Real wang’ang’ana Ronaldo majeruhi, Madaktari wa Timu ya Taifa ya Ureno kumcheki!!!
Winga wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amelazimika kusafiri hadi kwao Ureno ili Madaktari wa Timu ya Taifa ya Ureno wampime baada ya Klabu yake kugoma na kudai hayuko fiti kucheza na inabidi apumzishwe wiki mbili zaidi.
Ronaldo amechaguliwa Timu ya Ureno ambayo inakabiliwa na mechi muhimu sana za Mtoano ili kuingia Fainali Kombe la Dunia hapo Jumamosi Novemba 14 na Jumatano Novemba 18 watakapocheza na Bosnia-Herzegovina na mshindi kwenye mechi hiyo ndio anaetinga Fainali Kombe la Dunia mwakani.
Ronaldo aliumia enka yake Septemba 30 kwenye mechi ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE kati ya Real Madrid na Marseille na hajacheza mechi 7 kwa Klabu yake ingawa aliichezea Ureno Oktoba 10 walipocheza na Hungary kwenye mechi ya Makundi Kombe la Dunia na ndipo akajiumiza tena kwenye enka hiyo hiyo majeruhi.
Bosi wa Ureno, Carlos Queiroz, ambae aliwahi kuwa Meneja wa Real Madrid na pia Msaidizi wa Sir Alex Ferguson Manchester United, amesema: “Sheria za FIFA zinatulinda na hivyo tutampima. Tunaheshimu kila Klabu lakini hii ni haki yetu kuridhika kuhusu Mchezaji wetu.”
Bendtner kufanyiwa operesheni!!
Arsenal imethibitisha kuwa Mshambuliaji wao toka Denmark, Nicklas Bendtner, atafanyiwa upasuaji ili kumtibu nyonga na atakuwa nje ya uwanja kwa wiki 4.
Bendtner aliumia Oktoba 31 Arsenal ilipowafunga Tottenham 3-0 kwenye Ligi Kuu Uwanjani Emirates.
Mshambuliaji huyo, alieifungia Arsenal goli 3 msimu huu katika mechi 13, atafanya hiyo operesheni huko Ujerumani.
Goli la mwisho alilofunga Bendtner ni lile lililowaua na kuwatoa Liverpool nje ya Kombe la Carling alipopachika bao la pili na kuwapa Arsenal ushindi wa 2-1.
Liverpool: Uwanjani matokeo si mazuri, Wachezaji wazidi kujeruhiwa!!!
Ingawa Rafa Benitez amewapa faraja kidogo Wadau wa Liverpool pale alipotangaza Mhimili wao mkuu, Fernando Torres, halazimiki kufanyiwa upasuaji ili kutibu maumivu yake na pia Gerrard kuonekana uwanjani jana, lakini wasiwasi unazidi kutanda kwa matokeo ‘mabovu’ uwanjani na listi ya majeruhi kuongezeka kwa Wachezaji wanaotumainiwa.
Wachezaji Albert Riera na Yossi Benayoun waliocheza mechi ya jana Liverpool waliyotoka suluhu 2-2 na Birmingham walilazimika kutoka nje ya uwanja huku wakichechemea na Benitez amethibitisha itabidi wawe nje kwa muda pamoja na Mlinzi Dan Agger mwenye matatizo ya mgongo.
Tuesday, 10 November 2009
FIFA U-17 WORLD CUP NIGERIA 2009
Wenyeji Nigeria na Spain waingia Nusu Fainali!!!
Nigeria ambao ndio wenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia kwa Vijana Chini ya Miaka 17 wamefanikiwa kuingia Nusu Fainali baada ya kuifunga South Korea 3-1.
Katika Robo Fainali nyingine iliyochezwa jana, Spain waliitoa Uruguay kwa penalti 4-2 baada ya mechi kwisha bao 3-3.
Nigeria watakutana na Spain kwenye Nusu Fainali.
RATIBA NUSU FAINALI:
Alhamisi, Novemba 12:
Colombia v Uswisi
Nigeria v Spain

Mwana wa Fergie atimuliwa Umeneja Peterborough!!!
Peterborough United, Klabu inayocheza Daraja chini tu ya Ligi Kuu liitwalo Coca Cola Championship, imemwondoa kazini Meneja wao Darren Ferguson [pichani] ambae ni mtoto wa Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson kufuatia matokeo mabaya kwa Klabu hiyo.
Darren Ferguson, umri miaka 37, ndie alieibeba Timu hiyo na kuipandisha Klabu hiyo mfululizo Madaraja mawili juu kutoka LIGI 2 mpaka ilipo sasa kuanzia mwaka 2007.
Lakini msimu huu, kwenye Ligi ya Coca Cola Championship, Timu hiyo imekuwa ikifanya vibaya na Jumamosi ilipigwa 3-1 na Newcastle.
Katika mechi 140 alizokuwa Meneja hapo Peterborough, Darren Ferguson, ameshinda mechi 73 na kufungwa 40 tu.
KOMBE LA DUNIA: Mechi za Lala Salama, Nani kwenda Bondeni?
Tayari Nchi 23 zishapata Tiketi kucheza Fainali za Kombe la Dunia Afrika Kusini 2010, Fainali zitakazoanza Juni 11 na kumalizika Julai 11, na bado kuna nafasi 9 zikidai ili kufanya jumla ya Nchi 32 kwenye Fainali hizo.
LISTI KAMILI YA TIMU 23 ZILIZOINGIA FAINALI NI:
WENYEJI: Afrika Kusini
AFRIKA: Ghana na Ivory Coast [BADO TIMU 3]
ASIA: Australia, Japan, Korea Kaskazini, Korea Kusini
ULAYA: Denmark, England, Germany, Uholanzi, Serbia, Spain, Italy, Slovakia, Uswisi [BADO TIMU 4]
MAREKANI KUSINI: Brazil, Paraguay, Chile, Argentina
MAREKANI KASKAZINI, KATI NA CARIBBEAN: USA, Mexico, Honduras
TIMU ZITAKAZOINGIA FAINALI KUPITIA MECHI ZA MCHUJO [Moja kati ya mbili zifuatazo]:
-New Zealand au Bahrain [Mechi ya kwanza Nchini Bahrain ilikuwa 0-0]
-Costa Rica au Uruguay
-Urusi au Slovenia
-Ufaransa au Republic of Ireland
-Ureno au Bosnia-Herzegovina
-Ukraine au Greece
-AFRIKA [INATEGEMEA MATOKEO KWENYE MAKUNDI YAO]: Wenye matumaini makubwa kupata Nafasi 3 zilizobaki ni:
-KUNDI A- Cameroun au Gabon
Cameroun pointi 10
Gabon pointi 9
Cameroun, ambao watacheza ugenini huko Morocco, wanatakiwa waifunge Morocco ili watinge Fainali.
Gabon ni lazima washinde mechi yao na Togo itakayochezwa huko Togo na pia kuomba Cameroun watoke suluhu au wafungwe.
-KUNDI B- Tunisia au Nigeria
Tunisia pointi 11
Nigeria pointi 9
Tunisia watasafiri hadi Msumbiji na Nigeria watakuwa Kenya kwa mechi zao za mwisho.
Ikiwa Tunisia wataifunga Msumbiji basi watafanikiwa kwenda Fainali.
Lakini hata Tunisia wakitoka sare huko Msumbiji huku Nigeria afungwe au atoke sare na Kenya, Tiunisia watapita.
Nigeria ni lazima waifunge Kenya na kuomba Tunisia afungwe au atoke dro.
-KUNDI C- Misri au Algeria
Algeria pointi 13
Misri pointi 10
Ni Misri au Algeria ndio watafika Fainali na Timu hizi zinakutana Mjini Cairo, Misri Jumamosi.
Wakati Algeria inahitaji suluhu tu ili asonge mbele, Misri ni lazima ishinde kwa goli 3-0 ili wapite.
Mechi ikiisha kwa ushindi wa 2-0 kwa Misri mechi hii inabidi irudiwe Nchi nyutro [si Misri wala Algeria] kwani zitakuwa zimelingana kila kitu.
RATIBA:
Afrika
Novemba 14
Mozambique v Tunisia
Togo v Gabon
Morocco v Cameroun
Rwanda v Zambia
Kenya v Nigeria
Burkina Faso v Malawi
Ivory Coast v Guinea
Egypt v Algeria
Sudan v Benin
Novemba 15
Ghana v Mali
Asia na Oceania
Novemba 14
New Zealand v Bahrain [Mshindi mechi hii ataingia Fainali lakini sare yeyote ya magoli, Bahrain atakuwa Fainali kwa magoli ya ugenini kwani mechi ya kwanza huko Bahrain ilikuwa 0-0]
Marekani
Novemba 14
Costa Rica v Uruguay
Novemba 18
Uruguay v Costa Rica
Ulaya
Novemba 14
Urusi v Slovenia
Republic of Ireland v Ufaransa
Greece v Ukraine
Ureno v Bosnia-Herzegovina
Novemba 18
Ukraine v Greece
Bosnia-Herzegovina v Ureno
Ufaransa v Republic of Ireland
Slovenia v Urusi
LIVEPOOL 2 BIRMINGHAM 2
Wakiwa nyumbani Anfield, Liverpool jana chupuchupu kufungwa na Birmingham kama si kupewa penalti tata na Refa Peter Walton kwenye dakika ya 71 na Nahodha Steven Gerrard, alieingia toka benchi la akiba, kufunga bao la pili kwa penalti hiyo na kusawazisha.
Penalti hiyo ilikuja baada ya Fowadi wa Liverpool David Ngog kujiangusha bila kuguswa na kumhadaa Refa.
Liverpool walianza kupata bao dakika ya 13 Mfungaji akiwa Ngog na Birmingham wakasawazisha kupitia Benitez dakika ya 26 na Jerome akapachika bao la pili dakika ya 45.
VIKOSI:
Liverpool: Reina, Johnson, Agger, Insua, Skrtel, Riera [Gerrard, dak 45], Benayoun [Babel dak ya 77], Mascherano, Lucas [Aquilani, dak 82], Kuyt, Ngog.
Birmingham: Hart, Carr, Ridgewell, Johnson, Dann, Bowyer, Larsson, Tainio [Carsley, dak ya 15], Jerome, Benitez [McSheffrey, dak ya 86], Mac Fadden [Vignal, dak ya 76]

Monday, 9 November 2009
FA yampa onyo Rooney kwa kauli: "MTU 12!! MTU 12!!' aliyoitoa baada ya mechi ya Chelsea jana!!!
Mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney amepewa onyo na FA, Chama cha Soka England, na ametakiwa achunge mwenendo wake wa baadae baada ya kunaswa akipiga kelele kwenye Kamera ya TV 'MTU 12!! MTU 12!!', akimaanisha Refa kawabeba Chelsea, mara tu baada ya mechi ya Ligi Kuu jana kumalizika huko Stamford Bridge kwa Chelsea kuifunga Man U 1-0 kwa goli la utata.
Pia FA imesema Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, hana hatia baada ya kutamka maamuzi ya Refa Martin Atkinson yalikuwa ni upuuzi wa hali ya juu na pia kusema maamuzi kama hayo yanawafanya watu wakose imani kwa Marefa.
Kwa sasa Ferguson yupo matatani na FA akikabiliwa na kesi inayosubiri uamuzi baada ya kushitakiwa mwezi Oktoba pale alipodai Refa Alan Wiley hayuko fiti kuchezesha mara tu baada ya mechi kati ya Man U na Sunderland kwisha dro 2-2.

Fletcher: “Wenger ananiponza kwa Marefa!”
Darren Fletcher anaamini kabisa Marefa sasa wanamsakama mno kufuatia matamshi ya Meneja wa Arsenal Arsene Wenger, mwanzoni mwa msimu, alipokuwa akinung’unika baada ya Arsenal kupigwa 2-1 na Manchester United kwenye mechi ya Ligi Kuu Uwanjani Old Trafford, na kudai Man U imecheza 'kinyume na soka' na Wachezaji wake kucheza rafu.
Ingawa baada ya mechi hiyo Wenger hakumtaja kwa jina Kiungo huyo wa Man U, lakini ilikuwa ‘siri ya wazi’ maneno yake hayo na hasa alipotamka kwamba kuna Mchezaji katika mechi hiyo alikuwa akicheza rafu mfululizo bila ya kuonywa na Refa yalimlenga Fletcher.
Fletcher amesema: “Kauli ya Bwana Wenger sasa inaanza kuwafanya Marefa waone mie ni Mchezaji mchafu! Ile frikiki iliyowapa goli Chelsea sio faulo! Sikucheza rafu, niliupiga mpira kwa kisigino na Cole akajirusha juu! Sasa tunaanza kuona madhara ya Wenger! Lakini itabidi tuipandishe soka yetu ili maamuzi haya mabovu yasituumize zaidi!”
Tangu msimu uliopita chati ya Darren Fletcher imepanda juu sana hapo Manchester United na sasa anaonekana ni Mchezaji muhimu sana.
Wadau wengi wanaamini kukosekana kwake kwenye Fainali ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE, baada ya kupewa Kadi 'feki' kwenye Nusu Fainali ambazo Man U waliwapiga Arsenal nje ndani, ndiko kulisababisha Barcelona kushinda Fainali hiyo.

Baada ya mechi ya leo, Ligi Kuu kupisha kitimtim cha Kombe la Dunia hadi Novemba 21!!!
Baada ya mechi ya leo ya Ligi Kuu saa 5 usiku, saa za kibongo, Liverpool kuikaribisha Birmingham Uwanjani Anfield, Ligi Kuu England itakaa pembeni hadi Jumamosi, Novemba 21 ili kupisha mapambano ya kuwania kuingia Fainali za Kombe la Dunia Afrika Kusini 2010 ambayo yatachezwa Jumamosi Novemba 14 na marudiano ni Jumatano, Novemba 18.
Ratiba kuhusu mechi hizo tutawaletea kesho.
Vilevile, kwa Timu za Taifa ambazo zimefuzu kuingia Fainali hizo za Kombe la Dunia, kipindi hiki ni Kalenda ya FIFA kwa Timu za Taifa kucheza mechi kadhaa za kirafiki na hivyo kuna mechi kadhaa za kirafiki za Timu hizo.
RATIBA YA LIGI KUU NI KAMA IFUATAVYWO:
Jumatatu, 9 Novemba 2009
Liverpool v Birmingham
Jumamosi, 21 Novemba 2009
Birmingham v Fulham
Burnley v Aston Villa
Chelsea v Wolves
Hull City v West Ham
Liverpool v Man City
Man U V Everton
Sunderland v Arsenal
Jumapili, 22 Novemba 2009
Bolton v Blackburn
Stoke v Portsmouth
Tottenham v Wigan
Jumatano, 25 Novemba 2009
Fulham v Blackburn
Hull City v Everton

Ancelotti afurahia kumfunga “Mpinzani Bora!!!”
Carlo Ancelotti wa Chelsea amekiri kuwa amefurahishwa sana na kumfunga “Mpinzani Bora” baada ya Timu yake kuifunga Manchester United hapo jana kwenye Ligi Kuu Uwanjani Stamford Bridge bao 1-0.
Ingawa Chelsea walishinda kwa goli la utata lililolalamikiwa na Manchester United, mechi hiyo ilitawaliwa na Man U.
Ancelotti amesema: “Ilikuwa mechi ngumu! Kulikuwa hamna nafasi kwenye Kiungo, ilikuwa taabu kutengeneza nafasi! Sasa tuko pointi 5 mbele lakini inabidi tusilewe ushindi kwa kuifunga Timu Bora na Mpinzani wetu mkubwa!”
Wes Brown asisitiza Drogba alimchezea rafu Chelsea walipofunga goli!!
Rooney asikika akipiga kelele kwenye Kamera: “Mtu 12!! Mtu 12!!’
Mlinzi wa Manchester United Wes Brown amesisitiza kuwa Mshambuliaji wa Chelsea Didier Drogba alimchezea rafu wakati Chelsea wanafunga goli lao na Refa Martin Atkinson alipaswa kulikataa.
Chelsea walifunga goli lao dakika ya 76 kwa John Terry kupiga kichwa mpira wa frikiki ya Frank Lampard na mpira kumparaza Anelka, aliekuwa ofsaidi na kutinga wavuni.
Manchester United waliilalamikia frikiki hiyo kwa madai Darren Fletcher alicheza mpira na hakumgusa Ashley Cole aliejirusha.
Vilevile wamedai wakati Terry anapiga kichwa kufunga Drogba alimkamata na kumwangusha chini Brown.
Brown ametamka kwa masikitiko: “Sidhani Refa alichezesha vizuri! Lile goli si halali na hata frikiki ni utata mtupu! Lakini tutafanyaje ikiwa Refa haoni yote hayo?”
Mara baada ya mechi kwisha, mshambuliaji Nyota wa Manchester United Wayne Rooney alisikika akipiga kelele kwenye kamera: “Mtu 12!! Mtu 12!” bila shaka akimaanisha Refa alikuwa upande wa Chelsea.
Kikosi cha England kucheza na Brazil huko Doha, Qatar chatajwa!
Kocha wa England, Fabio Capello, amekitangaza Kikosi chake kitakachocheza mechi ya kirafiki na Brazil huko Doha, Qatar tarehe 14 Novemba 2009.
Katika Kikosi hicho wapo Darren Bent wa Sunderland ambae mara ya mwisho kuichezea England ni miezi 12 iliyopita kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Ujerumani na Beki wa Aston Villa, Stephen Warnock, ambae amechukuliwa badala ya Ashley Cole wa Chelsea anaesemekana kaumia.
Pia yupo Kiungo wa Tottenham, Tom Huddlestone, ambae ni mara ya kwanza kuitwa England.
Ingawa Beckham ametajwa kwenye Kikosi hicho lakini taarifa za baadaye zimesema hatowezi kujiunga na Timu kwa vile Klabu yake LA Galaxy ilishinda Nusu Fainali yake ya Ligi ya MLS hapo jana na hivyo kutinga Fainali.
Kikosi kamili ni: Foster (Manchester United), Green (West Ham), Hart (Manchester City); Bridge, Lescott (Manchester City), Brown (Manchester United), Cahill (Bolton), Johnson (Liverpool), Terry (Chelsea), Upson (West Ham), Warnock (Aston Villa); Barry, Wright-Phillips (Manchester City), Beckham (Los Angeles Galaxy), Carrick (Manchester United), Huddlestone, Jenas (Tottenham), Lampard (Chelsea), Milner, Young (Aston Villa); Bent (Sunderland), Crouch, Defoe (Tottenham), Rooney (Manchester United).

Sunday, 8 November 2009
Yemen 1 Bongo 1
Leo Timu ya Taifa ya Tanzania, baada ya kushushiwa kipigo cha 5-1 na Misri siku ya Jumatano, ilikuwa Nchini Yemen kucheza na Wenyeji wao na mechi kuisha sare 1-1.
Mpaka haftaimu ngoma ilikuwa 0-0.
Kipindi cha pili, Bongo walifunga dakika ya 68 kupitia Mchezaji alietajwa ni Poko na Yemen wakasawazisha dakika ya 79 Mfungaji akiwa Ali Mubarak.

Colombia kuikwaa Uswisi Nusu Fainali!!
Colombia na Uturuki zilitoka sare 1-1 hadi dakika 120 na mshindi akapatikana kwa matuta na Colombia amepita kwa penalti 5-3.
Katika mechi nyingine ya Robo Fainali, Uswisi imeitoa Italy 2-1 na hivyo kukutana na Colombia kwenye Nusu Fainali tarehe 12 Novemba 2009.
RATIBA Jumatatu Novemba 9:
ROBO FAINALI
Spain v Uruguay
Nigeria v South Korea
WASHINDI WA MECHI HIZI WATAKUTANA NUSU FAINALI.

Fergie: “Tumepoteza imani na Marefa!!”
Licha ya kuwalaumu Wachezaji wake kwa kushindwa kuugeuza umiliki wa mechi kuwa magoli, Sir Alex Ferguson amemlaumu pia Refa Martin Atkinson kwa kuwapa Chelsea frikiki iliyozua goli bila rafu kutendeka, kwa kukubali goli hilo huku Drogba akimuangusha Wes Brown na wakati huo huo mpira kuguswa na Anelka aliekuwa ofsaidi na kuingia wavuni ingawa Chelsea wanaficha kuwa Mfungaji si Anelka na kung’ang’ania Terry ndie aliefunga.
“Ni uamuzi mbovu!” Ferguson amelalamika. “Lakini utafanyaje? Unapoteza imani kwa Marefa! Wachezaji wote wanasema Refa hakututendea haki!”
Mbali ya goli hilo kukubalika, Man U wanadhani walionewa pale dakika ya 14 Valencia alipoangushwa na Terry kwenye boksi na Refa hakutoa penalti.
Na ikafuata Rooney kupewa pande tamu na akiwa akienda kumuona Kipa Cech, kwa mshangao, ikaamuliwa ni ofsaidi.
Lakini, juu ya yote, hakuna Mdau wa Man U anaeshangaa maamuzi ya Marefa kwa kipindi hiki ambacho Wadau hao wanadai Man U inaandamwa.

Chelsea 1 Man U 0
Chelsea mbele pointi 5!!!
Goli la dakika ya 76 alilofunga John Terry [au Anelka aliekuwa ofsaidi huku Drogba akimwangusha Brown!] kufuatia frikiki ambayo Washabiki wa Man U walilalamikia limewapa ushindi Chelsea wakiwa nyumbani Stamford Bridge wa bao 1-0 dhidi ya Mabingwa Manchester United na sasa kuongoza pointi 5 mbele kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
Ingawa leo Manchester United walichezesha ukuta dhaifu bila ya Masentahafu wao Nemanja Vidic na Rio Ferdinand ambao ni majeruhi, na ingawa Vidic alikuwa benchi, waliitawala mechi hii na pengine wangeweza kushinda.
VIKOSI:
Chelsea: Cech, Ivanovich, Carvalho, Terry, Cole, Essien, Lampard, Ballack, Deco, Drogba, Anelka.
Akiba: Hilario, Joe Cole, Mikel, Malouda, Paulo Ferreira, Kalou, Alex.
Manchester United: Van der Sar, O'Shea, Brown, Jonathan Evans, Evra, Fletcher, Carrick, Anderson, Valencia, Rooney, Giggs.
Akiba: Kuszczak, Owen, Vidic, Scholes, Fabio Da Silva, Obertan, Gibson.
Refa: Martin Atkinson

Matokeo Mechi za leo Ligi Kuu, Jumapili, Novemba 8:
Mechi zimeanza mapema [Chelsea na Man U inaendelea]
Hull 2 v Stoke 1
West Ham 1 v Everton 2
Wigan 1 v Fulham 1

Fergie atimiza Miaka 23 Man U na kutoboa Klabu nyingi za nje zilimtaka!!
Sir Alex Ferguson ametoboa kuwa katika miaka yake 23 aliyotimiza Ijuma iliyopita Klabu nyingi kubwa za nje ya England zimekuwa zikimpa ofa nono ya kwenda kufundisha lakini mwenyewe amekiri “huwezi ukaikimbia Manchester United!”
Sir Alex Ferguson ametoboa kuwa katika miaka yake 23 aliyotimiza Ijuma iliyopita Klabu nyingi kubwa za nje ya England zimekuwa zikimpa ofa nono ya kwenda kufundisha lakini mwenyewe amekiri “huwezi ukaikimbia Manchester United!”Katika miaka hiyo 23 akiwa Old Trafford na Manchester United, Sir Alex Ferguson amefanikiwa kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England mara 11, Ubingwa wa Ulaya mara 2, Kombe la FA mara 5, Kombe la Ligi mara 3, Kombe la Washindi Ulaya mara 1, Kombe Klabu Bingwa Duniani mara 2 na UEFA Super Cup mara 1.
Ferguson amekiri: “Nimepata ofa nyingi tu lakini hakuna hata moja iliyonivutia!”
LIVERPOOL HAIUZI MTU!!!
Mmojawapo wa Wamiliki wawili Liverpool, Tom Hicks, amewahakikishia Mashabiki wao kuwa hata kama Liverpool itatolewa mapema kwenye UEFA CHAMPIONS LEAGUE wao hawana nia ya kuuza Mchezaji yeyote.
Msimu huu Liverpool wameuanza kwa balaa kwani wapo nafasi ya 7 kwenye Ligi Kuu na pia wako hali mbaya kwenye UEFA CHAMPIONS LEAGUE huku wakitakiwa washinde mechi zao zote 2 zilizobaki Kundini mwao na pia kuomba wengine wapate matokeo mabaya ili wao wasonge mbele.
Hali hii mbaya imefanya kuzagae habari kuwa Mastaa kama Fernando Torres na Steven Gerrard huenda wakang’oka na imebidi Mmiliki huyo Tom Hicks ajitokeze kutuliza watu.
Kipa wa Sunderland avunjika mkono!!
Sunderland imethibitisha kuwa Kipa Craig Gordon ambae pia huidakia Timu ya Taifa ya Scotland amevunjika mkono baada ya kuumizwa na Jermaine Defoe, Straika wa Tottenham, kwenye mechi ya Ligi Kuu jana ambayo Tottenham iliifunga Sunderland 2-0 uwanjani White Hart Lane.
Kipa huyo mwenye umri wa miaka 26 alitolewa na nafasi yake kushikwa na Marton Fulop.
Meneja wa Sunderland Steve Bruce amethibitisha kuumia kwa Gordon lakini hakusema atakuwa nje kwa muda gani.
Capello aonya Wachezaji majeruhi!!
Bosi wa England, Fabio Capello, amesema Kikosi chake hakina nafasi kwa Mchezaji ambae hayuko fiti na wasitegemea watachukuliwa kwenda Fainali Kombe la Dunia huko Afrika Kusini Juni mwakani ikiwa hawakuthibitisha uimara wao.
Capello anategemewa kutangaza Kikosi chake kitakachocheza mechi ya kirafiki na Brazil Jumamosi tarehe 14 Novemba 2009 huko Doha, Qatar muda wowote leo.
Capello amemzungumzia Rio Ferdinand na kusema ikiwa atakuwa fiti kabla hajateua Kikosi chake cha mwisho basi ataenda nae Afrka Kusini lakini ameonya kuwa Ledley King, Beki wa Tottenham, na Kipa David James wana mashaka makubwa kutokana na kuwa majeruhi.
Kuhusu David James, Capello alisema: "James anacheza vizuri lakini tangu aumie akicheza mechi baadae hawezi kufanya mazoezi siku mbili!"

RATIBA ROBO FAINALI:
Jumapili Novemba 8:
Colombia v Turkey
Uswisi v Italy
Jumatatu Novemba 9:
Spain v Uruguay
Nigeria v South Korea
LIGI KUU England: Arsenal waibamiza Wolves 4-1 na kuchupa nafasi ya pili!!
Villa yaiua Bolton 5-1!!!
Matokeo Mechi za Jumamosi Novemba 7:
Wolves 1 Arsenal 4
Man City 3 Burnlay 3
Tottenham 2 Sunderland 0
Blackburn 3 Portsmouth 1
Aston Villa 5 Bolton 1
Jana Arsenal ikicheza ugenini iliibamiza Wolves mabao 4-1 na kushika nafasi ya pili wakiwa na pointi 25 sawa na Manchester United lakini Arsenal wana ubora wa magoli.
Chelsea yupo kileleni akiwa na pointi 27.
Mechi za leo Ligi Kuu, Jumapili, Novemba 8:
[saa 10 na nusu jioni]
Hull v Stoke
[saa 12 jioni]
West Ham v Everton
Wigan v Fulham
[saa 1 usiku]
Chelsea v Man U

Subscribe to:
Posts (Atom)