kwanza kabisa ya msimu mpya wa 2008/9.
Arsenal wakicheza nyumbani kwao Uwanja wa Emirates walitawala mchezo lakini walishindwa kupata mabao zaidi.

Mechi nyingine zinazochezwa leo zimeanza saa 11 jioni saa za bongo ni:

Bolton v Stoke

Everton v Blackburn

Hull v Fulham

West Ham v Wigan

Sunderland v Liverpool [SAA 1 NA NUSU USIKU]

SASA BENCHI LA AKIBA KUWA NA WACHEZAJI 7
LIGI KUU UINGEREZA imetoa uamuzi wa kuruhusu kila timu kuwa na Wachezaji 7 wa Akiba kwenye benchi la akiba la mechi za LIGI KUU kwa msimu huu wa 2008/9. Mtindo huu pia unatumika kwenye mechi zote za UEFA. Hapo nyuma kila timu iliruhusiwa kuwa na wachezaji watano tu wa akiba.
Lakini ingawa kila timu itakuwa na Wachezaji 7 wa Akiba kwenye benchi, timu inaruhusiwa kubadilisha si zaidi ya Wachezaji watatu katika kila mechi kama ilivyokuwa misimu iliyopita.
Mameneja wengi wa Timu za LIGI KUU wameusifia uamuzi huu kwani unawapa fursa kuwaweka wachezaji wao wadogo na chipukizi kwenye listi ya timu na pengine kuwatumia katika mechi na kuwapa uzoefu kwani wanaweza kuwaingiza ikiwa timu yao inafanya vizuri kwenye mechi mathalani timu inaongoza mabao 3-0 na dakika zimebaki labda 10 hivi basi ni rahisa kumuingiza chipukizi ili apate uzoefu. Awali timu zilikuwa zinaogopa kuwaweka chipukizi kwenye benchi la akiba kutokana na idadi ndogo ya Wachezaji wa Akiba wanaoruhusiwa na wasiwasi wa timu kujihujumu ikiwa mechi inaenda kombo. Hivyo timu zilihakikisha benchi la akiba lina Wachezaji watano mahiri na hivyo kuwakosesha chipukizi nafasi ya kucheza katika mechi ambazo zinageuka kuwa rahisi.
KIKOSI CHA MAN U NA NAMBA ZAO ZA JEZI
Kikosi cha Manchester United cha msimu wa 2008/9 kimewasilishwa rasmi kwenye LIGI KUU UINGEREZA huku kila Mchezaji akiwa na namba yake maalum atakayokuwa akiitumia kwenye jezi akicheza mechi.
Kikosi hicho kina Wachezaji wapya kama Mapacha wa Kibrazil Fabio na Rafael Da Silva pamoja na chipukizi wengine kama Danny Welbeck, Federico Macheda, Gibson, Campbell, Cleverley, Gray, Cathcart, Zieler, Chester na Kipa Amos.
Pia yumo Mshambuliaji hatari wa Angola aitwae Manucho ambae kwa sasa yuko mbioni kuombewa kibali cha kuishi Uingereza.

LISTI KAMILI NA NAMBA ZA JEZI NI KAMA IFUATAVYO:
1.Van der Sar, 2.Neville, 3.Evra, 4.Hargreaves, 5.Ferdinand, 6.Brown, 7.Ronaldo, 8.Anderson, 9.Saha, 10.Rooney, 11.Giggs, 12.Foster, 13.Park, 15.Vidic, 16.Carrick, 17.Nani, 18.Scholes, 19.Welbeck, 20.Fabio, 21.Rafael, 22.O'Shea, 23.Evans, 24.Fletcher, 26.Manucho, 27.Silvestre, 28.Gibson, 29.Kuszczak, 31.Campbell, 32.Tevez, 33.Hewson, 34.Possebon, 35.Cleverley, 36.Gray, 37.Cathcart, 38.Zieler, 39.Chester, 40.Amos, 41.Macheda

Friday 15 August 2008


MSIMU KUANZA KESHO!!!
Msimu mpya wa LIGI KUU UINGEREZA unaanza rasmi kesho Jumamosi miezi mitatu baada ya Manchester United kuchukua Ubingwa kwa mara ya 10 kwa mechi itakayoaanza saa 8 dakika 45 mchana kwa saa za bongo kati ya Arsenal na timu iliyopanda daraja West Bromwich Albion. Timu nyingine zilizopanda daraja na ambazo pia zitacheza kesho hiyo ni Stoke City na Hull City. Stoke watacheza na Bolton na Hull City watakwaana na Fulham.
Mabingwa Man U na washindi wa pili Chelsea wataanza kampeni Jumapili. Man U watawakaribisha Newcastle na Chelsea watakuwa wenyeji wa Mabingwa wa Kombe la FA Portsmouth.
Wakati Man U hawajamnunua mchezaji yeyote mpaka sasa ingawa muda wa usajili bado na mwisho wake ni tarehe 31 Agosti 2008, Chelsea washawabeba Wareno Deco na Bosingwa huku Arsenal wana wawili wapya Mfaransa Samir Nasri na tineja Aaron Ramsey. Liverpool wamemchukua mfungaji Robbie Keane.
Mabingwa Man U watauanza msimu bila ya mchezaji wao ambae ni Mfungaji na Mchezaji Bora wa msimu uliopita Cristiano Ronaldo anaeuguza enka aliyofanyiwa operesheni.
Timu zilizoshuka daraja msimu uliopita ni Derby,Birmingham na Reading.
Msimu huu mpya wadau wengi wanategemea bingwa atatoka kati ya timu zilizomaliza nafasi nne za juu msimu uliopita yaani Man U, Chelsea, Liverpool au Arsenal zinazoongozwa na Mameneja Sir Alex Ferguson, Scolari, Wenger na Benitez.
Chelsea alichukua ubingwa mara ya mwisho miaka miwili iliyopita. Liverpool hajatwaa ubingwa tangu 1990 na Arsenal tangu 2004.


JUMAMOSI 16 August 2008
[MECHI ITAANZA SAA 11 JIONI SAA ZA BONGO LABDA ITAJWE TOFAUTI]
Arsenal v West Brom [SAA 8 DAK 45 MCHANA]
Bolton v Stoke
Everton v Blackburn
Hull v Fulham
Middlesbrough v Tottenham
Sunderland v Liverpool [SAA 1 NA NUSU USIKU]
West Ham v Wigan

JUMAPILI 17 August 2008
Aston Villa v Man City [SAA 11 JIONI]
Chelsea v Portsmouth [SAA 9 NA NUSU]
Man Utd v Newcastle [SAA 12 JIONI
]
NEWCASTLE WAIMARISHA NGOME!
Newcastle wamethibitisha kumsaini Mlinzi wa Deportivo La Coruna Muargentina Fabricio Coloccini kwa mkataba wa miaka mitano.
Coloccini atakuwa mchezaji wa tatu kununuliwa na Meneja Kevin Keegan wengine wakiwa ni Danny Guthrie na Jonas Gutierrez.
Coloccini ni mlinzi mwenye nguvu alieanza kandanda akiwa na Klabu ya Argentina Boca Juniors na baadae akahamia Italia kuchezea AC Milan.
Kisha akatangatanga Klabu za Spain zikiwemo San Lorenzo, Alaves, Atletico Madrid na Villarreal.
Januari 2005 alijiunga na Deportivo La Coruna.
Coloccini ameshachezea Timu ya Taifa ya Argentina na mwaka 2006 alikuwemo kwenye kikosi cha timu hiyo kwenye Kombe la Dunia walipotolewa na wenyeji wa mashindano hayo Ujerumani.
....................MAN CITY WADODA NYUMBANI!!!
Manchester City jana wameadhiriwa vibaya nyumbani kwao baada ya kuchapwa bao 1-0 na timu hafifu ya Denmark FC Midtjylland katika mechi ya kwanza ya Raundi ya Pili ya Kombe la UEFA.
Timu hiyo ya Denmark ilifunga bao la la ushindi kupitia Danny Olsen dakika ya 15 baada ya kosa la mlinzi Richard Dunne.
Timu hizi zitarudiana huko Denmark baada ya wiki mbili.
...................ASTON VILLA WAPETA UGENINI!!
Wakati Manchester City wakila kibano, mchezaji Gareth Barry ambae wengi wanategemea yuko njiani kwenda Liverpool msimu huu aliifungia Aston Villa bao moja katika dakika ya 4 kwenye mechi ya Kombe la UEFA waliyocheza ugenini huko Iceland dhidi ya FH Hafnarfjordur na kushinda mabao 4-1.
Mabao mengine ya Aston Villa yalifungwa na Ashley Young ,dakika ya 6, Agbonlahor [38] na Laursen [64].
..................PORTSMOUTH WASHTAKIWA!!!
Portsmouth wameshitakiwa na Chama cha Soka Uingereza FA kwa kuvunja kanuni za uhamishaji Wachezaji kuhusiana na uhamisho wa Mchezaji wa Zimbabwe Benjani Mwaruwaru wakati alipojiunga na Portsmouth Januari 2006 akitokea Klabu ya Auxerre ya Ufarnsa na pale alipohama Portsmouth Januari 2008 kwenda Manchester City.
Utata wa uhamisho wa Benjani hasa unamuhusu ajenti wa Benjani aitwae Willie McKay ambae nae anahusishwa kwenye mashtaka hayo.
Sheria za FA zinakataza maajenti kuhusika na Klabu mbili katika uhamisho wa mara mbili mfululizo unaohusu mchezaji mmoja.
Portsmouth wanatakiwa kuwasilisha utetezi kabla ya Agosti 29, 2008 ingawa tayari wameshakana tuhuma hizo kwa kusema hawakumlipa Ajenti yeyote Benjani alipojiunga na Portsmouth Januari 2006 akitokea Klabu ya Auxerre na uhamisho wake kwenda Manchester City ulibarikiwa na LIGI KUU UINGEREZA pamoja na Kamati husika ya FA.


Thursday 14 August 2008

MATOKEO YA MECHI ZA Raundi ya Tatu ya Mtoano ya LIGI YA KLABU BINGWA ULAYA zilizochezwa jana 13 AGOSTI 2008.
Mechi ya Fiorentina vs Slavia Prague ilichezwa juzi.
Marudiano ni tarehe 27 AGOSTI 2008.


[TIMU INAYOTAJWA KWANZA NDIO MWENYEJI]


Anorthosis 3 v Olympiakos 0

Vitoria Guimaraes 0 v Basel 0

Shakhtar 2 v Dinamo Zagreb 0

Schalke 1 v Atletico Madrid 0

Aalborg 2 v Kaunas 0

Barcelona 4 v Wisla Krakow 0

Levski Sofia 0 v BATE 1

Standard Liege 0 v LIVERPOOL 0

Partizan 2 v Fenerbahce 2

FC Twente 0 v ARSENAL 2

Spartak Moscow 1 v Dinamo Kiev 4

Juventus 4 v Artmedia 0

SK Brann 0 v Marseille 1

Fiorentina 2 v Slavia Prague 0

Galatasaray 2 v Steaua Bucharest 2

Sparta Prague 1 v Panathinaikos 2

MTOANO LIGI YA KLABU BINGWA ULAYA:

Arsenal washinda 2-0!!

Arsenal walionyesha kiwango duni ingawa walishinda jana usiku huko Uholanzi dhidi ya FC Twente kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na Nahodha Gallas na Adebayor.
Wakicheza bila ya nyota wao kadhaa akiwemo mpishi Fabregas Arsenal hawakuonyesha cheche zozote zile zilizowafanya watishe msimu uliopita. FC Twente inayoongozwa na aliekuwa Meneja wa Timu ya Taifa ya Uingereza Steve McClaren walitawala mchezo na kukosa nafasi kadhaa katika mechi hii ya Raundi ya Tatu ya Mtoano katika mashindano ya LIGI YA KLABU BINGWA ULAYA.
Timu hizi zitarudiana Uwanja wa Emirates tarehe 27 Agosti 2008.
Timu zilikuwa:
FC Twente: Boschker, Wielaert, Tiote, Franco, Braafheid, Wilkshire, Brama, Arnautovic (Gerritsen 90), Janssen (Heubach 90), Elia (Huysegems 86), Denneboom.AKIBA HAWAKUCHEZA: Paauwe, Zomer, Wellenberg, Chery.
KADI: Janssen.
Arsenal: Almunia, Sagna, Djourou, Gallas, Clichy, Eboue, Ramsey, Denilson, Walcott (Randall 84), Adebayor, Van Persie (Bendtner 88).AKIBA HAWAKUCHEZA: Fabianski, Vela, Wilshere, Hoyte, Gibbs.
KADI: Denilson, Van Persie.
MAGOLI: Gallas 63, Adebayor 82.
WATAZAMAJI: 20,000.
Refa: Alberto Undiano Mallenco (Spain).
............LIVERPOOL ulimi nje...droo 0-0!!
Liverpool walijikuta wakipelekwa mchakamchaka huko Ubelgiji na Mabingwa wa huko Standard Liege katika mechi ya kwanza ya Raundi ya Tatu ya Mtoano katika mashindano ya LIGI YA KLABU BINGWA ULAYA iliyoisha 0-0.
Liverpool walinusurika kufungwa mara kadhaa na wamshkuru Kipa Reina alieokoa penalti.
Timu hizi zitarudiana Uwanja wa Anfield tarehe 27 Agosti 2008.
Timu zilikuwa:
Standard Liege: Aragon, Dante, Dalmat, Defour, Mbokani, De Camargo, Mikulic (Nicaise 90), Camozzato, Sarr, Fellaini, Witsel.AKIBA HAWAKUCHEZA: Devriendt, Goreux, Toama, Benko, Ingrao, Dembele.
KADI: Camozzato, Mikulic.
Liverpool: Reina, Arbeloa, Dossena, Carragher, Agger, Alonso, Plessis, Benayoun, Kuyt (El Zhar 83), Keane (Gerrard 67), Torres.AKIBA HAWAKUCHEZA: Cavalieri, Hyypia, Voronin, Pennant, Insua.
KADI: Alonso.
WATAZAMAJI: 25,000
Refa: Tom Ovrebo (Norway).

Wednesday 13 August 2008

KIMBEMBE KWA ARSENAL NA LIVERPOOL LEO!!
-FC TWENTE vs ARSENAL
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amekiri kuwa leo watu wengi wanategemea Arsenal wataifunga FC Twente katika mechi ya Raundi ya Tatu ya LIGI KLABU ULAYA inayochezwa Uholanzi na hivyo kuzidisha presha kwa Arsenal.
FC Twente inafundishwa na Steve McClaren aliekuwa Meneja wa Timu ya Taifa ya Uingereza kazi aliyotimuliwa Novemba 2007.
Arsenal imeenda Uholanzi bila mastaa wao kadhaa ambao ni majeruhi. Waliomo kwenye listi hiyo ni Fabregas, Kolo Toure, Abou Diaby, Tomas Rosicky, Philippe Senderos, Eduardo na Mchezaji mpya Samri Nasri.
Mechi hii itachezwa saa 3 dakika 45 usiku kwa saa za bongo. Mechi ya marudiano ni tarehe 27 Agosti kwenye Uwanja wa Emirates.
-STANDARD LIEGE vs LIVERPOOL
Liverpool leo saa 4 dakika 5 usiku huu watakuwa nchini Ubelgiji kupambana na Mabingwa wa Ubelgiji Klabu ya Standard Lige kwenye mechi ya Raundi ya Tatu ya LIGI KLABU ULAYA.
Liverpool imeshuka huko na kikosi chao kamili isipokuwa mchezaji Steve Finnan ambae inasemekana amegombana na Meneja wake Rafael Benitez.
Timu itachaguliwa kutokana wachezaji wafuatao:Reina, Arbeloa, Carragher, Agger, Dossena, Kuyt, Gerrard, Alonso, Benayoun, Torres, Keane.Subs (from): Cavalieri, Plessis, Ngog, Spearing, Hyypia, Pennant, Darby

Tuesday 12 August 2008


ASTON VILLA WAMCHUKUA MHISPANIA KUTOKA RANGERS
Klabu ya LIGI KUU UINGEREZA Aston Villa imemnunua Mlinzi Carlos Cuellar [26] kutoka Klabu ya Rangers ya Scotland kwa bei ya Pauni milioni 7.8.
Cuellar alikwenda Rangers mwaka jana akitokea Klabu ya Spain Osasuna na alikuwa moja ya nguzo thabiti kwa Rangers na kuuzwa kwake kumekuja kwa mshangao wa wadau wengi.
Cuellar ni mchezaji wa 6 kusainiwa na Aston Villa msimu huu.
Wengine ni Curtis Davies, Steve Sidwell, Luke Young, Nicky Shorey na Kipa Brad Friedel.
TOTTENHAM WAMNUNUA KIPA KUTOKA SPAIN
Tottenham wamethibitisha wamemnunua Kipa veterani Cesar Sanchez [36] kutoka klabu ya Spain Real Zaragoza na anategemewa kuwa Kipa namba mbili wa timu hiyo.
Kipa namba moja atakuwa Heurelho Gomes aliechukuliwa kutoka PSV Eindhoven ya Uholanzi kuziba pengo lililoachwa na kipa wa zamani wa Uingereza Paul Robinson aliehamia Blackburn Rovers.
Meneja wa Tottenham Spurs kwa sasa anafanya ‘mapinduzi’ klabuni hapo baada ya kuwauza wachezaji kadhaa wakiwemo Robbie Keane alieenda Liverpool, Steed Malbranque, Pascal Chimbonda, Teemu Tainio na Younes Kaboul.
Wachezaji walionunuliwa ni John Bostock (Crystal Palace, £700,000), Heurelho Gomes (PSV Eindhoven), Luka Modric (£15.8m), Giovani dos Santos (Barcelona, £4.7m) na David Bentley (Blackburn, £15m).

Monday 11 August 2008

KLABU BINGWA ULAYA
MCHUJO WAPAMBA MOTO!!!!!!!!!!!!

Mechi za Raundi ya Tatu ya Mtoano katika mashindano ya LIGI YA KLABU BINGWA ULAYA zinachezwa Jumatano tarehe 13 Agosti na marudiano ni Agosti 27.
Timu zilizoshika nafasi ya tatu na ya nne katika LIGI KUU UINGEREZA, Arsenal na Liverpool, zimo kwenye raundi hii.
Arsenal imepangwa kukutana na timu ya Uholanzi FC Twente inayoongozwa na aliekuwa Meneja wa Timu ya Taifa ya Uingereza Steve McClaren ambae alitimuliwa kazi hiyo Novemba 2007. Liverpool itakutana na Standard Liege ya Ubelgiji.
Arsenal na Liverpool wataanza mechi zao ugenini.
Washindi 16 wa mechi hizi watajumuika na timu nyingine 16 ambazo ni Mabingwa wa Nchi na washindi wa pili wa ligi za nchi [Timu kutoka Uingereza ni Mabingwa Man U na washindi wa pili Chelsea] kufanya jumla ya timu 32 zitakazogawanywa makundi manane ya timu 4 kila moja zitakazocheza mtindo wa ligi.
Mechi hizi za makundi zitaanza tarehe 16 Septemba na kumalizika Desemba 10.

RATIBA KAMILI: [TIMU INAYOTAJWA KWANZA NDIO MWENYEJI]
Anorthosis v Olympiakos

Vitoria Guimaraes v Basel

Shakhtar v Dinamo Zagreb

Schalke 04 v Atletico Madrid

Aalborg v Kaunas

Barcelona v Wisla Krakow

Levski Sofia v Bate

Standard Liege v LIVERPOOL

Partizan v Fenerbahce

FC Twente v ARSENAL

Spartak Moscow v Dinamo Kiev

Juventus v Artmedia

SK Brann v Marseille

Fiorentina v Slavia Prague

Galatasaray v Steaua Bucharest

Sparta Prague v Panathinaikos


WAFAHAMU WACHEZAJI WAPYA WA MAN U: NI NDUGU MAPACHA WAWILI KUTOKA BRAZIL!!!!
NI FABIO DA SILVA NA RAFAEL DA SILVA!!!
Fabio na Rafael Da Silva ni ndugu ambao ni mapacha waliozaliwa tarehe 9 Julai 1990 huko Petropolis, Rio de Janeiro, Brazil.
Ni vijana wenye vipaji sana na ni wachezaji wapya wa Manchester United.
Mapacha hawa hucheza kama mabeki wa pembeni mmoja kulia na mwingine kushoto na Manchester United waliwaibua kutoka Klabu ya Fluminense ya Brazil baada ya kuwaona wakicheza na kung’ara kwenye Timu ya Vijana ya Fluminense kwenye mashindano ya vijana huko Hong Kong mwaka 2005.
Mapacha hawa wameshachezea Timu ya Taifa ya Brazil ya Vijana chini ya miaka 17 na walijiunga na Manchester United Januari mwaka huu. Walishindwa kuanza kuichezea Man U mara baada ya kujiunga kwani maombi yao ya kibali cha kazi yalikwama kwa sababu yalitakiwa yawasilishwe kabla ya Januari.
Lakini walipotimiza miaka 18 [Julai 9, 2008] walikuwa huru kupata kibali cha kimataifa na wakaanza rasmi kuichezea Man U wiki iliyopita kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya Peterborough ambayo Meneja wake ni mtoto wa Meneja wa Man U Sir Alex Ferguson.

Katika mechi hiyo Man U walishinda 2-0 na mashabiki wote walikiri mapacha hao ni hazina.
Jana, hapo uwanjani Wembley, kugombea NGAO YA HISANI ambayo Man U waliwashinda Portsmouth, Fabio na Rafael Da Silva walikuwa miongoni mwa wachezaji wa akib
a wa Man U.
Portsmouth wamchukua Kaboul toka Spurs
Portsmouth wamefanikiwa kumsaini Mlinzi Younes Kaboul kutoka Tottenham.
Mfaransa huyu amesaini mkataba wa miaka minne baada ya vuta ni kuvute na Klabu za Sunderland na Aston Villa ambazo pia zilikuwa zinamgombea.
Kaboul, 22, alijiunga Tottenham Hotspurs kwa Pauni milioni 8 kutoka Klabu ya Ufaransa Auxerre mwezi July mwaka jana lakini alichezeshwa mechi 18 tu na Tottenham.

West Brom wamsaini Meite kutoka Bolton
West Bromwich Albion wamemnunua mchezaji wa Ivory Coast Mlinzi wa kati Abdoulaye Meite kutoka Bolton Wanderers kwa Pauni milioni 2.
Abdoulaye Meite mwenye umri wa miaka 27 ambae pia anaweza kucheza kama beki wa pembeni amesaini mkataba wa miaka mitatu kwa ada ya Pauni milioni 2 na nusu.
Meite alijiunga na Bolton mwezi Julai 2006 baada ya kuichezea Marseille ya Ufaransa kwa miaka mitano.
Alicheza mechi 56 alipokuwa na Bolton.

Sunday 10 August 2008


NGAO YA HISANI

MAN U 0 PORTSMOUTH 0
MAN U washinda kwa penalty 3-1!!
Mabingwa wa Ulaya na Uingereza wamefunua rasmi pazia la msimu wa 2008/9 kwa kuutawala kabisa mchezo uliochezwa nusu uwanja kwa muda mrefu dhidi ya Mabingwa wa Kombe la FA Portsmouth ingawa walishindwa kupata goli katika dakika 90.
Nafasi za wazi zilikoswa na MAN U na Refa alichangia baada ya kuwanyima penalti ya wazi pale Carlos Tevez aliposhikwa mguu na Mlinzi Hreidarsson ndani ya boksi.
Baada ya dakika 90 ikaja tombola ya penalti:
-MAN U wakafunga kupitia Tevez, Giggs na Carrick
-Portsmouth walikosa ya kwanza aliyopiga Diarra, kisha Defoe akafunga, Mvuemba na Johnson wakakosa zilizofuata.
VIKOSI VILIKUWA:
Man Utd: Van der Sar, Neville (Brown 66), Ferdinand, Vidic, Evra, Fletcher, O'Shea (Carrick 66), Scholes, Giggs, Nani (Campbell 79), Tevez. AKIBA HAWAKUCHEZA: Kuszczak, Evans, Possebon, Da Silva.
Portsmouth: James, Johnson, Campbell, Distin, Hreidarsson (Lauren 79), Diop, Pedro Mendes (Mvuemba 75), Diarra, Kranjcar (Utaka 60), Crouch, Defoe. AKIBA HAWAKUCHEZA: Ashdown, Sahar, Cranie, Traore.
WATAZAMAJI: 84,808
MATOKEO YA SOKA OLYMPIC BEIJING 2008:
Jumapili 10 Agosti 2008


KUNDI A:
Argentina 1-0 Australia
Serbia 2-4 Ivory Coast
KUNDI B:
Nigeria 2-1 Japan
Holland 2-2 USA
KUNDI C:
New Zealand 0-5 Brazil
China 0-2 Belgium
KUNDI D:
Cameroun 1-0 Honduras
Italy 3-0 South Korea
KAMPUNI YA RIO KUFYATUA ALBAMU YA KWANZA!!!

Staa wa MANCHESTER United Rio Ferdinand akitumia kampuni yake iliyoko Manchester iitwayo Chalk Records watafyatua albamu yao ya kwanza huku yeye binafsi akishirikishwa kidogo kwenye treki ya kwanza ya albamu hiyo.
Mfokaji wa kike aitwae Nia Jai ndie msanii wa albamu hiyo iitwayo ‘Black Ice’ itakayosambazwa Oktoba 1.
Kampuni ya Chalk Records iliianzishwa miaka miwili iliyopita na Rio Ferdinand akaanzisha shindano maalum kumtafuta msanii ataetoa albamu ya kwanza na kampuni yake.
Nia Jai, mwenye umri wa miaka 25 ambae ni muuguzi kitaaluma, alishinda shindano hilo na anammwagia sifa kubwa Rio Ferdinand kwa msaada aliompa hadi kufikia hatua ya kukaribia kuiingiza sokoni albamu hiyo.
Rio anamsifia msanii huyo kuwa ana bidii na kipaji maalum.
Powered By Blogger