Saturday 31 May 2008


EDUARDO ATARUDI UWANJANI JULAI!
Matibabu yake yameenda vizuri kupita ilivyotegemewa
Mchezaji wa Arsenal, mshambuliaji Eduardo da Silva anaweza kufanya maajabu na kurudi tena uwanjani mwezi Julai baada ya kupona mguu uliovunjika vibaya mwezi Februari mwaka huu katika mechi ya Birmingham na Arsenal.
Ilitegemewa itamchukuwa Eduardo miezi 15 kupona lakini taarifa zilizotoka kwenye kliniki inayomtibu mchezaji huyo huko RIO DE JANEIRO, BRAZIL zimesema amepata mafanikio na nafuu kubwa na atakuwa tayari kushuka uwanjani mwezi Julai au mwanzoni mwa Agosti.
Mchezaji huyo mwenye asili ya Brazil ana uraia wa Croatia na huchezea Timu ya Taifa ya Croatia.
************************************************************************************
Czech Republic 3-1 Scotland
Jana, katika mechi ya kirafiki ya kuinoa CZECH ambayo itacheza Kombe la Mataifa ya Ulaya EURO 2008 linaloaanza tarehe 7 Juni 2008, Czech iliibamiza Scotland mabao 3-1 mjini Prague, Czech.
Czech ni moja ya timu za kutumainiwa katika EURO 2008. Scotland haikufuzu kuingia fainali hizo.
Libor Sionko alifunga bao 2 na Michal Kadlec alifunga 1. David Clarkson alifunga bao la Scotland.
TIMU ZILIKUWA:
Czech Republic: Cech, Pospech, Ujfalusi, Kovac, Jankulovski, Sionko, Polak, Matejovsky, Galasek, Skacel, Koller.Subs: Blazek, Sivok, Grygera, Rozehnal, Kadlec, Plasil, Vlcek, Jarolim, Fenin, Sverkos, Baros, Zitka.
Scotland: Gordon, McNaughton, McManus, Caldwell, Naysmith, Robson, Hartley, Fletcher, Rae, Morrison, Miller.Subs: Marshall, Anderson, Berra, Dailly, McCormack, Maloney, Clarkson.
Referee: Eric Braamhaar (Netherlands)

Friday 30 May 2008




MANUCHO ANATEGEMEA MAFANIKIO MAN U!




Manucho Goncalves, mshambuliaji na mchezaji wa kimataifa wa Angola, aliesajiliwana MAN U Desemba mwaka jana na alieng'ara na Timu yake ya Angola kwenye mashindano ya Mataifa huru Afrika nchini Ghana Januari mwaka huu, ana imani kubwa atafanikiwa na timu yake ya MAN U.


Mchezaji huyo ilibidi apelekwe klabu ya Ugiriki ya Panathinaikos kwa mkopo baada ya kukosa kibali cha kazi nchini Uingereza kutokana na kucheza mechi chache kwenye timu yake ya Taifa ya Angola kama kanuni zinavyotaka kwa wachezaji wageni.


Kanuni hiyo inataka mchezaji ambae si Muingereza [ukitoa wachezaji toka Jumuia ya Ulaya] ni lazima achezee asilimia 70 ya mechi za timu yake ya Taifa katika miaka miwili iliyopita.


Manucho, mwenye umri wa miaka 25, alichezea mechi nane klabu hiyo ya Ugirki na kufunga bao moja. Amesema kuwa ametakiwa aripoti MAN U Julai 1 tayari kwa mazoezi ya kabla ya kuanza msimu mpya.

REPUBLIC OF IRELAND 1 COLOMBIA 0

Timu ya Taifa ya REPUBLIC OF IRELAND, ikiongozwa na Nahodha wao ambae pia ni nyota wa Timu ya LIGI KUU UINGEREZA TOTTENHAM HOTSPURS, ROBBIE KEANE, jana ilishinda kwa bao 1-0 kwa bao lilofungwa na Nahodha huyo katika dakika ya 3 ya mchezo katika mechi ya Kimataifa ya kirafiki dhidi ya COLOMBIA.
Republic of Ireland: Kiely, O'Shea, Dunne, McShane, Delaney, McGeady, Miller, Whelan, Keogh, Keane, Doyle. Subs: Joe Murphy, Kelly, McPhail, Long, Daryl Murphy, Scannell, Foley, Hoolahan, O'Dea, Westwood, Bruce, Garvan.
Colombia: Robinson Zapata, Cristian Zapata, Bustos, Luis Amaranto Perea, Gonzalez, Guarin, Sanchez, Escobar, Torres, Edixon Perea, Garcia. Subs: Julio, Walter Moreno, Motta, Amaya, Hernandez, Polo, Armero, Valencia, Vallejo, Soto.

INTER MILAN WAMTIMUA MENEJA ROBERTO MANCINI!
inasemekana yuko njiani kuelekea STAMFORD BRIDGE--CHELSEA!!!!
Meneja wa Mabingwa wa Serie A, INTER MILAN, Roberto Mancini, amefukuzwa huku kukiwa na tetesi kubwa kuwa yuko njiani kujiunga na CHELSEA ambao siku tano zilopita walimtimua Meneja wao AVRAM GRANT.
Uvumi huu umezidi kujengewa imani baada ya Chelsea nao kumtimua kazi aliekuwa Meneja Msaidizi, Mholanzi HENK TEN CATE ambae alijiunga na CHELSEA mara tu baada ya kuteuliwa AVRAM GRANT kuwa Meneja wa klabu hiyo. Hatua hii ya Chelsea inaonekana na wadadisi wa mambo kama kumjengea njia meneja mpya aje na utawala wake mpya.

Thursday 29 May 2008


UINGEREZA 2 USA 0

Jumatano usiku katika Uwanja wa Wembley, Timu ya Taifa ya Uingereza iliifunga Timu ya Taifa ya Mrekani [USA] kwa mabao 2-0 kwenye mechi ya kirafiki.
Goli la kwanza lilifungwa na Nahodha John Terry kwa kichwa kufuatia cross murua ya David Beckham. Goli la pili lilipachikwa na Steven Gerrard.
Jumapili, timu hiyo ya Uingereza itakumbuna na Trinidad and Tobago katika mechi nyingine ya kirafiki.
*********************************************************************************
REAL MADRID WANYWEA!
Kisanga cha Cristiano Ronaldo kusakwa kwa udi na uvumba na Klabu ya Real Madrid kimechukua hatua mpya baada ya Klabu hiyo kunywea kufuatia Man U kutishia kuishitaki FIFA.
Rais wa Real, Ramon Calderon, amesema wao ni marafiki na Man U na hawataki kugombana nao.

Tuesday 27 May 2008

MAN U WATOA ONYO KWA REAL!
Klabu ya MANCHESTER UNITED imeionya vikali REAL MADRID kwamba wataenda FIFA endapo klabu hiyo ya Uhispania itaendelea kumfuatafuata CRISTIANO RONALDO kwa misingi isiyokubalika.
Mreno RONALDO amekuwa mara kwa mara anahusishwa na kuhamia REAL msimu ujao ingawa MAN U siku zote wameng'ang'ania hahami.
Utata huu umezidishwa zaidi na kauli nyingi toka kwa viongozi wa REAL.
Sasa klabu ya MAN U imeonyesha kukasirishwa sana na imebidi watoe onyo kali kwa REAL waache kumrubuni RONALDO au watawashitaki FIFA.
Taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya MAN U [www.manutd.com] imeeleza: 'Manchester United imekuwa ikiangalia kwa kero kubwa habari kuwa REAL MADRID wana nia ya kumsajili RONALDO.'
'Ukweli ni kwamba: mchezaji huyo yuko kwenye mkataba wa muda mrefu na usajili wake uko chini ya Manchester United.'
' Mchezaji huyu hauzwi.'
' Klabu itakuwa haina njia nyingine isipokuwa kuishitaki REAL MADRID kwa bodi inayoongoza soka duniani FIFA endapo wataendelea katika tabia hii mbovu na isiyokubalika.'
' Haya majaribio ya waziwazi kumrubuni mchezaji na kumfanya ahamanike bila shaka ni kinyume cha taratibu na klabu haitavumilia tena.'
'Kwa nyongeza, klabu ina uhakika njama hizi vilevile zinaathiri maandalizi ya Timu ya Taifa ya Ureno wakati wanajitayarisha kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya.'
'Mtu yeyote asitegemee kwamba Manchester United itakaa tu bila ya kutumia nguvu zake zote kulinda wachezaji wake bora.'









RATIBA
7 Juni
Switzerland v Czech Republic
Basle, SAA 1 USIKU

Portugal v Turkey
Geneva, SAA 3.45 USIKU

8 Juni
Austria v Croatia
Vienna, SAA 1 USIKU

Germany v Poland
Klagenfurt, SAA 3.45 USIKU

9 Juni
Romania v France
Zurich - SAA 1 USIKU

Netherlands v Italy
Berne, SAA 3.45 USIKU

10 Juni
Spain v Russia
Innsbruck - SAA 1 USIKU

Greece v Sweden
Salzburg, SAA 3.45 USIKU

11 Juni
Czech Republic v Portugal
Geneva, SAA 1 USIKU

Switzerland v Turkey
Basle, SAA 3.45 USIKU

12 Juni
Croatia v Germany
Klagenfurt, SAA 1 USIKU

Austria v Poland
Vienna, SAA 3.45 USIKU

13 Juni
Italy v Romania
Zurich, SAA 1 USIKU

Netherlands v France
Berne, SAA 3.45 USIKU

14 Juni
Sweden v Spain
Innsbruck, SAA 1 USIKU

Greece v Russia
Salzburg, SAA 3.45 USIKU

15 Juni
Switzerland v Portugal
Basle, SAA 3.45 USIKU

Turkey v Czech Republic
Geneva, SAA 3.45 USIKU

16 Juni
Austria v Germany
Vienna, SAA 3.45 USIKU

Poland v Croatia
Klagenfurt, SAA 3.45 USIKU

17 Juni
France v Italy
Zurich, SAA 3.45 USIKU

Netherlands v Romania
Berne, SAA 3.45 USIKU

18 Juni
Greece v Spain
Salzburg, SAA 3.45 USIKU

Russia v Sweden
Innsbruck, SAA 3.45 USIKU

ROBO FAINALI
[MECHI ZOTE SAA 3.45 USIKU]


19 Juni
MSHINDI KUNDI A [A1] VS WA PILI KUNDI B [B2]
Basle,

20 Juni
MSHINDI KUNDI B [B1] VS WA PILI KUNDI A [A2]
Vienna,

21 Juni
MSHINDI KUNDI C [C1] VS WA PILI KUNDI D [D2]
Basle,

22 Juni
MSHINDI KUNDI D [D1] VS WA PILI KUNDI C [C2]
Vienna,

NUSU FAINALI
[MECHI ZOTE SAA 3.45 USIKU]


25 Juni
A1/B2 v B1/A2
Basle,

26 Juni
C1/D2 v D1/C2
Vienna,

FAINALI

29 Juni [SAA 3.45 USIKU]
Vienna,

GERARD PIQUE ARUDI BARCELONA!


FC BARCELONA na MANCHESTER UNITED zimeafikiana uhamisho wa chipukizi GERARD PIQUE mwenye umri wa miaka 21 kurudi tena kwenye klabu yake aliyoihama 2004 ya BARCELONA.

Mlinzi huyo Mhispania alidumu MAN U kwa miaka 4 alianza mechi 14 na kuingizwa katika mechi 9 akitokea benchi la akiba. Aliifungia MAN U magoli mawili katka LIGI YA MABINGWA WA ULAYA msimu huu katika mechi dhidi ya DYNAMO KIEV na AS ROMA.

Inasemekana MAN U italipwa pauni za Kiingerezamilioni 6 [SHS BILIONI 14 ZA KIBONGO] kama ada ya uhamisho.

BASEL, SWITZERLAND UWANJA WA ST JAKOB-PARK
MECHI YA UFUNGUZI YA EURO 2008 KATI YA WENYEJI USWISI NA CZECH ITACHEZWA HAPA JUNI 7.


CHINI NI PICHA YA UWANJA WA ENRST HAPPEL MJINI, VIENNA, AUSTRIA AMBAKO FAINALI YA EURO 2008 ITACHEZWA JUNI 29.
EURO 2008

VIWANJA VITAVYOTUMIKA

Nchi mbili za Ulaya, Austria na Switzerland, ndio watakuwa wenyeji wa Mashindano ya Mataifa ya Ulaya yajulikanayo kama EURO 2008 yatakayoanza JUNI 7 na kuisha JUNI 29.

Mechi ya ufunguzi kati ya wenyeji USWISI na CZECH itachezwa mjini BASEL uwanja wa ST JAKOB-PARK.

Fainali itachezwa nchini AUSTRIA mjini VIENNA kwenye uwanja wa ENRST HAPPEL.

Kila nchi itakuwa na miji minne na viwanja vinne vitakavyotumika kuchezwa mechi hizo.

AUSTRIA

VIENNA: ERNST HAPEL STADION

SALZBURG: STADION WALS-SIEZNHEIM

INNSBRUCK: TIVOLI-NEU STADION

KLAGENFURT: WORTHERSEE STADION

SWITZERLAND

ZURICH: LETZIGRUND STADION

GENEVA: STADE DE GENEVA

BERNE: STADE DE SUISSE WANKDORF

BASEL: ST JAKOB-PARK



Monday 26 May 2008


RONALDO: 'NINA FURAHA MAN U'
Nyota wa MAN U amesema ana mapenzi makubwa kuwa MANCHESTER UNITED ingawa angependelea siku moja acheze huko Spain.
Alisema: 'Magazeti siku zote yanaandika si REAL tu wananitaka hata BARCELONA pia. Ni vizuri kujua unazivutia klabu kubwa kwani hii inadhihirisha una thamani. Lakini kwa sasa kichwa changu kipo MAN U. Sasa, kama nilivyosema mara nyingi tu, ni Mungu pekee anaejua nini kitatokea hapo baadae. Sijamficha mtu kuwa ningependa hapo baadae kucheza Spain. Hiyo ni ndoto yangu lakini mara nyingi ndoto haziji. Nakuhakikishia nina mapenzi MAN U na ningependa kuendelea hapo.'


MENEJA ALIETIMULIWA ASIFU UZOEFU ALIOUPATA CHELSEA!!!

Myahudi Avram Grant, aliemwaga unga CHELSEA, amerudi kwao Israel jana na kusema kuwa amepata uzoefu mkubwa alipokuwa klbuni hapo.

Pia akatoa shukrani za dhati kwa Wayahudi wenzake kwa jinsi walivyomuunga mkono alipokuwa akiiendesha Chelsea.
Nae Meneja aliemtangulia Avram Grant hapo Chelsea, Mreno Jose Mourinho amekanusha vikali kuwa kuna mipango ya yeye kurudishwa tena Chelsea.
Kuna habari pia msimu ujao Jose Mourinho atarudi tena kwenye viwanja ingawa si Chelsea.

Sunday 25 May 2008







EURO 2008
JUNI 7-JUNI 29, 2008 nchini SWITZERLAND & AUSTRIA

Mashabiki wengi wa soka wanangojea kwa hamu Mashindano ya TIMU ZA TAIFA BARA LA ULAYA, EURO 2008, ambayo yatachezewa kwenye nchi mbili kwa pamoja, yaani USWISI na AUSTRIA, yatakayoanza 7 JUNI 2008 uwanjani ST JAKOB PARK, mjini BASLE, SWITZERLAND kwa mechi kati ya wenyeji wenza SWITZERLAND dhidi ya CZECH REPUBLIC.
Mechi ya FAINALI itachezwa Jumapili 29 JUNI 2008 uwanjani ERNST HAPPEL, VIENNA, AUSTRIA.
Timu za Mataifa 16 ya Ulaya zitashiriki zikigawanywa katika makundi manne ya timu 4 kila moja zitazocheza mechi za awali kwa njia ya ligi. Miongoni mwa timu hizo 16 ni wenyeji wenza AUSTRIA na SWITZERLAND.
MAKUNDI:
KUNDI A-CZECH, URENO, USWISI, UTURUKI

KUNDI B- AUSTRIA, CROATIA, UJERUMANI, POLAND,

KUNDI C- UFARANSA, ITALIA, UHOLANZI, ROMANIA

KUNDI D- UGIRIKI, URUSI, SPAIN, SWDEN

HULL CITY YATINGA LIGI KUU UINGEREZA!!!


HULL CITY 1 BRISTOL CITY 0


HULL CITY, kwa mara ya kwanza katika historia yao ya miaka 104, imefika kileleni mwa soka ya UINGEREZA baada ya kushinda fainali ya mtoano wa kuingia LIGI KUU UINGEREZA kwa kuifunga BRISTOL CITY 1-0 katika UWANJA WA WEMBLEY.

Kazi nzuri aliyoifanya chipukizi wa MAN U, FRAZIER CAMPBELL mwenye miaka 20, ambae yuko HULL CITY kwa mkopo, ilimfikia mkongwe DEAN WINDASS, mwenye miaka 39, ambae alifunga bao safi la ushindi. [PICHANI NI CAMPBELL AKIMRUKIA WINDASS KUSHANGILIA GOLI]


Timu hiyo ya HULL CITY ina maveterani wengine kama JAY JAY OKOCHA ambae hakucheza kwa kuwa ni majeruhi na NICK BARMBY ambae alicheza na kubadilishwa kipindi cha pili.


HULL CITY imeungana na WEST BROMWICH ALBION na STOKE CITY kuingia LIGI KUU UINGEREZA ambayo inatarajiwa kuanza msimu wa mwaka 2008/2009 mwezi AGOSTI.

MYAHUDI AVRAM GRANT AFUKUZWA KAZI CHELSEA


Siku tatu tu baada ya kuukosa UBINGWA WA ULAYA ambao MAN U waliunyakua, MENEJA wa CHELSEA, AVRAM GRANT, ametimuliwa. GRANT ambae alimrithi JOSE MOURINHO amedumu kama meneja kwa miezi minane tu.
Powered By Blogger